Taswira Mbalimbali Za Mikutano Ya Mwenyekiti Wa Chadema Freeman Mbowe Na Godbless Lema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taswira Mbalimbali Za Mikutano Ya Mwenyekiti Wa Chadema Freeman Mbowe Na Godbless Lema

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kiganyi, Aug 20, 2012.

 1. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #1
  Aug 20, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akiwasili kwenye Uwanja wa Kwa Mbombe katika kijiji cha Madizini, Kata ya Mtibwa mkoani Morogoro ambako alihutubia mkutano wa hadhara wa Opereshi Sangara juzi.
  [​IMG]
  Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini kabla ya Mahakama kutengua Ubunge wake, Mh Godbless Lema amefungua matawi katika Kata ya Daraja Mbili Jijini Arusha juzi August 18,2012.


  Katika ziara hiyo, Lema aliambatana na Mbunge wa Arumeru Masariki Mh Joshua Nassari(wa pili kulia) pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM kabla ya kujiengua na kujiunga na Chadema mapema mwezi Aprili mwaka huu, Ndg James Ole Millya, ambao nao kwa nyakati tofauti walipata fursa ya kuzunumza.

  Mbali na suala la uzinduzi na upokeaji wanachama wapya, Lema alifanya harambee ya kukusanya fedha kusaidia shughuli za chama hicho katika Kata hiyo ambapo jumla ya Sh 219,500 zilichangwa na wananchi.

  Akiondoka eneo hilo, Lema alilazimika kuwatuliza mamia ya watu waliokuwa wanafuatilia msafara wake ili kuepusha kutokea mwanya kwa watu wenye nia mbaya kuleta vurugu na uharibifu wa mali. Baadae msafara wake ulikatiza mitaa ya Stand Kuu ya mabasi makubwa na kisha kuelekea bustani ya City Park huku njiani akishangiliwa sana na baadhi ya watu wakinyoosha vidole kama ishara ya ushindi.
  [​IMG]
  Wanachama wapya aliojiunga na chadema wakigombania kadi za chama hicho
  [​IMG]
  Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini kabla ya Mahakama kutengua Ubunge wake, Mh Godbless Lema akiunguruma kwenye uzindusi wa matawi katika Kata ya Daraja Mbili Jijini Arusha juzi August 18,2012.
  [​IMG]
  Jitihada za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) za kuwafikia wanachi ili kunadi sera zake, hususan katika mikutano inayoendelea katika mkoa wa Morogoro, zilikumbana na vikwazo mbali mbali katika baadhi ya maeneo, kama inavyoonyesha pichani, mtaro uliochimbwa katika barabara ya kuingia kijiji cha Namgezi kitongoji cha Kambi ya Keya jimbo la Ulanga Mashariki, kwa lengo la kuzuia magari yasipite.Picha na Joseph Senga​

   
 2. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #2
  Aug 20, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,936
  Likes Received: 673
  Trophy Points: 280
  Dah ... napata matumaini makubwa sana kwa kizazi kijacho cha watanzania .. hii kazi inayofanywa na CDM ni nguvu ya mungu
   
 3. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #3
  Aug 20, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Kiganyi mambo vpi? Wapi kina Ritz na Tume ya katiba
   
 4. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #4
  Aug 20, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hahahahaha! Hapa wanapita kwa taadhari kubwa sana!
   
 5. M

  Molemo JF-Expert Member

  #5
  Aug 20, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mungu atukuzwe milele
   
 6. M

  Malata Junior JF-Expert Member

  #6
  Aug 20, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 2,780
  Likes Received: 1,207
  Trophy Points: 280
  kwa kweli hao viongozi wa ccm na serikali waliowatuma watu kuchimba mtaro magari yasipite hawakuwatendea haki kwani wamewachosha bure na bado mkutano ukafanyika. M4C haizuiliki!
   
 7. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #7
  Aug 20, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,130
  Trophy Points: 280
  Jamaa wanatumia mikakati ya Vyama vya KIKOMONST, hii mikakati ilitumiwa miaka ya 50 sasa nashangaa CCM kuitumia mida hii,
   
 8. C

  Concrete JF-Expert Member

  #8
  Aug 20, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Safiii,safi sanaaaa
  Mchakamchaka mpaka magamba wakimbie nchi hii.

  Naona mwitikio mkubwa sana wa akina mama huko morogoro, hii ni dalili njema sana kwamba ukombozi wa nchi yetu umekaribia sana.

  Mungu ibariki Chadema na harakati zake.
   
 9. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #9
  Aug 20, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  magamba lazima watepete, lazima wakae chini. hiki kimbunga kinawazidi nguvu.
   
 10. B

  Bahati Risiki JF-Expert Member

  #10
  Aug 20, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 531
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Na huku kwenye mitandao watachimba mitaro? Kweli CCM imekwisha kabisa. Ni afadhali hata wangekaa tu kimywa huku wakitazama wenye nguvu wakichukua madaraka. Kwa kuifanyia CDM hivi hata kipofu ataondoka CCM. Madhara ni makubwa sana kwa CCM kuliko hata CDM. Mungu ibariki CDM. Wasaidie viongozi wake watukomboe watanzania tumeteseka ya kutosha.
   
 11. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #11
  Aug 20, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,161
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Nimeipenda hiyo picha waliochimba mtaro, ukiona wameanza kucheza rafu za aina hii ujue game umeshawashinda
   
 12. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #12
  Aug 20, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kweli ccm imewaumiza watu c kiuchumi tu bali kiakili,sasa nn significance ya kuharibu miundombinu kuzuia tu M4C?kesho washindwe kupitisha mama mjamzito kumwahisha hospital kisa waliharibu barabara
   
Loading...