Tasnifu za njano5: Kilichomliza kitanda kuta nne wakijua?

Dotto C. Rangimoto

JF-Expert Member
Nov 22, 2012
1,994
1,282
Alichonong'ona mwezi, Kiza imekisikia,
Wanga masikio wazi, macho wameyatoa,
Mtabane kwa ujuzi, kitu hamtang'amua,
Loo!!! ufanye kazi, Poo!!! umegumiwa.

Kilichosemwa na jua, Nuru imekisikia,
Mimi ni wake tambua, nia amenisafia,
Wangu nyonda anijua, nitakacho anipatia,
Loo!! nawe wajua? Poo!!! waja jutia.

Alichotega mawingu, mvua imekitegua,
Mimi kwake ni mkungu, yeye ni chungu tambua,
Si mapenzi ya kizungu, haya tunayoringia,
Ya kiswahili mwenzangu, Loo!!! wajakimbia.

Alichoficha mlozi, Jini amekifichua,
Fatma hana ajizi, Penzi kulipigania
Subiani kawa chizi, wala hataki sikia,

Loo!!! u mkizi, Ujinini wapasikia?

Alichonena Njano, Msabazi kasikia,
Kawa juu ya chano, Njano nalifunua,
Wali wenyewe ni uno, Mh!! mbona nitalia.
Loo!!! hicho kiuno, Kama Nyigu nawaambia.

Kilichomliza kitanda, kuta nne wakijua,
Jalabibi kulitanda, wasipate kulijua,
Pete kwenye changu chanda, penzi imeliumbua,
Loo!!! nimevishwa sanda, ya manjano nawambia.

Kilichompata ala, Kisu anakitambua,
Mkataji wa milala, Chatu huwagumia,
Mapenzi si masihala, Vitimbi tegemea,
Tamati si kulala, Nautia kasi subiria.

Niulize kitu nikujibu bi idhini Allah!!

Njano5.
0715845394.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom