Tasnia ya ufundi wa magari imejaa watu wasio na elimu, wasomi tunakwama wapi?

Hata wewe ukikaa gereji kwa muda aliokaa huyo unaemuona hajasoma utakuwa mkali kuliko yeye na atakufuata umfundishe baadhi ya vitu kikubwa uvumilivu.

Wa shule wanachokosa ni uzoefu tu, ambao unapatikana baada ya kukaa field kwa kipindi fulani cha muda.
umenena vema kiongozi
 
kama ni hivyo mkuu basi kuna maana gani ya kukaa chuoni miaka mitatu au minne na kusoma mikozi migumu na kulipia mamilioni ya ada halafu mwisho wa siku mtu asiye na elimu awe bora kuliko wewe
Kwa maneno haya tu, una kila dalili ya kupenda ukubwa wa kazi! Ukiwa field jishushe.
Siku utayoweza kuhusianisha ulichosoma na unachokifanya ndiyo utaalamu wako utakapojidhihirisha.. acha utaalamu ujidhihirishe wenyewe ukubwa wa kazi utakuja wenyewe pia.
 
Kitu ambacho mleta mada nimeshindwa kumuelewa ni tofauti ya msomi na ambaye si msomi. Navyofahamu mm kuna aina mbili za Elimu, elimu rasmi (formal education) ambayo mwisho wake mwanafunzi anakuwa certified na pia hutolewa na taasisi za elimu rasmi, na yapili ni informal isiyo rasmi ambayo mara nyingi sana huwa ni ya viyendo, na utolewa tu, kijana anaweza ipata kwenye workshop mfano gereji, kwa baba ake, mjomba... nk

Faida: ya aliepitia formal education ni kwamba anajirika, hii nikutokana na certification alizonazo tofauti na aliepitia elimu isiyo rasmi kwa ukakasi wa ajira unawezakuwa mingi

Lakini ikumbukwe kuwa Elimu zote hizi mbili lengo lako ni moja, nikubadilisha tabia (behaviour ) ya mwanafunzi. Yani tunategemea mabadiliko ya tabia yatokea kwenye utendaji na maisha ya mwanafunzi. Yaani na maana gani, kama mwanafuzi alikuwa hajui kufunga nut kwenye tairi la gari bas baadae ya masomo yake tabia yake ibadilike na aweze kufanya hivo

Basi moja kwa moja naomba kumpinga mleta mada, kwa kuweka matabaka ya wasomi na ambao si wasomi kwa maelezo yake. Kwan wote hawa niwasomo, sema tofauti iyopo nikwamba njia walizopita ni tofauti
 
Mimi binafsi natupia lawama kwenye huu mfumo wetu wa elimu.. kwa nini tunatumia muda mwingi na nguvu nyingi kusoma mambo ambayo tukienda mtaani hatuoni uhalisia wake? kwa nini tusiwekeze nguvu zaidi kwenye kujijengea uwezo wa kufanya kazi tukaachana na hizi theory ambazo hazina ulazima
Ni kweli mkuu yan wange base kwenye practical sana mtu anakuambia ana master au degree muingize field utashangaa.
 
Kitu ambacho mleta mada nimeshindwa kumuelewa ni tofauti ya msomi na ambaye si msomi. Navyofahamu mm kuna aina mbili za Elimu, elimu rasmi (formal education) ambayo mwisho wake mwanafunzi anakuwa certified na pia hutolewa na taasisi za elimu rasmi, na yapili ni informal isiyo rasmi ambayo mara nyingi sana huwa ni ya viyendo, na utolewa tu, kijana anaweza ipata kwenye workshop mfano gereji, kwa baba ake, mjomba... nk

Faida: ya aliepitia formal education ni kwamba anajirika, hii nikutokana na certification alizonazo tofauti na aliepitia elimu isiyo rasmi kwa ukakasi wa ajira unawezakuwa mingi

Lakini ikumbukwe kuwa Elimu zote hizi mbili lengo lako ni moja, nikubadilisha tabia (behaviour ) ya mwanafunzi. Yani tunategemea mabadiliko ya tabia yatokea kwenye utendaji na maisha ya mwanafunzi. Yaani na maana gani, kama mwanafuzi alikuwa hajui kufunga nut kwenye tairi la gari bas baadae ya masomo yake tabia yake ibadilike na aweze kufanya hivo

Basi moja kwa moja naomba kumpinga mleta mada, kwa kuweka matabaka ya wasomi na ambao si wasomi kwa maelezo yake. Kwan wote hawa niwasomo, sema tofauti iyopo nikwamba njia walizopita ni tofauti
lengo langu sio kuweka matabaka ya waliosoma na wasiosoma don't misquote me...
labda mkuu ufanye tathmini ni wasomi wangapi waliotoka vyuo vikuu utawakuta wapo na ujuzi wa kuaminika kwenye ufundi wa magari?
labda cku moja uje utembelee kwenye magereji uchunguze vizuri, utakuta mtaalamu wa umeme, fundi body, fundi rejeta, fundi wa pampu.. wote hawa msomi hayupo... na cha ajabu utakuta hata waliosomea fani za engineering wanawapelekea mafundi haohao wa mtaani ndio wawatengenezee magari yao.. wakati wenyewe ndo walikaa darasani wakaisoma engine wakafanya na hadi calculation za diesel cycle na Otto cycle, na mahesabu ya RPM, na torque (kwenye engineering) mwisho wa cku cjui wanapotelea wapi
 
Kweli na kuna watu wamesoma veta wako vizuri, msomi wa degree akijipambanua na kuacha ubishooo akakubali kuchafuka oil daaah tungekuwa na wataalam wa kuunda magari yetu .
 
Kuna ukweli sana katika hili jambo lkn hili limechangiwa na jamii yetu kuwa na mtazamo wa kusoma na badae kuenda kuajiliwa ofisini tu huku tukisahau fursa zingine zaidi

Lkn pia kuna vitu unaweza kusoma au kukariri kama kizazi hiki kilivyo zoea lkn kwenye hii fani ya ufundi inahitaji kuelewa kwelikweli na sio kukariri sasa hapa ndio mshikemsike unaanza mtu anaenda na degree ya kukaririsha field lazima achemke
lakini mimi nahisi hili tatizo lipo tu kwenye hizi nchi zetu... hivi hata huko kwa wazungu kweli kwamba na wenyewe hali itakua ni kama huKu?
 
Nimesoma mawazo ya wengi hapa namimi naomba nichangie kama ifuatavyo, katika tasnia ya elimu kuna ngazi mbali mbali na kila ngszi ina kazi yake, watu ambao wanasomea degree hawa kwa kawaida huandaliwa kuwa wasimamizi kwenye kazi yoyote ile na si watendaji....ndo maana watu hawa hujazwa theory nyingi sana ili wawe wanajua kwa upana kile wanachotakiwa kukisimamia, watu wa diploma kushuka chini hawa kwa kiswahili wanaitwa mafundi mchundo hawa kwa kawaida wameandaliwa kuwa watendaji zaidi.

Sasa basi katika maana hiyo ndo tumapata tofauti ambayo wengi mmeiona kati ya aliyesoma Diploma na aliyesoma degree au yule ambaye kajifunza kwa mafundi wenzie, mtu mwenye degree anaweza mdomoni akaielezea kwa ufasaha kabisa cabulator lakini kumbe hata haifahamu lakini fundi mchundo anaifahamu cabulator ila haijui kiundani, sasa akikutana na msimamizi wake yeye anamsimamia kwa kumuelekeza vizuri kisha yeye anayeijua inapokaa anaenda kuifanyia kazi........sawa tu na mafundi ujenzi....mafundi wa mtaani hawajui jui kuzingatia kanuni za kitaalamu, ndo maana vitu kama expansion joint ye kwake haviko akilini kwahiyo akisimamiwa na mtaalamu wanafanya kazi nzuri.

Daima wanakuwaga kama hawajui maana wana theory nyingi kichwani lakini wakipata muda na wakiwa na moyo wa kujui huwa wabaya sana....reasoning yao huwa kubwa kuliko wa kawaida. Lakini mwisho na mimi huwa nasikitika kama alivyosikitika mtoa hoja kuwa watu wanasoma mechanical engineering halafu wanapoteza muda wakTi kazi zao zinafanywa na watu wasioenda shule huko mitaa
 
Baada ya kupitia hoja ya Mada pendwa "wasomi tunakwama wapi " nimeona nije na haya machache.

Nipongeze wote mlipanga hoja na kupangua kwa kadri mlivyoongozwa na halmashauri ya ubongo wenu. Ni hivi swala la ku-generalize wasomi wa degree wote kwa kada hii ya UFUNDI kuwa wapo kinadharia zaidi Kuliko vitendo, na hupelekea kuwa na uwezo mdogo wa kutenda nakataa. Si wote wanasomea mechanical wana passion ya hii fani. wengine ni kenge tu kwenye msafala wa mamba. Na si katika kada hii tu hata kada zinginezo Education, Health, media nk.

Sasa unakuja na hoja zako hapa unasema una diploma.... oooh degree ama PhD amekuuliza jambo unaona weye ni nguli. Au hujui kila mahali kuna code of ethics.... ni vigumu kuja kiwandani, garage, ofisini, nk. kisa nina ujuzi basi na kurupuka tu, kumbe wakati mwingine hata hata kutumia baadhi ya vitendea kazi kuna taratibu Mara umuone A Mara Z... Ila kuuliza tu unakuja jukwaani unasema Hakuna kitu Degree.

LAKINI
Nilisema kenge nao wapo... na wewe uliyekimbilia Degree ukahitimu hapa nchini.. jitafakari wewe.. "unakwama wapi... na degree yako hiyo "

#chuo kikuu ni chuo Kama vyuo Vingine ukizingua tafuta cha kufanya
 
Back
Top Bottom