Tasnia ya ufundi wa magari imejaa watu wasio na elimu, wasomi tunakwama wapi?

Little Dreamer

Senior Member
Sep 12, 2017
178
149
Kama kichwa kinavyojieleza!

Mimi nikiwa mhitimu wa fani ya Uhandisi wa Mitambo (Mechanical Engineering) katika moja ya vyuo hapa nchini, nimeamua kujikita katika tasnia hiyo ya ufundi magari ili nizidi kuongeza ujuzi.

Lakini kitu cha kushangaza nimekuta asilimia kubwa ya watu walio mahiri katika kazi hizo ni wale ambao hawakwenda shule (waliowahi kufanya field gereji watakuwa mashahidi), na kuna wengine hata kusoma na kuandika ni taabu, wakati huo sisi tunao onekana wasomi ndiyo tunajikuta hatujui chochote na tunaishia kuwa chini yao.

Hali inayonipelekea kujiuliza swali hili, "Wasomi tunakwama wapi? Je, elimu yetu haitusaidii?"
 
Asilimia kubwa watu wengi wanachukulia kazi ya ufundi magari inaitaji nguvu, pia watu wanajua kulala chini ndiyo ufundi.

POINT: Serikali ingeondoa gereji bubu ingesaidia kupunguza watu ambao hawajapitia shule.

Elimu inayotolewa chuoni ni theory sana kuliko vitendo. Mfano, mimi nina Diploma ya Mechanics lakini yupo mtu tupo naye yeye ana degree lakini kuna vitu vinamshinda ananiuliza mimi.

So, je mtu kakaa gereji ya mtaani miaka 10, wewe umekaa chuo miaka 4, kwenye vitendo nani atakua zaidi? Wewe utakuwa una utambuzi zaidi yake lakini fanya sasa modifikesheni aisee!
 
[QUOTE="Hazchem plate, Naona ujamuelewa lengo lake. E.g
1/ vifaa vya magari vimeandikwa kwa kiingereza yeye hajapita hata shule hata kusoma hafamu itakuaje ktk utambuzi
2/gari lina mfumo wa umeme mtu hatambui ECU au ECM àu hafamu kwanini huu wayaa ni mkubwa alaf yeye anaweka mdogo
3/ hafamu prisipo ya tairi za magari. N.k huyo ni fundi kweli
 
Asilimia kubwa watu wengi wanachukulia kazi ya ufundi magari inaitaji nguvu pia watu wanajua kulala chini ndio ufundi

POINT:- serikali ingeondoa gereji bubu itasaidia kupunguza watu ambao hawajapitia shule.

Elimu inayo tulewa chuoni ni theory sana kuriko vitendo e.g mimi na diploma ya Mechanics lakini yupo mtu tupo nae yeye ana degree lakini kuna vitu vinamshinda ananiuliza mimi so jee'! Mtu kaka gereji ya mtaani miaka 10 wewe umekaa chuo miaka 4 so kwenye vitendo nani hatakua zaidi sema wewe utakuwa unautambuzi zaidi yake lakini fanya sasa modifikesheni aisee !!!!?!!
Andika vizuri bana!
 
Mafundi
Kwaujumla Serikali Ya Viwanda Ikiwaondoa Hao Mafundi Kwa Siku Moja Tu Wananchi Wote Tutalia
Hao Mafundi Wapo Wataalam Ambao Hata Gharama Zao Ni Nafuu Sana Kuliko!!!!

Toyota Tanzania Limited
Wana Mafundi Wazuri Sana Na Vipuri Lakini Watu Wengi Sana Kwanza Wanaogopa Gharama Ingawa Unaweza Kununua Vipuri Huko Ukafunga Mtaani
 
Asilimia kubwa watu wengi wanachukulia kazi ya ufundi magari inaitaji nguvu pia watu wanajua kulala chini ndio ufundi

POINT:- serikali ingeondoa gereji bubu itasaidia kupunguza watu ambao hawajapitia shule.

Elimu inayo tulewa chuoni ni theory sana kuriko vitendo e.g mimi na diploma ya Mechanics lakini yupo mtu tupo nae yeye ana degree lakini kuna vitu vinamshinda ananiuliza mimi so jee'! Mtu kaka gereji ya mtaani miaka 10 wewe umekaa chuo miaka 4 so kwenye vitendo nani hatakua zaidi sema wewe utakuwa unautambuzi zaidi yake lakini fanya sasa modifikesheni aisee !!!!?!!
Wewe mwenye elimu ndogo kuulizwa na mtu mwenye elimu kubwa wala sio tatizo.

Mtu mweny PHD anaweza kuongozwa na mtu ambaye ni mbumbumbu.

Wewe unauzoefu.

Uzoefu maana yake ni kuwa wewe umefanya hio kazi kwa muda mrefu.
Uzoefu na elimu y kwenye makaratasi ni vitu viwili tofauti
 
Kuna ukweli sana katika hili jambo lkn hili limechangiwa na jamii yetu kuwa na mtazamo wa kusoma na badae kuenda kuajiliwa ofisini tu huku tukisahau fursa zingine zaidi

Lkn pia kuna vitu unaweza kusoma au kukariri kama kizazi hiki kilivyo zoea lkn kwenye hii fani ya ufundi inahitaji kuelewa kwelikweli na sio kukariri sasa hapa ndio mshikemsike unaanza mtu anaenda na degree ya kukaririsha field lazima achemke
 
kama ni hivyo mkuu basi kuna maana gani ya kukaa chuoni miaka mitatu au minne na kusoma mikozi migumu na kulipia mamilioni ya ada halafu mwisho wa siku mtu asiye na elimu awe bora kuliko wewe
 
Mimi binafsi natupia lawama kwenye huu mfumo wetu wa elimu.. kwa nini tunatumia muda mwingi na nguvu nyingi kusoma mambo ambayo tukienda mtaani hatuoni uhalisia wake? kwa nini tusiwekeze nguvu zaidi kwenye kujijengea uwezo wa kufanya kazi tukaachana na hizi theory ambazo hazina ulazima
 
kama ni hivyo mkuu basi kuna maana gani ya kukaa chuoni miaka mitatu au minne na kusoma mikozi migumu na kulipia mamilioni ya ada halafu mwisho wa siku mtu asiye na elimu awe bora kuliko wewe
Hujaelewa ninachomaanisha.

Wewe kuwa na uzoefu haimaanishi kuwa uanijua kazi vizuri kuliko mwe elimu.
Theory and practical ni vitu viwili tofauti.
Na wewe kuulizwa usije ukajiona kwamba umemzidi.
Kakuzidi vitu vingi sana na anachokuuliza sio kwamba hakifahamu anakifaau na anaweza kukufundisha.
 
kama ni hivyo mkuu basi kuna maana gani ya kukaa chuoni miaka mitatu au minne na kusoma mikozi migumu na kulipia mamilioni ya ada halafu mwisho wa siku mtu asiye na elimu awe bora kuliko wewe
Huyo mwenye degree anakuuliza leo, mpe muda apata uzoefu. Aweze kujua ni wapi anatakiwa ku-apply elimu, wapi nguvu etc halafu urudi hapa kuhoji umuhimu wa yeye kukaa chuoni miaka mitatu.

Unachomzidi ni wewe uliwahi field basi
 
Hata wewe ukikaa gereji kwa muda aliokaa huyo unaemuona hajasoma utakuwa mkali kuliko yeye na atakufuata umfundishe baadhi ya vitu kikubwa uvumilivu.

Wa shule wanachokosa ni uzoefu tu, ambao unapatikana baada ya kukaa field kwa kipindi fulani cha muda.
 
Back
Top Bottom