Tasnia ya filamu Tanzania ni sekta ya 'kuganga njaa'



Angali Hollywood, hawatishwi na piracy ya Wachina kwa kuwa wana uhakika wa kurudisha gharama zao
zote na kutengeneza faida maradufu.
isitoshe kwenye tafiti zilizofanywa (kama ile iliyokuwa presented na
Bishop J. Hiluka; The Perspective of Film and Television Industry in Tanzania) zinaonesha kuwa
Tanzania ni nchi yenye kiwango nafuu sana Afrika katika uharamia huu wa kazi za sanaa, huku nchi tano
zinazoongoza katika Afrika kwa kiwango kikubwa cha uharamia wa kazi za sanaa zikiwa ni Nigeria,
Cameroon, Togo, Kenya, na Benin, na nchi zenye unafuu sana katika uharamia huu ni Afrika Kusini
(kwa sababu imerekebisha sana sheria zake ikilinganishwa na nchi nyingine za Afrika), Namibia,
Ghana, Tanzania na Zimbabwe.



WS katika post yako hii nimekubali about yoote uloongea na kukupata vizuri zaidi sasa... Lakini the above kipengele pauses a problem kwangu... Ukiizungumzia TZ kwa kufanananisha na nchi zingine katika issue ya Piracy ni wazi lazima wao wataonekana nafuu tokana na ukweli kua Piracy goes hand in hand na technology ambazo zina liquidate the whole complicated issue of piracing... hivyo in that sense naweza kubali.. BUT hata hivyo ukweli unabaki kua Piracy ni serious case in TZ for tunaona the way wasaniii kazi zao zinapokelewa positively na jamiii mpaka kukuza majina but the Matunda wanayo pata hio ndo issue... Katika watu 10 ambao nawafahamu woote waweza kua na kazi ya msanii fulani but alonunua the origina kazi ni 1 or 2.. huoni kama ilo ni tatizo saana, kwa msanii mwenyewe na the entertainment business??? Na bora hataa wa filamu a bit, but music... Hawa ndo huchakachuliwa to the maximum!
 
Ili soko la filamu lifikie kiwango kizuri, kuna vigezo muhimu viwili ambavyo vinaweza
kutuongoza katika dhana nzima ya mafanikio katika usambazaji filamu:
(1) Maudhui/Mahitaji ya Watazamaji (Content/Audience Connection) na
(2) Jukwaa la Uwasilishaji (Media Delivery Platforms)



Hii post nimeikubali na maelezo yoote na iko pouwa, ila nina swali kabla sijaenda mbali... Maana tunapoongelea nini cha kuzingatiwa ili soko la filamu lifike vizuri umetoa muongozo moja kwa moja kua ni kutu gani cha weza tuongoza katika dhana nzima ya mafanikio katika usambazaji... naona kama umeenda mbele saana bila kutaja kwanza vitu vya kuzingatia katika soko la filamu.. In other words kua hicho kipengele cha kutuongoza katika usambazaji pamoja na the sub-vipengele ni moja tu ya sababu na zipo nyingine (in what to zingatia for the soko to be prosperous if not satisfying...)
 
Nina swali hivi kabla script writers wa movie zetu bongo hawajaanza kuandika uwa wanafanya research?


Mimi naona researches hua zinahusisha nyumba nzuri ni ipi and who is the owner...
au waki diverge hapo wanafanya research mwenye boutique ambae anapenda kuuza sura na jina....
Research ya kuhusiana na content naona ni at minimal or huuliza vijiwe vyao...
 
Wow! Nasubiri kuona synopsis na script yako kabla hujaingia kwenye shooting. Tunahitaji watuwenye kuthubutu kama wewe... Ukihitaji msaada wa kitaalam niambie nikutafutie mtaalam mzuri zaidikatika mausla ya script
No problemo.....thanks for the support!!
 
kumbe wataalamu wapo! Nikipata muda nitaweka script zangu hapa ili niweze kukosolewa na kufundishwa zaidi.Ahsanteni
 
kumbe wataalamu wapo! Nikipata muda nitaweka script zangu hapa ili niweze kukosolewa na kufundishwa zaidi.Ahsanteni


Itabidi uwe makini... kabla hujapost hakikisha una copywrites,
hili jamvi members na non-members woote wana access...
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Mimi naona researches hua zinahusisha nyumba nzuri ni ipi and who is the owner...
au waki diverge hapo wanafanya research mwenye boutique ambae anapenda kuuza sura na jina....
Research ya kuhusiana na content naona ni at minimal or huuliza vijiwe vyao...
Haha sasa hao wanaotafuta nyumba si ndio wanaitwa scouts fall under set designer na location people, jamaa wa hollywood waacheni tu waingize billions maana kazi wanazofanya mpaka movie inakuuja kuingia kwenye theatre si ndogo.
 
Haha sasa hao wanaotafuta nyumba si ndio wanaitwa scouts fall under set designer na location people, jamaa wa hollywood waacheni tu waingize billions maana kazi wanazofanya mpaka movie inakuuja kuingia kwenye theatre si ndogo.


Alafu wewee... umeanza kuita director/producer/promoter kua yeye ni scout under set designing??
 
WS katika post yako hii nimekubali about yoote uloongea na
kukupata vizuri zaidi sasa... Lakini the above kipengele pauses a problem kwangu...
Ukiizungumzia TZ kwa kufanananisha na nchi zingine katika issue ya Piracy ni wazi
lazima wao wataonekana nafuu tokana na ukweli kua Piracy goes hand in hand na
technology ambazo zina liquidate the whole complicated issue of piracing... hivyo in
that sense naweza kubali.. BUT hata hivyo ukweli unabaki kua Piracy ni serious case
in TZ for tunaona the way wasaniii kazi zao zinapokelewa positively na jamiii mpaka
kukuza majina but the Matunda wanayo pata hio ndo issue... Katika watu 10 ambao
nawafahamu woote waweza kua na kazi ya msanii fulani but alonunua the origina kazi
ni 1 or 2.. huoni kama ilo ni tatizo saana, kwa msanii mwenyewe na the entertainment
business??? Na bora hataa wa filamu a bit, but music... Hawa ndo huchakachuliwa to
the maximum!

You know what, kwa mfumo wa soko letu kazi yoyote iliyokuwa pirated anayeumizwa si msanii au mtayarishaji
bali distributor. Wasanii wetu huwa wanauza hakimiliki zao zote kwa distributor na inashangaza hata pale
wanapoamua kulalamika kuibiwa wakati walishalipwa na kuuza haki zao. Naamini kabisa kama mfumo wa soko
utaboreshwa na tasnia itakuwa rasmi, wanaweza kufaidi jasho la kazi zao no matter kuna piracy au hakuna.

Tutafanikiwa tu endapo tutafanya haya: Serikali kupitia Mpango wa Kurasimisha Biashara na Rasilimali za wanyonge
nchini (Mkurabita) itairasimisha tasnia hii ili kuwafanya wasanii wafanye kazi kwenye mazingira yaliyo rasmi kwa kuwa
hali ilivyo sasa inawafanya wakose fursa nyingi za kukuza kazi zao na kuongeza vipato.


Bahati mbaya katika nchi hii tumekuwa tukiishi katika nadharia zaidi, kwani matamko yoyote yanayotolewa
na viongozi huwa hayafanyiwi kazi, hata kama kinachoongelewa kina tija. Nakubaliana kabisa na malalamiko
ya wasanii kukosa fursa za kupata mikopo kwenye asasi za kifedha, mianya ya kufanya kazi mbalimbali za
serikali, na hata kama kazi zao za sanaa zinakua lakini hazithaminiwi ipasavyo kutokana na wao kutokuwa rasmi.


Sifa za kuwa rasmi ni kusajiliwa kwa kazi zao, kuwa na jina la biashara, zenye ubia, zikifanywa kikampuni,
zenye leseni ya biashara, zenye eneo/mahali maalum pa kufanyia kazi, zilizo kwenye kumbukumbu inayoeleweka,
zinazotofautisha mali ya biashara na binafsi.


Hakuna 'excuse' yoyote ambapo wasanii wanaweza kukuza pato lao, kuondokana na umaskini na hata
kushindana kimataifa kama hawataingizwa kwenye mfumo rasmi ambao utawafanya watambulike ndani
na nje ya nchi ili kujenga mazingira ya wao kuweza kukopesheka, kupata fursa za kikazi na kukuza kazi
wanazozifanya. Katika mataifa mengine wasanii wako rasmi na wameweza kuvuma na kupaa kiuchumi.


Serikali iangalie uwezekano wa kuanzisha mfuko maalum kwa ajili ya kuwawezesha watengenezaji wa filamu,
ili kuondoa mfumo uliopo kwa baadhi ya wafanyabiashara wachache kushikilia biashara hiyo, pengine tunatakiwa
tuwe na Tume ya Filamu (Tanzania Film Commission) itakayotoa misaada kwa watengenezaji wa filamu ikiwa
na jukumu la kuongeza ujuzi katika uandishi wa miswada (script) na utayarishaji wa filamu.


Lakini huwa napata shida kidogo kutokana na ukweli kwamba watengenezaji wa filamu waliopo kwenye soko letu
wamekosa mfumo mzuri wa kuwawezesha kupata msaada wa mitaji kwa kazi zao. Hata hivyo, kwa mtazamo
wangu,tunapaswa kuangalia kwa makini jinsi watengenezaji filamu wanavyoandaa miundo ya kihazina
(funding structure) katika kampuni zao kabla hatujaelekeza nguvu katika kusaidia sekta hii.


Nitarudi baadaye...
 
Hii post nimeikubali na maelezo yoote na iko pouwa, ila nina swali
kabla sijaenda mbali... Maana tunapoongelea nini cha kuzingatiwa ili soko la filamu lifike
vizuri umetoa muongozo moja kwa moja kua ni kutu gani cha weza tuongoza katika dhana
nzima ya mafanikio katika usambazaji... naona kama umeenda mbele saana bila kutaja kwanza
vitu vya kuzingatia katika soko la filamu.. In other words kua hicho kipengele cha kutuongoza
katika usambazaji pamoja na the sub-vipengele ni moja tu ya sababu na zipo nyingine
(in what to zingatia for the soko to be prosperous if not satisfying...)

Maudhui/Mahitaji ya Watazamaji:
Ashadii, napenda sana challanges zako ambazo zinanifanya kufikiria zaidi ya uwezo wangu ili kuzikabili,
elewa kuwa kwa miaka kadhaa, sekta ya filamu Tanzania imeshuhudia utofauti mkubwa kati ya maudhui
katika hadithi zetu na kile watazamaji wanachokihitaji, na matokeo yake yameendelea kuyumbisha
mikakati ya soko na sera za usambazaji. Maudhui lazima yahusishwe moja kwa moja na mahitaji ya
watazamaji ili kuwe na nafasi ya mafanikio kwenye soko.


Maudhui yanayofaa katika kizazi cha leo ni yale yanayokwenda sambamba na watazamaji ndani ya akili zao
na kuihusisha jamii directly. Mafanikio yanayotokana na maudhui yanategemea sana mmenyuko wa
watazamaji, na kujenga maudhui yaliyo kwenye mstari na mwelekeo wa watazamaji na matarajio yao
imekuwa vigumu, na sasa inahitajika kwa watayarishaji/ waandishi wa miongozo ya filamu kujihusisha
moja kwa moja na mtazamo wa watazamaji katika mazingira waliyomo. Kwa matokeo haya, utafiti ni suala
la kupewa umuhimu mkubwa kabla ya kuandaa kazi husika.


Katika utazamaji filamu hizi, kuna dhana ambayo huendana na mitazamo ya watazamaji (matamanio,
maadili, na mtazamo wa mtu binafsi kulingana na uzoefu wake katika kuangalia kazi mbalimbali) na vitu hivi
huathiri namna watazamaji wanavyohusiana na dunia inayowazunguka, ikiwa ni pamoja na maudhui.


Kabla hadithi haijawafikia watazamaji, tayari mtazamaji atakuwa na picha ya kipi anataka kukiamini na
kama hadithi imeandaliwa katika mtazamo mzuri, mtu wa aina hii huamini na hununua kazi bila kusita.
Kama hadithi itaifikia jamii ya watazamaji ambao mtazamo wao utalingana na kisa, wigo wake utapanuka,
watu watapeana taarifa kwa njia ya neno kwa neno (ambayo ni njia ya ufanisi zaidi kwa mkakati wa soko)
na hujenga nidhamu ya utazamaji wa filamu.


Hakuna hadithi inayofanikiwa kama watazamaji hawapati kitu wanachokiamini - na kwa wastani wa filamu 100
za Kitanzania, watazamaji wetu hawataweza na wala hawataona kila kitu wanachohitaji, watachukua na kuchagua
kati ya filamu nyingi wanazoziona ili kuridhisha matakwa yao.


Maudhui yanayokubalika sana ni yale yanayosimulia jambo linalofahamika zaidi kwa watazamaji. Hii inaweza
kupimwa kwa njia mbalimbali, wengi hasa, utafiti wa msingi unaweza kutusaidia kutambua aina ya hadithi
tunazohitaji kuwaambia walengwa, aina ya wahusika tunaowahitaji kutusaidia kwenye hadithi zetu, aina ya
watazamaji tunaowahitaji kuwaambia hadithi zetu, na majukwaa sahihi kwa ajili ya kusambaza hadithi zetu.

Kuwaelewa watazamaji ni hatua moja muhimu sana katika mchakato wa biashara ya filamu. Kubainisha
maudhui ili yaendane na matarajio yao ni muhimu sana. Kama huwezi kuambatanisha maudhui yako
yaende sambamba na mtazamo wa watazamaji, basi, hadithi itapuuzwa.


Kama mtayarishaji wa filamu, suala la kwanza unatakiwa kuwajengea msingi watazamaji katika maudhui
uliyoyakusudia, ukielewa kwamba unaweza kuwa bosi kwenye kampuni yako ya production;
LAKINI UNACHOKIFANYA SI KWA AJILI YAKO! NI KWA AJILI YA WATAZAMAJI NA HADITHI ZAO!


Kuandaa hadithi iendane na ladha ya watazamaji - hasa kwa kuelewa kuwa watazamaji hawataki kubadilishwa
mitazamo yao, they want it to be reinforced - itakusaidia kuanzisha mijadala kuhusu masuala muhimu kwa
watazamaji wako.


Vizuri tu kama, utaambatanisha ubora wa kiufundi wa filamu yako uendane na ubora wa watazamaji wako
waliouzoea. Hutoweza kufanya biashara - kwa mfano, kuwapa low quality film watazamaji ambao wamezoea
kuangalia sinema za kigeni, ambazo zimetengenezwa kwenye tasnia za filamu zilizoendelea zaidi kwa kiwango
cha juu cha ubora.


Jukwaa la Uwasilishaji:
Haitoshi tu kuwekeza nguvu nyingi kwenye kutafuta maudhui yanayofaa, jukwaa la uwasilishaji ni muhimu pia.
Siku hizi, watazamaji wanahitaji pia majukwaa ya habari kama wanavyojali kuangalia maudhui. Falsafa hii ni
muhimu pia wakati unaposhughulikia maudhui yanayowafaa watazamaji.


Ukipata bahati ya kuhudhuria Jukwaa la Sanaa pale Basata utagundua kuwa hii njia nzuri sana katika biashara
ya usambazaji wa kazi za sanaa.
Maudhui ya jukwaa la uwasilishaji katika dunia ya kisasa ya filamu hayaishii tu
kwenye kazi ya usambazaji, yanakwenda ndani zaidi ya kile hasa soko la filamu lilivyo leo. Jukwaa litakusaidia kuwasilisha
mawazo yako kwa watu katika njia itakayojumuisha mitazamo yao, na si kupambana nayo.

Ufanisi katika uwasilishaji unachangia utoaji haki ya kuchagua; kuyaleta maudhui kwa watazamaji katika dunia
yao wenyewe. Kulingana na uwezo mkubwa wa soko la Tanzania kama litawezeshwa (ndani na nje ya bara
la Afrika), jukwaa muafaka litamfanikisha kwa urahisi mtengenezaji wa filamu kuendana na ushindani wa soko.

Mustakabali wa biashara ya usambazaji wa filamu na masoko Tanzania unatokana na watazamaji vijana.
Watoaji filamu wanatakiwa kuandaa kwa uangalifu demography hii ya watazamaji na kukutana nao katika
dunia yao. Dunia hiyo hustawi kwenye kundi la kweli la teknolojia ya digitali.


Katika hatua hii itakuwa vizuri pia kuuchunguza mfumo wa usambazaji ili mfumo wa promotion and
distribution solutions usaidie kurekebisha tasnia kama ilivyokuwa katika nchi nyingine, na uigwe kwetu.
Film is a brand, kama zilivyo nembo/ bidhaa nyingine, kuzitangaza na kuzisambaza ni vitu vyenye
umuhimu sawa.


Pia kuna tatizo kubwa hapa kwetu kwamba Tanzania bado haina kiwango kikubwa cha watu wanaotumia
intaneti ukilinganisha na nchi zingine katika Afrika, ni asilimia ndogo sana ya wakazi wake wanatumia mtandao.
International Telecommunications Union (ITU) katika ripoti yake inaonyesha kuwa kati ya watu takriban
milioni 42 waliopo nchini, kuna watumiaji wa intaneti 676,000 (1.6%) ya wakazi. Watumiaji wa facebook
ni 141,580 (0.3%) ya wananchi wote.


Wakati Uganda (watu milioni 33) ina watumiaji wa intaneti 3,200,000 (9.6%), facebook 196,000 (0.6%).
Kenya yenye watu milioni 40 ina watumiaji wa intaneti 3,995,500 (10.0%), facebook 864,760 (2.2%).
SOURCE: www.internetworldstats.com/africa

Ili tuweze kupiga hatua kwenye suala hili tunahitaji nguvu kubwa kuielimisha jamii faida za kutumia mitandao
ya jamii inayoweza kusaidia utoaji habari za filamu na kujenga jamii yenye wafuasi, na humo, mijadala
inaweza kujadilika, kipengele muhimu kabisa cha kuleta ufahamu au kampeni ya kujitangaza. Jumuiya hizi
ni maeneo ambayo watu wanaotembelea wanaweza kupata habari zaidi, kushiriki katika mijadala, kujiunga na
majarida, na kubadilishana ujuzi na mawazo na watu wengine, kwa lengo la kupanua wigo mkubwa wa
watazamaji.


Katika miaka michache iliyopita, mitandao imesaidia sana kufanya uwepo wa gharama nafuu katika
promotion and marketing kwa filmmakers na hata kwa studio. Katika baadhi ya tasnia za filamu za nchi
zilizoendelea, ni kosa kubwa kutokuwa na tovuti ya kutangaza filamu kabla haijaoneshwa kwenye majumba
ya sinema.


Kwa takwimu za ITU, tunahitaji kuelekeza namna nzuri mitandao ya jamii inavyoweza kusaidia na kufanya
kampeni yenye kuleta mwamko wa namna ya kujitangaza kwa ajili ya watoaji filamu. Njia ya haraka na
madhubuti ya kujenga jamii ya watazamaji kupitia vyombo vya habari za mtandao ni kutengeneza
films dedicated website ili kutoa documentaries, film clips kwa ajili ya kuangalia bure, ku-downloads picha,
musics, soundtrack, wallpapers, nk.


Kuwapa mashabiki fursa ya kupata habari kuhusu maudhui/hadithi, wasifu wa waigizaji, na kuchangia
maoni yao na hata kuonesha interest zao katika filamu kwa jumla kutasaidia kuenea kwa taarifa au
tetesi za filamu.


Filmmaker anaweza kuwa na ukurasa wake wa uchapishaji kwa habari za filamu, ambapo taarifa mbalimbali
kuhusiana na filamu na maendeleo yake zitapatikana kwa wasomaji kwa kipindi cha muda fulani. Kutokana
na uwezo wake wa kuonesha filamu kwa watazamaji wengi kwa haraka, kuwafichua nyota wa filamu,
trailers, mahojiano na director wa movie nk, inaweza kuwekwa kwenye maonesho ya televisheni, au vipindi
vya habari za burudani.


Advance trailers na behind-the-scene footage pia vinaweza kuwekwa kwenye documentary kwa ajili ya
vituo vya televisheni.


Kuzionesha filamu kwenye film festivals pia ni jambo zuri sana ambalo linaweza kusaidia kuongeza wigo
wa taarifa. Film festivals husaidia kueneza taarifa miongoni mwa wakosoaji wa filamu na watazamaji,
na inaweza kuongeza umaarufu wa filamu na watazamaji kuwa wengi kama mapitio yake yalikuwa ya kuvutia.


Wakati Tanzania tukiendelea kukaa katika ulimwengu wetu wa 'uvivu wa fikra' sehemu nyingine ya dunia
inasonga mbele kwa kasi zaidi kuliko tunavyodhani.


Mchanganyiko wa vyombo vyote vya habari hutoa fursa ya kipekee kwa watengeneza filamu, tofauti na
mfumo uliozoeleka wa usambazaji. Kutokana na mipango madhubuti, mtengenezaji wa filamu anaweza
kusambaza filamu yake mwenyewe na kupata faida nzuri.


Katika jitihada za kibiashara, marketing is a battle-field, na biashara ya filamu haiwezi kukwepa hili.
Baadhi ya njia makini zinaweza kutafsiri upya mfumo na kuweka kiwango kipya. Kwa mfano, filamu inaweza
kutolewa kwenye vyombo vyote vya habari kwa wakati huohuo, ikiruhusu watazamaji tofauti kuchagua lipi
jukwaa linalowafaa.


Je, watazamaji wa Kitanzania wapo tayari? Kumbuka kuwa: Hivi sasa, mipango ipo njiani kwa nchi kuhama
kutoka matangazo ya Analog kwenda digital – kunakoongeza mahitaji makubwa ya vituo vya televisheni;
hii inatoa nafasi kubwa ya kuingia.


Jambo la muhimu zaidi, mfumo huu mpya unaweza kuwa majibu ya Mungu dhidi ya intellectual property
katika Sekta ya Filamu Tanzania.


Naomba kuwasilisha...
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
kumbe wataalamu wapo! Nikipata muda nitaweka script zangu hapa ili
niweze kukosolewa na kufundishwa zaidi.Ahsanteni

Nakusahuri kama unahitaji msaada jaribu kuwasiliana moja kwa moja na wachangiaji fulanifulani
ambao kwa mtazamo wangu wameonesha ukomavu mkubwa katika kuchangia mijadala hii,
kwa mfano: Ashadii, 3D, Mbongo, na pengine hata mimi ambaye nitaweza kukuunganisha na
mtaalam ninayemuamini sana ambaye pia ni mwalimu wangu, anaitwa Bishop J. Hiluka
 
Itabidi uwe makini... kabla hujapost hakikisha una copywrites,
hili jamvi members na non-members woote wana access...

Sure, lakini natumai wewe pia unaweza kumsaidia endapo atawasiliana na wewe moja kwa moja,
au siyo?
 
Anaweza kuiweka kwenye haki miliki na kisha akaiweka hapa ili kuona watu wanaweza kuchangia vipi... Hii inaweza kusaidia kupanua uwezo wa watu mbalimbali katika tasnia ya filam.
 
Anaweza kuiweka kwenye haki miliki na kisha akaiweka hapa ili kuona watu wanaweza kuchangia vipi...
Hii inaweza kusaidia kupanua uwezo wa watu mbalimbali katika tasnia ya filam.

Inawezekana lakini itabidi achanganue pumba na mchele maana yanawezatokea mengine yatakayopotosha.
Hili ni angalizo tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom