Tasnia ya filamu Tanzania ni sekta ya 'kuganga njaa'

M'bongo

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
265
298
Na Bishop J. Hiluka


FILAMU kama zitachukuliwa kwa umakini mkubwa zinaweza kuwa chanzo kikubwa na muhimu sana katika kujenga taifa na zinaweza kutumika kama jukwaa la kuchochea mijadala nchini kote, lakini bahati mbaya bado tasnia hii hapa nchini imekuwa inakabiliwa na changamoto kadhaa.


Tasnia hii imekuwa ni sekta ya kujikimu, licha ya ukuaji wa haraka unaoonekana. Ukweli ni kwamba bado mavuno halisi ya tasnia hii katika kukuza pato la Taifa na hata watayarishaji walio wengi bado hawajafanikiwa kupata matokeo mazuri kiuchumi kupitia filamu.

Pia bado tasnia hii ya filamu inabakia kuwa aina ndogo ya sekta ambayo imekuwa mfano wa "ili mradi mkono uende kinywani", huku watayarishaji na wasanii wakiwa wanaitumia ili kujaribu kuweka mambo yaende sawa mezani. Kamwe haijawahi kuwa sekta endelevu ambayo taifa linaweza kujivunia.

Ingawa kumekuwepo juhudi nyingi kutoka kwa wadau mbalimbali kutaka sekta hii ikue na iweze kuleta tija, lakini juhudi hizo bado hazijaweza kutoa mavuno stahiki katika kile tunachoweza kuita pato linalotokana na uchumi wa kweli wa tasnia ya filamu.



Hali halisi ya soko la filamu la Tanzania linaifanya hatma ya wasanii wengi kuishia kulipwa pesa kiduchu (peanuts) ambazo wala haziwasadii kujiendeleza bali kwa mlo wa siku chache. Pia watayarishaji wengi wamekuwa wanapendelea kuwatumia wasanii walewale (hasa wakongwe) katika kila sinema kwa kuogopa kwamba nyuso mpya 'haziuzi', kitu ambacho kwa kiasi kikubwa kimekuwa kikiathiri sana ukuaji wa vipaji.


Bahati nzuri kwa Tanzania, na nchi ya Rwanda, ingawa hazimo katika ngazi moja na mataifa ya Magharibi au Afrika ya Kusini, lakini zimekuwa na mafanikio kiasi katika Ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati.


Tafiti nilizowahi kufanya zimeonesha kuwa filamu zinaweza kuwa chombo muhimu sana cha kijamii na kiutamaduni kwa ajili ya kujenga umoja miongoni mwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.


Watazamaji wa Kitanzania kati ya wana-Afrika Mashariki wameonekana kuzipenda sana sinema zao pamoja na kuwepo kasoro nyingi na wamekuwa na hamasa kubwa. Kama zilivyo sinema za Nigeria ambazo alama yake kubwa ya kibiashara ni Kiingereza chao aina ya Pidgin, Kiswahili cha kisasa cha Tanzania kinazipa utambulisho wa kitaifa filamu zetu.

Ili kuiendeleza sekta ya filamu, serikali ya Tanzania na wadau, kwa dhati kabisa wanapaswa kulisaidia Shirikisho la Filamu Tanzania ili kuwawezesha watayarishaji na wasanii kupata mafunzo ya kitaalam kwa njia ya warsha na semina ili kuongeza uwezo wao.

Pia Bodi ya Ukaguzi wa Filamu na Michezo ya Kuigiza inapaswa kuwa macho zaidi na kuhakikisha kuwa filamu zote zinakaguliwa kabla hazijaingia sokoni kwa sababu ya unyeti wa maudhui yake ili kulinda maadili ya nchi hasa kwa taifa kama letu linaloendelea.

Taarifa zozote zinazopatikana hazipaswi kuchukuliwa kiutani au kama 'anasa' kama ilivyo katika nchi zilizoendelea, Bodi ya Ukaguzi kiwe ni chombo kwa ajili ya maendeleo, uzoefu wa kitamaduni na kwa ajili ya kuleta maana katika maisha yetu ya kila siku.



Makala zangu kadhaa zilizopita zilileta tafsiri tofauti kwa baadhi ya wasomaji kwamba nilionekana wazi kuipinga Bodi ya Ukaguzi kwa "kuirushia mawe", lakini ukweli ni kwamba sina ugomvi wowote na bodi wala mtendaji yeyote ndani ya bodi bali kama mwanaharakati wa masuala ya filamu, nina jukumu la kuhakikisha maadili ya Taifa yanalindwa.

Kamwe hatutakiwi kukaa tu na kusema filamu ni burudani tu, hapana; siamini kabisa katika kaulimbiu hii. Naamini kuwa tunapaswa kuona filamu, mbali ya kuwa ni burudani lakini kama chombo maalum kwa ajili ya maendeleo ya Taifa kwa sababu ndivyo imekuwa ikitumiwa na nchi nyingine zilizoendelea.



Ili kujihakikishia soko katika Afrika, Ulaya na hata Marekani, filamu zetu zinapaswa kukaguliwa kwa umakini zaidi na kusajiliwa na Chama cha Hakimiliki (Cosota). Pia lazima ziwe zilizotokana na script nzuri, zilizotengenezwa kiufundi, zenye ubora na utaalam wa kitaalam. Pia hazitakiwi kutengenezwa kwa mtindo uliozoeleka sasa wa sehemu mbili (Part 1 na 2) kitu kinachoshusha ubora wa filamu husika.


Jumamosi ya wiki iliyopita nilipata mwaliko wa kuwa mzungumzaji kwenye kipindi cha moja kwa moja cha asubuhi "Baragumu" kinachorushwa na kituo cha televisheni cha Channel Ten, ambapo mada kuu ilikuwa changamoto zilizopo katika tasnia ya filamu hapa nchini.


Kwa kweli katika kipindi hicho sikutegemea kabisa kama hoja nilizoanzisha zingeweza kuibua mjadala mpana sana kiasi cha waandaaji kuona haja ya kunialika tena kwenye kipindi kama hicho wiki chache zijazo ili kumalizia yale niliyoyaanzisha. Lakini niseme tu ukweli, Watanzania wanazipenda sinema zetu ingawa wanakatishwa tamaa na kasoro zilizopo kwenye filamu ambazo hazionekani kutafutiwa ufumbuzi.


Niliweza kuhisi uchungu na hasira walizokuwanazo wadau pindi wakipiga simu kuchangia kwenye mada hiyo, lakini nawaomba watambue kuwa changamoto ni nyingi zinazoikabili tasnia yetu, mbali ya kukosa ufahamu wa namna ya utengenezaji wa filamu kwa watayarishaji wetu, uelewa mdogo wa wasanii, ukosefu wa miundo ya soko la kuuza kazi, tatizo lingine kubwa ni ukosefu wa mitaji.

Mtaji limekuwa ni tatizo kubwa linaloumiza vichwa vya watayarishaji wa filamu kwa muda wote tangu Watanzania walipoanza kufanya filamu mpaka sasa.

Angalia sinema za Marekani, India au Afrika Kusini utaona jinsi zinavyoashiria uwekezaji mkubwa katika filamu zao, mavazi, mandhali ya kuvutia, ufundi, uongozaji na kadhalika, vyote hivi ni kutokana na uwekezaji. Wazalishaji wangapi wa Kitanzania wanaweza kumudu kutumia japo robo ya robo ya robo (1/64) ya kinachotumika Ulaya, India, au Marekani?

Tasnia ya filamu Tanzania ipo katika mparaganyiko mkubwa mno kutokana na ukosefu wa fedha katika sekta ya filamu, kitendo kinachochangia kikundi kidogo cha watu fulani kulihodhi soko la filamu huku serikali ikijua na bila kuchukua hatua.



Kwa takriban miaka 10 sasa kilio cha wasanii na watayarishaji wa filamu, mbali ya wizi wa kazi zao kimekuwa ni ukosefu wa mtaji wa kutengeneza filamu, ingawa mwezi Septemba 1998, ulianzishwa Mfuko wa Utamaduni na Serikali, ambao hata hivyo haukuwa na ufanisi kwa kuwa uligubikwa na matatizo lukuki.


Madhumuni makuu ya mfuko huo yalikuwa kuimarisha na kuiwezesha sekta ya Utamaduni (filamu zikiwemo) kuchangia kikamilifu katika mipango ya maendeleo ya uchumi wa Taifa kwa kuhamasisha jamii kujituma kufanya shughuli za utamaduni zenye kuchochea ubunifu, kuzingatia ubora wa bidhaa na huduma, kuongeza kipato katika kaya na kuhimiza ajira za kujitegemea.

Tangu mwaka 1998 ulipoanzishwa Mfuko, Mawaziri wote waliopita Wizara ya Utamaduni wameshindwa kuandaa mkakati mzuri wa kusaidia upatikanaji wa pesa au kusaidia Mfuko kwa ajili ya watengeneza filamu kwa maendeleo ya Taifa, kwa sababu hakuna yeyote kati yao aliyeifahamu vizuri nguvu ya sekta ya filamu.



Pia kulikuwepo madai ya ufisadi au kutotumia pesa zilizotolewa na wahisani kwa ajili ya kuwawezesha wasanii na wadau wa utamaduni katika kufanikisha malengo. Walionufaika aidha walikuwa wanajuana na wahusika au ni ndugu, marafiki au maswahiba wa kibiashara. Binafsi sina uhakika katika hilo.


Lakini wakati nafanya utafiti kuhusu tasnia ya filamu nilielezwa na mmoja wa wajumbe wa bodi ya Mfuko kuwa maombi yaliyotumwa kwao yalikuwa mengi kuliko pesa iliyotolewa, ila maombi kadhaa yaliambatana na 'memo' kutoka kwa wakubwa kutaka kiasi kikubwa cha pesa. Ili kuhakikisha kuwa watu wengi wanawezeshwa, watendaji walilazimika kutoa fedha kwa watu wenye maombi ya pesa ndogondogo ambazo hata hivyo hazikuweza kuleta tija katika kazi zao.


Mfuko wa Utamaduni uliopaswa kutoa 'grants' kwa wasanii na wazalishaji katika sekta na tasnia ya sanaa nchini, ulifanya wachache kujinufaisha kinyume na sheria ingawa ushahidi wa wazi katika hili sina lakini kimazingira ushahidi upo.

Inasemekana kuwa serikali ambayo ilikuwa na jukumu la kuchangia katika mfuko huo haijawahi kufanya hivyo mpaka wafadhili walipoamua kujiondoa kwani pesa walizokuwa wanachangia zilianza kufanya kazi tofauti na kile kilichokusudiwa.



Tasnia ya filamu hapa nchini itaendelea kuwa sekta ya kuganga njaa kama hali itaachwa kama ilivyo ingawa serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inajaribu kuangalia namna itakavyoweza kuingiza mapato kupitia tasnia za filamu na muziki.


Kwa kweli ubunifu katika sekta ya burudani na sanaa - filamu - katika nchi karibu zote za Afrika umekuwa unakwazwa na ukosefu wa fedha jambo ambalo limekuwa ni tatizo kubwa katika jitihada za kukuza na kuendeleza sekta.


Ili tasnia ikue pande zote, serikali na sekta binafsi zinapaswa kuwa na sera nzuri, kinyume na ilivyo sasa ambapo hawana sera nzuri za sekta na wala hawafikirii kuipa kipaumbele tasnia hii. Hata hivyo, sekta hii imekuwa chanzo cha pato la mabilioni ya dola kwenye mabara mengine.


Alamsiki.


Bishop Hiluka ni mtafiti wa masuala ya filamu, mwandishi miongozo ya sinema (script) na muongozaji wa sinema.
Anapatikana kwa namba 0755 666964
bjhiluka@yahoo.com
bishophiluka.blogspot.com

SOURCE: KULIKONI, MEI 13, 2011
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Nimeisoma hiyo habari hapo juu, kuna mambo ambayo mimi binafsi sikubaliani nayo hata kidogo.

Hivi sister Asha D, filamu kama why I did get married? 1 & 2, Meet the Browns, I Can Do Bad All By Myself. kuna vitu gani vya kushindwa Watanzania kuwa navyo?

Kuna filamu nyingine wala haziitaji mitaji wala bajeti kubwa kiasi icho, ni mtiririko tu wa hadith na umahiri wa waigizaji tu basi.
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Nimeisoma hiyo habari hapo juu, kuna mambo ambayo mimi binafsi sikubaliani nayo hata kidogo.

Hivi sister Asha D, filamu kama why I did get married? 1 & 2, Meet the Browns, I Can Do Bad All By Myself. kuna vitu gani vya kushindwa Watanzania kuwa navyo?

Kuna filamu nyingine wala haziitaji mitaji wala bajeti kubwa kiasi icho, ni mtiririko tu wa hadith na umahiri wa waigizaji tu basi.


Sasa zile ndo picha, walau wangeacha kuiga wa Nigeria (so it has been said)
wangeanza kuangalia hizo kwa umakini ili kuona kazi za wenzao... hamna hata
haja ya kuvaa nusu uchi ili dada atazamwe au aonekane mrembo....
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Sasa zile ndo picha, walau wangeacha kuiga wa Nigeria (so it has been said)
wangeanza kuangalia hizo kwa umakini ili kuona kazi za wenzao... hamna hata
haja ya kuvaa nusu uchi ili dada atazamwe au aonekane mrembo....
Ni kweli huyasemayo, tatizo ni haraka haraka walizo nazo, wao katika mwezi mmoja tu wanataka kuwa na filamu zaidi ya mbili...! Ndio kunaitwa kulipua kazi.
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Kwanza naomba nitoe angalizo:

  1. Naomba nivumiliwe kwa kuwa nitaandika maneno mengi kwani naguswa moja kwa moja na mada hii. Nitajitahidi kuandika mambo ya msingi tu. Nashauri wadau wasome. Vumilieni, Someni.
  2. Mimi si mtazamaji "nguli" wa filamu kwa sababu nilizotazama si nyingi sana. Hata hivyo kwa zile "nilizochagua" kuzitazama nimezitazama kwa undani sana, nukta kwa nukta, sekunde kwa sekunde.
  3. Nafikiria hapo baadaye kuwa aidha director au visual effects (For film) artist. Currently nafanya motion graphics (for TV broadcast). Moja ya kazi nilizofanya hivi karibuni ni hii (Sauti inayozungumza ni ya Maximilian Rioba (Producer wa Tamthilia ya 69 Records :Clouds TV) nimefanya visual part):
YouTube - ‪TEYA AWARDS COMMERCIAL.flv‬‏

UTENGENEZAJI FILAMU TANZANIA (Mazingira na Changamoto):

UBUNIFU (Story na Script):

1. Sinema bora huanza na story nzuri. Tatizo letu, waandishi wazuri hawako katika sekta ya filamu. Walio katika sekta ya filamu si waandishi wazuri na wala si wasomaji wazuri. Akina Kanumba (sorry kwa kutaja majina) wanang'ang'ania kuandika stori ilhali wao kipaji chao ni kuigiza au kuongoza (direct). Ukimpa Director wa Avatar James Cameron kitabu cha Shaaban Robert: Adili na Nduguze atakutengenezea filamu nzuri sana yenye effects matata. Tanzania tuna hazina ya waandishi kama Hammie Rajab (RIP), Elvis Musiba (RIP), Ben R. Mtobwa (RIP), John Mwakingili, John Msimbe Simon Simbamwene, Eddie Ganzel, Said M. M. Bawji, Amri M. M. Bawji, Hussein Tuwa, Faraj Hussein Hassan Katalambula, E. J. Shigongo (....anajitahidi bwana!!...anajitahidi bwana!!), Wilson Kaigarula (Hadi sasa), Shaaban Robert (RIP), Edwin Semzaba na wengine wengi sana, sana. Kuna vitabu kama Panga la Shaba vikifanywa sinema (vizuri) itakuwa bomba. Hivyo sisi wadau kama tunaona hatuwezi kuja na stori kali, tutumie za wenzetu kwa utaratibu unaokubalika then sisi tuigize au tuwe waongozaji au tufanye effects. NB. Ninafikiria kufanyia kazi hadithi ya Adili na Nduguze (nimenunua kitabu tayari), ila effects zake balaa, jasho linanitoka.

2. Mfano wa filamu ambazo waongozaji hawakuzitunga (and vice-versa)ni kama Pirates of the Caribbean (Tim Powers), Alice in Wonderland (Linda Woovlverton), Lord of the Rings (J.R.R. Tolkien), Tears on Valentine's Day (Tanzania, Writer: E. J. Shigongo, Director: Hammie Rajab) n. k. Hata hivyo sina tatizo na mtu kuigiza na kudirect kama anamudu. Mfano Mel Gibson hudirect na wakati mwingine kuigiza, hata Peter Jackson. Msimamo wangu: Kanumba na Ray ni Actors na Somehow Directors na si Writers.

TECHNICALITIES

Ukiangalia sinema zilizoongoza kwa mauzo duniani (List of highest-grossing films - Wikipedia, the free encyclopedia) asilimia zaidi ya tisini ni za Visual Effects. Kufanya visual effects za kompyuta si lelemama. Inatakiwa mtu ajue computer pamoja na programu zake vizuri sana from 3D Animation (ni muhimu/lazima kujua scripting pia), Compositing, Matte Painting, Sound. Hapa kuna tatizo. Sinema inayopigiwa chapuo (debe) ya Visual Effects ya Tanzania: Roho Sita imejitahidi. Pongezi zangu. Hata hivyo tatizo imecopy na kupaste tutorials za Andrew Kramer (VIDEO COPILOT | After Effects Tutorials, Plug-ins and Stock Footage for Post Production Professionals). Si vibaya kujifunza kwa kuiga lakini nashauri tutumie concept za wenzetu kujenga idea zetu wenyewe.

Watu walio katika filamu Tanzania (wenyewe wanajiita Editors) hawawezi kufanya effects serious. Imagine filamu kama Avatar iliandikwa tangu mwaka 1994 (Avatar (2009 film) - Wikipedia, the free encyclopedia) lakini ikabidi kuwekwa kapuni kwa kuwa dunia haikuwa na teknolojia ya kuisupport hadi teknolojia ilipopatikana (Thanks to Autodesk, Inc. (http://www.autodesk.com)kwa programu kama MotionBuilder without which Avatar ingekuwa mashakani).

Najifunza on my own visual effecting. Tough. Ila kuna kampuni ya Wahindi: Pilipili Entertainment nadhani hii itakuja kufanya vizuri hapo baadaye katika filamu zetu za Bongo.


MAZINGIRA (LOCATIONS)/Set/Make-ups/Physical Effects (Special Effects)

Kuandaa locations ni changamoto pia. Partly inahitajika location design artists ambao wanaweza kufanya constructions za set na decorations ambazo mtazamaji hawezi kujua ni fake aidha digitally (digital matte painting) au physical effects. Kanumba atawatoa wapi hawa watu? Tunahitaji make-up artists wanaoweza ku-mould masks kwa ajili ya effects (eg in Chronicles of Narnia, Lord of the Rings etc). Huku Tanzania wapo akina Mayasa Mrisho (Maya) ambao nao wana changamoto kujifunza yote haya. Je, wanajua wanamiss nini?


ACTRESSES/ACTORS

Si kila mtu anaweza kuigiza (wapo baadhi wanaoigiza wanaigiza). Mtu akitoka kwenye u-miss tayari anakuwa actress. Hili ni tatizo. Tunajisahau juu ya mionekano yetu pia. Nilisikitika kuona Steven Kanumba na Hissan Muya (Tino) wanact kuwa ni wanafunzi darasani wakati kichwani wameweka wave. Kwanini wasitafute wanafunzi au wanaofanana na wanafunzi waact? Kuna personalities ambazo hazifai kwa muktadha fulani, mfano siwezi kumweka Mahsen Awadh (Dk Cheni) awe Mkuu wa majeshi hata kama filamu ni "ya kwake."


Sipendi vituko vya walizi wa magetini. Sipendi waigizaji wawe wanajirudiarudia katika movies. Tatizo watunzi ndiyo waigizaji hivyo wanajichagua wenyewe. Niko tayari kwenda kumshawishi bosi fulani TRA kama nadhani anafaa na anafundishika ili aact nafasi ya bosi.

BUDGET

Si kila filamu nzuri duniani basi imetumia pesa nyingi sana. Gharama hutegemea na content ya film. Filamu ya Steven Kanumba, Vincent Kigosi, Irene Uwoya na Jacob Steven (JB) iligharimu TShs Hamsini Milioni (Kanumba na Ray waliigharimia) lakini sijaona kilichofanyika kiasi cha gharama kufikia kiwango hicho. Ni kweli hizo si pesa nyingi kwa film (linganisha na List of most expensive films - Wikipedia, the free encyclopedia ) ila film is too weak to cost that much.

Sinema nzuri hata hivyo hugharimu sana kuandaa. Inabidi kulipa waandishi wa script, actors (plus wakati wa mazoezi), editors/visual fx artists, directors, producers, drivers, locations etc. Sasa hebu niambie mauzo yenyewe haya ya Bongo kwanini Kanumba asiact, kudirect na kuproduce? (Ray na Kaumba hulipwa kati ya 25-30 Milioni per film kwa mujibu wa mikataba yao na Steps Entertainment (kwa taarifa nilizonazo)). Pesa hii haiwezi kuwafanya wakaact Makambako then Mpanda kisha Mwanza halafu Amboni Caves katika filamu moja. Sinema kama Chronicles of Narnia: The Lion, The Witch and the Waldrobe nadhani "imeektiwa" New Zealand na Czech (nadhani). Currently the most expensive film ni Pirates of the Caribbean: At World's End (USD 300M).

SERIKALI:

Hivi nikitaka kuandaa sinema ambayo itamwonesha Rais anatekwa na Mkuu wa majeshi ameasi hapa si kuna kuzuiwa kwa sababu za kiintelijensia? Generally, kuna vitu vingi ambavyo serikali inaweza kuzuia. King Crazy GK alitoa wimbo ft Lady JayDe: Komaa nao, ambapo walivaa magwanda ya JWTZ, waziri wa Ulinzi (wakati huo) Prof. Philemon Sarungi aliwajia juu (Hata hivyo alishauri wawe wanaomba ruhusa).

MWISHO:

Zipo aina ya filamu ambazo tuna uwezo nazo, sema tunazembea na kuridhika mapema. Nafikiria kutoa filamu mwezi Juni 2013 kama mambo yataenda navyodhani. Nitajitahidi kusahihisha makosa yanayofanyika sasa. Haitakuwa na "Part 1 na 2." Kama itakuwa ndefu itakuwa sequel kama Lord of the Rings, Chronicles of Narnia, Star Wars, Pirates of the Caribbean etc. Nitaileta humu jamvini ichambuliwe.

Nitatoa mchango wangu pia wa knowledge kwa filamu za Tanzania. Nimepata kuongea na wasambazaji na kuwaeleza "hasira" yangu dhidi ya "Part 1 na 2." Walisema wanafanyia kazi.

Niliyoyaandika hapa ni scratch tu lakini changamoto zilizopo ni kubwa zaidi. Inshallah, tutayafanyia kazi malalamiko ya watazamaji.

Asante M'bongo na wachangiaji wengine kwa thread hii.
 
Kwanza naomba nitoe angalizo:


  1. Naomba nivumiliwe kwa kuwa nitaandika maneno mengi kwani naguswa moja kwa moja na mada hii. Nitajitahidi kuandika mambo ya msingi tu. Nashauri wadau wasome. Vumilieni, Someni.
  2. Mimi si mtazamaji "nguli" wa filamu kwa sababu nilizotazama si nyingi sana. Hata hivyo kwa zile "nilizochagua" kuzitazama nimezitazama kwa undani sana, nukta kwa nukta, sekunde kwa sekunde.
  3. Nafikiria hapo baadaye kuwa aidha director au visual effects (For film) artist. Currently nafanya motion graphics (for TV broadcast). Moja ya kazi nilizofanya hivi karibuni ni hii (Sauti inayozungumza ni ya Maximilian Rioba (Producer wa Tamthilia ya 69 Records :Clouds TV) nimefanya visual part):


Nilijua utachambua saana na kuelezea mpaka niridhike na ndo maana nilisubiri kwa hamu... nimepata post yako nimesoma na kuipenda... Naomba nawe utanivumilia maana ni ndefu mno and very rich in details hivyo pia naomba uwe patient... sitaki nikurupuke....
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
UTENGENEZAJI FILAMU TANZANIA (Mazingira na Changamoto):

UBUNIFU (Story na Script):

1. Sinema bora huanza na story nzuri. Tatizo letu, waandishi wazuri hawako katika sekta ya filamu. Walio katika sekta ya filamu si waandishi wazuri na wala si wasomaji wazuri. Akina Kanumba (sorry kwa kutaja majina) wanang’ang'ania kuandika stori ilhali wao kipaji chao ni kuigiza au kuongoza (direct). Ukimpa Director wa Avatar James Cameron kitabu cha Shaaban Robert: Adili na Nduguze atakutengenezea filamu nzuri sana yenye effects matata. Tanzania tuna hazina ya waandishi kama Hammie Rajab (RIP), Elvis Musiba (RIP), Ben R. Mtobwa (RIP), John Mwakingili, John Msimbe Simon Simbamwene, Eddie Ganzel, Said M. M. Bawji, Amri M. M. Bawji, Hussein Tuwa, Faraj Hussein Hassan Katalambula, E. J. Shigongo (....anajitahidi bwana!!...anajitahidi bwana!!), Wilson Kaigarula (Hadi sasa), Shaaban Robert (RIP), Edwin Semzaba na wengine wengi sana, sana. Kuna vitabu kama Panga la Shaba vikifanywa sinema (vizuri) itakuwa bomba. Hivyo sisi wadau kama tunaona hatuwezi kuja na stori kali, tutumie za wenzetu kwa utaratibu unaokubalika then sisi tuigize au tuwe waongozaji au tufanye effects. NB. Ninafikiria kufanyia kazi hadithi ya Adili na Nduguze (nimenunua kitabu tayari), ila effects zake balaa, jasho linanitoka.

2. Mfano wa filamu ambazo waongozaji hawakuzitunga (and vice-versa)ni kama Pirates of the Caribbean (Tim Powers), Alice in Wonderland (Linda Woovlverton), Lord of the Rings (J.R.R. Tolkien), Tears on Valentine’s Day (Tanzania, Writer: E. J. Shigongo, Director: Hammie Rajab) n. k. Hata hivyo sina tatizo na mtu kuigiza na kudirect kama anamudu. Mfano Mel Gibson hudirect na wakati mwingine kuigiza, hata Peter Jackson. Msimamo wangu: Kanumba na Ray ni Actors na Somehow Directors na si Writers.


3D nimependa saana this part na the way umedadafua... impressive.. Kwa hapa kwetu Bongo Katika eneo la ubunifu naona sio tatizo saana maana mara nyingi wana story nzuri but stori line mbovu tokana na ukweli kama ulivyosema kua waandishi wazuri hamna… Baada ya ushauri wa X – PASTER nimenunua hio movie ya yellow banana (only to find inatakiwa ninunue mbili) na kuangalia… ukweli ni kwamba hadithi ni nzuri ndio but I had to have a remote close for nimeforward half the movie…

Na pia kuna tofauti ya mtu ambae ni mwandishi wa hadithi na mtu wa hadithi ya script ambayo filamu inabidi ichezwe… Mfano mzuri mwandishi J. K. Rowling wa vitabu vya Harry Poter vilivyotoa squels katika movies from one to seven… Movie nne za kwanza mtunzi ni script writer Steve Klowevs.. hizo nyingine sijafuatilia ni nani… hii inaonesha umakini wa hali ya juu ya jinsi wenzetu wanavyo jail na kuthamini Entertainment industry hasa movies. Kwa hapa Bongo mtu ninae fahamu ni mtunzi mzuri wa hadithi na tamthiliya na ni mzuri katika script ni Dr. Edwin Semzamba maarufu kwa kitabu cha Ngoswe penzi kitovu cha uzembe akipatikana University of Dar es Salaam.

Tukija upande wa wenzetu hasa Hollywood, unakuta kua wako makini saana na yupi atahusika katika script writing ya aina ipi na mtindo gani… Kuna vitabu ambavyo viliandikwa na waandishi na pia hao waandishi wakaandika script za hizo movie… Mfano Mario Puzo na movies za The God father, The Last Don, Super man Myth to mention but a few. Wewe kama ni msomaji mzuri wa vitabu na pia kama muangaliaji mzuri wa movie una appreciate kazi zoote in a different way but both unique and superb.

Advice to the film industry…
Waangalie upya suala la script writing na pia wazingatie vigezo pia wasiwe wachoyo wa kugawa majukumu; sio wewe ndo writer, Actor and Director hii itafanya maendeleo katika hio sector yameanza vizuri but wasipo angalia yatadumaa..

3D to be cont..... very soon




 
Mkuu, uchambuzi wako si mbaya, lakini kwa kuwafananisha waigizaji, waandikaji wa script na watunzi wa filamu za kibongo na wale wa hollyhood, kwa kweli ni sawa na kufananisha maji ya kijito, au bwawa lililotokana na mvua za vuli na bahari ya Hindi. Hujawatendea haki, maana hata mifano yako ni kwenye zile filamu zilizo kula budget kubwa kubwa, zaidi ya bajeti ya serikali ya KiAfrika.

Ni kweli Tanzania kuna simulizi na hadithi zuri zuri zinazofaa kuigiziwa filamu, ila mimi masikitiko yangu ni kwamba karibu watunzi wote ulio wataja wamesha fariki dunia, na ikitokea watengenezaji wa filamu uchwala kuzitumia kazi zao watakuwa hawajazitendea haki hizo liwaya.

Kazi za mtu kama Marehemu Shabani Robert, Marehemu Mohammed Said Adullah Bwana (Msa), Marehemu Amie Rajab, Marehemu Elvis Musiba, Marehemu Ben R. Mtobwa na magwiji wengine wa utunzi, zinatakiwa kuchukuliwa na watu makini sana kwenye utengenezaji wa filam na si hawa tulio nao sasa.

Mimi siku zote inapokuja suwala la kujadili waigizaji, huwa nasema kuwa Tanzania tuna vipaji vizuri sana vya waigizaji, tatizo linakuja tu pale waigizaji ambao wanavipaji hawataki kwenda kujifunza au kujinoa kwenye chuo cha uigizaji (Chuo cha Sanaa Bagamoyo), kwa kuwa tu wanaona kazi zao zinanunulika na wanapata pesa kidogo, I mean kidogo ya kubadilisha mboga, na wanafuatwa fuatwa na mabinti, basi wao wanaridhika kwa ilo.

Kuhusu vifaa vya kufanyia kazi, wapo watu wana camera nzuri tu za kuchukulia filamu, program za kuhariri video zipo na ni nzuri tu, maana si lazima tuwe na simulizi zenye speacial effect nyingi na ngumu. Vitu vingine wala haviitaji complicated or sophisticated programme, kuna filamu nimezitolea mfano hapo juu.

Kwa ufupi naweza kusema kuwa Tanzania tuna kila sababu ya kutengeneza filam nzuri na zenye kueleweka, pale tu wahusika watakapo amua kuwa makini na kazi zao, ebu fikiria swala dogo tu la subtitle, jinsi lugha wanavyo ikoroga mpaka inakera, mi naita wote huo ni uzembe na kutaka kuwaisha kazi. Vipi filamu yenye part 1 & 2 ukazitoa with in a one month...! Yaani nashangaa hata uliposema kuwa wanalipwa kati ya milioni 25 mpaka 30 kwa mchezo mmoja... I don' think so.

Wakubali kwenda kujifunza, Uhandishi wa script, jinsi ya kufanya makeup, jinsi ya kuchaguwa wahusika wa mchezo (casting), wajifunze jinsi ya kuendeleza mchezo (continuity), na uhariri wa filamu na hata simple special effect za visual and sound.

Kuna mmfano mmoja umetoa hapo juu, kuhusiana na matumizi ya mavazi ya kijeshi na jinsi yalivyo shughulikiwa. alichofanya Pro. Sarungi ni sawa kabisa, kwa nchi hizi zetu, raiya wa kawaida wakiruhusiwa kutumia mavazi ya kijeshi na kipolisi, kutasababisha matatizo mengine, yakiwemo ujambazi n.k. Lakini kama wanataka kutumia, wanatakiwa wapate ruhusa maalum kutoka kwa wahusika, na kama kwenye michezo yao kuna vipande ambavyo vinawahusisha polisi basi wawahusishe polisi wa kweli kwa malipo maalum, sidhani kama Kamanda mkuu wa Polisi akiletewa hiyo proposal ataikataa. Au kama wanataka kuigiza hospitalini watumie kweli hospitali kama Muhimbili au Amana Hospitali kwa malipo, na wanaweza kuwatumia mdaktari wa kweli aidha kwa kuwauliza maswala ya kitabibu na yanayo husiana na hayo.

Kuna filam nilikuwa naiangalia ya kibongo inaitwa Yellow Banana, Vicent Kigosi ameigiza kama kijana anayetafuta ajira kwenye ulimwengu wa IT, na ni mwenye shahada ya uzamili. Lakini cha ajabu Muhusika anamuuliza mwenyeji wake mwenye tatizo la kuingiza data kuwa anatumia database gani... Quote "... samahani dada kwani unatumia program gani katika database... ni SQL silver ama visual basic? Anajibiwa ...Visual Basic. (English Traslation: excuse me sister, what program do you use in Database... is it SQL saver (na si silver tena) or visual basic? (sahihi ni SQL server) anajibiwa ...it's visual basic.

Ajabu sasa, hapa kuna vitu viwili tofauti, matumizi ya SQL server ni tofauti na Visual basic na kwenye monitor kulikuwa na ms word kama sikosei.

Sasa vitu kama hivi vidogo vidogo wanashindwa hata kuwauliza wenye fani zao. unategemea nini?

Anyway kuna mengi sana ya kujadili, ila kwa taarifa yako wenyewe walioko kwenye hii tasnia hawapendi kukoselewa, mimi nilisha wahi kumwandikia Kigosi na nikampa review yangu katika moja ya michezo yake, lakini hakutaka kuchapisha kwenye blog yake, nadhani alinipotezea kama wanasema watoto wa mjini.

NB
3D said:
Ninafikiria kufanyia kazi hadithi ya Adili na Nduguze (nimenunua kitabu tayari), ila effects zake balaa, jasho linanitoka.
Mkuu umenunua kitabu na hatimiliki au...!?
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
TECHNICALITIES

Ukiangalia sinema zilizoongoza kwa mauzo duniani (List of highest-grossing films - Wikipedia, the free encyclopedia) asilimia zaidi ya tisini ni za Visual Effects. Kufanya visual effects za kompyuta si lelemama. Inatakiwa mtu ajue computer pamoja na programu zake vizuri sana from 3D Animation (ni muhimu/lazima kujua scripting pia), Compositing, Matte Painting, Sound. Hapa kuna tatizo. Sinema inayopigiwa chapuo (debe) ya Visual Effects ya Tanzania: Roho Sita imejitahidi. Pongezi zangu. Hata hivyo tatizo imecopy na kupaste tutorials za Andrew Kramer (VIDEO COPILOT | After Effects Tutorials, Plug-ins and Stock Footage for Post Production Professionals). Si vibaya kujifunza kwa kuiga lakini nashauri tutumie concept za wenzetu kujenga idea zetu wenyewe.

Watu walio katika filamu Tanzania (wenyewe wanajiita Editors) hawawezi kufanya effects serious. Imagine filamu kama Avatar iliandikwa tangu mwaka 1994 (Avatar (2009 film) - Wikipedia, the free encyclopedia) lakini ikabidi kuwekwa kapuni kwa kuwa dunia haikuwa na teknolojia ya kuisupport hadi teknolojia ilipopatikana (Thanks to Autodesk, Inc. (http://www.autodesk.com)kwa programu kama MotionBuilder without which Avatar ingekuwa mashakani).

Najifunza on my own visual effecting. Tough. Ila kuna kampuni ya Wahindi: Pilipili Entertainment nadhani hii itakuja kufanya vizuri hapo baadaye katika filamu zetu za Bongo.


Nikikuta such a paragraph, a paragraph or statement with Avatar movie in it i can not talk of any thing else... ater all tayari umeongelea mambo ya visual effects ipasavyo... na the way mimi ninavyoelewa visual effects, i know kua if a person wants to master visual effects inatakiwa usome saaana, u browse saaana, u watch movies saaana, u practice saana na pia usomee course za hapa na pale... mengine umeelezea to the extent anybody interested is satisfied... wadau wenye maswali watauliza wapi they don't get.

When we talk about the Avatar movie we talk in the lines of not only the movie but the science, the technology combined with brilliance giving an end result of a movie so incredible, unique, wonderful, impossible, overwhelming, beyond imaginable world and you really have to give it to the guy who made it... when i heard matangazo about it i knew it was going to be a hit especially when i also held the new technology of 3D was being lauched... And then i heard James Cameroon was the director nikajua basi! He is going to make another world record afunike na records za movie zake za nyuma kama za Teminator(s) na Titanic.... And of course he didn't disappoint me (as usual) mpaka leo am jealous kwa wale woote waliokua able kuangalia kwa kutumia hio technology ya 3D... najua woote tumeangalia the same movie but completely different exposure and effect...

Director kama Cameroon; what do we learn from him??

Ni mengi mno! Jamaa huyu hafanyi kazi kwa papara hata siku moja, kama ulivyogusia hio picha ya Avatar imechukua more than tend years kutoka... very impressive (inanifanya nikumbuke my old avatar); Ukiangalia The Terminator yeye ndio moja wa waanzilishi wakubwa wa ku introduce the use of machines in the movie which turned out to make a mark in the movie industry... ukija kwenye Titanic ilimchukua miaka sita mpaka kuweza kuitoa kutokana na research kwa documentaries mbali mbali alizokua anachukua kuhusiana na hio ajali ya kweli ya Titanic... I can go on forever but JAMANI kwa wale woote ambao wako katika movie industry ni muhimu kufuatulia mambo kama haya iwe wewe ni actor/actress, director, producer or what ever as long as you are related to the show biz... I can go on forever ....

Nakupongeza saana kua uko interested na vitu ambavyo ni muhimu saana kwako kama fani yako ni visual effects, I believe utakua mmoja wa Watanzania watanyanyua hii sector ya visual effects for i can see the passion.

Kwa leo 3D inatosha will be cont......

 
  • Thanks
Reactions: 3D.

Kwa post ulotuma/uloweka, am telling you siwezi gusa hii kitu, but napenda tuitafutie siku, in what ever way we can huwezi zungumzia 2012 in one post bila mjadala... Visual effects to a whole new level, nafikiri hollywood saizi wame concetrate kidogo na the use of those visual effects, uki refer to movies such as The Transformers, Inception, Limitless ....

 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Wakuu, hizi special effects mnazo zieleza hapa na kufananisha na filam industry ya kibongo, ni sawa na kufananisha bwawa la mvua na bahari, ni kuwakatisha tamaa wenzetu...! Sisi mpaka kufikia uko itachukuwa miaka mingi sana.

Tunaweza kufanya baadhi ya special effects lakini si zile za kwenye 2012 au Avatar, si leo wala kesho.

Bado tuna mifano mingi sana ya kuelezea kuhusiana na walioko kwenye hii tasnia ya filamu, tatizo lingine ambalo mimi naliona ni kubwa ni ili la kukataa kukoselewa, japo kukoselewa kwa nia nzuri. Je mnakumbuka hii thread https://www.jamiiforums.com/enterta...cartoon-ya-kiswahili-kwa-jina-la-manzese.html, ambayo mimi ndio niliyeiweka hapa, lakini angalia jinsi ya muhusika/mtengenezaji wa hiyo filamu alivyokuwa anajitetea na kusifia kazi yake kuwa ni very excellent, sikatai kuwa amejitahidi sana tena sana, ila pale ambapo ameelekezwa kuwa ni kosa alitakiwa kukubali na ndio kujifunza, kwani hata hao madirectors na watunzi wakubwa wa hollyhood nao ukosolewa na wanakubali, na hizo ndio challenge za kazi.... Lakini wenzetu hawa... tuna kazi kubwa yenye kuitaji uvumilivu wa hali ya juu sana.
Asha D said:
...Baada ya ushauri wa X – PASTER nimenunua hio movie ya yellow banana (only to find inatakiwa ninunue mbili) na kuangalia… ukweli ni kwamba hadithi ni nzuri ndio but I had to have a remote close for nimeforward half the movie…

Sasa hapo kwenye ku-forward ndio umeharibu, sasa utahakiki vipi namna hiyo...!? Anyway just iangalie na kusikiliza, kisha utupe maoni yako, sisi ambao tupo mbali na Bongo mpaka tuletewe zawadi ndio tunapata nafasi za kuangalia kazi za Wabongo wenzetu.
 
@Asha D;

Ni kweli kuwa mtu anayehitaji kufanya Visual Effects ni lazima asome sana. Ukweli ni kuwa Visual Fx ni combination ya science na art/artistry. Nikijisema mimi, honestly nasoma sana, tena sana, nabrowse sana, tena sana, nafuatilia habari nyingi politics, science, art, history etc. Fahamu jambo moja, nasoma sana. Kuna moment naogopa ntakuwa chizi. Nasoma sana kwa sababu kwa mazingira yetu tunalazimika kufahamu mambo mengi kwa kuwa hatuna wataalamu wa kutosha.

AVATAR na JAMES CAMERON
Niseme nini? Cameron is said to be partly artist partly inventor. Katika Avatar ali-device miniature camera ambazo zilikuwa zinarekodi facial expressions (emotions) ili animators waweze kurudia the same/similar emotions kwenye models zao. Teknolojia ya Motion Capture imesaidia kufanya seamless/smooth animations za characters katika filamu ya AVATAR. Filamu hii imefanyiwa effects na Studio mbalimbali duniani zikiongozwa na Weta Digital ya New Zealand. Niseme tu kuwa storage capacity wakati wa development ya Avatar ilikuwa takribani 1 petabyte (1 million gigabytes), imagine! James Cameron ni mtuu mwingine kabisa. Hata hivyo Steven Spielberg alitikisa dunia na filamu ya Jurassic Park kwa upande wa effects za filamu.

Teknolojia ya 3D stereoscopy ni kitu kingine wenzetu wanachotuacha. Visual experience yake ni beyond imagination kwa wale ambao hawajawahi kuiona. Mtaani watu wanweza kukimbia kama filamu ni ya kutisha. Mlimani City wamekuwa wakionesha 3D stereoscopy ya filamu ya Thor. Hata Fast Five na Pirates of the Caribbean: On Stranger Tides zimekuwa zikioneshwa this week (Japo hizi hazikuwa 3D stereoscopic).

FILAMU BONGO
Kuna kizazi fulani kipo kwenye filamu za bongo huwezi kukiambia kitu. Utawaambiaje wakasome wakati "filamu zao zinauza" na magazeti yanawaandika kila siku? Challenge itakuja pale zitakapoanza kutoka filamu zenye viwango ndipo watapogundua wanachopungukiwa. Well, let's see.

POROJO:
Wakati niko O'level mwalimu mmoja wa Kiswahili alikuja na mgeni darasani. Akatuuliza tunasoma kitabu gani cha Kiswahili katika literature, tukataja "Ngoswe, Penzi kitovu cha uzembe." Akatuambia, "Mwandishi wake ndiye huyu mbele yenu"! Alikuwa ni Edwin Semzaba!!! Nafahamu aliwahi kuandika hadithi gazetini "Tausi wa Alfajiri" sikumbuki gazeti maana nadhani ni zaidi ya miaka 10 iliyopita.

@X-PASTER
Nimelazimika kucheka mara kadhaa pale ulipokuwa unafananisha Tanzania na Wenzetu na Bahari na mto. Nakubaliana nawe. Actually, si kwamba wametuacha ila ni kuwa hatuko pamoja nao katika ulimwengu wa filamu. Lakini kompyuta inaweza kuboresha sinema zetu mara tano ya sasa. Ila kikubwa zaidi ni userious, kama unavyosema. Kwa mfano sinema ya Sarafina haijafanya Visual Effects ambazo ni exceptional yet gap lake ni kubwa compared na zetu.

HAKIMILIKI
Ni kweli kuwa niliowataja wengi wameffariki. Hata hivyo kuna publishers ambao ndiyo husimamia hakimiliki ya kazi zao. Shaaban Robert alifariki zamani lakini vitabu vyake kama kusadikika nadhani vinatumika mashuleni hadi leo (kama sijakosea) hii inamaanisha vinachapishwa. Nilinunua Adili na Nduguze toka kwa publishers ambao ndiyo wana copyright. Hatujakubaliana kuwa tutengeneze sinema ila nilimweleza afisa mmojawapo juu ya dhamira yangu, alionekana kushangaa as if ni jambo la kutoka ahera. Aliniambia nikiwa tayari niende ofisini kwao kwa mazungumzo. NIlikinunua ili nirudie kusoma stori yake na kuangalia challenges zitakazokuwepo. Stori ni nzuri. Visual Effects zikifanyika vizuri huenda ikawa exceptional film. Ina composition nzuri kwa maana ya stori pamoja na chance ya kufanyika visual effects. Shaaban Robert nadhani alikuwa-inspired na hadithi za Kiarabu ama Kiajemi.

Tunachokosea sisi ni kutengeneza sinema na kujaza effects bila sababu ya msingi as long as tunaweza kufanya. Ngoja tuone tutafika wapi. Kuhusu post uliyoweka ya Filamu ya Manzese, Dr Mhella naona mwanzoni alipata pressure kwa kuhisi watu wana nia ya kumkatisha tamaa, kumbe sivyo. Kuna vijana wazanzibari (Kwa uongozi wa Mazd, member wa JF) wameandaa filamu "The Crazy." ambayo wanasema wameweka visual effects, For trailer cheki link The Crazy_TRAILER_2011 (1).mpg - 4shared.com - online file sharing and storage - download. Bado wanarudia makosa yanayoweza kuepukwa kama Kiingereza na uhalisia hata wa mazungumzo tu. Kazi bado ipo. Nitawatumia waandaaji review yangu nikiishaiona filamu yote.
 
Tunahitaji fikra pevu kama hizi kutuletea thread zenye kutuelimisha.
Thanks M'bongo na wanaJF mliochangia kwenye thread hii.
Mimi bado mgeni nahitaji kujifunza mengi kutoka kwenu
 
Wakuu, hizi special effects mnazo zieleza hapa na kufananisha na filam industry ya kibongo, ni sawa na kufananisha bwawa la mvua na bahari, ni kuwakatisha tamaa wenzetu...! Sisi mpaka kufikia uko itachukuwa miaka mingi sana.

Tunaweza kufanya baadhi ya special effects lakini si zile za kwenye 2012 au Avatar, si leo wala kesho.

.


hahahahahaha.. umenifurahisha X-PASTER.... Kweli we are way over our head...
but hata hivyo there are things twaweza jifunza.. in other words wahusika
wajitume katika kazi zao... for instance simfahamu 3D but i gurantee
ni mtu anajituma na kufuatilia kwa ukaribu...

Sasa hapo kwenye ku-forward ndio umeharibu, sasa utahakiki vipi namna hiyo...!? Anyway just iangalie na kusikiliza, kisha utupe maoni yako, sisi ambao tupo mbali na Bongo mpaka tuletewe zawadi ndio tunapata nafasi za kuangalia kazi za Wabongo wenzetu.

X-PASTER nilikua na forward sehemu wanayojishebedua kama kutoa gari, na swagger nyingine za muhimu nilikua na concetrate, uahlisia wa kupotray mdada ilikua problem kidogo..niliipenda na walijitahidi the suspense kidogo walu unaweza kisia itavyo isha... thank you again for recommending.. labda tell me another..
 
  • Thanks
Reactions: 3D.

Similar Discussions

Back
Top Bottom