TASAF Mwanza ni kichaka cha wajanja kupigia pesa

Nyanswe Nsame

Senior Member
Jul 9, 2019
158
175
TASAF Mwanza ni kichaka cha wajanja kupigia pesa

Mkoa wa Mwanza ni miongoni mwa mikoa nchini yenye watu wanaoishi katika mazingira magumu na maisha duni.

Mkoa huu ni kati ya mikoa nchini ambayo imeingizwa katika mpango wa kusaidia kaya zinazoishi maisha duni.

Agosti 2012 Serikali ilizindua mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF) kwa lengo la kusaidia kaya masikini nchini.

Inaelezwa mfuko wa maendeleo ya Jamii (TASAF) katika mkoa wa Mwanza, fedha za mfuko huo zimebadilishiwa matumizi na kutumika kwa kulipa posho za vikao.

Fedha za mfuko huo kwa miaka yote, zimekuwa zikitumika katika matumizi ambayo sio sahihi na kuacha wananchi wenye uhitaji wakitaabika.

Pamoja na mpango huo wa serikali wa kusaidia kaya masikini lakini mkoa huu no miongoni mwa mikoa ambayo fedha hizo hazina msaada kwa watu wenye uhitaji was msaada nothuo.

Ukiachana na hilo, mkoa huu wakazi wake kwa kipindi kirefu wamekuwa wakidai kutonufaika na fedha za TASAF ambazo wanadai zinawanufaisha matajiri wachache wanaochukua fedha zao.

Uchunguzi unaonyesha kuwa, watu wanaonufaika na fedha za TASAF ni maafisa wake pamoja na ndugu na marafiki wa maafisa hao.

Maafisa hao wanatajwa wamekuwa wakiandikisha majina ya watu ambao sio wanufaika na kupiga pesa hizo.

Pamoja na hilo, katika mkoa wa Mwanza, fedha za TASAF zimekuwa zikitumika kulipa watu posho za vikao ambavyo havihusiani na TASAF.

Katika halmashauri nyingi za mkoa huu na mikoa mingine, fedha za TASAF zimekuwa zikitumika katika shughuli mbalimbali za halmashauri badala ya kuwasaidia walengwa.

Kaya zinazoishi katika mazingira duni hazina taarifa kama kuna fedha zinazotoka kwa ajili yao zaidi kushangaa na kuuliza namna fedha hizo zinapopatika.

Mfuko wa maendeleo ya Jamii ulizinduliwa agosti mwaka 2012 na Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete, mpaka sasa mpango uliokusudiwa haujaleta manufaa.

TASAF kwa mwaka imekuwa ikipokea kiasi cha Trioni 2 (mbili) kwa ajili ya kusaidia kaya masikini ziweze kujikwamua kiuchumi. Lengo kuu ni kuiwezesha nchi kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2030.

Lengo la fedha za mfuko wa TASAF mpaka sasa halijaonyesha matumaini ya kutimia na badala yake fedha hizo, zinatumika kujilipa posho na maafisa wa TASAF kujinufaisha.

..........................................................................
 
Sio Zama hizi mkuu

Taarifa zao za fedha zinafanyiwa uhakiki na auditors wa kutosha na ni mara kwa mara

Nachelea kusema hii habari haipo sawa!!
 
Unajihangaisha na tuvichaka wakati chaka kubwa la kupotezea kodi za Watanzania lipo kwenye ujenzi wa Chato capital.

Mnawaonea wanaodokoa vijisenti lakini mnaogopa kupaaza sauti juu ya mabilioni yanayopotelea Chato!!
 
Tupe chanzo cha habari...au we ni mhanga wa fedha hizo? Tusiwe tunashiba tu mihogo kwa mama ntilie tunapata nguvu za kuandika chochote.
 
Back
Top Bottom