TASAF: Hali ya Umaskini Tanzania yapungua, Makonda atakiwa kurejesha fedha za TASAF kama alizitumia

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
Imeelezwa kuwa takwimu za hali ya umaskini wa kipato hapa nchini kwa mwaka 2017, zimepungua kwa kiasi kikubwa na kufikia asilimia 26.

1581935963595.png

Hayo yamebainishwa leo Februari 17, 2020 na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt Albina Chuwa na kusema kuwa jukumu la kuondoa umaskini kwa mtu mmoja mmoja ni jukumu la watu wote.

"Hali ya umaskini wa kipato hapa nchini Mwaka 1991-92 ulikuwa Asilimia 39, 2007 umaskini ulikuwa asilimia 34, 2012 Asilimia 28.4 na 2018 hali ya umaskini likuwa 26.4, kasi ya kupungua umaskini hapa nchini inaenda kwa mwendo wa kasi" amesema Dkt Albina Chuwa Mkurugenzi wa Takwimu.

Aidha akitoa takwimu za umaskini kwa nchi zingine za Afrika Dkt Chuwa amesema,"Rwanda utafiti wao wa mwisho ulikuwa Mwaka 2015, na hali ya umaskini ilikuwa Asilimia 38.2, Kenya 2015 ni asilimia 36.3, Afrika Kusini Asilimia 55.5, Zambia Asilimia 54.4,na kwa mwaka huo huo Zimbabwe ilikuwa ni Asilimia 72.3, hii ndiyo hali ya umaskini ya mahitaji ya msingi kwa Nchi za Afrika".

1581936210431.png

Hayo yamejiri katika uzinduzi wa Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya TASAF, mpango ambao utazinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.

RAIS MAGUFULI AMTAKA MAKONDA KUREJESHA FEDHA ZA TASAF KAMA ALIZITUMIA

1581936238930.png
Rais Magufuli amesema katika Uhakiki wa Kaya maskini uliofanyika kuanzia Novemba 2015 hadi Juni 2017 zilithibitika Kaya hewa 73,561 na Kaya 22,034 zilithibitika sio maskini.

Amesema anafikiri fedha hizo ni zilizotolewa kwa Kaya ambazo sio maskini zilitumiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda kwenda Dodoma huku akiwa sio maskini.

Amesisitiza kuwa kama ni kweli Makonda alitumia fedha za TASAF akaenda nazo huko alikokuwa anaeleza na yeye hahusiki kwenye Kaya maskini basi ni lazima azirudishe fedha hizo.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati akizindua Kipindi cha Pili cha Awamu ya tatu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).

Awali, RC Makonda alisema na yeye ni mnufaikaji wa mfuko huo kwani alipewa fedha na Rais Mstaafu Mkapa ambaye ni mwanzilishi wa mfuko huo kwenda Dodoma kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa UVCCM.

View attachment 1360570
Rais Magufuli amesema katika Uhakiki wa Kaya maskini uliofanyika kuanzia Novemba 2015 hadi Juni 2017 zilithibitika Kaya hewa 73,561 na Kaya 22,034 zilithibitika sio maskini

Amesema anafikiri fedha hizo ni zilizotolewa kwa Kaya ambazo sio maskini zilitumiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda kwenda Dodoma huku akiwa sio maskini

Amesisitiza kuwa kama ni kweli Makonda alitumia fedha za TASAF akaenda nazo huko alikokuwa anaeleza na yeye hahusiki kwenye Kaya maskini basi ni lazima azirudishe fedha hizo

Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati akizindua Kipindi cha Pili cha Awamu ya tatu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)

Awali, RC Makonda alisema na yeye ni mnufaikaji wa mfuko huo kwani alipewa fedha na Rais Mstaafu Mkapa ambaye ni mwanzilishi wa mfuko huo kwenda Dodoma kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa UVCCM.

Kama amechukua huyo ni kama wahujumu uchumi wengine ashughulikiwe
 
Imeelezwa kuwa takwimu za hali ya umaskini wa kipato hapa nchini kwa mwaka 2017, zimepungua kwa kiasi kikubwa na kufikia asilimia 26.

Hayo yamebainishwa leo Februari 17, 2020 na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt Albina Chuwa na kusema kuwa jukumu la kuondoa umaskini kwa mtu mmoja mmoja ni jukumu la watu wote.

"Hali ya umaskini wa kipato hapa nchini Mwaka 1991-92 ulikuwa Asilimia 39, 2007 umaskini ulikuwa asilimia 34, 2012 Asilimia 28.4 na 2018 hali ya umaskini likuwa 26.4, kasi ya kupungua umaskini hapa nchini inaenda kwa mwendo wa kasi" amesema Dkt Albina Chuwa Mkurugenzi wa Takwimu.

Aidha akitoa takwimu za umaskini kwa nchi zingine za Afrika Dkt Chuwa amesema,"Rwanda utafiti wao wa mwisho ulikuwa Mwaka 2015, na hali ya umaskini ilikuwa Asilimia 38.2, Kenya 2015 ni asilimia 36.3, Afrika Kusini Asilimia 55.5, Zambia Asilimia 54.4,na kwa mwaka huo huo Zimbabwe ilikuwa ni Asilimia 72.3, hii ndiyo hali ya umaskini ya mahitaji ya msingi kwa Nchi za Afrika".

Hayo yamejiri katika uzinduzi wa Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya TASAF, mpango ambao utazinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.

RAIS MAGUFULI AMTAKA MAKONDA KUREJESHA FEDHA ZA TASAF KAMA ALIZITUMIA

View attachment 1360570
Rais Magufuli amesema katika Uhakiki wa Kaya maskini uliofanyika kuanzia Novemba 2015 hadi Juni 2017 zilithibitika Kaya hewa 73,561 na Kaya 22,034 zilithibitika sio maskini.

Amesema anafikiri fedha hizo ni zilizotolewa kwa Kaya ambazo sio maskini zilitumiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda kwenda Dodoma huku akiwa sio maskini.

Amesisitiza kuwa kama ni kweli Makonda alitumia fedha za TASAF akaenda nazo huko alikokuwa anaeleza na yeye hahusiki kwenye Kaya maskini basi ni lazima azirudishe fedha hizo.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati akizindua Kipindi cha Pili cha Awamu ya tatu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).

Awali, RC Makonda alisema na yeye ni mnufaikaji wa mfuko huo kwani alipewa fedha na Rais Mstaafu Mkapa ambaye ni mwanzilishi wa mfuko huo kwenda Dodoma kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa UVCCM.

Wote wamoja hao wasitutoe kwenye agenda
 
Back
Top Bottom