Tarzan: Fahamu machache kuhusu filamu hii ya mwaka 1985

Justine Marack

JF-Expert Member
Jul 31, 2014
563
1,546
Jina halisi la filamu ni “Adventure of Tarzan”. Washiriki wakuu katika filamu hii ni Hemant Birje (Tarzan) na Kimi Katkar (Rubi). Mtunzi na muongoaji wa filamu hii anaitwa Babbar Subash akishirikiana na rafiki yake. Subhash alikua ni muongoza filamu mashuhuri katika nyakati hizo huku akiwa anapewa sifa baada ya kuongoza vema filamu ya Disco dancer ya mwaka 1982.

Umaarufu wa waigizaji wa filamu hii ulikua juu sana miaka ya 80 lakini hata hivyo walipotea katika anga la uigizaji ambapo mpaka sasa taarifa zao kisanaa zimekua hazijulikani. Mwana dada Kimi au Rubi mara ya mwisho kujihusisha na sanaa ilikua mwaka 1991 baada ya hapo amekua kimya mpaka sasa.

Filamu hii ilikuja kama dharula tu kwani mtunzi wa filamu hii awali hakuwa na wazo la kuandika filamu ya namna hii bali alikua tayari ameandaa filamu ya Dance Dance ambayo alitaka Mithun Chakraborthy aicheze( filamu hii ni tofauti na disco dancer, hii ilitoka baadae mwaka1987), lakini wakati huo ilikua ngumu kumpata Mithun kwani huo ni wakati ambao alikua juu kisanaa na ndio star mkubwa namba mbili akimfuatia Amitabh Batchan, hii ilikua baada ya mafanikio ya filamu ya Disco dancer na Kasam paida karnewale ki.

Ratiba ya Mithun ilikua ngumu sana kucheza filamu hiyo na kumtaka Subhash kusubiri kwa muda wa miezi sita mpaka saba ili akamilishe kazi zilizo tangulia. Ni wakati huo akimsubiri Mithun apate Muda ndipo akaona isiwe taabu inabidi nitafuta project ya kupotezea muda ndipo Subhash akaandika filamu ya Adventure of Tarzan. Baada ya filamu ya Tarzan kutoka mnamo 1985 aligeuka kuwa gumzo kila kona.

Hamesh Anand ambaye aliteuliwa awali kucheza nafasi ya Tarzan lakini Subhash hakufurahishwa kwani alitaka kuleta sura mpya katika filamu hiyo ambayo hakutaka kutumia mtu maarufu kwani Hamesh tayari alikua ameshiriki filamu kadhaa pamoja na uchezaji wa dansi na alikua maarufu. Ndipo Subhash alimuibua Hemant bhirje(tarzan) toka katika club za mchezo wa mieleka huko Mtaani.

Wazo la kuandika filamu hii awali lilipingwa na Rajendra Kumar rafiki na mshirika wa karibu wa Subhash kwakua aliiona kuwa itakuwa filamu ya daraja C , lakini Subhash alimuhakikishia rafiki yake kuwa ataifanya kutoka daraja C mpaka daraja A na ndicho kilicho tokea baada ya kutoka na kutimua vumbi kila kona.

Jambo lililo waacha watu midomo wazi ni ushiriki wa waigizaji wakuu ambao wote walikua ndio filamu zao za kwanza kucheza na wakafanya vizuri sana. Mwana dada Kimi(Rubi) aliletwa na rafiki yake amabye naye ni muigizaji na muongoza filamu Danny Dinzongpa na kumtambulisha wa Subhash ili apate nafasi ya kucheza filamu. Wakati wa kushuti Filamu ya tarzan Mama yake Rubi alikua anampa kampani kila siku wakiwa location ili kuhakikisha mwanaye anafanya vema katika filamu hiyo.

Wimbo "Tarzan oh Tarzan" uliimbwa na muimbaji mchanga kwa wakati hio na kumpa umaarufu mkubwa baada ya filamu hiyo kutoka. Muimbaji huyo kwa sasa ni maarufu sana anaitwa Alisha Chinai. Kama umewahi kusikia wimbo “Made in índia” au ingia you tube utajua hapa naongelea muimbaji wa wimbo gani. Nyimbo zingime maarufu alizo imba baade ni pamoja na "Zooby zooby" katika filamu ya Dance Dance 1987 na "Commando Commando" katika filamu ya Mithun Commando mwaka 1988. Tunaweza kusema filamu ya Tarzan iliwaibua wengi na kuwapa nafasi ya kujulikana. Huyo ndiye Alisha Chinai mwana dada mwenye sauti tamu aliye imba Tarzan oh Tarzan, pia aliimba nyimbo nyingine kadhaa katika filamu hii kama "Mere paas aonge mere paas saath"

Katika filamu hii Adui mkuu anitwa Gorilla ambaye alicheza kama mtawala wa kimila anaye muwinda binti Rubi ili awe malikia wa watupori. Baada ya kuonekana na kufanya vema katika movie hii Gorilla naye aliendelea kupata dili nyingi za kucheza filamu zenye maudhui ya kimila.

Nyimbo zingine katika filamu hii ni pamoja na "Jee le le jee lele",Tamahsa banke aaye hain" na "Do Re Me"
 
Kuna sehemu hii movie ukiiangalia katika ile scene alipokamatwa tarzan utamsika yule jamaa anayemchunga tarzan asitoroke akisema "gania watoto gania gania watoto"
 
Back
Top Bottom