TARURA wanavyotuibia kupitia ada za Maegesho DSM

Vyamavingi

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
5,737
5,438
Utaratibu wa kulipia maegesho kwa njia ya kielectoniki ni mzuri sana. Hata hivyo kuna mapungufu ambayo lazima yafanyiwe kazi. Mapungufu hayo ni:
1. Hawatoi tiketi za madai kwa parking nje ya CBD. Nimewauliza wanao-scan kwa nini hawatupi tiketi, tutapataje namba za kulipia? Wanasema hawapewi tiketi, tunatakiwa tucheki kupitia simu. Kwenye simu huwa ni shida sana kuangalia deni la maegesho ya TARURA, mara nyingi mtandao husumbua.

2. Hawatumi madai kwa wakati, wanasubiri siku kadhaa zipite ndipo wakutumie. Mimi nimejisajili ili niweze kupokea msgs za ankara, hata hivyo hawazitumi kila unapoegesha, ankara hukusanywa (cummulation) na kutumwa baada ya siku kadhaa, haziainishi mteja alipaki wapi na lini. Maana yake ni kuwa mara nyingine mfanyakazi anaweza ku-scan hata kama umesimama barabarani kwa dharura!

Maana yake ni kuwa kuna uwezekano mkubwa sana kubabimbikiziwa madai ya maegesho maana mteja hajui madai kwa wakati kwa kuwa huwa hawatoi tiketi za madai.

Naomba Wizara husika ifanyie kazi suala hilo ili liwe fair kwetu. Tunayo haki ya kupata tiketi ya madai kwa wakati tunapoegesha badala ya kusubiria wiki nzima na kutubambikia madeni yasiyojulikana.

Tarehe 5 Machi
Ndugu mteja, chombo namba T732AGW, Deni la Maegesho ni Tsh. 2,500.00. Lipa kwa kutumia Kumbukumbu Namba 994572594027 ili kuepuka faini.(Piga 0733149658/59/60 Huduma kwa wateja).

Tarehe 19 March
Ndugu mteja, chombo namba T732AGW, Deni la Maegesho ni Tsh. 500.00. Lipa kwa kutumia Kumbukumbu Namba 994572718962 ili kuepuka faini.(Piga 0733149658/59/60 Huduma kwa wateja).

Tarehe 26 March
Ndugu mteja, chombo namba T732AW, Deni la Maegesho ni Tsh. 3,000.00. Lipa kwa kutumia Kumbukumbu Namba 994572718962 ili kuepuka faini.(Piga 0733149658/59/60 Huduma kwa wateja).

Tarehe 2 April
Ndugu mteja, chombo namba T732AW
, Deni la Maegesho ni Shilingi 5,000.00. Lipa kwa kutumia Kumbukumbu Namba 994572810852 ili kuepuka faini.(Piga0733149658/59/60 Huduma kwa wateja).

Vv
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom