TARURA, ni wakati sasa mkajikita kurekebisha kwa kiwango cha lami barabara za mitaani Dar es salaam

Mkuu upo sahihi TARURA wana wajibu wa kufanya yote hayo ila maendeleo ya kweli yanaanzia ulipo.

Naamini kama viongozi wa ngazi za chini kila mmoja akisimamia vema eneo lake na kuripoti maeneo ambayo TARURA wanatakuwa kuyafanyia kazi basi kero zitapungua na hatimaye kuisha kabisa.

Tuanze na wenyeviti wa mitaa na madiwani. Hawa wana wajibu wa kusimamia mitaa na kata zao na kuhakikisha kero zote za barabara zinazosimamiwa na TARURA zinafanyiwa kazi.
 
Mkuu kuuliza sio ujinga. Hivi force account inafanyaje kazi na ikoje hasa uhalali wake kisheria nk
Force account kwenye taratibu za ujenzi inaitwa In-house design maana yake wanafanyakazi wao wenyewe Kama Wana mitambo wananunua disel, na kutengeneza barabara bila kuweka mkandarasi.​
 
Force account kwenye taratibu za ujenzi inaitwa In-house design maana yake wanafanyakazi wao wenyewe Kama Wana mitambo wananunua disel, na kutengeneza barabara bila kuweka mkandarasi.​
Kwamba pia hakuna maelewano ya pricing si ndio
 
Kwamba pia hakuna maelewano ya pricing si ndio
Ipo ila Ni upande wa operational cost Kama wanavyofanya Zanzibar barabara nyingi inajenga serikali ya mapinduzi ya Zanzibar wakandarasi kule Ni wachache.​
 
Mkuu kuuliza sio ujinga. Hivi force account inafanyaje kazi na ikoje hasa uhalali wake kisheria nk
Nadiriki kusema Force Account inatumika na watu serikalini kiushabiki tu.
Na hata huko serikalini hawajui maana yake.
Sasa hivi wasiojua maana yske ,hasa waziri wa Maji aliyepite, mh Marawa, wameiweka Force Account kuwa mbadala wa mkandarasi.

Madudu yanayojitokeza yatsua watu.

Force Account eti mradi una fedha, basi unaajiri fundi-twende kazini.

Hili halijakemewa ngazi za juu.
Hivyo kama ndiyo norm ya kiujenzi serikalini, TARURA wanunue magreda na wajenge barabara.
 
Back
Top Bottom