N'yadikwa
JF-Expert Member
- Aug 10, 2014
- 6,825
- 9,532
Nawakumbusha tu TARURA wakati serikali mpya ikiingia madarakani ni muhimu sasa barabara za mitaani katika jiji la kibiashara la Dar es salaam zikajengwa kwa kiwango cha lami. kusema kweli ni aibu kwamba barabara nyingi za mitaani hata katika maeneo yaliyopangiliwa kama vile Mbezi Beach, Mbweni,Bunju Beach,Makongo, Tegeta Masaiti Nakadhalika zina mashimo ya kiwango cha mahandaki. Ili wananchi wa Dar es salaam wajenge imani kwa serikali hii iliyoingia madarakani. Aidha barabara zote hata kwa maeneo yasiyopangiliwa zijengwe kwa kiwango hicho cha lami.
Ujenzi wa barabara hizi utasaidia pia kudhibiti mafuriko ya mara kwa mara Dar es Salaam kwa kuwa utaambatana na mifereji inayotoa maji mengi yanayokusanyika kutoka kwenye bati na kuelekea kwenye mkondo wake.
Sambamba na hilo TAMISEMI tafakarini kwa kushirikiana na Wizara ya Miundombinu njia ya kuondoa kero ya mafuriko Dar es salaam hasa pale Jangwani ambapo barabara hufungwa kwa mvua ya mm kidogo tu.