TARURA na mfumo wa maegesho kuna tatizo kubwa

Scaramanga

JF-Expert Member
Aug 19, 2020
401
538
Nakumbuka mwanzo mwezi wa oktoba 2021 mfumo huu ulipokuja ulikuwa na changamoto nyingi mpaka ikabidi usimamishwe kwanza ili kuangalia namna mpya ya mfumo unavyofanua kazi ili kuepusha usumbufu kwa watumiaji wa maegesho.Lakini cha kushangaza mfumo huu umerudi na mbaya zaidi tatizo badala kuwa limetatuliwa ndiyo kwanza limezidi. Sasa hivi ni foleni ofisi zao watu wanalalamika na ukifatilia ni hii habari ya kukutana na deni ambalo kila mtu anashangaa limetokea wapi na adhabu juu

1: Wengi wamekutwa mfano mtu yupo na Dar na hajawahi safiri na gari lake ila Tarura inasoma maegesho mkoa mwingine

2: Mfumo wao wa kuangalia deni yaani *152*00# ukitumia hakuna majibu yoyote unapata na hata namba zao za simu walizoweka 0733149658/0733149659/0733149660 hazipokelewi kabisa

3: Pili kwanini wasiwe na namba za huduma zile special ambazo naona tra wanatumia 0800 ambazo ukipiga kwa wewe uliyepiga hukatwi pesa yako ya salio ,wao wameweka bado namba ambazo unakutana tena na changamoto ya kukatwa pesa kwa kuuliza deni au kutaka kupata huduma au kujua kitu toka ofii yao.

4: Je haya malengo wanayopewa hawa ndugu zetu wanaosimamia maegesho ( vijana wa pakini) hawawezi kuwa nao wanavizia tu gari hata barabarani na kuliweka kwenye mfumo,maana unakuta hujawahi hata kuta tiketi lakini unakutana na adhabu ya kutolipa.

5: Tarura kabla ya kuja na mfumo au adhabu mliwahi toa elimu kwenye mitandao,TV,redio au hata magazeti? Watu wanapambana kutafuta pesa ya kujikimu na nyinyi mnakuja na mfumo wenu ambao kiukweli ni maumivu kweli parking ya 500 unampiga myu adhabu ya 10,000? Polosi wao adhabu yao 30,000 ukichelewa unakuta 8000 na huwa inalimit isizidi 60,000 kama ntakuwa sijakosea sasa wenzangu nyinyi utakuta mtu 100,000 na kuendelea. Au ndiyo mmeona kitega uchumi sasa? Polisi mfumo wao pamoja na changamoto yao lakini wapo angalau vizuri kwasababu wanarekodi na liseni hivo huwezi kataa deni, sasa Tarura wenu umekuwa wa kuviziana ujanja ujanja .

Sasa tusaidieni maana tunahangaika kupata pesa ya kujikimu na siyo kuineemesha Tarura, huu mfumo bado ni changamoto kwa watumiaji wa maegesho na ni kero sababu kama hizo chache ambazo nimeweza kuzitaja ni baadhi tu.
 
Lakini lipeni madeni jamani. Jero tu siku 14 hulipi? Hilo gari uuze tu
 
Lakini lipeni madeni jamani. Jero tu siku 14 hulipi? Hilo gari uuze tu
HDM tatizo siyo deni ,tatizo hujawahi paki eneo la malipo unakuta unadaiwa ndicho kinachokera zaidi na pia kama umepaki wakupe basi risiti ujue unadaiwa ukalipe.

Na hata kama mtu hajalipa 10,000 kwa kosa la kutolipa 500 ni nyingi sana ,sikatai fine ila waboreshe rates za fine,watoe elimu,ukipaki ukute risiti siyo kubambikiana
 
Jamani mwenye namba ya malalamiko TARURA kwani ninashida na malipo walioniwekea.Mkmi nimepaki gari sehemu moja napata Bill 10 kwa kipingi cha siku moja .Nikilipa naona inajiongeza nyingine na nyingine wakati gari nimepaki nyumbani.Au system inashida
 
Back
Top Bottom