Tarime: Zaidi ya ekari 263 za mashamba ya bangi na magunia 262 ya bangi kavu zakamatwa

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
bangi 01.jpg

Zaidi ya ekari 263 za mashamba ya Bangi yakiwemo magunia 262 ya Bangi kavu yamekamatwa na kuteketezwa katika oparesheni kali inayoendeshwa na vyombo vya ulinzi na usalama wilayani Tarime mkoani Mara.

Kamanda wa polisi wa kanda maalum wa Tarime na Rorya kamishina msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi Henry Mwaibambe,amesema katika oparesheni hiyo ambayo imehusisha vyombo vyote vya ulinzi na usalama,wakiwemo watumishi wa halmashauri ya Tarime, pia kilo 75 za mbegu za bangi zimekatwa zikiwa zimeandaliwa kwa ajili ya kupandwa,huku watumiwa 20 wakikatwa kuhusiana na kilimo hicho.

Akizungumzia oparesheni hiyo,mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Tarime Bw. Glorious Luoga,amesema serikali imechukua uamuzi wa kukabidhi mlima Nkongore kwa jeshi la Magereza baada ya mlima huo kutumika kwa kilimo cha bangi.
Hata hivyo jeshi la polisi kanda maalum ya Tarime na Rorya,limetangaza kuwakamata watu wanne baada ya kutumiwa kuwaua watu wawili wakati wakigombea mashamba ya bangi

Chanzo: Mwananchi
 
Back
Top Bottom