Tarime: Wasimulia kuwashwa, kuharisha, kutapika, kuhara damu, mifugo kufa kisa maji ya Mto Mara

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,456
Baada ya tetesi na hatimaye matamko rasmi kutolewa mara kadhaa kuhusu madhila yanayotokana na maji ya Mto Mara, ripoti zaidi zimeendelea kutolewa kupitia vyombo mbalimbali vya habari kuhusu kinachoendelea katika mto huo.

Awali ilidaiwa kuwa kuna kimikali zenye sumu katika Mto Mara ambazo nyingi baadhi ya vyanzo vilidai kuwa zinatoka kwenye migodi mbalimbali Mkoani Mara.

Mamlaka za Serikali zikajitokeza kufanya uchunguzi na kutoa ripoti mbili ambazo sababu zake pia zilikuwa zikitofautiana juu ya uchafuzi unaoendelea ndani ya mto huo.

Ripoti ya kwanza ilidai kufa kwa samaki mtoni humo ni kwa kuwa kuna wingi wa mafuta hasa oil na grisi kisha wakasema wanaendelea na uchunguzi kujua kwa nini maji yamekuwa meusi. Ripoti ya pili ikadai kuwa uwepo wa kinyesi na mkojo mwingi wa ng’ombe kutiririsha mtoni ndiyo sababu na kuwa hakuna kemikali zenye sumu.

UCHUNGUZI ZAIDI
Baada ya ripoti hizo uchunguzi wa waandishi umeendelea kufanyika na unaonyesha kuwa Kata ya Manga Wilayani Tarime na vijiji vyake kama vile Bisarwi na Kembwi, kuna kitu kisicho cha kawaida katika afya za wakazi wa maeneo hayo.

Kuna msamiati wa utani wanaotaniana wenyeji kuwa 'kwangua vocha' ukisikia hivyo ujue mtu ana kazi ya kujikuna pamoja na kukohoa.

Pia, inaendana na suala la kuhara na kutapika, tumbo kuvimba na madhila mengine, kibaya zaidi ni kuwa huduma za afya kama zahanati au kituo cha afya vipo umbali wa kilomita nne kutoka walipo.

Uchunguzi uliothibitishwa na wenyeji wanavijiji, umebaini kuwapo madhara kwa mifugo ambayo ni moja ya nyenzo zao kuu kiuchumi, kwamba wanadhurika hata kufa.

SHIDA NINI?
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Burongo kilichoko Kijji cha Bisarwi, Juma Matinde amezungumza na Gazeti la Nipashe akidai madhara hayo ya kiafya kwa binadamu na wanyama, pia mimea jirani, yamekuwa hali endelevu tangu kutokea anachokiita mkasa wa kuchafuliwa Mto Mara miaka minne iliyopita.

Kwa mujibu wa Matinde, hali hiyo imekuwa ikijitokeza tangu mwaka 2018 kila unapofika msimu wa mto kufurika, maji yake yamekuwa yakiwasha, wanapoyanywa tumbo linanguruma, kuharisha, wanatapika na kukohoa ikiendana na mikasa kadhaa ya kutapika na kuhara damu.

Mifugo nayo ikitumia maji ya mto huo imekuwa ikivimba tumbo, kulegea na hata kufa. Mwenyekiti Matinde anasema pindi mifugo iliyodhurika ikichinjwa, waligundua nyama yake kuwa nyeusi na inayotoa harufu mbaya.

WALIVYOIPOKEA
Mwenyekiti Matinde anaeleza: "Hii ni wiki ya pili sasa kuna hali hii, tumesitisha kwa muda kula samaki, ng'ombe walipokufa siku za mwanzoni mwa mwezi huu, tuliwachinja na kuuziana nyama. Kila aliyekula alihara, yaani ukishakula, tumbo linanguruma kisha unaanza kuhara kidogokidogo na kutapika.

"Zahanati iko mbali na hapa. Ukishagundua shida hii, unakwenda kwenye duka la dawa hapa kijijini, unawaeleza unavyojisikia, wanakupatia dawa."

MKASA WA WAVUVI
Mwenyekiti Matinde anasimulia kwamba wavuvi walipokuwa kazini mapema mwezi huu, waliwakuta samaki wakielea mtoni, wengi aina ya gogogo na sato.

Anasema baadhi yao waliothubutu kuwachukua ama kwa ajili ya kuuza ama kuwala, watumiaji wengi katika vijiji jirani waliharisha na kutapika.

Anasema muda mfupi baadaye, wavuvi hao waliufikishia taarifa uongozi wa maeneo yao kuwapo maji yenye mwonekano tofauti, meusi kwa rangi yakiashiria hatari kiafya na mazingira.

Hapo Mwenyekiti Matinde anasema viongozi walichukua hatua za tahadhari ikiwamo kuelimisha wananchi kwamba maji hayo na maudhui yake si salama kiafya, vinavyopatikana humo visiliwe.

Mbali na kudokeza hata mbwa waliokula nyama za mifugo iliyokufa walidhurika, pia anasema binadamu walipokula samaki kutoka maji hayo, wana sifa hawachelewi kuharibika, pia wanakosa ladha iliyozoeleka kwa samaki na wana harufu mbaya.

Mwenyekiti anatoa takwimu alizonazo kwamba madhara kwa wanavijiji ni kudhurika kwa namna mbalimbali zilizotajwa, huku baadhi ya walioripoti wamewasilisha vifo vya ng’ombe 54 na mbuzi wanane katika kipindi cha wiki mbili za mwanzo wa mwezi huu.

Namna wanavyoshughulikia mifugo iliyokufa, Mwenyekiti Matinde anaeleza: "Kwa sasa mifugo inayokufa karibu na Mto Mara tunaitupa ndani ya maji, kwa inayokufa mbali na mto, tunachimba shimo na kuifukia."

HATUA ZA KISERIKALI
Mwanzoni mwa mwezi huu Machi 202 mamlaka za serikali kama vile Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria na kamati ya kitaifa iliyoundwa na Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira zilichunguza na kutoa ripozi zilizokindana kama ilivyoelezwa juu.

Source: Nipashe

Pia soma...

~Madai ya sumu Mto Mara kutoka migodini, wananchi wazuiwa kutumia maji, kula samaki, uvuvi, Serikali yatoa tamko
~Kamati: Kinyesi na Mikojo ya Mifugo ndiyo chanzo cha kufa samaki mto Mara, sio sumu ya maji ya Migodini
~Naibu Waziri Abdallah Sagini: Mto Mara hauna sumu, endeleeni kutumia maji
 
Duh haya nayo yanasababishwa na kinyesi cha hiyo mifugo au??!!
 
Hapa unakuta mijitu imevembewa Haina hata uchungu.

Yaani eti vinyesi na mikojo. Kwanza miaka iyo ya zamani ng'ombe walikuwepo kwa idadi kubwa Sana mbona Sasa haya Mambo hayakuwepo.

Yaani mvua ikishanyesha maji or runoffs inatembea na simu nyingi Sana kutokea nyamongo mgodini.

Kuna bwawa pale wamejenga la kukinga maji Ila wakati wa mvua linafurika maji yanatembea Sana.

Ila ni njaa za sisi waafrika. Yaani afrika ni umasikini.

Kiongozi anaingia madarakani hajawahi hata kuishika 10M akipewa Mia anaalewa hata tak000 anashikwa tu.
 
Mkojo na kinyesi cha ng'ombe kwa mujibu wa Le Profeseri wawe wavumilivu watapona
N’gombe anaingia vipi ziwani kujisaidia hadi kinyesi kiingie kwenye mto.

Ni baharani tu ndio kina cha maji kinapanda na kushuka; unaweza bishia wanyama walijisaidia kima cha maji kiliposhuka wakajisaidia.

Vinginevyo hadi kinyesi cha mnyama kiingie kwenye maji yasiyo na ‘tides’ inabidibi aingie kujisaidia ndani ya maji contrary na tabia za wanyama.

Hizi report ni kiwango cha dharau wa uongozi wa utawala Samia kwa watanzania.
 
Hili suala linahitaji uchunguzi huru kabisa na huo uchunguzi uje na suluhisho la kudumu .
 
Baada ya tetesi na hatimaye matamko rasmi kutolewa mara kadhaa kuhusu madhila yanayotokana na maji ya Mto Mara, ripoti zaidi zimeendelea kutolewa kupitia vyombo mbalimbali vya habari kuhusu kinachoendelea katika mto huo.

Awali ilidaiwa kuwa kuna kimikali zenye sumu katika Mto Mara ambazo nyingi baadhi ya vyanzo vilidai kuwa zinatoka kwenye migodi mbalimbali Mkoani Mara.

Mamlaka za Serikali zikajitokeza kufanya uchunguzi na kutoa ripoti mbili ambazo sababu zake pia zilikuwa zikitofautiana juu ya uchafuzi unaoendelea ndani ya mto huo.

Ripoti ya kwanza ilidai kufa kwa samaki mtoni humo ni kwa kuwa kuna wingi wa mafuta hasa oil na grisi kisha wakasema wanaendelea na uchunguzi kujua kwa nini maji yamekuwa meusi. Ripoti ya pili ikadai kuwa uwepo wa kinyesi na mkojo mwingi wa ng’ombe kutiririsha mtoni ndiyo sababu na kuwa hakuna kemikali zenye sumu.

UCHUNGUZI ZAIDI
Baada ya ripoti hizo uchunguzi wa waandishi umeendelea kufanyika na unaonyesha kuwa Kata ya Manga Wilayani Tarime na vijiji vyake kama vile Bisarwi na Kembwi, kuna kitu kisicho cha kawaida katika afya za wakazi wa maeneo hayo.

Kuna msamiati wa utani wanaotaniana wenyeji kuwa 'kwangua vocha' ukisikia hivyo ujue mtu ana kazi ya kujikuna pamoja na kukohoa.

Pia, inaendana na suala la kuhara na kutapika, tumbo kuvimba na madhila mengine, kibaya zaidi ni kuwa huduma za afya kama zahanati au kituo cha afya vipo umbali wa kilomita nne kutoka walipo.

Uchunguzi uliothibitishwa na wenyeji wanavijiji, umebaini kuwapo madhara kwa mifugo ambayo ni moja ya nyenzo zao kuu kiuchumi, kwamba wanadhurika hata kufa.

SHIDA NINI?
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Burongo kilichoko Kijji cha Bisarwi, Juma Matinde amezungumza na Gazeti la Nipashe akidai madhara hayo ya kiafya kwa binadamu na wanyama, pia mimea jirani, yamekuwa hali endelevu tangu kutokea anachokiita mkasa wa kuchafuliwa Mto Mara miaka minne iliyopita.

Kwa mujibu wa Matinde, hali hiyo imekuwa ikijitokeza tangu mwaka 2018 kila unapofika msimu wa mto kufurika, maji yake yamekuwa yakiwasha, wanapoyanywa tumbo linanguruma, kuharisha, wanatapika na kukohoa ikiendana na mikasa kadhaa ya kutapika na kuhara damu.

Mifugo nayo ikitumia maji ya mto huo imekuwa ikivimba tumbo, kulegea na hata kufa. Mwenyekiti Matinde anasema pindi mifugo iliyodhurika ikichinjwa, waligundua nyama yake kuwa nyeusi na inayotoa harufu mbaya.

WALIVYOIPOKEA
Mwenyekiti Matinde anaeleza: "Hii ni wiki ya pili sasa kuna hali hii, tumesitisha kwa muda kula samaki, ng'ombe walipokufa siku za mwanzoni mwa mwezi huu, tuliwachinja na kuuziana nyama. Kila aliyekula alihara, yaani ukishakula, tumbo linanguruma kisha unaanza kuhara kidogokidogo na kutapika.

"Zahanati iko mbali na hapa. Ukishagundua shida hii, unakwenda kwenye duka la dawa hapa kijijini, unawaeleza unavyojisikia, wanakupatia dawa."

MKASA WA WAVUVI
Mwenyekiti Matinde anasimulia kwamba wavuvi walipokuwa kazini mapema mwezi huu, waliwakuta samaki wakielea mtoni, wengi aina ya gogogo na sato.

Anasema baadhi yao waliothubutu kuwachukua ama kwa ajili ya kuuza ama kuwala, watumiaji wengi katika vijiji jirani waliharisha na kutapika.

Anasema muda mfupi baadaye, wavuvi hao waliufikishia taarifa uongozi wa maeneo yao kuwapo maji yenye mwonekano tofauti, meusi kwa rangi yakiashiria hatari kiafya na mazingira.

Hapo Mwenyekiti Matinde anasema viongozi walichukua hatua za tahadhari ikiwamo kuelimisha wananchi kwamba maji hayo na maudhui yake si salama kiafya, vinavyopatikana humo visiliwe.

Mbali na kudokeza hata mbwa waliokula nyama za mifugo iliyokufa walidhurika, pia anasema binadamu walipokula samaki kutoka maji hayo, wana sifa hawachelewi kuharibika, pia wanakosa ladha iliyozoeleka kwa samaki na wana harufu mbaya.

Mwenyekiti anatoa takwimu alizonazo kwamba madhara kwa wanavijiji ni kudhurika kwa namna mbalimbali zilizotajwa, huku baadhi ya walioripoti wamewasilisha vifo vya ng’ombe 54 na mbuzi wanane katika kipindi cha wiki mbili za mwanzo wa mwezi huu.

Namna wanavyoshughulikia mifugo iliyokufa, Mwenyekiti Matinde anaeleza: "Kwa sasa mifugo inayokufa karibu na Mto Mara tunaitupa ndani ya maji, kwa inayokufa mbali na mto, tunachimba shimo na kuifukia."

HATUA ZA KISERIKALI
Mwanzoni mwa mwezi huu Machi 202 mamlaka za serikali kama vile Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria na kamati ya kitaifa iliyoundwa na Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira zilichunguza na kutoa ripozi zilizokindana kama ilivyoelezwa juu.

Source: Nipashe

Pia soma...

~Madai ya sumu Mto Mara kutoka migodini, wananchi wazuiwa kutumia maji, kula samaki, uvuvi, Serikali yatoa tamko
~Kamati: Kinyesi na Mikojo ya Mifugo ndiyo chanzo cha kufa samaki mto Mara, sio sumu ya maji ya Migodini
~Naibu Waziri Abdallah Sagini: Mto Mara hauna sumu, endeleeni kutumia maji
Masikini itakua hawajazoea kunywa maji ya vinyesi vya wanyama.
 
Hivi huyo Prof na tumeyake hawana mshipa wa aibu.

Nimejua ni kwanini ripot nyingi za tume huozea mezani, kumbe majibu huwa yakiwekwa hadharani ni kuwaumbua wajumbe wa tume na serikali tu.
 
Back
Top Bottom