Tarime wamkumbuka Chacha Zakayo Wangwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tarime wamkumbuka Chacha Zakayo Wangwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TUNTEMEKE, Aug 3, 2009.

 1. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2009
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Tarehe 28/07/2009 ilikuwa ni siku ya pekee Tarime kwani kulikuwa na maadhimisho ya mwaka mmoja tangu apate ajali na kufariki Mbunge na Mwanaharakati mpigania haki za wanyone Mh. Chacha Zakayo Wangwe "Chacha Rasta".

  walichofanya katika siku hiyo ni kuwa na maandamano makubwa hadi katika shule ya Sekondari Nkende, ambayo ni moja ya shule zilizoasisiwa na kujengwa na Kamanda Wangwe akiwa diwani wa kata ya Tarime Mjini mwaka 2004, katika shule hiyo wananchi wa Tarime walipanda miti zaidi ya 30 kama sehemu ya kumbukumbu hiyo.

  baada ya hapo waliandamana hadi katika hospitali ya wilaya ya Tarime na kufanya usafi katika mochwari ya kisasa ya wilaya hiyo, kufyeka na kupanda miti pia, kisha wakarudi kwa maandamano na miziki ya reagae na ngoma za asili hadi kwenye uwanja wa mpira wa Tarime kulipokuwa na tamasha la kumuenzi ambapo watu mbalimbali na vikundi vilijitokeza na kutoa burudani kamambe ikiwa na msg za kuthamini kazi aliyoifanya katika uhai wake ya kuwatetea wana Tarime hadi kufungwa huku wakionyesha hisia kuwa kutetea haki kwake ndiyo kumegharimu hata maisha yake.

  Tamasha hilo liliandaliwa na Kampuni ya Kind Brothers ikishirikiana na NGO iitwayo Tukamilishane Women Home Association (TUWHA)
   
 2. W

  WildCard JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Tarime na CHADEMA watusaidie jambo moja; huyu waliempa nafasi ya Marehemu Chacha Wangwe haonekani kama ataimudu nafasi hii. Watutafutie mtu mwingine mwakani. Huyu nafasi ya UDIWANI inamtosha kabisa. Angalia jinsi anavyoishughulikia ile sumu inayomwagwa na ule mgodi wa North Mara.
   
 3. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #3
  Aug 3, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nafikiri Mwita anaweza kazi hiyo kwa sasa; maana nimeona upambanaji wake uko makini kidogo; sijui wanajamvini mnasemaje; kijana nimecomment sijui wenzangu mnasemaje?
   
 4. K

  K4jolly JF-Expert Member

  #4
  Aug 3, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 366
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waliomchagua ni wananchi jamvini hawaingizi mtu mjengoni
   
 5. J

  Jobo JF-Expert Member

  #5
  Aug 3, 2009
  Joined: May 15, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hata mimi naona huyu Mwera viatu ya Chacha Wangwe vimempwaya! Marehemu Chacha tunaendelea kukuombea kwa Mungu mwenyezi akurehemu na hatimaye urithi ufalme wa Mbinguni!
   
 6. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #6
  Aug 3, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Guys did you want a copy cat? let him be with time he will mellow and develop his own style. Marehemu Wangwe had his own style and charisma.

  MAY GOD BLESS HIS SOUL
   
 7. Kamende

  Kamende JF-Expert Member

  #7
  Aug 4, 2009
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 415
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Tarime hawawezi kuondokana na hisia za Wangwe.
  • Alifanana nao
  • Alifanya walichotaka, kama walivyotaka
  • Aliwaambia walichotaka kusikia namna walivyotaka kusikia
  • Aliwaongoza kufanya walilotaka kufanya namna walivyotaka kuongozwa kufanya.
  R.I.P Chacha Zakayo Wangwe
   
Loading...