Tarime: Viongozi wa CCM Newton Mongi na Richard Tiboche wanashikiliwa na polisi kwa amri ya Kigwangalla

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Wilaya ya Tarime, Newton Mongi na Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya chama hicho wilayani humo, Richard Tiboche wanashikiliwa na polisi kwa amri ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla.

Amri ya kukamatwa kwa viongozi na makada hao wa CCM ilitolewa na Waziri huyo jana Julai 16,2018 wakati wa ziara yake ya kukagua maeneo yenye migogoro kati Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (Senapa) na vijiji vya kata za Nyanungu, Gorong’a na Kwiwamcha wilayani Tarime.

“RPC (Kamanda wa Polisi mkoa) mtie mbaroni huyo kiongozi wa UVCCM kwa kuitukana Serikali. Mkuu wa mkoa mnakaaje na watu kama hawa; mwajiriwa anayelipwa mshahara wa CCM anawezaje kuitukana Serikali ya chama ambacho yeye ni mtumishi wake?” aliamuru Dk Kigwangala na kuongeza:

“Nimemsikia kwa maskio yangu akiitukana Serikali ya CCM ambayo yeye ni kada na kiongozi wake. Kamata na afikishwe mahakamani.”

Amri hiyo ilitekelezwa mara moja na askari polisi waliokuwepo kwenye msafara huo kwa kiongozi huyo kuwekwa chini ya ulinzi huku mwenzake ambaye hakuwepo eneo hilo wakati huo alikamatwa baadaye.

Hata hivyo, hakujulikana mara moja maneno yaliyotamkwa na viongozi hao wa CCM yaliyotafsiriwa na Waziri Kigwangala kama matusi kwa Serikali.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara, Athuman Mkilindi ambaye yuko kwenye ziara ya Waziri amesema hajui makosa yaliyosababisha amri ya kuwatia mbaroni makada hao wa chama kutolewa na kushauri atafutwe Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Tarime/Rorya, Henry Mwaibambe kwa ufafanuzi kwa sababu ndiko makosa yalikotendeka.

Mwananchi lilipomtafuta Mwaibambe alisema makada hao wanashikiliwa na uchunguzi dhidi yao unaendelea.

“Ndiyo yuko kwenye uchunguzi lakini inadaiwa kuwa alimkashifu Waziri wa Maliasili,” alisema

kigwanga%2Bpic.jpg
 
Wadadavuzi wa sharia watu saidie. Nilikuwa najua amri ya kukamata katiba imewapa RC na DC sikujua kuwa hata mawaziri nao wana mamlaka ya kusema tia ndani huyo! maana tuendako nadhani hata Katibu mkuu wa wizara mkikutana njiani naye anaweza sema kamata piga teke huyo, na wengine wote wateule wa jiwe.
Tusaidieni ili tukikutana na amri hizo toka kwa wasio pewa dhamana hiyo na Katiba mumkute kasha tema meno tayari
 
Wao wanadhani mambo haya yataishia kwa wapinzani tu.
 
Majizi Hayana Nafasi Awamu Ya Tano
Ccm Hoyee ! :rolleyes:
Mungu Ni Mwema Wakati Wote
 
Huu ni uthibitisho Kuwa ukivunja sheria un ashughulikiwa bila ya kujali mlengo wako wa Kisiasa
Ingekuwa wamekamatwa Nyumbu ingehusishwa Na Siasa utadhan nje ya Siasa hakuna jinai
 
Wadadavuzi wa sharia watu saidie. Nilikuwa najua amri ya kukamata katiba imewapa RC na DC sikujua kuwa hata mawaziri nao wana mamlaka ya kusema tia ndani huyo! maana tuendako nadhani hata Katibu mkuu wa wizara mkikutana njiani naye anaweza sema kamata piga teke huyo, na wengine wote wateule wa jiwe.
Tusaidieni ili tukikutana na amri hizo toka kwa wasio pewa dhamana hiyo na Katiba mumkute kasha tema meno tayari

Chakaza, mbona unakuwa kama mgeni ndani ya nchi hii aisee na uzoefu mkubwa ulionao kuhusu hali ya nchi yetu ilivyo sasa hivi? Au ndio kujiwekea matumaini kidogo kwamba hali itabadilika iwe nafuu?
Ni nani ndani ya serikali na chama anayefuata hiyo katiba unayoizungumzia wewe! Hakuna cha kudadavua wala nini kitakachotusaidia kwa lolote. Tukubali tu hali halisi, kwamba afanyacho mkuu wetu na wasaidizi wake havidadavuliwi, kwani kufanya hivyo ni kupoteza wakati.
Mathalani, hivi hivyo vyama vya upinzani hawajadadavua katiba na sheria zinazoruhusu wafanye siasa? Hivi chaguzi kama zile zinazotazamiwa hivi karibuni kule Kigoma na Songwe, hivi wadadavuzi hawapo? Angalia mambo yanayotendeka huko zidi ya wapinzani!

Samahani sana Mkuu, kama ninakuudhi, lakini wewe ni baadhi ya watu ninao heshimu sana michango yao humu jukwaani. Ninasikitika sana kama bado unamatumaini tena juu ya udadavuzi kuwa utatuletea ahueni ndani ya hali ya nchi yetu hii chini ya utawala huu.
 
Amri hiyo ilitekelezwa mara moja na askari polisi waliokuwepo kwenye msafara huo kwa kiongozi huyo kuwekwa chini ya ulinzi huku mwenzake ambaye hakuwepo eneo hilo wakati huo alikamatwa baadaye

Kielelezo ni kuwa akamatwe kwakuwa alimsikia kwa masikio yake, je huyu mwingine alimsikiaje kwa masikio yake kama hakuwepo kwenye eneo la tukio?
 
Back
Top Bottom