Tarime this is too much: Kijana akatwa mkono kwa deni la laki 3

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Mkazi wa Kijiji cha Keisangora, Wilaya ya Tarime Mkoani Mara, Mwita Magige, amekatwa mkono wa kushoto kwa kile kinachodaiwa kushindwa kulipa deni la sh 300,000 baada ya ng’ombe wake wane kukamatwa na mdeni wake.

Tukio hilo lilitokea kijijini hapo baada ya ng’ombe wake waliokuwa wakichungwa na mkewe kukamatwa na mdeni wake ili kumshinikiza amlipe.

Magige alisema, Aprili 5 akiwa safarini alipigiwa simu kuwa mifugo yake imekamatwa na uongozi wa Kijiji na alitakiwa kwenda kuikomboa, baada ya hapo alisitisha safari na kurejea nyumbani, alikwenda kwa Mwenyekiti wa Kijiji, Nuru Magacha alimweleza kuwa mifugo yake ipo na anadaiwa sh 300,000.

Magige alisema muda mfupi baadaye yowe lilipigwa kuashiria hatari na kwamba, akiwa hajui kinachoendelea wananchi walikusanyika na kijana mmoja alimkata mkono wa kushoto kwa panga na kuucha ukining’inia.

Chanzo: Kwanza TV
 
Not only tarime...... Wazazi wanaua watoto kwa sh 100
 
Umeileta kishabiki mbona husemi Syria ambako maelefu wanauwawa kabisa wala sio kukatwa mkono..acheni mambo ya kienyeji haya...kuna mwanamke alimchoma moto mtoto hapo Dar kisa elf 2 wala hakuna haya makelele meengi...lakini hili ni habari
 
Ungeleta mada ya mdada wa kazi kateswa huko "nje" ungepata wachangiaji wengi sana,ingetukanwa jamii nzima pamoja na dini yao kua ni makatili.
 
Mkazi wa Kijiji cha Keisangora, Wilaya ya Tarime Mkoani Mara, Mwita Magige, amekatwa mkono wa kushoto kwa kile kinachodaiwa kushindwa kulipa deni la sh 300,000 baada ya ng’ombe wake wane kukamatwa na mdeni wake.

Tukio hilo lilitokea kijijini hapo baada ya ng’ombe wake waliokuwa wakichungwa na mkewe kukamatwa na mdeni wake ili kumshinikiza amlipe.

Magige alisema, Aprili 5 akiwa safarini alipigiwa simu kuwa mifugo yake imekamatwa na uongozi wa Kijiji na alitakiwa kwenda kuikomboa, baada ya hapo alisitisha safari na kurejea nyumbani, alikwenda kwa Mwenyekiti wa Kijiji, Nuru Magacha alimweleza kuwa mifugo yake ipo na anadaiwa sh 300,000.

Magige alisema muda mfupi baadaye yowe lilipigwa kuashiria hatari na kwamba, akiwa hajui kinachoendelea wananchi walikusanyika na kijana mmoja alimkata mkono wa kushoto kwa panga na kuucha ukining’inia.

Chanzo: Kwanza TV
Sasa na yule aliyechomwa moto mumewe kisa mhindi wa kuchoma
 
Ungeleta mada ya mdada wa kazi kateswa huko "nje" ungepata wachangiaji wengi sana,ingetukanwa jamii nzima pamoja na dini yao kua ni makatili.
Nje kwa warabu na wahindi wangetukanwa ile mbaya na mapovu kwa wiiiiingi.
Lakini ingekua nje kwa wazungu mambo ya kawaida tu. Watu wala wasingetoa mapovu
 
Tarime siku nafika mara ya kwanza nilisikia Damu inasisimka sana (Ilikuwa kipindi Chacha Wangwe kafariki,siku mwili unaletwa)
 
Back
Top Bottom