Tarime, Tarime yangu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tarime, Tarime yangu.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ghati Makamba, Mar 10, 2010.

 1. G

  Ghati Makamba Member

  #1
  Mar 10, 2010
  Joined: Jun 29, 2009
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tarime, Tarime yangu, Tarime unapendeza,
  Tarime mekutwa fungu, Ufanisi kuongeza,
  Rorya pasipo majungu, Ulipaswa kupunguza,
  Tarime maisha bora, Kabisa yawezekana.

  Mito, ziwa migodi, Tarime yote unayo,
  Mbuga, mabonde na milima, Tarime haki unayo,
  Hata ngano ungelima, Tengeneze wako mvinyo,
  Maisha bora Tarime, yawezekana hakika.

  Rutuba, maji, migodi, Kweli kajalia Mungu,
  Mazao, nyama, madini, Tarime kwako si haba,
  Baridi, joto na jua, Hizo zote hali zako,
  Maisha bora Tarime, hakika yawezekana.

  Tarime wewe kiungo, Afrika Mashariki,
  Kenya, Uganda na Bongo, Kufika hakupingiki,
  Tarime kweli kiwango, Bila wewe hatufiki,
  Maisha bora Tarime, Yawezekana hakika.

  Ninapatwa na simanzi, Damu kwako nikiona,
  Mauaji kwako enzi, Majeraha yasopona,
  Kuwa mbaya balozi, Tanzania kukuona,
  Tarime damu simwage, Tarime nifute chozi.

  Nakiri kweli nakiri, Hasira kwako asili,
  Mejichimbia kaburi, Thamaniyo kwenda mbali,
  Uukane ukatiri, Upige goti usali,
  Tarime nifute chozi, Tarime damu simwage.

  Makazi, Afya, Elimu, Maishayo kweli duni,
  Nyamongo kunyweshwa sumu, Mekuwa utamaduni,
  Watu wako kujikimu, Uhai wao rehani,
  Siyo laana Tarime, Tarime jenga umoja.

  Mtimbaru, Mryanchoka, Mnchali na Mnyabasi,
  Yatupasa badilika, Mwirege pia Msweta,
  Amani kuimalika, Jaluo pia sibezwe,
  Amani ii langoni, Tarime fumbua macho.

  Tarime simwage damu, Watu si tambiko tena,
  Uwaone binadamu, Watuwo kutouana,
  Tarime muombe Mungu, Mungu atawaepusha,
  Mungu wangu nakuomba, Kumwaga damu epusha.
   
Loading...