Tarime: Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa ahojiwa na Polisi

Status
Not open for further replies.
mpaka sasa kwa mujibu wa taarifaza viongozi wa chama walioko huko plice sirari wilayani tarime inasemekana kuna kesi zaidi ya tatu ammbazo mh heche anakabiliwa nazo ikiwemo
1 kumuita rais ombo omba
2kutangazia umma kuwa polisi kanda maalum tarime na rorya wamekithiri kuwabambikiza vijana kesi za mauaji;robary;na hata kuzuia fursa za wafanyabiashara ndogondogo hatimaye polisi ndio wanaomiliki magari na hata pikipkiki
3rais kusababisha maisha ya wanatarime kuwa magumu kwa kuachia dhahabu inaenda ulaya huku yeye anarudi na net
heche ameambatana na wakil wake na amewaonya polisi wasimhoji kwa mashinikizo
Kwani hayo yote si yana uthibitisho? Kama watanzania tunaona ni sifa mbaya kwa Taifa tujirekebishe na kumweleza mkuu wa nchi ili kurejesha heshima ya Taifa letu. Kuwatisha na kuwashitaki wanaotuonesha aibu hii siyo suluhu ya tatizo hili bali ni kuandaa aibu kubwa kwa Taifa.
 
MWENYEKITI wa Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA), John Heche amehojiwa na polisi kwa saa nne kwa madai kuwa alitoa lugha za matusi dhidi ya Rais Jakaya Kikwete kwa kumwita ombaomba.

Taarifa zilizolifika gazeti la Mwananchi, jana zinaeleza kuwa Heche alihojiwa na polisi wa Kanda Maalumu ya Tarime-Rorya kwa madai ya kutoa lugha hiyo ya matusi katika mkutano wa hadhara alioufanya Jumamosi iliyopita, Sirari mkoani Mara.

Ilielezwa kuwa baada ya mkutano huo uliofanyika kwenye Viwanja vya Sirari kumalizika, Heche alipigiwa simu na polisi akitakiwa kwenda kutoa maelezo kuhusu kauli yake hiyo dhidi ya Rais Kikwete.

Mwenyekiti huyo wa BAVICHA aliliambia gazeti la Mwananchi jana kuwa, "Nilihojiwa jana (juzi) kuanzia saa 11:00 jioni hadi saa 2:30 usiku na polisi wa Kanda Maalumu ya Tarime Rorya."

Aliendelea kusema, "Aliyenihoji ni OC CID wa Wilaya ya Kipolisi Sirari ambaye anadai kuwa, kumwita Rais ombaomba ni lugha ya matusi."

Heche alikiri kufanya mkutano huo eneo la Sokoni, Sirari mkoani Mara na akasema alishangaa kupigiwa simu na polisi akiitwa kwenda kutoa maelezo baada ya mkutano huo kumalizika.

"Siku hiyo sikwenda kwa kuwa sikuwa na mwanasheria wangu kwa hiyo nikawaambia kuwa ningefika baada ya kuwa naye hivyo jana (juzi) nikaenda," alisema Heche.

Alisema siku ya kwanza kufika polisi alikutana na viongozi wa ngazi ya juu wote wa Kanda Maalumu ya Tarime – Rorya, ambao walikuwa wakimsubiri kumhoji.

Kaimu Kamanda wa Polisi Tarime - Rorya, Sebastian Zacharia alithibitisha kuhojiwa kwa kiongozi huyo wa CHADEMA na kusema hii ni kutokana na taarifa kwamba alitoa maneno ya kashfa kwa kiongozi wa nchi., "Alihojiwa juzi katika kituo cha Sirari na sasa tunakamilisha upelelezi," alisema Kamanda Zacharia.

Kamanda huyo alisema hivi sasa wanakamilisha upelelezi wa suala hilo kabla ya kupeleka jalada kwenye ofisi ya mwanasheria wa serikali kwa ajili ya hatua zaidi, "Siwezi kujua alihojiwa kwa kwa muda gani kwa sababu mahojiano yalifanyika huko Sirari, ila ninachoweza kusema tunamalizia upelelezi kabla ya kupeleka faili kwenye ofisi ya mwanasheria wa serikali kwa hatua zidi," alisema Zacharia.

Kauli ya Kamanda huyo imekuja baada ya OC CID wa Wilaya ya Kipolisi Sirari, George Wilbard aliyemhoji Heche kusema kwamba, hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa yeye siyo msemaji wa polisi kwenye Kanda hiyo.


Source: wavuti - wavuti
 
Hahahaaaaaaaa kashindwa kutoa capital kwa kiwanda cha neti cha Tanzania anasubili net za msaada? Kwanza kingesaidia kutoa ajira kwa vijana wa kitanzania hata 20 walioko mtaani.
 
MWENYEKITI wa Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA), John Heche amehojiwa na polisi kwa saa nne kwa madai kuwa alitoa lugha za matusi dhidi ya Rais Jakaya Kikwete kwa kumwita ombaomba.

Taarifa zilizolifika gazeti la Mwananchi, jana zinaeleza kuwa Heche alihojiwa na polisi wa Kanda Maalumu ya Tarime-Rorya kwa madai ya kutoa lugha hiyo ya matusi katika mkutano wa hadhara alioufanya Jumamosi iliyopita, Sirari mkoani Mara.

Ilielezwa kuwa baada ya mkutano huo uliofanyika kwenye Viwanja vya Sirari kumalizika, Heche alipigiwa simu na polisi akitakiwa kwenda kutoa maelezo kuhusu kauli yake hiyo dhidi ya Rais Kikwete......

Mbona kila kitu kipo wazi, omba omba ni omba omba tu hata avae suti na kupanda ndege
 
Serikali ya magamba inakwenda vibaya.
Baba Riz1 anajisifu na kutuaga kila siku kwamba anakwenda kuomba kwa wajomba na kwamba bila kuomba tutakufa njaa? Au policccm hawasomi magazeti wala kusikiliza redio?
Vilevile nadhani waTz hatushibi wala hatuendelei pamoja na yeye kuombaomba miaka yote hii kwani ni ombaomba dhaifu!
 
MWENYEKITI wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), John Heche amehojiwa na polisi kwa saa nne kwa madai kuwa alitoa lugha za matusi

dhidi ya DHAIFU kwa kumwita ombaomba.Taarifa zilizolifika gazeti hili jana zinaeleza kuwa Heche alihojiwa na polisi wa Kanda Maalumu ya

Tarime-Rorya. Anadaiwa kutoa lugha hiyo ya matusi katika mkutano wa hadhara alioufanya Jumamosi iliyopita, Sirari mkoani Mara.

Lini mtaacha kutumika polisi?

Kwani hamjui kila kukicha Dhaifu anaenda ughaibuni kuombaomba hadi yakamkuta yale ya nanii?.

source Mwananchi 16/08/2012
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom