Tarime:Mwalimu jela miaka sita kwa kutafuna pesa shule Tsh mil tatu.

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Mahakama ya Wilaya ya Tarime imemuhukumu kwenda jela miaka mitatu aliyekuwa mwalimu mkuu shule ya msingi Mwege iliyopo wilayani Rorya mkoani Mara,Issaya Gwidana kwa makosa 6 ikiwemo la kughushi hundi za shule na kuchukua Sh. milioni 4.965 ambazo ni kwa ajili ya ujenzi wa madarasa https://t.co/J55ZyPF4xV
20220520_204626.jpg
 
Huyu anaibaje tupesa kidogo hivyo?pesa ht huwezi kumhonga Hakimu wala kumlipa wakili?
Ajifunze kwa wenzie serikalini, wanakwiba mabilioni then wanaigawa kwa watu watakao mlinda kikisanuka.
 
HUYO MWAMBA ALIVYOKAA INAONESHA DHAHIRI MI MWINGI WA HABARI😂😂😂
ILA DAAH MBONA KAIBA KIDOGO TU
 
Mahakama ya Wilaya ya Tarime imemuhukumu kwenda jela miaka mitatu aliyekuwa mwalimu mkuu shule ya msingi Mwege iliyopo wilayani Rorya mkoani Mara,Issaya Gwidana kwa makosa 6 ikiwemo la kughushi hundi za shule na kuchukua Sh. milioni 4.965 ambazo ni kwa ajili ya ujenzi wa madarasa https://t.co/J55ZyPF4xVView attachment 2232187
Inasikitisha sana,waalimu nao wameanza kuwa mafisadi
 
Duuh pesa kiduchu miaka sita, kwanini wasimkate kwenye mshahara wake tuu. Aliyeiba mabilioni anakula kiyoyozi kwenye prado.
 
MSD waliiba bilioni ngapi na wapi nje wanatanua?

Ama kweli sheria duniani, haki mbinguni.
 
Kuna wapuuzi juzi tu hapa wamefutiwa mashataka ya uhujumu uchumi,
Alafu kuna bwege mwingine kalipishwa eti milion 8 mahakamani baada ya kosa la kutafuna mabilioni,
Huku mwalimu kaiba ela iyo miaka 6, asee Tanzania ukiwa na Ela unanunua hadi haki na sheria zote.
 
Huyu anaibaje tupesa kidogo hivyo?pesa ht huwezi kumhonga Hakimu wala kumlipa wakili?
Ajifunze kwa wenzie serikalini, wanakwiba mabilioni then wanaigawa kwa watu watakao mlinda kikisanuka.
Hivi Kwa uelewa wako shule ya msingi ya kata, inapelekewa bilioni ngapi?
 
Duuh pesa kiduchu miaka sita, kwanini wasimkate kwenye mshahara wake tuu. Aliyeiba mabilioni anakula kiyoyozi kwenye prado.
Dpp hapa alionesha nia ya kuendelea na hiyo kesi.... Liwe funzo kwa wanaoiba centi za chapati!! Ukitaka kuiba Iba billions au trillions.. hapa unaweza ukasema Mzee nitakuachia za vieeeit !!

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Asamehewe jamani. Akatwe kwenye mshahara.
Hiyo sura yake moja kwa moja anaonyesha anajutia kosa lake.
Tafadhali Mheshimiwa Mkuu, msamehe.
 
Back
Top Bottom