Tarime, Mara: Mmiliki wa mabasi ya Zacharia awapiga risasi maafisa wa Usalama wa Taifa, ashikiliwa na Polisi

“Kwa siku tatu mfululizo nililishuhudia gari lililohusika katika tukio likiwa limeegeshwa nyuma ya kituo cha mafuta cha Zakaria wakijifanya kulifanyia matengenezo, hii inaonyesha walikuwa kwenye mtego kufuatilia nyendo za Zakaria.” - Bashiri Selemani, M/Kiti wa Mtaa
aibu sana !
 
Wenye kituo wamesema saa kumi na mbili huwa wanafunga kituo chao sasa saa mbili walikuja kufanya nini?
Hilo swali muhimu. Lakini mie nilikua namjibu anaesema kwamba serikali huwa haijazi mafuta kwenye vituo binafsi!
 
Kufikia 2020 tutaona mengi - hapa ni mwanzo wa mkanda. Madai ya katiba mpya kama mwongozo na dira kwa taifa letu yataonekana ya maana katika kipindi hiki.
 
Kwa hiyo mkapa alisaini kitu asichokijua? Sheria hiyo imetakataza usalama wa Taifa wasikamate sasa basi kumbe mkapa nae alikuwa mbumbumbu?
Mkuu niuelewa tu wa sheria ndiyo unagomba! Anakatazwa kukamata kwa mgongo wa kazi yake ya Usalama wa Taifa! Lakini kumbuka pia ni raia wa TZ kwa hiyo sheria ya CPA inamruhusu kumkamata mtu ambaye anatenda kosa la jinai mbele yake kama ambavyo raia mwingine yoyote anavyoweza kamata mhalifu yoyote anayetenda kosa la jinai mbele yake!!
 
Mkuu niuelewa tu wa sheria tu ndiyo unagomba! Anakatazwa kukamata kwa mgongo wa kazi yake ya Usalama wa Taifa! Lakini kumbuka pia ni raia wa TZ kwa hiyo sheria ya CPA inamruhusu kumkamata mtu ambaye anatenda kosa la jinai mbele yake kama ambavyo raia mwingine yoyote!!
Nimekuelewa mkuu.
 
Mkuu. Mnabishana kitu simple sana jApo sijui sheria ila iko hivi
Uko sahihi sheria inamruhusu mtu yoyote kumkamata muhalifu .
Sasa zitto anaongelea sheria ya usalama yaani watu wa usalama wamekatazwa kukamata mtu.ila ww unaweza kumkamata mhalifu as long as haupo kwenye system
Mkuu sheria ya CPA hajabagua kuwa Afisa wa Usalama wa Taifa au raia mwingine yeyote asikamate ila sheria ya usalama wa taifa hairuhusu kama taasisi kukamata ila CPA inaruhusu raia yeyote kukamata mhalifu wa jinai ndio maana raia wanakamata waharifu kila siku na kuwafikisha polisi au ofisi za serikali. Haiwezekani na wala haiingii akilini Afisa Usalama wa Taifa aone mhalifu anatenda kosa mbele yake asimkamate eti kwa kuwa sheria ya Usalama wa Taifa inamkataza kukamata. Just interpretantion of laws ndiyo inakusumbua mkuu.
 
usalama sio law enforcement agency
Kwani wewe kama raia wa kawaida huruhusiwi kukamata mhalifu akiwa anatenda kosa mbele yako?? Kwa taarifa yako CPA yaani Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai inamruhusu raia yoyote kumkamata mhalifu wa makosa ya Jinai na kumfikisha kwa Askari Polisi ambaye atamkamata na kumfikisha Mahakamani. Mkuu kasome sheria ya CPA utajua!!
 
Kwel naamini taratibu juu ya karma juzi tu kuna uzi ulikua unazengea mmiliki wa mabasi ya zakaria kanizurum maliyangu Leo tenaa asee"
 
Yaani maafisa usalama watano,wanashindwa kumteka mtu ,RAIA mmoja?
Huwa naambiwa wengi wao watokea jeshini,sasa wajeda gani dhaifu kiasi hiki,?haya ndio madhara ya kupeana kazi kimjomba mjomba,
Sasa kama MTU mmoja kawashinda,watawezaje kukamata magenge ya kimafia?
Hiyo ilikuwa kazi ya MTU mmoja tu,
Sio kila MTU ni mzembe mzembe,hata muwe kikosi usiombe kuwekwa kati na RAIA,
 
Back
Top Bottom