Tarime: Mama na wanawe wawili wauawa kinyama

Ilisolokobwe

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
1,856
811
Mama mmoja na wanawe wawili wa kiume wameuawa usiku wa kuamkia leo na mtu asiyejulikana, kana kwamba hiyo haitoshi huyo muuaji pia alimbaka binti wa familia hiyo.

Tukio hilo la kusikitisha na la aibu limetokea usiku wa kuamkia leo katika kijiji cha Nyantira wilayani Tarime.

Hadi sasa haijajulikana lengo la muuaji lilikuwa nini, polisi walifika katika eneo la tukio na wakafanikiwa kumkamata kijana mmoja kwa jina Koroso Mahenye.

Zaidi nitawajulisha kinachoendelea
 
Kunahitajika Elimu ya watu kuheshimu uhai. Tarime mtu kumtoa uhai mwezake ni rahisi kama kuchinja kuku.
Dhamani ya uhai inatakiwa ifahamike.
 
Hukumu ya kifo ianze kutekelezwa sasa tena hadharani wakianzia na huko mara watu watakoma.
 
Huko sindo anakotoka yule mbunge anaetaka ngada ihalalishwe?
 
Ukifuatilia sababu za mauaji unakuta ni za kijinga kabisa. Unaweza kukuta jamaa kanyimwa penzi!!!
 
Huko panahitaji Mkuu wa Wilaya jasiri kama Makonda ili akakomeshe haya mauaji.
 
Back
Top Bottom