TARIME: Diwani aapishwa akiwa Jela! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TARIME: Diwani aapishwa akiwa Jela!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pasco_jr_ngumi, Dec 25, 2010.

 1. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #1
  Dec 25, 2010
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,811
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  DIWANI wa Kata ya Bumera, wilayani
  Tarime, Tengera Marwa (CHADEMA),
  amelazimika kula kiapo akiwa rumande
  wakati wa kikao cha kwanza cha baraza la
  madiwani wa halmashauri hiyo mwishoni
  mwa wiki.
  Tengera ambaye pia alichaguliwa huku
  akiwa mahabusu katika uchaguzi mkuu wa
  Oktoba, anakabiliwa na kesi ya mauaji.
  Awali shughuli katika kikao hicho
  zililazimika kusimama kwa zaidi ya saa nne
  baada ya madiwani kutoka chama chake
  kutoka nje ya ukumbi katika kile
  kilichodaiwa kutoridhika na kukwamishwa
  jitihada zao na waendeshaji wa kikao
  kutaka mwenzao huyo aletwe katika
  ukumbi huo aapishwe.
  Hata hivyo, kutokana na kuingilia kati ofisa
  mmoja mwandamizi wa polisi wilayani
  hapa aliyefahamika kwa jina moja la
  Massenga ilielezwa kuwa kutokana na hali
  tete ya usalama kisiasa wilayani humu
  isingekuwa rahisi kumleta diwani huyo
  ukumbini hapo na akaelekeza hatua za
  haraka kumpatia udhuru ili apelekwe kuapa
  mahakamani.
  Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Fidelis
  Lumato, aliyekuwa akiendesha kikao hicho
  kwa muda alilazimika kuamuru kikao hicho
  kihamie katika mahakama ya wilayani hapa
  ambapo diwani huyo aliletwa chini ya
  ulinzi mkali na kula kiapo chake na kisha
  kurejeshwa mahabusu.
  Baadaye kikao hicho kiliendelea ambapo
  katika uchaguzi wa kumtafuta mwenyekiti
  wa Halmashauri ya Tarime, Diwani wa
  kata ya Sirari, Amos Sagara CCM
  alichaguliwa kwa kura nyingi na
  kumshinda mgombea wa CHADEMA na
  mwenyekiti wa mkoa wa Mara wa chama
  hicho, Machage Machage.
   
Loading...