Tarime: Bhoke Matiko, acharangwa mapanga na vijana wa sungusungu

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,490
54,884
ukatiri-mara-1.jpg

Bhoke Matiko akiugulia mkono

MARA: Jamani Mara; ukatili huu hadi lini? Hayo ni baadhi ya maneno yaliyotamkwa na watu baada ya mwanamke aitwaye Bhoke Matiko, 45, (pichani), mkazi wa Mtaa wa Nyamiobho Mogabiri, wilayani Tarime mkoani Mara, kufanyiwa ukatili wa kutisha wa kucharangwa mapanga na vijana waliodaiwa ni sungusungu katika ‘grosari’ yake eneo la Mogabiri Senta na kupoteza fahamu.
2.jpg

Tukio hilo lililothibitishwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum Tarime na Rorya, liliripotiwa na mama huyo Alhamisi iliyopita katika Kituo cha Polisi Bomani mjini hapa na kufunguliwa jalada namba TAR/IR/2421/2016 – KUJERUHI.

Baada ya mama huyo kucharangwa mapanga saa 2.46 usiku na vijana aliodai wanafahamika kwa majina na makazi yao, walipasua chupa zilizokuwa na bia na kupasua balbu katika grosari yake hiyo kisha kutoweka bila kukamatwa.

Akisimulia mkasa huo mama huyo alisema:

“Nilishitukia vijana ninaowafahamu ambao ni sungusungu wakimtaka kijana aliyekuwa mteja wangu akiwa anakunya kinywaji, wamchukue kwenda naye ofisini kufuatia makosa waliyokuwa wanamtuhumu.
3.jpg

“Kabla ya kumchukua niliwaomba wamuache kwanza alipe fedha za vinywaji alivyokunywa likawa kosa, walinigeuzia kibao na kunicharanga mapanga huku wakinilazimisha niwapatie fedha ya mauzo ya siku hiyo, nikakataa.

“Walianza kunikata mapanga, nilipiga mayowe lakini baada ya muda nilianguka na kupoteza fahamu, kumbe wasamaria wema walifika lakini hawakufanikiwa kuwakamata vijana hao.

“Nilichukuliwa na kupelekwa Kituo cha Afya cha Tarime Goodwil na kulazwa wodi namba tatu baada ya kupitishwa kituo cha polisi na kupewa PF3,” alisema.
44.jpg

Muuguzi wa zamu wa kituo hicho, Tatu Manyama alisema kuwa mama huyo alifikishwa kituoni hapo akiwa na hali mbaya baada ya kutokwa damu nyingi.

Afisa mmoja wa polisi aliyeomba jina lake kutoandikwa gazetini kwa kuwa siyo msemaji, alisema jeshi la polisi linawasaka vijana hao ili liwafikishe mahakamani kwa makosa ya kumjeruhi mama huyo.

“Vijana hao wanaendesha ulinzi wa jamii maarufu kama sungusungu lakini baadhi yao wanatumia nafasi hiyo kufanya uhalifu kwa baadhi ya watu,” alisema afisa huyo.

Licha ya kuanzishwa kwa kanda maalum ya kipolisi, Mkoa wa Mara umekithiri kwa wananchi kukatana mapanga na gazeti hili limekuwa likiripoti matukio ya aina hiyo mara kwa mara kwa miaka mingi, jambo ambalo linatia doa eneo hilo la nchi.

Chanzo: Uwazi
 
Mkoa wa Mara sio salama kwa kuishi,kukaa bila kucharangana mapanga hawaoni raha kabisa,bila kuona damu mikono yao inawawasha sana.
 
Mkoa wa Mara una makabila mengi, kabila korofi ni hili la wakurya ambao wanapatikana kwa wingi wilaya ya Serengeti (Mugumu) na Tarime huko ndiko utasikia mapanga kila siku.Makabila mengine kama Waikizu,wasizaki,wajita,wataturu, na wazanaki wanaopatikana katika wilaya za Bunda,Rorya,Butiama na Musoma hawana shida.
 
Pole sana mama, nchi imesimama kwa muda kulinda raia wake, now ili uwe salama inabidi uishi Dodoma.
 
Pole mama....

Huwa nawaza sana kuhusu kupata PF3.
Mgonjwa anavuja damu, uhai wake uko hatarini lakini mpaka kituo cha polisi kitafutwe, apelekwe kwanza huko halafu ndio safari ya hospitali ianze tena. ..

Hakuna namna ya kufupisha hii process, ili tumuokoe mgonjwa kwanza?

Mfano katika hospitali ya Mkoa 1 au 2 kuwe na kiofisi cha polisi hapo kwa ajili ya cases kama hizi kurahisisha hiyo process ya PF3.
 
Ifi
police kazi yao ni kuwachunga Chadema.

swissme
Ifikie kipindi bwanakaka uwe unajiangalia huko chini Kama manyoya meusi yamerefuka ili uyakate... Huwezi kuwaweka polisi katika kila nyumba, grocery, maduka, na maeneo yote wakati wote. Kinachohitajika ni jamii kubadilika na kuachana na Uhalifu. Umeambiwa walikuwa na shida na mtu wao huyo mama alikumbwa na mkasa usio wake. Halafu ulivyo kiherehere unaanzisha uharo wa chadema kwenye uzi wenye kuhitaji mjadala wa kuishauri jamii ya watu wa Tarime kuachana na ukatili.
Napenda kuchukua nafasi hii kumpa Pole Dada Huyu na kuwaomba wazee wa Mila mkoani Mara kwa ujumla kuwa na mjadala wa pamoja wa jinsi ya kumaliza Tatizo hili
 
Asee huo mkoa wenyeji wa kule wanaroho mbaya sana nakumbuka kipindi nimehamishiwa huko kikazi kuna mmoja wetu alitoka akaenda uraiani kupata mahitaji maalum alipokuwa anarudi majamaa wakamuweka kati katika majibishano wakamchoma kisu ila mungu si jecha yule mwenzetu alienda kuzindukia hospital ya bungando mwanza
 
Ifi

Ifikie kipindi bwanakaka uwe unajiangalia huko chini Kama manyoya meusi yamerefuka ili uyakate... Huwezi kuwaweka polisi katika kila nyumba, grocery, maduka, na maeneo yote wakati wote. Kinachohitajika ni jamii kubadilika na kuachana na Uhalifu. Umeambiwa walikuwa na shida na mtu wao huyo mama alikumbwa na mkasa usio wake. Halafu ulivyo kiherehere unaanzisha uharo wa chadema kwenye uzi wenye kuhitaji mjadala wa kuishauri jamii ya watu wa Tarime kuachana na ukatili.
Napenda kuchukua nafasi hii kumpa Pole Dada Huyu na kuwaomba wazee wa Mila mkoani Mara kwa ujumla kuwa na mjadala wa pamoja wa jinsi ya kumaliza Tatizo hili
Acha matusi dogo, kumbe wewe yakirefuka huwa yanakusumbua hivyo?
 
Ifi

Ifikie kipindi bwanakaka uwe unajiangalia huko chini Kama manyoya meusi yamerefuka ili uyakate... Huwezi kuwaweka polisi katika kila nyumba, grocery, maduka, na maeneo yote wakati wote. Kinachohitajika ni jamii kubadilika na kuachana na Uhalifu. Umeambiwa walikuwa na shida na mtu wao huyo mama alikumbwa na mkasa usio wake. Halafu ulivyo kiherehere unaanzisha uharo wa chadema kwenye uzi wenye kuhitaji mjadala wa kuishauri jamii ya watu wa Tarime kuachana na ukatili.
Napenda kuchukua nafasi hii kumpa Pole Dada Huyu na kuwaomba wazee wa Mila mkoani Mara kwa ujumla kuwa na mjadala wa pamoja wa jinsi ya kumaliza Tatizo hili
Hujaona jana walivyokuwa wanaandamana Dodoma.. Waambie kuna mkutano wa CHASO utaona wingi wao
 
Mkoa wa Mara una makabila mengi, kabila korofi ni hili la wakurya ambao wanapatikana kwa wingi wilaya ya Serengeti (Mugumu) na Tarime huko ndiko utasikia mapanga kila siku.Makabila mengine kama Waikizu,wasizaki,wajita,wataturu, na wazanaki wanaopatikana katika wilaya za Bunda,Rorya,Butiama na Musoma hawana shida.
Huo sasa ubaguzi, kumbuka kuwa hiyo koo ndo imekuwa kinga ya hizo nyingine dhidi ya Wamasai katika wizi wa mifugo, tangu enzi za Ukoloni Masaai walikuwa wakipata taabu kukatisha Serengeti (Mugumu) na Tarime kwenda kuiba mifugo katika maeneo mengine, kama walifanikiwa kukatisha, siku ya kurudi wakiwa na mifugo walikiona na cha mtema kuni ikiwa ni pamoja na kunyang'anywa hiyo mifugo. Hata hivyo, kadri elimu inavyozidi kuingia katika eneo la watu hawa, matukio haya mabaya yanazdi kupungua, ni matumaini yangu kuwa ipo siku yataisga ingawa sio miaka ya hivi karibuni.
 
Mkoa wa Mara una makabila mengi, kabila korofi ni hili la wakurya ambao wanapatikana kwa wingi wilaya ya Serengeti (Mugumu) na Tarime huko ndiko utasikia mapanga kila siku.Makabila mengine kama Waikizu,wasizaki,wajita,wataturu, na wazanaki wanaopatikana katika wilaya za Bunda,Rorya,Butiama na Musoma hawana shida.
Hujanishawishi...Mkoa wa Mara mnauweza wenyewe
 
Back
Top Bottom