Elections 2010 Tarehe ya uchaguzi yatangazwa; majimbo ya kugawanywa yatangazwa!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

“TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UGAWAJI WA MAJIMBO NA RATIBA YA UCHAGUZI MKUU WA 2010”

1.Ugawaji wa Majimbo

Tume ya Taifa ya Uchaguzi ,Kwa mamlaka iliyopewa chini ya Ibara ya 75 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977,inawatangazia wadau wa Uchaguzi na Wananchi kwa ujumla kuwa itagawa Majimbo ya Uchaguzi yafuatayo.

i.Nkasi

ii.Tunduru
iii.Maswa
iv.Kasulu Mashariki
v.Bukombe
vi.Singida Kusini
vii.Ukonga

Taarifa zaidi kuhusu Majimbo hayo mapya yatakayoanzishwa itatolewa baada ya Tume kukutana na wadau wa Majimbo husika.

2. Ratiba ya Uchaguzi Mkuu wa 2010

Kwa mujibu wa Vifungu vya 37(1)(a) na 46(1) vya Sheria ya Uchaguzi, Sura ya 343 na Vifungu vya 41(1) na 48(1) vya Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ,Sura ya 292, Tume ya Taifa ya Uchaguzi pia inawatangazia Wananchi wote kuwa Ratiba ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010 kwa Uchaguzi wa Rais, Bunge na Madiwani itakuwa kama ifuatavyo;

1. UTEUZI WA WAGOMBEA - 19 AGOSTI,2010

2. KAMPENI ZA UCHAGUZI -20 AGOSTI, HADI 30 OKTOBA,2010

3. UPIGAJI KURA 31 OKTOBA, 2010

Kwa mujibu wa Sheria za Uchaguzi, Tume itawatangazia Wananchi rasmi, tarehe ya kutoa Fomu za Uteuzi kwa wagombea.

JAJI MSTAAFU LEWIS M.MAKAME
MWENYEKITI WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
 
Sawa ila nahisi pamoja na kwamba kugawanya majimbo ni vizuri kwa maandeleo yetu ghalama nazo duh, halafu chama cha matumbo wanataka kuongeza idadi ya mafisadi mjengoni tu. Ni mtazamo tu!
 
wameongeza majimbo lakini kuongeza muda watu kujiandikisha hawataki...wizi mtupu
 
aisee.. CCM imewaathiri sana watu.. maana reactions za kwanza ni towards the negative. Nafikiri ni vizuri sasa tunajua timeline ya mambo mbalimbali ingawa nafikiri baadhi ya tarehe zitachenji baada ya Hukumu ya Mahakama..
 
Sawa ila nahisi pamoja na kwamba kugawanya majimbo ni vizuri kwa maandeleo yetu ghalama nazo duh, halafu chama cha matumbo wanataka kuongeza idadi ya mafisadi mjengoni tu. Ni mtazamo tu!

Uzuri wake nini na kwa maendeleo gani kuliko gharama?
 
aisee.. CCM imewaathiri sana watu.. maana reactions za kwanza ni towards the negative. Nafikiri ni vizuri sasa tunajua timeline ya mambo mbalimbali ingawa nafikiri baadhi ya tarehe zitachenji baada ya Hukumu ya Mahakama..

Mambo iko hapo mkuu!!!

By the way, with improved communications systems and road; i do not see the reasons why dividing constituents!!! Any mambo ya kutumia mawazo ya zamani kwenye karne nyininge.
Mungu Ibariki Tanzania
 
aisee.. CCM imewaathiri sana watu.. maana reactions za kwanza ni towards the negative. Nafikiri ni vizuri sasa tunajua timeline ya mambo mbalimbali ingawa nafikiri baadhi ya tarehe zitachenji baada ya Hukumu ya Mahakama..

usijifurahishe mwanakijj, kutokana na vyanzo vya uhakika, hakuna mgombea binafsi mwaka na katika uchaguzi huu. ni hayo tu wapendwa
 
Hivi hakuna namna ambayo tunaweza kuitumia kukataa kuongezwa gharama kwa kuongeza idadi ya majimbo?
 
Tatizo letu ni kufikiria siku zote wingi wa wabunge badala ya ubora na uwakilishi wa maana...Ukonga ina haja gani kuongezewa mwakilishi?? Jaji Bomani aliyasema haya hawakumsikiliza sijui km kelele zetu wenye uchungu na Tanganyika na wazawa wa kikweli kikweli tutakuja kusikilizwa???
 
Back
Top Bottom