Tarehe ya kuzaliwa na utabiri wa kesho yako

bonvize

JF-Expert Member
Feb 4, 2010
323
233
Sehemu ya Kwanza

Tarehe ya kuzaliwa uwa inabeba taarifa zote muhimu kuhusu maisha ya muhusika na hii ni kwa mujibu wa elimu ya namba (Numerology). Katika hatua ya mwanzo nitaanza kwa kuzungumzia kitu muhimu ambacho kinapatikana kwa kukokotoa tarehe, mwezi na mwaka wa kuzaliwa, kitakachopatikana katika ukokotozi huo kitaitwa Mzunguko wa maisha (Tafsiri Binafsi). Kuna mambo muhimu ya kuzingayia katika ukokotozi wa mzunguko wa maisha ambayo ni namba mama na namba kiongozi.

Namba Mama
Namba mama ambazo zitakuwa zikitumika katika uchambuzi ni 1,2,3,4,5,6,7,8,9, namba yoyote baada ya 9 inaweza kurudiswa katika namba mama. Zingatia mfano unaofuata
10=1+0= 1
27= 2+7= 9=
389= 3+8+9=20=2+0=2


Kila namba mama kuanzia namba 1 hadi 9 inakuwa imebebe nguvu maalum, na hiyo nguvu inakuwa imegawanyika katika pande mbili, nguvu chanya na nguvu hasi.

Namba Kiongozi
Namba kiongozi ni namba ambazo zina sifa maalumu, nazo ni 11 na 22, namaba hizi zinapojitokeza wakati wa kukokotoa uwa zinabaki kama zilivyo, zingatia mifano ifuatayo;
155= 1+5+5=11
949=9+4+9=22


Namba hizi zinakuwa zimebeba sifa za Namba Mama na Namba Kiongozi, zingatia mfano ufuatao;

155= 1+5+5=11=1+1=2
949=9+4+9=22=2+2=4


Wakati mwingine hizo Namba Kiongozi uwa zinaandikwa 11/2 na 22/4.



Sehemu ya Pili

Mzunguko Wa Maisha​
Mzunguko wa maisha ni funguo ya kufungua kile ambacho mwenyezi Mungu amekiweka ndani yako wakati wa kukuumba. Hii ni namba ya kudumu katika kipindi chako chote cha uhai, daima haitabadilika kwa kuwa inatokana na tarehe yako ya kuzaliwa.
Mzunguko wa maisha utakuwezesha kutambua mambo unayotakiwa kuyatimiza katika kipindi chako cha uhai kwa kuzingatia fursa na vipaji ambavyo Mungu amekuumba navyo. Mzunguko wa maisha utakuwezesha kwa urahisi kufanya maauzi kuhusu;
Uelekeo wa maisha
Kupanga na kutimiza Malengo
Mahusiano
Mipango ya mbeleni
Kazi ambayo itakufikisha katika kilele cha mafanikio

Hivyo basi Mzunguko wa maisha utatuwezesha kutambua mazingira ambayo yataambatana na fursa ambazo Mungu ameziumba kwa ajili yako.



Mzunguko wa maisha ni namba inayopatikana kwa kuzipunguza tarehe, mwezi na mwaka wa kuzaliwa hadi kufikia katika Namba Mama au Namba Kiongozi, mfano wa kwanza unahusu Namba Mama na wa pili unahusu Namba Kiongozi

Mfano wa kwanza 21/04/1990
Tarehe 21= 2+1 = 3
Mwezi 04= 0+4= 4
Mwaka 1990=1+9+9+0=19=1+9=10=1+0= 1

Baada ya kupata hizo Namba Mama kutoka katika tarehe ya kuzaliwa, mwezi na mwaka unazijumlisha zote;
3+4+1=8
Mfano wa pili 14/01/1985
Tarehe 14= 1+4 = 5
Mwezi 01= 0+1= 1
Mwaka 1985=1+9+8+5=23=2+3=5

Baada ya kupata hizo Namba Mama kutoka katika tarehe ya kuzaliwa, mwezi na mwaka unazijumlisha zote;
5+1+5=11

Sehemu ya 3

MZUNGUKO WA MAISHA 1
Mzunguko huu unahusika na wale wote ambao ukokotozi wa tarehe zao za kuzaliwa unaleta jibu la 1. Kitovu cha mtu wenye mzunguko wa maisha 1 ni kujitegemea, mtu mwenye huu mzunguko lazima ajifunze na kuweza kusimama kwa miguu yake miwili ili kutumia vipaji vyake katika kuzitumia vizuri fursa atakazokutana nazo katika kipindi cha uhai wake. Bila kujitegemea malengo yako hayawezi kufikiwa.

KAZI
Mwanasiasa
Mtaalamu wa maabara
Msanii

TABIA CHANYA
Afya njema
Uongozi
Utawala na usimamizi
Kujiamini
Ubunifu
Ugunduzi
Shahuku

TABIA HASI
Majivuno
Ubinafsi
Kutopenda ushirikiano
Kiburi
Unyanyasaji
Ukatiri
Hofu
Kukosa uvumilivu
Woga
Kukosa hamasa/Kutojikubali

Maelezo/Ushauri
Mtu mwenye mzunguko wa maisha 1, katika hatua za awali za mzunguko uwa rahisi kwake kuwa tegemezi kuliko kujitegemea. Mtu yoyote mwenye mzunguko wa maisha 1, kama atatumia vema tabia chanya ambazo Mungu ameziweka ndani yake ana uhakika wa kufikia kitovu chake ambacho ni kujitegemea.

MZUNGUKO WA MAISHA 2
Mzunguko wa maisha namba 2 una maana ya Mahusiano na Ushirikiano, Mtu mwenye mzunguko huu ni muhimu kutumia uwezo aliojaliwa na Mungu kwa maslahi mapana ya umma, ingawa mara chache mchango wake utajulikana kwa umma wote. Mambo ambayo wengine watatumia nguvu kuyakamilisha yeye ataweza kuyakamilisha kwa urahisi, mara nyingi uwezo wa mtu mwenye mzunguko huu uwa unatumiwa na watu wengine. Pia ni muhimu kujifunza namna ya kuweza kufanya kazi na watu tofauti, furaha ya mtu huyu ni kuona kazi inafanyika hata kama sifa watapata watu wengine.

KAZI
Katibu Muhktasi,
Msanii,
Mfanyakazi wa Viwandani,
Mwanadiplomasia,
Mwanamuziki,
Muimbaji.
Mfanyakazi katika sekta ya elimu
Mfanyakazi wa Umma.
VIPAWA

TABIA CHANYA
Kujali Hisia
Machale/Maguto
Ushirikiano
Dilpomasia
Kupangilia Mambo
Uaminifu
Urafiki
Ulezi
Mikakati
Mvuto wa Kimapenzi
Upole
Uwakilishi
Kujali

TABIA HASI
Kuona Haya
Kutojali
Woga
Utegemezi
Kutopenda ushirikiano
Kuficha/Kukosa hisia
Kuendeshwa na hisia
Kujifanya mjuaji
Kutokutimiza maono
Kulaumu


MAELEZO/USHAURI
Mtu mwenye mzunguko wa namba 2 ili aweze kufanikiwa anatakiwa kudhibiti hisia zake, lazima afanye shughuli ambayo haitakuwa na madhara katika hisia zake kali ivyo kutokuwa anaumizwa. Muhimi kujifunza kukabiliana na hisia za watu wengine ivyo kupunguza uwezekano wa kuumizwa. Hisia zake kali anaweza kuzitumia katika kujenga urafiki, mahusiano au shughuli za kidiplomasia.

Sehemu ya 4

MZUNGUKO WA MAISHA 3
Kitovu cha Mzunguko wa Maisha namba 3 ni kuonyesha furaha ya maisha, ni rahisi kukubalika na wengine endapo utakuwa muwazi na mchangamfu na mwenye furaha. Mwenye mzunguko huu lazima awe makini katika kuendeleza uwezo wake wa kimaono na kisanaa.


KAZI
Mwanasayansi
Mhasibu
Usimamizi wa Biashara
Mtaalamu wa kompyuta
Mtafiti
Mwandishi
Muigizaji
Mshauri wa kazi za sanaa
Msanii
Mkalimani

TABIA CHANYA
Kuburudisha
Mchangamfu
Afya njema
Mvuto
Kuona maono
Usanii
Welevu
Uwezo wa kuwasiliana
Kupokea ushauri

TABIA HASI
Kutokuaminika
Kukosa mvuto
Kukosa msimamo
Uharibifu
Kukwempa majukumu/Watu
Kutotimiza malengo
Kufanya mambo nusu nusu
Kutapanya
Chuki
Vijembe
Kuthibiti kwa manufaa binafsi
Kukasirika haraka
Kutokujiamini

MAELEZO/USHAURI
Mtu mwenye mzunguko wa 3 ana uwezo mkubwa wa kukamilishha mabo kiurahisi ambayo wa mzunguko mwingine angeyakamilisha kwa ugumu ili kufanikisha hilo ni muhimu kuwa anaweka wazi matatizo yake kwa watu anaowaamini
WATU MASHUHURI

MZUNGUKO WA MAISHA 4
Mtu mwenye mzunguko wa maisha 4, lazima afuate mpangilio na mifumo rasmi katika kila jambo analotaka kulikamilisha kwa ufasaha. Mtu wa mzunguko huu lazima ujue kila kitu katika maisha kina ukomo wake, ukomo wa kimazingira, mitizamo na kimwili. Ni muhimu kulitambua hili kwa kuwa mara nyingi uhisi kuwa ni yeye tu ukutwa na mikwamo ya kikomo ukilinganisha na watu wengine.
KAZI
Mfanyabiashara
Mhunzi
Mtaalamu wa mashine
Meneja
Mwalimu wa sanaa, michezo na kujenga mwili
Mwanamichezo wa kulipwa
Technician
Machinist
Mwandishi wa vitabu na majarida
Mhasibu
Afisa Mikopo
Afisa wa Bank

TABIA CHANYA
Mfanyakazi hodari
Kutegemewa
Kupangilia mambo
Mzalendo
Kupenda familia
Mwema
Kutopindisha mambo
Mantiki
Umakini
Uangalifu


TABIA HASI
Kujisikia
Kukosa msimamo
Kutokuwajibika
Kujihami
Kukwepa majukumu
Kutokushaurika
Kudhibiti,
Kukosa ubinadamu
Udhalilishaji
Kutopenda mabadiliko
Ugomvi/ Majibizano
Kuficha hisia
Hofu
Kufanya kazi kupita kiasi

MAELEZO/USHAURI
Ni jambo gumu kwao kukubali kuwa kila jambo lina ukomo wake, lakini ni muhimu kutatumbu kuwa mafanikio ya mtu mwenye Mzunguko wa Maisha 4 yatafikiwa kwa kutambua uwepo wa ukomo katika kila jambo. Ukomo kwako si lazima pia uwe ukomo kwa mwingine.

Sehemu ya 5

MZUNGUKO WA MAISHA 5
Mtu mwenye mzunguko wa maisha 5, lazima ajifunze kutumia uhuru wake katika namna chanya ya kujenga na si kubomoa. Maisha yanakuwa na fursa nyingi kwa mtu mwenye mzunguko huu zikiambatana na mabadiliko ya mara kwa mara wakati mwingine bila kutarajiwa. Mtu huyu ana uwezo wa kufanya kazi nyingi kwa ufanisi kutokana na vipaji ambavyo Mungu amemjalia, lakini ni muhimu kuchambua fursa zenye manufaa na kuwekeza nguvu na si kuwekeza nguvu katika kila fursa. Ni lazima kuwa makini ili usipoteze muda katika anasa za kimwili katika vitu kama , chakula, mapenzi, ulevi na madawa ya kulevya.

KAZI
Mauzo
Mwanasiasa
Muigizaji
Mwandishi
Msanii
Mjasiriamali
Mbunifu
Mgunduzi
Usafirishaji
Malazi
Shughuli za kijamii

TABIA CHANYA
Uhuru/Kujitawala
Kubadilika kulungana na mazingira
Mvuto wa Kimapenzi
Mchangamfu
Kuburudisha
Usanii
Huruma
Shahuku
Kupenda kujaribu mambo mapya
Kuvuta hisia za watu
Kutimiza mataka ya mwili

TABIA HASI
Kufanya Jambo bila tafakari ya kina
Kutokuwajibika
Kudadilika badilika
Kujijali/kujali kupita kiasi
Kukosa msimamo
Kutokuwa mwaminifu
Woga
Kuficha ukweli/Uongo
Urafi
Kuchanganyikiwa kwa kutotimiza malengo
Kukosa utulivu

MAELEZO/USHAURI
Mtu mwenye mzunguko wa maisha huu ni muhimu kuchanganua kila fursa anazokutana nazo ili aweze kuwekeza nguvu na maarifa katika fursa zenye tija kwako, kama atakosa umakini kila siku utakuwa ukihama kutika fursa moja kwenda nyingine bila kupata matokeo chanya katika fursa iliyopita. Mara nyinine utokea kwa mtu mwenye mzunguko huu kusita katika kutumia uhuru alionao au kufurahia uhuru bila kuutumia katika namna ya kujenga. Kutokana na vipaji alivyoumbwa navyo na kukutana na fursa kila wakati uwa ni vigumu mtu huyu kutambua fursa zenye tija na zisizo na tija.


MZUNGUKO WA MAISHA 6
Mtu mwenye mzunguko huu lazima ajifunze kuyakubali majukumu kwa kuwa Mungu amemjalia uwezo mkubwa wa kusaidia na kufariji wengine pale inapohitajika. Tegemea watu wengi kuja kwako ili kupata msaada na faraja zaidi ya vile unavyofikiri ivyo ni muhimu kuyakubali majukumu na kujifunza namna kusaidia familia, ndugu na marafiki. Ni muhimu kujifunza kujitoa katika urafiki na matendo ya upendo kwa kuwa kile unachopanda ndicho utakachovuna, ni muhimu kutofautisha kati ya kusaidia na kuingilia mambo ya wengine.

KAZI
Tabibu
Msanii
Mbunifu
Uimbaji
Uigizaji

TABIA CHANYA
Upendo
Uwajibikaji
Upole
Vitendo
Huruma
Mvuto wa kimapenzi
Ulezi
Uwezo wa kujadiliana
Ushirikiano


TABIA HASI
Kujiona sahihi wakati wote
Kutokuwajibika
Kuthibiti kwa manufaa binafsi
Usiri
Kukasirika haraka
Kufatilia yasiyokuhusu
Kuwa na hasira
Kukosa furaha
Kukosa misimamo
Ufukara
Kutokukamilisha mambo aliyoanzisha

MAELEZO/USHAURI
Kuna nyakati ambazo mtu mwenye mzunguko huu uchoshwa na mzigo wa majukumu ambayo anayo, lakini kikubwa cha kutambua ni kuwa wengi uja kwake kwa kuwa hawawezi kujisaidia wenyewe. Mtu huyu wakati mwingine uwa tayari kujitoa sadaka kwa ajili ya wengine, ni jambo la muhimu kuangalia kuwa majukumu yasizidi uwezo wako kiasi kwamba ushindwe kutimiza malengo yako.

Sehemu ya 6

MZUNGUKO WA MAISHA 7
Mtu mwenye mzunguko wa maisha namba 7 lazima ajifunza kupata amani katika ufahamu wake ambayo upatikana kwa kujitambua mwenyewe. Lazima kulijua jambo kiundani kabla ya kufanya maamuzi pia ni vema kuwekeza muda wa kutosha katika kujitambua kiundani, kuamini maono yake katika kuitafuta busara. Mtu huyu anatakiwa kutotumia nguvu kubwa katika kutafuta anasa za dunia au kimwili, cha muhimu ni kujikita katika masuala ya kiroho. Ni muhimu kujitengea muda wa kuwa pekeyako ivyo kuweza kutafakari mabo kwa kina. Ni muhimu kusubiri fursa ambazo zitakuwa na manufaa katika upand wako na si kutumia kila fursa inayojitokeza

KAZI
Mwanasheria
Mwanafalsafa
Mwalimu
Mwanasayansi
Fundi seremala
Uchongaji wa Vinyago
Kiongozi wa dini
Mtaalamu wa wanyama/mimea
Muuza bucha
Mfanyakazi wa machinjio.


TABIA CHANYA
Welevu
Uwezo wa kutafakari
Usomi
Uchunguzi
Maono
Unyenyekevu
Busara
Kutafuta ukweli
Kuheshimiwa
Kufanya kazi kiusahihi
Kuelewa jambo kwa mapana
Kuchambua mambo

TABIA HASI
Woga
Kujitenga
Mashaka
Kudhibiti kwa njia ovu
Majibizano
Kutokuaminiwa
Kuaminisha
Hasira za ndani
Hisia zilizojificha
Udanganyifu


MAELEZO/USHAURI
Changamoto kubwa kwa mtu mwenye mzunguko huu ni kushindwa kutega muda wa kukaa pekeyake na kutafakari mambo ya kiroho na ivyo kujikuta anakuwa mhanga wa anasa za dunia. Jambo la muhimu ni kuweza kutumia uwezo wake wa kiroho katika kufanikisha mambo yake tofauti.

MZUNGUKO WA MAISHA 8
Mtu mwenye mzunguko wa maisha 8 lazima ajifunze kuridhika na mahitaji ya kimwili na anasa za dunia. Mtu huyu uwa na ndoto na maono machache sana, kitu alichojaliwa ni uwezo wa kujituma katika kutafuta fedha kwa namna yoyote ili kupata nguvu inayoletwa na uthibiti wa fedha. Mtu wa mzunguko huu uwa wana amani zaidi wanapokuwa na wadhifa wa juu katika maisha

KAZI
Uongozi katika biashara
Nafasi za juu za utawala
Mfanyakazi wa benki
Biashara ya usafirishaji
Nahodha wa meli/Ndege
Mwalimu
Muuguzi
Muigizaji
Mtaalamu wa Kifedha
Mhudumu wa wanyama
Dalali wa bima/hisa



TABIA CHANYA
Ubobezi
Kuelewa jambo kwa undani
Kusimamia jambo
Mafanikio
Uongozi
Kupenda mamlaka
Ugunduzi
Kusimamia maneno yao
Kukumbatia jambo
Ushawishi
Ukinyonga
Kusaidia

TABIA HASI
Kukosa uvumilivu
Moyo mgumu
Anasa za dunia
Udhalilishaji
Kujisikia/Majivuno
Mwepesi wa kuhukumu
Kuchanganyikiwa kirahisi
Kupenda madaraka
Kudhibiti
Usumbufu
Matumizi mabaya ya Fedha
Majibizano
Kupenda anasa

Sehemu ya 7

MZUNGUKO WA MAISHA 9

Mtu mwenye mzunguko huu wa maisha ni lazima ajifunze kujitoa katika kutimiza mahitaji ya watu wenye uhitaji. Lakini ni lazima asitegemee kupata makubwa kama malipo ya kujitoa kwake.

Ni mtu wa shughuli za kijamii na kujitoa kwa wengine, kujitoa kwa mtu huyu kunaweza kujitokeza kwa namna mbili
Kusaidia wengine
Kujitoa mwenyewe katika kujifunza zaidi kibunivu

KAZI
Kazi zote zinazohusiana na dini
Kazi zinazohusiana na elimu
Mtafiti
Tabibu
Mshauri
Msanii

TABIA CHANYA

Magutu/Machale
Ubunifu
Mvuto wa Kimahaba
Hisia
Kusaidia
Kupenda masuala ya kiroho
Fikra pevu
Kuona mbali
Kujali
Kupenda kujua zaidi
Kufanya mambo mengi kwa pamoja
Kuvutia
Mpole/Mnyenyekevu
Kuona maono

TABIA HASI

Utegemezi
Kutojikubali
Kutojiamini
Kukosa malengo
Ndoto za linacha
Kukosa maono
Kujiwekea vikwazo
Kutopea
Kuwa mtu si wa vitendo
Kutapanya
Kukimbia majukumu
Kusitasita
Kupenda anasa za dunia

MAELEZO/USHAURI

Mtu mwenye mzunguko wa namba 9 ana nafasi kubwa ya kufanikiwa katika kutafuta wadhifa, kujenga urafiki na kuasambaza upendo. Kujitoa kwako lazima kuwe ni kule kusikotarajia malipo ya aina yoyote.


MZUNGUKO WA MAISHA 11

Mtu mwenye mzunguko wa namba 11 ni lazima uwe na uelewa mpana wa masuala ya kiroho na mahusiano yake katika maisha yetu ya kila siku hapa duniani.

Mtu mwenye mzunnguko huu ana faida ya ziada katika kuelewa na kufahamu mambo ukilinganisha na watu wa mizunguko mingine.

Jambo la kuzingatia ni kuwa huu uelewa na ufahamu vinachukua muda ili kujijenga na vikishajijenga mtu mwenye mzunguko huu anakuwa na uwezo wa kukamilisha mambo ambayo watu wa mizunguko mingine hawawezi kuyakamilisha kwa urahisi.

Mtu mwenye mzunguko huu pia ni lazima kujifunza kuamini na kuboresha uwezo wake wa kupata maono uwe unaongozwa kiroho.

Lazima ujitambue kuwa wewe ni njia katika kuhakikisha kuwa unainua maisha ya watu wengine kwa kuwapatia mwanga kupitia uwezo mkubwa wa ufahamu na uelewa wa mambo.

KAZI
Mwalimu
Kiongozi wa dini/Mshauri wa kiroho
Mbunifu
Mgunduzi
Usanii
Mshauri

TABIA CHANYA

Kujiamini
Upole
Uchangamfu
Ukinyonga
Kujali hisia za wengine
Msikivu
Kuona maono
Kuwa na machale/Magutu
Kutafuta ukweli

TABIA HASI

Majivuno
Kukosa heshima
Kujitenga na jamii
Kukimbia majukumu
Kupangilia uongo
Hisia kali
Kutokushirikiana
Utegemezi
Kupenda kupita kiasi

MAELEZO/USHAURI

11 ni namba maalum, lakini ni wachache sana wanaoweza kutumia uwezo uliopo katika mzunguko wa maisha 11 kwa kuwa uwa hawapendi kujihusisha na ulimwengu wa kiroho.

Kutopenda kufahamu ulimwengu wa kiroho uleta tabu katika kufahamu na kuelewa uhusiano wake na ulimwengu wa kawaida.

Mtu huyu uwa na uwezo mkubwa lakini ni mara chache uweza kutumi uwezo alionao katika vitendo.

Kutokana na kuwa na hisia kali pamoja na ufahamu anaweza pata tabu kubwa ya msongo wa mawazo endapo hatakuwa hana uwelewa mkubwa wa mambo ya kiroho.

Ni watu wachache wenye mzunguko wa 11 ndio uweza kufikia kelele cha matumizi ya uwezo ambao Mungu amewaumba nao.


MZUNGUKO WA MAISHA 22

Mtu mwenye mzunguko wa namba 22 lazima aweze kutumia ipasavyo uwezo wake wa kifikra katika kufanikisha mambo makubwa.

Mtu mwenye mzunnguko huu ana faida ya ziada katika kuelewa na kufahamu mambo ukilinganisha na watu wa mizunguko mingine hivyo kumfanya awe na uwezo wa ziada katika kuanikisha jambo lolote endapo ataliwekea mkazo.

Pamoja na uwezo alioumbwa nao ni lazima mtu mwenye mzunguko huu wa maisha ajifunze kutumia nguvu zake katika namna ya kujenga na si kubomoa.

Mtu huyu mafanikio yake yapo katika kufanya mabo yenye maslahi mapana kwa kwa jamii na si kutanguliza ubinafsi.

KAZI
Mwanasiasa
Mwanadiplomasia
Mfanyabiashara
Mtaalamu wa computer
Mwalimu

TABIA CHANYA

Welevu
Mchangamvu
Ubunifu
Uhalisia
Kufanikisha ndoto
Ugunduzi
Upambanaji

TABIA HASI
Ulafi
Majivuno
Kutokujali hisia za wengine
Kutoridhika
Ubinafsi
Kuvunja sheria
Kupenda anasa
Kukosa uadirifu
Kujiona bora
Kuthibiti ili kujinufaisha
Kukosa shukrani

MAELEZO/USHAURI

Inachukua muda mrefu kwa mtu mwenye mzunguko huu kufanikisha mambo makubwa kwa kutumia uwezo ambao Mungu amemuumba nao kwa kuwa mara nyingi ujikuta katika msongo wa mawazo kutokana na nguvu kubwa ambayo ameumbwa nayo.

Uwezo mkubwa ambao ameumbwa nao si kificho upo wazi kwa watu, ivyo watu ushangaa pale anaposhindwa kufanikisha mambo makubwa.


Siku nyingine nitamalizia mzunguko wa maisha 33, pia naandaa masomo yafuatayo;
√ Maajabu ya namba 9
√ Miduara ya maisha
 
Tarehe ya kuzaliwa uwa inabeba taarifa zote muhimu kuhusu maisha ya muhusika na hii ni kwa mujibu wa elimu ya namba (Numerology). Katika hatua ya mwanzo nitaanza kwa kuzungumzia kitu muhimu ambacho kinapatikana kwa kukokotoa tarehe, mwezi na mwaka wa kuzaliwa, kitakachopatikana katika ukokotozi huo kitaitwa Mzunguko wa maisha (Tafsiri Binafsi). Kuna mambo muhimu ya kuzingayia katika ukokotozi wa mzunguko wa maisha ambayo ni namba mama na namba kiongozi.

Namba Mama
Namba mama ambazo zitakuwa zikitumika katika uchambuzi ni 1,2,3,4,5,6,7,8,9, namba yoyote baada ya 9 inaweza kurudiswa katika namba mama. Zingatia mfano unaofuata
10=1+0= 1
27= 2+7= 9=
389= 3+8+9=20=2+0=2


Kila namba mama kuanzia namba 1 hadi 9 inakuwa imebebe nguvu maalum, na hiyo nguvu inakuwa imegawanyika katika pande mbili, nguvu chanya na nguvu hasi.

Namba Kiongozi
Namba kiongozi ni namba ambazo zina sifa maalumu, nazo ni 11 na 22, namaba hizi zinapojitokeza wakati wa kukokotoa uwa zinabaki kama zilivyo, zingatia mifano ifuatayo;
155= 1+5+5=11
949=9+4+9=22


Namba hizi zinakuwa zimebeba sifa za Namba Mama na Namba Kiongozi, zingatia mfano ufuatao;

155= 1+5+5=11=1+1=2
949=9+4+9=22=2+2=4


Wakati mwingine hizo Namba Kiongozi uwa zinaandikwa 11/2 na 22/4.


Itaendelea...........
Sa si ungejiandaa full kabisa, badala yake unakuja nusu nusu.
 

Similar Discussions

24 Reactions
Reply
Back
Top Bottom