Tarehe ya kutoka, bei na orodha ya nyimbo zilizomo kwenye album ya ‘A boy From Tandale’ ya Diamond, zatajwa

Rosh Hashannah

JF-Expert Member
Sep 13, 2017
3,334
2,000
Hakuna ubishi kwa mwaka huu mashabiki wengi wa muziki walikuwa wanasubiria kwa hamu kuipokea album ya ‘A Boy From Tandale’ ya msanii maarufu zaidi Tanzania, Diamond Platnumz ukweli ni kwamba album hiyo haitatoka mwaka huu tena badala yake itatoka mwakani.

Album ya ‘A Boy From Tandale’ itatoka tarehe 12 Januari 2018, na itakuwa na nyimbo 18, ambapo zaidi ya wasanii 13 kutoka Tanzania, Nigeria na Marekani watasikika kwenye album hiyo.

Wasanii hao ni Vanessa Mdee, P-Square, Mr Flavour, Young Killer, Tiwa Savage, Rayvanny, Davido, Jah Prayzer wengine ni Miri Ben-Ari, Omarion, Rick Ross, Ne-Yo na Morgan Heritage wote kutoka Marekani.

Kupitia mtandao wa iTunes unaweza ku-order sasa hivi kabla haijatoka album hiyo kwa dola 6.99 sawa na tsh 15,666/=. Kumbuka bei hiyo ni kwa wale watakaonunua album hiyo kabla ya kutoka tar 12 Januari, 2017.

Tazama orodha ya nyimbo hizo hapa chini;
 

Rosh Hashannah

JF-Expert Member
Sep 13, 2017
3,334
2,000
List ya nyimbo
 

Attachments

 • 24955410_2007911386144567_4529900488974427531_o.jpg
  File size
  159.9 KB
  Views
  62

joseph1989

JF-Expert Member
May 4, 2014
6,408
2,000
Sasa hapo ndio, utawajua mashabiki wa kweli sio wale wazee wakukimbizana YouTube kuongeza view, huku ukisubiri bekaboy aiconvert video na kuwa audio, ili udownload wazee wa vitonga .Ila diamond platnumz atafute njia ya kuuza hiyo album kwa njia ya Mpesa, tigopesa na airtel money ,wengine hizo VISA au MasterCard hawana .
 

Root

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
37,666
2,000
Kumbe ile Universal Music Group ni ile ya Afrika Kusini

Anyway hongera wenye kununua watanunua, sisi wengine tutabaki sikia na kukopi
 

Rosh Hashannah

JF-Expert Member
Sep 13, 2017
3,334
2,000
Sasa hapo ndio, utawajua mashabiki wa kweli sio wale wazee wakukimbizana YouTube kuongeza view, huku ukisubiri bekaboy aiconvert video na kuwa audio, ili udownload wazee wa vitonga .Ila diamond platnumz atafute njia ya kuuza hiyo album kwa njia ya Mpesa, tigopesa na airtel money ,wengine hizo VISA au MasterCard hawana .
Yeah
 

Maberere

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
318
225
Hiyo orodha ya nyimbo ipo wapi?
 1. Hallelujah (feat. Morgan Heritage)
 2. Waka (feat. Rick Ross)
 3. Baikoko
 4. Pamela (feat. Young Killer)
 5. Iyena (feat. Rayvanny)
 6. Kosa Langu
 7. Nikuone
 8. Baila (feat. Miri Ben-Ari)
 9. Sijaona
 10. African Beauty (feat. Omarion)
 11. Eneka
 12. Fire (feat. Tiwa Savage)
 13. Marry You (feat. Ne-Yo)
 14. Number One (feat. Davido) [Remix]
 15. Nana (feat. Flavour)
 16. Kidogo (feat. P-Square)
 17. Amanda (feat. Jah Prayzah)
 18. Far Away (feat. Vanessa Mdee)
 

Mtarban

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
3,774
2,000
Albamu ya kipuuzi sana! Kama ni kumsapoti tulishamsapoti kwa nyimbo hizohizo sasa bado anafanya ujanja wa kuziunganisha pamoja eti album. Mi nikajua anakuja na album ya vitu vipya! Poor diamond
 

Sambusa kavu

JF-Expert Member
May 4, 2015
700
1,000
Albamu ya kipuuzi sana! Kama ni kumsapoti tulishamsapoti kwa nyimbo hizohizo sasa bado anafanya ujanja wa kuziunganisha pamoja eti album. Mi nikajua anakuja na album ya vitu vipya! Poor diamond

Kwani mmesahau albamu za wabongo uwa zinakuwa na nyimbo ngapi jamani??....mara nyingi utakuta nyimbo 9 mpaka 11 albau nzima..

Kwenye iyo list naona kuna mapini kama 9 hivi bado hayajasikika kabisaaa(Baikoko,pamela,iyena,Nikuone,baila,sijaona,african beauty,amanda na far away)...kwa mtu atakaelalamika kwenye hii albamu itabidi apimwe mkojo!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom