Freetown
JF-Expert Member
- Apr 6, 2008
- 883
- 73
Mkuu ngonalugali, sikubaliani na maelezo yako!
Ukweli ni kwamba, mbegu za kiume (yaani Y) ni nyembamba kwa umbile na ni faster ukilinganisha na zile za kike (yaani X).
Hii ni kwa sababu ya ukweli kwamba, 'wembamba' wa umbo la mbegu za kiume huziwezesha kuogelea kwa urahisi kuliko zile za kike katika yale majimaji ya uke wa mwanamke. Hii inamaana kwamba, kama yai la mwanamke litakuwa tayari kwenye sehemu ya kurutubishia (yaani kama mwanamke atakutana kimwili na mwanaume siku ile ya mimba) basi mbegu moja tu ya kiume itakayotangulia kulifikia yai itaweza kurutubisha na kisha yai huvaa koti gumu ambalo huyazuia mamillioni ya mbegu zingine za kiume zilizochelewa pamoja na zile za kike zisiingie ndani ya hilo yai badala yake hubaki nje ya yai zikisubili kufa. Mtoto wa hii mimba ni wa kiume, yaani YX.
Kama mwanamke atakutana na mwanaume siku 3 kabla ya siku ya mimba (fertile day) basi kuna uwezekano mkubwa wa kuzaliwa mtoto wa kike, yaani XX. Hii ni kwa sababu zile mbegu za kiume zitaogelea kwa kasi kubwa lakini zikifika kwenye sehemu ya kurutubishia hazitalikuta lile yai kwa sababu litakuwa halijafika sehemu yake. Zitasubili kwa siku mbili kisha zinakufa! Mbegu za kike zitaogelea polepole mpaka ile sehemu ya kurutubishia kisha zitakaa hapo kwa siku 3 zikilisubili lile yai lifike. Likifika tu ndani ya hizo siku 3 basi mbegu moja tu ya kike itakayochangamkia tenda italirutubisha yai hilo na kutengeneza mtoto wa kike, yaani XX.
Kama itatokea kwamba mbegu zaidi ya moja zitafanikiwa kulirutubisha yai, basi yai hilo litagawika katika vipande vyenye idadi sawa na mbegu zilizorutubisha na kupata watoto mapacha wasiofanana! Kwa mfano, kama mbegu 2 zitarutubisha yai basi watazaliwa mapacha wawili wasiofanana. Na kama mbegu 6 zitarutubisha yai, basi watazaliwa mapacha 6 wasiofanana; kitu ambacho hata hivo ni nadra sana kutokea, yaani mapacha 6.
Kama mbegu moja itarutubisha yai halafu muungano huo ukawa na idadi ya chromosomes zinazozidi kiwango kinachotakiwa, basi yai hilo litagawika sehemu mbili zilizo sawa na kupata mapacha wawili wanaofanana na ambao ni wa jinsia moja kufuatana na mbegu ipi kutoka kwa mwanaume ilirutubisha yai, ya kiume au ya kike.
very educative. Asante sana kwa mchango wako