Tarehe kama ya leo miaka miwili iliyopita watanzania tulifanya maamuzi ya kusimika utawala uliopo

Miaka miwili iliyopita taifa lilifanya uchaguzi mkuu wa kuchagua raisi wa nchi, wabunge na madiwani, maisha ya sasa hivi ya raia wa Tanzania ni matokeo ya uamuzi wa kura yake siku ya jumapili tarehe 25/10/2015. Katika kipindi cha muda mfupi inasemekana ukusanyaji wa mapato umeongezeka na pia uchumi wa nchi unakua na kuimarika. Cha kujiuliza ni namna gani tumejiandaa kikamilifu kuhakikisha tunakuwa na taifa linaloelekea uchumi wa kati, taifa la viwanda, elimu, afya na miundombinu iliyo bora.? Bila kuwa na kizazi cha watu waoga na wanaojipendekeza.

Tunapokuwa tunaiongelea zaidi sekta ya viwanda nchini ni vizuri kuwa na mipango stahiki na endelevu kuanzia mtaani, shuleni, vyuoni mpaka serikalini kuhusu namna sahihi ya kufufua viwanda vilivyokufa na kuviendeleza na kuongeza vingine vipya, na hii itawezekana endapo tu tutaamua kuwaacha wataalamu wenye ujuzi kufanya kazi zao bila kuleta siasa katika maarifa.

Elimu, elimu, elimu, maamuzi makini, ninachokiamini elimu bure itakuwa na manufaa makubwa kama itatusaidia kutatua changamoto zinazotukabili nchini. Hayati baba wa taifa alipata kusema maneno haya, namnukuu "Acha watu wa America na Ulaya waende katika sayari za mbali, ila sisi wa Africa tupeleke maji ya bomba kwa wananchi"

emmaloy72@gmail.com
+255 656 629352
Emmanuel...@Public Figure (PF)
 
Najuta kwa uamuzi wangu wa kumpigia kura magu...
Maana vyuma vimekaza kweli nchi inaliwa ma wachache kama bashite...

Lkn sikuwa na option kwani bora magufuli kuliko mzee Wangu Lowasa na genge lake la wezi
 
Nawakumbusha tu ndugu zangu kwamba tarehe kama ya leo miaka miwili iliyopita tulimchagua rais aliyepo madarakani!!! Tuchukue muda kumuombea
 
Nawakumbusha tu ndugu zangu kwamba tarehe kama ya leo miaka miwili iliyopita tulimchagua rais aliyepo madarakani!!! Tuchukue muda kumuombea
unashindana na agizo la jeshi la polisi marufuku kuombea watu,huo ni uchochezi, iwe siri yako tu
 
Kikwete huku anachekacheka km kawaida yake bila stress yeyote alisema "mlisema mimi mpole sasa nimewaletea chuma" *****....mlitaka maendeleo tulieni muone mbilinge mbilinge la kuyatafuta maendeleo..
 
Jamani acheni uongo ni miwili tu?it feels like four already duh,kwahyo bado mitatu?vurugu zote hz na ugumu huu ndan ya miaka miwili tu?
 
Staki kukumbuka tulivolala kituoni kulinda kura za Mbunge wetu Kubenea. Kila alieingia na kutoka kituoni tulimhoji na kumsachi pale Ubungo Kisiwani
 
bb483ef72e0372139a565be0f5f28d57.jpg

Ni miaka miwili sasa imepita tokea nilipomshudia Ndugu John Pombe Magufuli akiwa anazinadi Sera za chama chake cha mapinduzi

Sikuwahi kumpenda Magufuli kutokana na chama ambacho alikuwa anakiwakilisha katika mbio zake hizo za kupokezana kijiti cha Magogoni

Nilimuona mgombea huyu kama wenzie wanne ambao watanzania walikuwa wamewaamini nakuwakabidhi madaraka makubwa yakututawala sisi watanzania ambao tumekuwa tunaishi kama wakimbizi ndani ya taifa letu

Nilivutiwa sana na Ahadi ambazo mgombea huyu alikuwa akizitoa katika majukwaa mbalimbali nilimuona akitumia muda mrefu kuwashawishi wapiga kura kumchagua kitu kilichonipa imani kuwa bwana huyu hakuwa na uhakika wa kushinda katika nafasi hiyo kitu kilicho mfanya kukosa confidence jukwaani nakujikuta akiahidi kurasa za ahadi zilizokosa number

Siku ambayo nilimuona Bwana huyu kuwa anauchu tu wa madaraka ni siku ambayo aliruka kutoka katika gari lake nakuacha kituko kwa wapambe wake huku akiwahi jukwaaani kuongea na umati uliovaa magwanda ya kijani yaliopambwa kwa Nembo ya Jembe na Nyundo..

Sauti za shangwe zilikuwa ni burudani tosha kwetu wangaa macho hasa zile sauti zilizobeba kibwagizo cha CCM ni ile ile number one
Wapinzani mtaisoma number..
Hakika sikufahamu hizo number zilizokuwa zikimaanishwa na nguli wa dance la chama marehe Kolimba.

Kilichonivuta zaidi ni pale Bwana huyu alipo amua kutumia kibwagizo kilichokuwa kinatumiwa na wapinzani uchwara katika uchaguzi ule kibwagizo cha Magufuli four Change yani M4C

Hii ilikuwa ikitumiwa na jamaa wa Chadema kupitia mgombea wao alieasi kutoka chama cha Mizimu nakuamua kupata mapumziko ya heshima kwenye kambi hii ya wapinga hoja..

Magufuli 4 change imenikaa kila uchao maisha yangu yanazidi kuandamwa nyota ya mafanikio katika nchi hii inazidi kufunikwa tu na moshi wa Magufuli for change nimejitahidi kuzima moto ulio washwa na bwana huyu kupitia vifaa vyote vya kuzimia lakini Nguvu yake inalingana na lile Bomu la Hiroshima nchini Japani..

Magufuli for change nilitegemea ongezeko la ajira katika sekta za uma na sekta binafsi lakini kinyume chake ongezeko la watu kupoteza ajira ni zaidi ya 75% nchini Tanzania

Magufuli for change imeua sekta ya UJENZI mafundi uaashi wamegeuka vinyozi idadi ya watu wanaopanda na vibegi mgongoni kwenye daladala imeshuka..

Magufuli for change imeua biashara ya mabasi yaendayo mikoani
Magufuli 4 change imefuta private schools kitu ambacho kimepunguza ubora wa elimu sababu wenye shule hizo wanashindwa kuajiri walimu wazuri kutokana na mlundikano wa kodi katika shule zao..

Magufuli 4 change imeua sekta ya bandari kutokana na watendaji wengi wa idara ya mapato kukosa uzoefu katika ukokotoaji wa kodi kwa mizigo inayoingizwa nchini..

Magufuli 4 change imeua vyuo vikuu nchini kwa kuwapa wahadhiri vyeti vya PhD vinavyotokana na msaada wa Google.

Magufuli for change imeua morality kwa watu ambao wangependa kuikosoa serikali yao pale inapochemka

Magufuli for change imekosa ubunifu kama ilivyo kwa timu za Simba na Yanga ambazo miaka zaidi ya 65 hazimiliki hata uwanja wake wa mazoezi..

[HASHTAG]#M4C[/HASHTAG] Down:
By Nyandutwa
 
Hongera watanzania na JPM kwa ajili ya siku hii muhimu katika democrasia ya Tanzania katika kubadilisha uongozi wa nchi
 
Ili kula bata inakupasa kuwa ama zero brain, uwe mwenye PhD na kuitwa profeseri au uwe shango. Hapo aaah utakula mpk uwembeve
 
Back
Top Bottom