Tarehe kama ya leo miaka kadhaa nyuma

Lumbi9

JF-Expert Member
Oct 12, 2014
8,563
11,799
Kipindi hiko ndo naanza maisha ya kujitegemea, nikapanga nyumba flani' uswazi, nilimkuta mama mwenye nyumba, binti yake aliyepo kidato cha tatu(kipindi hiko binti wa kidato cha tatu mkubwa sio kama hawa wa sasa) na mdogo wa kike tena. Walikuwa wanajiweza kiuchumi sababu mama alikuwa na biashara zake anafanya.

Ishu ilikuwa ni mapenzi ya bintiye kwangu, alikuwa akinipenda kweli lakini mimi sikuwa na mpango naye kwanza, alikuwa nwanafunzi pili, sikutaka uhasama na mamaye ukizingatia ndo kwanza naanza kujitegemea. Nikawa namkwepa binti, hilo halikumsumbua tatizo lilianza nilipoanza kuingiza wanawake mle ndani, akawa anaona wivu.

Alipochoka na hayo akanifuata akaniuliza, hivi unapenda mwanamke wa aina gani? Nikamwambia anayejiheshimu tu, akaniambia, kujua kama anajiheshimu ni mpaka ukae naye japo hata kwa masaa mawili, namaanisha umekutana na mwanamke ghafla unapenda nini, nikampa sifa za kawaida walizonazo wanawake wengi maana sikujua lengo lake ni nini kwa wakati ule. Akaniuliza, kwa hiyo mimi sina sifa hizo? Nikamwambia unazo zote na zaidi, kwani vipi, akanambia naona kila siku unaingiza wanawake zako tu ina maama hujui kama nakupenda au dharau? Sasa kama ni dharau mimi nitakufanyia makusudi na hutonisahau, UTAHAMA HUMU.

Siku hiyo nipo ghetto nishashiba ugali wangu nimetulia na kibukta, nyu.mba ipo kimya kila mtu na mishe zake, nikasikia hodi kufungua dada mamu, akaingia ndani, tumekaa kama dakika tatu hadi tano akatoka nduki na chupi tu huku tenge kaliacha ndani akilalamika nambaka, nikapaniki, mama katoka anauliza vipi binti anasema nilikuwa natoka msalani kaka p akaniita kumbe alikuwa anataka kunibaka, mama kaingia ndani mikono kiunoni kuchukua tenge kanikuta na bukta, akaamini, akaenda kwake akaja na hela akanipa akaniambia, naomba utafute nyumba uhame katika nyumba yangu akaondoka.

Tarehe kama ya leo nilianza mkataba mwingine katika nyumba nyingine, kweli mpaka leo sijamsahau yule binti kama alivyoniahidi.

peterchoka
 
hahahaaa...watoto wa wenye nyumba na wenye nyumba wenyewe wana vituko..

Ila na wapangaji pia....!!!

Juzi mpangaji wangu kanitokea aiseehh...nafkiria kumpa notisi mkataba ukiisha...!!

Huyo mpangaji jasiri sana
Hata kuogopa au kuwaza litakalotokea hajawaza kajilipua tu
 
Haha inaonekana hako kabint kalikuwa ni na so ugly ndio maana ulikazembea.
 

Huyo mpangaji jasiri sana
Hata kuogopa au kuwaza litakalotokea hajawaza kajilipua tu
Yaani nilichoka sana... halafu ananiita sista...!

Na hivi nikiwa home najiachia....!!

Akanipigia simu tuonane nilchekaaaa...

Sasa dawa notisi tu!
 
hahahaaa...watoto wa wenye nyumba na wenye nyumba wenyewe wana vituko..

Ila na wapangaji pia....!!!

Juzi mpangaji wangu kanitokea aiseehh...nafkiria kumpa notisi mkataba ukiisha...!!
sasa unataka kumpa notsi kisa kakutongoza? kwan cha ajabu kipi? si ombi tu ni hiari kukubali au kukataa tatizo nini? angetaka kukubaka sawa.
 
Nampa notisi kwa sababu anabadili sana wadada mpk kero then pale home watu wanapaheshimu sana

Mpk juzi nimeitwa kupewa mashtaka kumbe huku nyuma wadada washataka kupigana kisa yy..wakatumiliwa n mdogo wangu!

Nakaaje nae sasa...?!!
sasa unataka kumpa notsi kisa kakutongoza? kwan cha ajabu kipi? si ombi tu ni hiari kukubali au kukataa tatizo nini? angetaka kukubaka sawa.
 
Back
Top Bottom