Tarehe kama hii mwaka jana (14.8.07), Kuna mafanikio yoyote?

I can see many regressive changes just as I anticipated them since last general election. Frankly speaking we're already a decade behind,
 
Hamna kilichoendelea Mkuu!Kila kitu kiko vilevile hata sielewi tunakoelekea!Uchumi unazidi kudorora,inflation iko at the highest rate,unemployment ipo juu,ufisadi nao wazidi kutuumiza vichwa maana hamna hatua inayochukuliwa na mauaji ya kimafia yasiyoeleweka!
I am so worried will be a failed state maana tunakoelekea hapaeleweki!!!!!!!!!
Tunakutakia kila lakheri katika uwajibikaji wako bungeni ila nothing my firend has changed!

Has Tanzania ever been a successful state? Kuna watu wanaamini wakati wa Nyerere tulikuwa tumefanikiwa.....Kama ni mafanikio basi ni kuweka misingi imara kama miamba ya kusitawi kwa ufisadi.
 
Has Tanzania ever been a successful state? Kuna watu wanaamini wakati wa Nyerere tulikuwa tumefanikiwa.....Kama ni mafanikio basi ni kuweka misingi imara kama miamba ya kusitawi kwa ufisadi.
1.Tanzania is not a state.


2.Tuambie mafanikio wwe unayapima vipi,ila as far as i know Tanzania imepiga hatua kubwa katika maendeleo hasa ya Teknolojia ukilinganisha na miaka ya nyuma


3.Panga hoja zako vizuri na usijumuishe kuwa kitu kimoja,leo mie siwezi kusema CHADEMAni chama kibaya hata kama kina viongozi wabaya,kuna mazuri yamefanywa na viongozi wao na mengine ni mabaya,vivyo hivyo na Mwalimu,Mwinyi,Mkapa(angali picha hapo juu) kuna yale mazuri waliyofanya na mabaya ambayo yalitokea
 
Bwana Zitto mbona hujajibu hoja ya msaada wa millioni 78 wa magari na pikipiki?

na uwiano wa kugawa ruzuku makao makuu na majimboni? mimi nilikuwa na mpango wa kujiunga na chama chenu lakini kwa hizo hoja nasita.

tunawaaminia kwa juhudi zenu hasa kwa hiii hoja uliyoileta lakini kwa nza safisha hali ya hewa bwana.

Nakutakia uwajibukaji mwema ukumbini wakati na mimi nawajibika hapa kijiweni kwangu.

Mzee nadhani unashida na uelewa wako wa mambo, mbona unataka kubadili uelekeo wa hii mada, hii wa wewe kujiunga na hicho chama chao nadhani haisaidii sana kwenye mada halisi tarehe 14.8.07 kama alivyoweka mwanzishaji. Nivizuri ukaanzisha thread yako kuliko kukurupuka bila kufikiria ama kweli sasa JF imeingiliwa.

Ushi
 
Mabadiliko HAKUNA na MAMBO NI MBAYA ZAIDI...Hilo liko WAZI!
Hata wanafunzi na wafanyakazi pamoja na wakulima mambo yao ni WORSE!
Kwa mafisadi...MAMBO SHWARI SANA TU NA MABILIONI NI VIJISENTI.
Watu kama hao kelele za MLANGO HAZIWANYIMI "USINGIZI"
 
KAMA UNA USHAHIDI PELEKA POLISI???????

the list goes on


....gembe basi tuanze kutafuta ushahidi wa vifo vingine masterminded na UWT ..kabla ya kuanza ..kupiga propaganda iliyoshindwa hapa ya kuhusisha upinzani..ambao hawana jeshi,usalama ,polisi hata TVIIIIIT....nadhani ingekuwa vinginevyo sasa hao viongozi wa chama ...wangekuwa shimoni...wananyea debe.....

......style iliyotumika ni ileile....waliyoitumia majasusi wa kenyatta,mwalimu.iddi amin...ets.....

style ambayo ni exactly kama aliyokufa sokoine ..tukaambiwa hakufunga mkanda ...na akiwa amekaa kiti cha nyuma alirushwa akajigonga...mbele...ndio dereva wake na bodyguard walipona....na yule jasusi wa ANC dube PIA alipona ...baadaye akaachiwa ...traffic offence!!!

....yes sokoine hakufunga mkanda ..WAKATI INAJULIKANA KWA YEYOTE ALIYEFANYA HATA ELEMENTARY VIP PROTECTION UNIT....JUKUMU LAKO LA KWANZA NI KUHAKIKISHA KUWA BOSI WAKO ANAINGIA GARINI KWA USALAMA.......PILI KUHAKIKISHA UMEMFUNGA MKANDA WEWE MWENYWE...TATU HAKIKISHA UMEUFUNGA MLANGO VEMA ...NA LOCK,....NNE HAKIKISHA WAKATI WOTE WA SAFARI AMEFUNGA MKANDA NA HAKUNA MAZINGIRA YEYOTE HATARISHI NDANI AU NJE YA GARI ..IKIWEMO KUWASILIANA KWA REDIO NA DESTINATION ....NA TRAFFIC ANAYEONGOZA MSAFAARA...PAMOJA NA KUSIKILIZA MAWASILIANO WAKATI WOTE...........mbona hamkupeleka ushahidi polisi!!!!?????...style ile ile!!

...tatizo la huyu kijana wa sasa ..hakuwa JASUSI ALIYEFUZU.....
 
...kilichobadilika tangu JK aingie ni kuongezeka kwa foleni za magari mjini,ufisadi na wizi wa mali za umma,umaskini uliokithiri kwa wananchi walio wengi,serikali isiyowajibika na kujaa rushwa,magonjwa na watu kukata tamaa ya maisha....nilikuwa bongo less than a yr ago niliyojionea yanakatisha tamaa!
 
1.Tanzania is not a state.


2.Tuambie mafanikio wwe unayapima vipi,ila as far as i know Tanzania imepiga hatua kubwa katika maendeleo hasa ya Teknolojia ukilinganisha na miaka ya nyuma


3.Panga hoja zako vizuri na usijumuishe kuwa kitu kimoja,leo mie siwezi kusema CHADEMAni chama kibaya hata kama kina viongozi wabaya,kuna mazuri yamefanywa na viongozi wao na mengine ni mabaya,vivyo hivyo na Mwalimu,Mwinyi,Mkapa(angali picha hapo juu) kuna yale mazuri waliyofanya na mabaya ambayo yalitokea

Kama mimi nahitaji kupanga hoja zangu vizuri, wewe unahitaji kuelewa kilichoandikwa na wengine. Sio kukurupuka tu.

Kwanza mimi nilikuwa namjibu yule niliyem-quote. Jaribu kusoma na kuelewa alichoandika.

Suala la teknolojia ni la wakati. Niambie ni nchi ipi ambayo haitumii teknolojia tunayotumia sisi. Na bado tunaambiwa Sub-saharan Africa ni sehemu pekee ya dunia hii ambayo imerudi nyuma kimaendeleo(umasikini umeongezeka) katika muda wa miaka zaidi ya 25.
 
Zitto Sioni Mafanikio Bali Ni Setback Too Tumeludi Nyuma Napima Uchumi Wa Nchi Yangu Kwa Vile Shilling 1000 Ilikuwa Ina Fanya Agost 1
 
Kipimo Ni Hiki
14 August 2007 Kilo Ya Mchele 6000tsh,and Now 14 August 2008, 8000tsh.
Kilo Ya Maharagwe 6000tsh Now 1000tsh.
Chakoal 10,000tsh Now 25,000tsh.
 
KAMA UNA USHAHIDI PELEKA POLISI???????

the list goes on


....gembe basi tuanze kutafuta ushahidi wa vifo vingine masterminded na UWT ..kabla ya kuanza ..kupiga propaganda iliyoshindwa hapa ya kuhusisha upinzani..ambao hawana jeshi,usalama ,polisi hata TVIIIIIT....nadhani ingekuwa vinginevyo sasa hao viongozi wa chama ...wangekuwa shimoni...wananyea debe.....

......style iliyotumika ni ileile....waliyoitumia majasusi wa kenyatta,mwalimu.iddi amin...ets.....

style ambayo ni exactly kama aliyokufa sokoine ..tukaambiwa hakufunga mkanda ...na akiwa amekaa kiti cha nyuma alirushwa akajigonga...mbele...ndio dereva wake na bodyguard walipona....na yule jasusi wa ANC dube PIA alipona ...baadaye akaachiwa ...traffic offence!!!

....yes sokoine hakufunga mkanda ..WAKATI INAJULIKANA KWA YEYOTE ALIYEFANYA HATA ELEMENTARY VIP PROTECTION UNIT....JUKUMU LAKO LA KWANZA NI KUHAKIKISHA KUWA BOSI WAKO ANAINGIA GARINI KWA USALAMA.......PILI KUHAKIKISHA UMEMFUNGA MKANDA WEWE MWENYWE...TATU HAKIKISHA UMEUFUNGA MLANGO VEMA ...NA LOCK,....NNE HAKIKISHA WAKATI WOTE WA SAFARI AMEFUNGA MKANDA NA HAKUNA MAZINGIRA YEYOTE HATARISHI NDANI AU NJE YA GARI ..IKIWEMO KUWASILIANA KWA REDIO NA DESTINATION ....NA TRAFFIC ANAYEONGOZA MSAFAARA...PAMOJA NA KUSIKILIZA MAWASILIANO WAKATI WOTE...........mbona hamkupeleka ushahidi polisi!!!!?????...style ile ile!!

...tatizo la huyu kijana wa sasa ..hakuwa JASUSI ALIYEFUZU.....
Ndugu PM.....

Huyo Mwalimu hapo juu wakusudia Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.......?Na hiyo ya Sokoine......ina maana BABA WA TAIFA ALIHUSIKA....?maana majasusi hapo umehusisha na MARAIS wa NCHI...........
Hofu yangu ni kwamba huyo mtu hatajwi kwa mabaya kabisa hapa JF....ni mtakatifu kama alivyokuwa ANUARIKE.

Ingawa ukweli utabaki palepale, pamoja juhudi zinafanywa kutufanya tusahau yale ya kuvaa magunia,kuteketeza mali kwa kisingizioa cha uhujumu uchumi na sera za azimio la Arusha,kulazimisha watu kuhama makazi yao na kupoteza vitega uchumi vyao kwa hoja za ujamaa n.k

anyway,Mh.Zitto Kabwe....
Bado tu tupo katika kiza totoro.........maana kashfa nzito zaenea hadi kwa wale tuliokuwa tunawaona kuwa ni wakombozi,mbaya zaidi baadhi ya hizo kashfa kama vile za ubaguzi wa kidini,kikabila,kielimu na kimawazo hapo makao kuu Ya CHADEMA yanapoonekana waziwazi kiasi cha kuepelekea hizo zilizojificha kuhisiwa kuwa ni za kweli.
Kwa hiyo hakuna mafanikio...badala yake kuna loss kila upande.
 
Kuna msemo kwamba "kwa kadiri vitu vinavyobadilika, ndivyo vinavyobakia vile vile". Kuna mabadiliko makubwa yametokea nchini lakini ni mabadiliko ambayo bado yanaonesha kuwa vitu vimebakia vile vile japo kuwa vilipaswa kubadilika pia. Lakini kubwa zaidi ni je mabadiliko tunayoyaona yamesababisha taifa kubadilika kwa ubora zaidi au yanapaswa kusababisha taifa kubadilika kwa ubora zaidi? Lakini swali kubwa zaidi ni tunaweza kupima vipi matokeo ya mabadiliko hayo?

Kwangu mimi naamini mabadiliko makubwa yametokea upande wa Bunge. Kwanza upande wa ubora na uthubutu wa uchangiaji lakini pia kufungiwa kwa Zitto kulisababisha watu kuliona Bunge kwa jinsi lilivyo hasa kuwa limejaa wabunge wa CCM ambao wako tayari kufanya lolote kutetea serikali yao.

Jinsi Bunge lilivyotumika kumfungia Zitto kulisababisha wananchi kuelewa kuwa Bunge linaweza kufanya lolote lile hasa likiwa limejaa watu wa chama kimoja. Hata hivyo CCM baada ya kugundua jinsi walivyoboronga wakageuka na kufanya triangulation ya upinzani na wao wenyewe wakaanza kuzungumza kama wapinzani na matokeo yake ni mashujaa wa Februari, na kuibuka kwa wabunge kama yule wa Sikonge, n.k Hivyo, utaona kuwa matokeo makubwa ya suala la Buzwagi ni kuimarika kwa wabunge wa CCM na hivyo CCM kujijengea mashujaa wapinzani ndani yake na kuwakubali.

Huko nyuma ilikuwa mbunge au kiongozi wa CCM akisema kitu kinyume na "vikao vya chama" basi atakabwa na lile dubwasha la "nidhamu ya chama". Kuanzia sakata la Buzwagi na baadaye mjadala wa Richmond, CCM imepoteza uwezo wake wa kuzima mijadala kinyemela. Imejaribu Butiama lakini pasipo mafanikio makubwa na sasa ndani ya CCM kuna new alignment of political positions. CCM imewahi kuwa na makundi lakini hakuna wakati ambapo imewahi kuwa na makundi yenye milengo ya kibinafsi kama wakati huu. Hii alignment inayoendelea ndiyo (naamini) kiini cha kuvunjika na kuanguka kwa CCM.

Lakini jingine ambalo limedhihirishwa tangia mwaka jana ni kuwa wapinzani bado hawajajua mchezo wa siasa. Naamini hakuna wakati ambapo upinzani Tanzania ungeweza kujijenga na kukita katika mioyo ya Watanzania kama wakati wa sakata la Buzwagi.

Na hasa upande wa Chadema. Chadema ilishindwa kutumia nafasi waliyopewa na fate ya kujipatia wanachama wapya, kutangaza sera zake na kusahihisha mambo yote yaliyokuwa yanakisonga chama hicho toka ndani na kuibuka better, bigger and stronger. Kosa kubwa walilolifanya ni kudhania (kwa makosa) mjadala wa Buzwagi ulikuwa ni suala la "Kitaifa" tu na siyo la chama. Na kosa hilo (nilisema wakati ule) linadhihirika sasa hivi katika ushirikiano wao wenye mashaka na vyama vya TLP, CUF na NCCR.

Sasa hivi kufuatia msiba wa Wangwe vyama vya TLP, CUF na NCCR vimeamua kutumia nafasi hii kujijenga na kujitafutia jimbo kule Tarime na kuna uwezekano mkubwa kwa NCCR kuchukua jimbo hilo wakikubaliana na TLP kuwaunga mkono kule Biharamulo. Wakifanya hivyo vyama hivyo viwili vitarudi na angalau mbunge mmoja mmoja Bungeni.

Lakini pia kuna jingine limedhihirika nalo ni kutokana na hilo la Buzwagi; Chadema na wabunge wake walionekana (kama bado sijui) kuwa ndio watetezi wa raslimali za nchi na wabunge wake vinara katika vita dhidi ya ufisadi. Wanasiasa wake walisimama kama wajenga hoja wakubwa pale Temeke, na wakasimama Bungeni kama mashujaa wasio na mzaha. Kitu kimoja kilikosekana na naamini bado kinakosekana. Uongozi.

Nasema uongozi na hapa simaanishi watu wenye vyeo vya uongozi kwani nitakuwa si mkweli. Uongozi ninao uzungumzia ni uwezo wa kutambua tatizo, kulichambua katika sehemu zake, kuona uzito wake na kutafakari njia za kulikabili. Uongozi huo ni wa kuweza kutafuta usuluhishi wa matatizo ndani ya chama na kuhakikisha kuwa chama bado kinaendelea kuwa kimoja, imara, na chenye msimamo mmoja.

Binafsi naamini kuwa suala la hoja za Wangwe na watu waliokuwa wanamuunga mkono lilikuwa ni suala la hoja dhidi ya hoja na lingeshughulikiwa kwa kujibiwa na mazungumzo na siyo mabishano na tuhuma. Ninaelewa watu wako tofauti na personalities tofauti. NI wazi kulikuwa/bado upo mgongano wa personalities za Wangwe na Mbowe. Mgongano huu ulikuwa ni laana kwa Chadema ingawa ungeweza kutumika kuwa baraka kubwa sana. Waswahilli wanasema "mafahali wawili hawaki zizi moja"; lakini naamini "mafahali wawili wanaweza kulima pamoja".

Wangwe na Mbowe wasingelazimika kukaa pamoja lakini walipoamua kufungwa nira pamoja (Mwenyekiti na Kaimu Makamu Mwenyekiti) kama ng'ombe wa maksai katika kulima shamba la Chadema lilikuwa ni jukumu lao kuhakikisha wanalima pamoja. Hilo halikuwezekana kwani inaonekana katika kufanya hivyo mmoja alitaka aanzishe juu na mwingine alitaka aanzie chini. Na kwa kufanya hivyo ku polarize the party. Ni wazi kuwa wanasiasa hao wawili wasingeweza kukaa katika nafasi hizo wakiwa wanarushiana tuhuma nzito kama tulizozishuhudia. Binafsi naamini ilikuwa ni ukosefu mkubwa wa kiuongozi hadi kufikia walipofikia. Labda ililazimu kufika huko lakini naamini kuna mambo ambayo yangeweza kufanywa na mwisho wake ingawa ungeendeleza tofauti ya mambo fulani kwa hakika ungefanya chama chao kiendelee kuonesha mfano.

Kosa ambalo naamini bado lipo katika Chadema ni wao pia kwa namna kubwa kufuata mfumo wa muundo wa CCM kama chama. Muundo huu umepitwa na wakati kwani unafuata mfumo wa kikomunisti na una lengo kubwa la control of party machinery. Hauko loose enough to allow dissent while maintaining unity.

6.1.1 Kutakuwa na ngazi saba za uongozi wa Chama kama ifuatavyo:
(a) Ngazi ya Msingi (Shina kwenye CCM)
(b) Tawi
(c) Kata/Wadi
(d) Jimbo/Wilaya
(e) Mkoa
(f) Jimbo.
(g) Taifa - Katiba ya Chadema

Je ingeweza kuwa na muundo mwingine tofauti? ndiyo. Sitalizungumzia hilo kwa sasa.

Kwa upande wa chama cha CUF kwa kweli ni chama ambacho naamini kiko kama na kigugumizi. Kinataka kusema kitu lakini hakisemi ingawa kimsingi kinapaswa kusema jambo hilo. Ndicho chama Kikuu cha upinzani nchini chenye wabunge wengi na wawakilishi wengi.

Lakini mabadiliko tunayoyazungumzia hayajakigusa sana chama hicho na matokeo yake hayaonekani sana upande wa Tanzania bara. Binafsi naamini kuwa CUF ingeweza kuwa kichocheo kikubwa cha mabadiliko na kuwa tishio la CCM Tanzania bara endapo kingeweza kujijenga zaidi bara. CUF kinapokea fedha nyingi zaidi za ruzuku kuliko chama kingine cha upinzani na kina uwezo mkubwa wa kuwa tishio la CCM bara.

Lakini kwa namna wanayoielewa wao inaonekana maslahi yao makubwa yako Zanzibar kuliko bara na hivyo kujikita zaidi Zanzibar. Bado sijajua ni jinsi gani CUF inaweza kusimama na kuwa mtetezi wa maslahi ya Taifa zima na kuongoza vita dhidi ya ufisadi nchini? Kikiwa na raslimali zaidi ya kifedha, kikiwa na wabunge wengi zaidi (kwenye Bunge la Muungano) ni kwanini sauti ya CUF inasikika kama mwangwi tu?

Ndio maana utaona hata juzi walipotoa kauli ya kuwalalamikia wafadhili haikuchukua muda Ubalozi wa Marekani ukajibu. Nina uhakika CUF ni lile "JITU LILILOLALA) (the sleeping giant). Naamini kwenye mjadala mzima wa ufisadi CUF imekuwa ni kama mpiga makofi wakati wa ngoma na yeye mwenyewe hataki kucheza. Sielewi kama ulikuwa ni mkakati kuwa Chadema ndio wacheze na CUF washangilie au ni kuwa CUF hawataki kuingilia sana kashfa zinazohusu bara?

CUF inaweza kabisa kuwa chama mbadala wa CCM kwanza kwa sababu hakijagubikwa na kashfa nzito au misuko suko ya juu ya uongozi na ile iliyotokea imekuwa ikihusu Zanzibar zaidi kuliko CUF bara. Na hata wakati wanachama wake walipomeguka na kurudi CCM CUF haikupigiwa kelele sana. Inawezekana ni kutokana na uongozi wa Seif na Dr. Lipumba au uthabiti wa jinsi ambavyo viongozi hao wawili wamekuwa wakiiendesha CUF kwani hata wakati ambapo unaweza kufikiri CUF inaweza kulipuka Zanzibar utaona kuwa mambo yanaziimwa chini kwa chini.

Nilitarajia kuona CUF baada ya kupitia migogoro ya kiuongozi na tuhuma za hapa na pale wangeweza kujikita katika kukiimarisha chama chao bara na kufanya siyo tu wakubalike zaidi lakini waonekane ni chama cha kitaifa zaidi. Hili bado halijatokea. Lakini swali kubwa kuhusu ni CUF ni je CUF inaweza kuendelea kuwa na nguvu na sura ile ile ya mtetezi wa Zanzibar pasipo Maalim Seif katika nafasi ya uongozi? Je Seif akiondoka CUF itaendelea kuwa moja au itakuwa ni kama yaliyotokea baada ya kifo cha Alexander the Great?


Kwa upande wa CCM, nimekwisha elezea kidogo hapo juu mabadiliko ambayo yametokea. Lakini naamini kuna kubwa zaidi ambalo linatokea ndani ya CCM ni kujiimarisha kwa CCM kutoka ndani. Kwa nje mtu anaweza kuona CCM inagawanyika lakini naamini kinachofanyika sasa ni mkakati wa kujiimarisha kutoka ndani kwa kukubali internal dissent bila kulazimishwa kutoka ndani ya Chama.

Siamini kama sasa hivi CCM itamfukuza mtu kwa kuwa na maoni yasiyo kuwa sera au yasiyo lingana na ilani ya CCM. CCM itamfukuza mtu kwa kula fedha za chama au kuliharibia jina chama kwa vitendo fulani lakini si kwa maoni. Ni kwa sababu hiyo anayetegemea kuwa mama Kilango au Dr. Mwakyembe watatoka CCM kwa sababu ya kupingwa maoni watakuwa wanaota. Wana CCM watatoka pale watakapotambua kuwa hawakaribishwi tena CCM. Sasa hivi CCM inajiandaa kwa kuruhusu wagombea huru na ili kuhakikisha watu wake wanabakia ndani basi ina jiandaa kuruhusu mawazo na fikra tofauti.

Kwa kufanya hivyo, CCM naamini itarudisha nguvu za uamuzi wa mwisho kwa wagombea kufanyika kwenye kura za maoni na ya kuwa kura za maoni zitakuwa ni za mwisho. Watalifanya hili kwa sababu wameshatambua kuwa kuwalazimisha wananchi wamchague mtu wasiyemtaka kumewagharimu sana na gharama kubwa ambayo naamini hadi kesho watakuwa wanaijutia ni kumuengua Dr. Slaa mwaka 1995 licha ya kukubalika kwake Karatu kuliko Patrick Qoro.

Siyo hilo tu hata Tarime ni somo kubwa kwao na pia kilichotokea Bunda watu wanakumbuka. Umaarufu wa wabunge wa kuchaguliwa na kuamka kwa wananchi kifikra kutalazimisha CCM kujenga mazingira ya kutambua kura za maoni kama uamuzi wa mwisho na ya kuwa hakuna tena kubeba wagombea wake.

Nimesema vitu vimebadilika lakini pia vimeendelea kubakia vile vile. Je mabadiliko yote haya tunayoyaona kwenye upande wa siasa yamesababisha mabadiliko ya kiutendaji? Kwa kiasi inawezekana lakini kiukweli bado utendaji wetu uko vile vile kwani bado watendaji hawajajitahidi kushikamana na mabadiliko ya kisiasa.

Matokeo yake, kiutawala na kiutendaji serikalini bado tunahangaika na mambo yale yale, maamuzi mabovu, utawala wa kibabe, na sheria zile zile ambazo zimetufikisha hapa tulipofika leo. Hakujawa na haraka ya kubadilisha vitu kwa haraka. Sheria ya Madini bado ni ile ile, sheria ya Usalama wa Taifa ni ile ile, Mkataba wa Buzwagi ni ule ule, n.k Hatujafanya hima kubadilisha matendo yetu ya kiutawala. Hadi leo hakuna mtu aliyefikishwa mahakamani kwa kosa lililotokana na tuhuma mbalimbali na kuna uwezekano wa kutofikishwa mahakamani.

Safari bado ni ndefu, lakini hata safari ndefu huanzwa kwa hatua moja. Naamini tumepiga hatua moja mbele, tuilinde tusije tukapiga hatua mbili nyuma halafu tukashangilia kuwa "tumepiga hatua tatu"!
 
Mabadiliko HAKUNA na MAMBO NI MBAYA ZAIDI...Hilo liko WAZI!
Hata wanafunzi na wafanyakazi pamoja na wakulima mambo yao ni WORSE!
Kwa mafisadi...MAMBO SHWARI SANA TU NA MABILIONI NI VIJISENTI.
Watu kama hao kelele za MLANGO HAZIWANYIMI "USINGIZI"

Mushi mabadiliko yapo,yaani toka nafuu kwenda mbaya zaidi.waswahili wanasema "kila kukicha bora jana"
 
Nimesema vitu vimebadilika lakini pia vimeendelea kubakia vile vile. Je mabadiliko yote haya tunayoyaona kwenye upande wa siasa yamesababisha mabadiliko ya kiutendaji? Kwa kiasi inawezekana lakini kiukweli bado utendaji wetu uko vile vile kwani bado watendaji hawajajitahidi kushikamana na mabadiliko ya kisiasa.

Matokeo yake, kiutawala na kiutendaji serikalini bado tunahangaika na mambo yale yale, maamuzi mabovu, utawala wa kibabe, na sheria zile zile ambazo zimetufikisha hapa tulipofika leo. Hakujawa na haraka ya kubadilisha vitu kwa haraka. Sheria ya Madini bado ni ile ile, sheria ya Usalama wa Taifa ni ile ile, Mkataba wa Buzwagi ni ule ule, n.k Hatujafanya hima kubadilisha matendo yetu ya kiutawala. Hadi leo hakuna mtu aliyefikishwa mahakamani kwa kosa lililotokana na tuhuma mbalimbali na kuna uwezekano wa kutofikishwa mahakamani.

Mwanakijiji, thank you for your lengthy and scary analysis ambayo hata hivyo imerudi kulekule—kwamba: bado mambo yako vilevile. Hakuna mabadiliko. Sikuona umuhimu wowote kabisa wa wewe kutu-lecture kwa muda wote huo kuhusu tactical adjustments zilizofanywa na vyama vya siasa (esp.CCM), hali ukijua kuwa these morons had no other choice but to do so ili wazidi kubaki hapo walipo/madarakani.

My advice: Next time, please try harder to go straight to the point.
 
Mwanakijiji, thank you for your lengthy and scary analysis ambayo hata hivyo imerudi kulekule—kwamba: bado mambo yako vilevile. Hakuna mabadiliko. Sikuona umuhimu wowote kabisa wa wewe kutu-lecture kwa muda wote huo kuhusu tactical adjustments zilizofanywa na vyama vya siasa (esp.CCM), hali ukijua kuwa these morons had no other choice but to do so ili wazidi kubaki hapo walipo/madarakani.

My advice: Next time, please try harder to go straight to the point.


hahahah sasa nikifanya hivyo si nitakuwa naonesha kuna kitu kimebadilika... ?
 
1.Tanzania is not a state.


2.Tuambie mafanikio wwe unayapima vipi,ila as far as i know Tanzania imepiga hatua kubwa katika maendeleo hasa ya Teknolojia ukilinganisha na miaka ya nyuma


3.Panga hoja zako vizuri na usijumuishe kuwa kitu kimoja,leo mie siwezi kusema CHADEMAni chama kibaya hata kama kina viongozi wabaya,kuna mazuri yamefanywa na viongozi wao na mengine ni mabaya,vivyo hivyo na Mwalimu,Mwinyi,Mkapa(angali picha hapo juu) kuna yale mazuri waliyofanya na mabaya ambayo yalitokea

wewe jamaa kaa kimya yaani unachemka mpaka noma! aidha unaongea sana bila kufikiria au ni mweupe, a dingus...inaboa kukusoma!!
 
Ndugu zangu,

Tarehe kama hii mwaka jana nilitoa hoja Bungeni kuhusu Mkataba wa Buzwagi uliosainiwa kifisadi huko Uingereza.

Mengi yametokea katika Taifa letu toka Agosti mwaka 2007. Hebu tuangalie nyuma ili kuona tumefanikiwa nini katika vita dhidi ya ufisadi na pia wapi tumekosea na kuongeza nguvu zaidi ili Taifa letu liwe mahala pazuri pa kuishi. Kila mtu mwana JF, aseme anaona nini kimebadilika katika uendeshaji wa Taifa letu, katika vyama vya upinzani na katika chama tawala!

Vipi katika vyombo vya habari na Asasi zisizo za kiserikali?

Nawatakia kila la kheri, naenda ukumbini kuwajibika.............................. Lets look back and learn

Zitto, baada ya mwaka tangu Watanzania tufahamu kuhuzu ufisadi katika kusaini mkataba wa Buzwagi hakuna chochote kilichobadilika, ukiondoa vyombo vya habari ambavyo vinastahili pongezi kubwa katika juhudi zao za kupambana na mafisadi.

1. Bado mikataba ya madini imefanywa siri pamoja na JK kwa Watanzania wote na hata wabunge.
2. Bado mikataba hiyo ya madini haina maslahi yoyote kwa manufaa ya Watanzania. Pamoja na kupanda kwa kasi sana kwa bei ya dhahabu katika soko la dunia, Watanzania hatukunufaika na chochote kufuatia bei ya juu ya dhahabu. Walioendelea kufaidika ni Barrick, na makampuni mengine ya uchimbaji wa madini mengine pamoja na shareholders wao.
3. Pamoja na kujiuzulu kwa mawaziri wanne akiwamo Waziri Mkuu kwa kuhusika na kashfa mbali mbali, lakini mawaziri hao bado wanalipwa mishahara na marupurupu kupitia pesa za walipa kodi waliowafisadi kama Wabunge. Pamoja na Watanzania kupiga kelele ili wahusika hao wavuliwe ubunge mpaka leo hii bado wanapeta bungeni.

4. Tumesikia mengi kuhusu ufisadi uliofanywa BoT na wahusika mbali mbali wakiwamo viongozi wa juu wa chama na serikali lakini kwa msghangao wa wengi hadi hii leo hakuna yeyote aliyefilisiwa au kuadhibiwa kufuatia wizi mkubwa wa mabilioni.

5. Tumesikia kuhusu ufisadi mkubwa uliofanywa na fisadi Mkapa kwa kujiuzia nyumba yeye na mawaziri wengine kwa bei poa kabisa na pia fisadi Mkapa kujimilikisha katika mazingira ya kifisadi mgodi wa Kiwira wenye thamani ya shilingi bilioni nne kwa kulipa shilingi 70 millioni tu. Hadi hii leo bado SIRI KALI imepata kigugumizi kuhusiana na maswali chungu nzima yalioulizwa na Watanzania kuhusiana na umiliki wa mgodi huo.

Kwa maoni yangu bado tuna safari ndefu sana katika kupambana na ufisadi wa kukupua mali za Watanzania na kusaini mikataba ambayo itakuwa na maslahi kwa nchi yetu. Na sioni mafanikio yoyote hadi hivi sasa.

Vyombo vya habari hasa magazetii kama Mwananchi, This Day, Mwanahalisi, Raia Mwema, Tanzania Daima na yanajitihidi sana kuandika mambo mazito kuhusiana na ufisadi unaofanywa au uliofanywa na 'viongozi' mbali mbali. Hata mabalozi wa nchi za wafadhili na baadhi ya wabunge wamesifia sana vyombo vya habari kuwa mstari wa mbele katika kupambana na ufisadi. Hapa hali inaridhisha sana na kutia moyo.

Vyama vya upinzani bado vinatuchanganya Watanzania. Pamoja na kupiga kelele kila kukicha kuhusu umuhimu wa nyinyi kuungana ili kuunda chama kimoja chenye nguvu kitakachokuwa na uwezo wa kuking'oa chama cha mafisadi madarakani, bado mmetia pamba masikioni kuhusu kelele zetu hizo. Kwa kifupi, Watanzania hatuwaelewi.

Mmeshashiriki chaguzi tatu za vyama vingi Tanzania za mwaka 1995, 2000 na 2005 lakini matokeo yenu kwa kweli si ya kuridhisha, pamoja na kuwa 1995 matokeo yalikuwa yanatia moyo kuliko chaguzi zilizofuata. Tunashangaa hamjiulizi kulikoni mpaka hatufanyi vizuri pamoja na CCM kugubikwa na kashfa chungu nzima na ambazo wameshindwa kuzichukulia hatua zozote. Tunashangaa bado mnang'ang'ania kuwepo mijini wakati wapiga kura wengi Watanzania wanaishi vijijini. Hatuoni wala kusikia juhudi zozote mnazozifanya ili kujitangaza huko vijijini bali huwa mnasubiri mpaka wakati wa kampeni ndipo mnaonekana katika vijiji vichache ambavyo mnadhani mtafanya vizuri.

Ombi la Watanzania kwenu sikilizeni maoni yetu ili myafanyie kazi kwa faida ya nchi yetu. Wekeni ubinafsi pembeni ili muunde chama kimoja chenye nguvu kitakachokuwa na uwezo wa kuishinda CCM katika uchaguzi ujao. Tanzania ni nchi kubwa sana tunahitaji viongozi wengi tu mawaziri, makatibu wakuu, wakuu wa mikoa, mabalozi n.k. na viongozi wote wa upinzani watapata vyeo vikubwa mara mtakapokuwa madarakani kama chama kimoja. Kumbukeni UMOJA NI NGUVU NA UTENGANo ni udhaifu. Kuendelea kwenu kujitenga ni kuwapa mwanya CCM waendelee kuwapo madarakani pamoja na kuwa wameshindwa kabisa kuongoza nchi. Kazi kwenu, Yes we can have a beautiful Tanzania without MAFISADI but with good leadership.
 
Hakika hakuna jipya, wananchi wanaendelea kukata tamaa, wamechoka na hawana matumaini tena. Diesel iliyokuwa inauzwa Sh.1,400/= hivi sasa ni Sh.2000/= Zitto nakumbuka wewe pamoja na kambi upinzani mlilia sana kuhusu kupandisha kodi katika mafuta wakasema ongezo ni dogo.

Ona sasa hali ilivyo, vitu vyote vimepanda bei kwa kutaa ushauri kisa wameutoa wapinzani. Madukani na magulioni watu wanaenda kwa kuvizia mwisho wa mwezi. Vuguvugu la madaktari na Walimu kutaka kugoma na wadogo zetu wa shule za msingi na sekondari kuandamana ni ushaidi tosha hali ni mbaya kuliko ilivyokua mwaka jana tarehe kama ya leo.
 
Back
Top Bottom