Tarehe kama hii mwaka jana (14.8.07), Kuna mafanikio yoyote?

Zitto

Former MP Kigoma Urban
Mar 2, 2007
1,562
10,879
Ndugu zangu,

Tarehe kama hii mwaka jana nilitoa hoja Bungeni kuhusu Mkataba wa Buzwagi uliosainiwa kifisadi huko Uingereza.

Mengi yametokea katika Taifa letu toka Agosti mwaka 2007. Hebu tuangalie nyuma ili kuona tumefanikiwa nini katika vita dhidi ya ufisadi na pia wapi tumekosea na kuongeza nguvu zaidi ili Taifa letu liwe mahala pazuri pa kuishi. Kila mtu mwana JF, aseme anaona nini kimebadilika katika uendeshaji wa Taifa letu, katika vyama vya upinzani na katika chama tawala!

Vipi katika vyombo vya habari na Asasi zisizo za kiserikali?

Nawatakia kila la kheri, naenda ukumbini kuwajibika.............................. Lets look back and learn
 
Bwana Zitto mbona hujajibu hoja ya msaada wa millioni 78 wa magari na pikipiki?

na uwiano wa kugawa ruzuku makao makuu na majimboni? mimi nilikuwa na mpango wa kujiunga na chama chenu lakini kwa hizo hoja nasita.

tunawaaminia kwa juhudi zenu hasa kwa hiii hoja uliyoileta lakini kwa nza safisha hali ya hewa bwana.

Nakutakia uwajibukaji mwema ukumbini wakati na mimi nawajibika hapa kijiweni kwangu.
 
Hamna kilichoendelea Mkuu!Kila kitu kiko vilevile hata sielewi tunakoelekea!Uchumi unazidi kudorora,inflation iko at the highest rate,unemployment ipo juu,ufisadi nao wazidi kutuumiza vichwa maana hamna hatua inayochukuliwa na mauaji ya kimafia yasiyoeleweka!
I am so worried will be a failed state maana tunakoelekea hapaeleweki!!!!!!!!!
Tunakutakia kila lakheri katika uwajibikaji wako bungeni ila nothing my firend has changed!
 
Ndugu zangu,

Tarehe kama hii mwaka jana nilitoa hoja Bungeni kuhusu Mkataba wa Buzwagi uliosainiwa kifisadi huko Uingereza.

Mengi yametokea katika Taifa letu toka Agosti mwaka 2007. Hebu tuangalie nyuma ili kuona tumefanikiwa nini katika vita dhidi ya ufisadi na pia wapi tumekosea na kuongeza nguvu zaidi ili Taifa letu liwe mahala pazuri pa kuishi. Kila mtu mwana JF, aseme anaona nini kimebadilika katika uendeshaji wa Taifa letu, katika vyama vya upinzani na katika chama tawala!

Vipi katika vyombo vya habari na Asasi zisizo za kiserikali?

Nawatakia kila la kheri, naenda ukumbini kuwajibika.............................. Lets look back and learn

Mabadilioko ni makubwa sana ingawa hayaonekani kirahisi, kwa mfano kwa sasa ukiwa na baba fisadi au wewe ni fisadi ni aibu lakini kabla ya tarehe 14.8.07 ilikuwa sifa. Huu ni ushindi mkubwa sana ingawa tunaweza kuupuuza.. ni mwanzo mzuri
 
Karamagi amedhihirika kwamba ni fisadi na kulazimika kuachia uwaziri. Kuondoka kwa karamagi Serikalini kunaleta unafuu kwani alikuwa mbabe sana. Nasikia kwamba Kamati ya bunge ipo/ilikuwa Morogoro inachambua ripoti ya madini, huenda hili ndo litaleta mafanikio ya hoja yako ya August 2007. Go on Zitto.
 
Ndugu zangu,

Tarehe kama hii mwaka jana nilitoa hoja Bungeni kuhusu Mkataba wa Buzwagi uliosainiwa kifisadi huko Uingereza.

Mengi yametokea katika Taifa letu toka Agosti mwaka 2007. Hebu tuangalie nyuma ili kuona tumefanikiwa nini katika vita dhidi ya ufisadi na pia wapi tumekosea na kuongeza nguvu zaidi ili Taifa letu liwe mahala pazuri pa kuishi. Kila mtu mwana JF, aseme anaona nini kimebadilika katika uendeshaji wa Taifa letu, katika vyama vya upinzani na katika chama tawala!

Vipi katika vyombo vya habari na Asasi zisizo za kiserikali?

Nawatakia kila la kheri, naenda ukumbini kuwajibika.............................. Lets look back and learn

Tumeona mengi na hongereni sana kwa kazi kubwa mulioifanya na mnayoifanya. Mna mitihani mingi na yote mtayaashinda katika yeye atiaye nguvu. Haki inacheleweshwa ila haipotei na njia ya mwongo ni fupi hata kama itapindishwa ionekane ndefu na yakukata tamaa. Don giv up!

Nimesikitika wakati mnafanya ziara zenu kwnye kamati hamkutoa special request ya meetings na graduates ambao wanafanya/walifanya kwa hawa jamaa. nafikiri wana cha zaidi cha kueleza kutokana uelewa wao. Naamini yangesaidia sana kwenye write-up.

Tatu, sioni kama kifo cha Mhe Wangwe kimewasambaratisha but you, Dr Slaa, Mbowe muwe makini kupita kiasi. wapo wavivu wa kufikiri wanaweza wakawakatisha tamaa na wapo ambao kazi yao ni kuvizia. Hapo kwenye uteuzi wa wabunge maalumu sielewi naomba mjibu hizo hoja ila naomba sana kama mtu alikosea mkemeeni then muweke utaratibu ili lisijirudie tena. Naami chama cheni ni chama makini.

I believe success is when skill meets opportunity not when fantasy meets reality.

All the best
 
Mabadiliko yapo. MAFISADI wakubwa kabisa angalau hawako SERIKALINI moja kwa moja ingawa MAKUWADI wao bado wamo. Kasi ya KUSAINI mikataba ya kuitafuna NCHI imepungua kidogo. JF imeendelea KUKOMAA na kutekeleza jukumu lake kikamilifu; Bunge linaendelea "kufufuka" kidogo;
 
Kama Makuwadi wapo mkuu unategemea nini?Hao makuwadi wanaendeleza ufisadi then wanakuwa mababa lao!Hawa mafisadi wakubwa bado wanaendeleza cheche zao chini chini!Ila mimi naona kama wangeshughulikiwa kama Watanzania wanavyotaka hapo ningeridhika ila bado wapeta tuu na madharau kibao halafu watoto wao nao wanajitapa kwa waliyofanya wazazi wao hapa kuna ahueni kweli?
 
Naweza kusema mabadiliko yapo, lakini ya kurudi nyuma. Say negetive development. Kila kitu kimepanda, maisha yako juu ili hali kipato cha Mtanzania wa kawaida kikiwa kidogo mno. Nchi imewekwa rehani kwa wageni, naweza kuona hata wamachinga toka nje ya nchi wakiuza karanga na mitumba mitaani, nawaona bar maids toka ulaya wakiuza baa. There is no control atall kwa kazi za foreigners na zile tunazoweza kuwapatia wenzetu ili wajikimu na haya maisha ya kasi, ari, na nguvu mpya kwa kwenda nyuma.

Binafsi nawakubali wapinzani mnavyo tuwakilisha, KEEEP IT UP. There comes a time matunda ya kelele zenu tutayaona.
 
Mimi nawapongeza sana wapinzani, kwamba mmefungua ukurasa mpya katika Tanzania. Sasa "tunahoji" na angalau tunaona watu wamejiuzulu. Na pia sasa tunataja mafisadi kwa "majina". Hiyo ni hatua kubwa. Mambo ya "Cheche". Goodluck
 
Tarehe kama hii mwaka jana nilitoa hoja Bungeni kuhusu Mkataba wa Buzwagi uliosainiwa kifisadi huko Uingereza.

Binfasi, nakupongeza kwa hoja uliyoitoa bungeni August mwaka jana. Ulionyesha ujasiri wa hali ya juu and you absolutely deserve some credit for that!
Mengi yametokea katika Taifa letu toka Agosti mwaka 2007. Hebu tuangalie nyuma ili kuona tumefanikiwa nini katika vita dhidi ya ufisadi na pia wapi tumekosea na kuongeza nguvu zaidi ili Taifa letu liwe mahala pazuri pa kuishi.

Yes, tumeona kuundwa kwa ya Kamati ya Bomani ku-review mikataba ya madini.Tumeona ripoti ya wakaguzi kuhusu EPA ikitolewa. Na tumeshuhudia pia kamati ya Dr. Mwakyembe ikitoa ripoti yake iliyopelekea Lowassa kujiuzuru. Lakini kando ya hayo yote, I must, however, say, nothing really has changed. In other words, bado hatujafanikiwa.

Kwamba: as long as Lowassa bado yuko mtaani akitesa. As long as waliokomba mabilioni ya pessa za EPA bado hawajawajibishwa. As long as mikataba mibovu ya madini bado iko palepale/haijawa-nullified. As long as things are fundamentally in the same way as they were before, then you can't tell me that tumefanikiwa.

As Clinton once put it, " successful political change must begin to improve people's daily lives."
 
Bwana Zitto mbona hujajibu hoja ya msaada wa millioni 78 wa magari na pikipiki?

na uwiano wa kugawa ruzuku makao makuu na majimboni? mimi nilikuwa na mpango wa kujiunga na chama chenu lakini kwa hizo hoja nasita.

tunawaaminia kwa juhudi zenu hasa kwa hiii hoja uliyoileta lakini kwa nza safisha hali ya hewa bwana.

Nakutakia uwajibukaji mwema ukumbini wakati na mimi nawajibika hapa kijiweni kwangu.

Soma heading. Usichanganye mada....hii sio ya mapikipiki...kuna thread yake kule. We need to celebrate our achievements!
 
...tuna bomu pale magogoni na hatuna hope kabisa...kajaa uswahili tuu na porojo huku marafiki zake wnamaliza nchi huku yeye kabakia kutuundia vitume vinavyomaliza pesa zetu zaidi,hasara tupu bora ifike muda aondoke tuu ila najua kuna siku akili itarudi na atajiona mjinga sana huyu JK maana kapewa dhamana ya nchi yeye anacheza tuu
 
Hatuwezi kusema kuwa hakuna mabadiliko lakini ukifanya comperative analysis, hata ndogo unaweza kufikia maamuzi mazuri.
Hoja aliyotoa Zitto ilikuwa na masuala mawili makubwa ya msingi namely 1. Mkataba wa kinyonyaji na 2. Ulisainiwa kifisadi
Katika mazingira kama hayo, achievement kubwa nilizozitaraajia ni mbili. 1. Mkataba ubatilishwe au kurekebishwa na 2. waliohusika kuusaini wawajibishwe.
Yaliyotokea ni kuwa 1. Mkataba bado upo vile vile na unaendelea kurtekelezwa na 2. Aliyehusika (na si waliohusika) amejiwajibisha (na si kuwajibishwa)
Lakini kwa mapana yake ni lazima tukubali kuwa hoja ilikuwa chachu iliyozua mjadala mpana katika masuala ya rasilimali za nchi, hasa madini. Tatizo ni kuwa utekelezaji wa matokeo ya mijadala hiyo ni wa taratibu sana ukilinganisha na mahitaji ya taifa kwa sasa.
Lakini bravo Zitto, umeonyesha njia na ni matumaini yangu kuwa wabunge wengine watafuata hiyo njia kwa sababu kinachotakiwa si miujiza, ni kujituma kufikiri tu na kupata ujasiri wa kuhoji
 
...tuna bomu pale magogoni na hatuna hope kabisa...kajaa uswahili tuu na porojo huku marafiki zake wnamaliza nchi huku yeye kabakia kutuundia vitume vinavyomaliza pesa zetu zaidi,hasara tupu bora ifike muda aondoke tuu ila najua kuna siku akili itarudi na atajiona mjinga sana huyu JK maana kapewa dhamana ya nchi yeye anacheza tuu

Ni hasara tupu kwa kweli. Lakini hasara zingine zina faida. Angekuwa BWM tusingegundua ufidhuli unaofanywa na baadhi ya viongozi wetu. Uswahili nao una faida zake. Hata hivyo hatutaki kendelea na hasara kama hizi.
 
Lakini pia uelewa wa mambo ya siasa kwa upande wa raia umeongezeka kwa kiasi kikubwa. Watu wanaelewa na wana uwezo wa kuichambua siasa ya Tanzania sasa hasa mikataba na kuhoji matumizi ya pesa za EPA. Hilo tumepiga hatua kuelekea Democrasia anbayo inaweza ikatuletea Maendeleo.

Tuna hakika uwa tukiendelea na munkari huu na moyo huu wa kizalendo, basi ni wazi kuwa vigogo wa Richmond, EPA na hata wazee wa vijisenti watatiwa hatiani na wao kuhukumiwa jela miaka 240 ndani......mradi tu

Tusichoke kuhoji na kufuatilia maendeleo ya hoja tuzianzishazo.

Mafisadi
 
Bwana Zitto mbona hujajibu hoja ya msaada wa millioni 78 wa magari na pikipiki?

na uwiano wa kugawa ruzuku makao makuu na majimboni? mimi nilikuwa na mpango wa kujiunga na chama chenu lakini kwa hizo hoja nasita.

tunawaaminia kwa juhudi zenu hasa kwa hiii hoja uliyoileta lakini kwa nza safisha hali ya hewa bwana.

Nakutakia uwajibukaji mwema ukumbini wakati na mimi nawajibika hapa kijiweni kwangu.
Kandambili,

Mhehsimiwa yuko hapa atakujibu tu,wanaiogopa hii maada kuhsu CHADEMa na wamemwachia Mnyika awasaidie kujibu
 
Ambaye hana Masters......

Shalom,

Kisomo changu hakina faida kwako wewe,na kw akifupi haikuhusu..umekosa hoja sasa unaleta vioja..

Mambo ya zitto na mtu kuwa na Master yametoka wapi,after all i know zitto kwa muda mrefu sasa(though hajui kama mimi ndiyo Gembe)..kwa taarifa yako!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom