Tarehe 9 Decemmber huwa tunasherehekea Uhuru wa nchi Gani??

The Khoisan

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
15,385
12,970
Tarehe 9 December ni sherehe ya Uhuru wa Tanganyika. Lakini tangu tuungane na Zanzibar Tanganyika itilikufa. Sasa kuna haja gani ya kusherehekea hii siku. Je tunaposherehekea kwa nini huwa hatuitaji Tanganyika?? Next year najua kutakuwa na mnuso wa nguvu Bongo na Balozi zote kwa ajili ya miaka 50. Je waalikwa wataambiwa wanakuja kusherehekea sherehe ya nchi gani hasa Tanganyika au TZ bara (nchi ambayo haipo). Naomba kuwasilisha.
 
Hivi ndivyo vitendawili vya katiba yetu ambavyo Mtikila anayo tayari majibu yake, lakini tunamwona kama kichaa!
Tanganyika ipo, ipo hai, na hakuna aliyewahi kuiua, wala atakayethubutu...Ni matter ya muda tu!
 
uhuru wenyewe haupo ni kiini macho.uhuru wa nchi gani?ulikuwa uhuru wa mwafrika wa Tanganyika kuwa mtumwa kwa hiari.
 
Kumbe ndio maana nilikutana na Mfiji mmoja akasema yeye anaasili ya Kitanganyika nikamuona kuwa amepitwa na wakati kumbe anajua kuliko mimi ninayejiona Mtanzania asilia......

Nyuma ya Muungano kuna Mengi!
 
Back
Top Bottom