Tarehe 9 December uwa tunasherekea uhuru wa Tanganyika au Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tarehe 9 December uwa tunasherekea uhuru wa Tanganyika au Tanzania?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nzi, Dec 5, 2010.

 1. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #1
  Dec 5, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,854
  Likes Received: 4,528
  Trophy Points: 280
  WanaJF ivi toka mwaka 1964 baada ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania,kila tarehe 31 ya Disemba uwa tunasherekea uhuru wa Tanganyika au Tanzania? Maana kama ni wa Tanzania,then nafikiri tumeingizwa chaka. Naomba kuwakilisha.
   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Dec 5, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Katiba mpya!
   
 3. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #3
  Dec 5, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,854
  Likes Received: 4,528
  Trophy Points: 280
  Well said Gad.
   
 4. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #4
  Dec 5, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,566
  Likes Received: 3,861
  Trophy Points: 280
  Kuna Tanganyika na Tanzania

  ila huo uhuru haupo wala haukuwepo!! uhuru wa bendera na wimbo wa taifa siyo uhuru, acha huo uongo, na kamwe usiwaeleze watoto wako hatuna uhuru kwa ccm hii, wala haukuwepo, still todate tunatawaliwa!

  nani aliwapa uhuru weye? uhuru kamili ni ikipatikana katiba mpya, wakati kila raia kwa itikadi yake atakuwa na uhuru na kujimwaga kenye taifa lake!!! Baada ya kuondoka waingereza, walifuata CCM ambao wanatutawala mpaka leo hii! Tanzania sio huru kwa CCM hii! hii!

  Katiba mpya is a solution
   
 5. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #5
  Dec 5, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,854
  Likes Received: 4,528
  Trophy Points: 280
  Asante Waberoya kwa mtazamo wako.
   
 6. e

  ejogo JF-Expert Member

  #6
  Dec 5, 2010
  Joined: Dec 19, 2009
  Messages: 994
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tanzania ipo huru tangu izaliwe kutoka Tanganyika na Zanji. Hapo tunasheherekea uhuru wa Tanganyika.
   
 7. Mbaha

  Mbaha JF-Expert Member

  #7
  Dec 5, 2010
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 697
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Thats right!! Ni uhuru wa Tanganyika na si Tanzania!!... Historia inapotoshwa!!!
   
 8. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #8
  Dec 6, 2010
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,507
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 180
  Tanganyika
   
 9. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #9
  Dec 7, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,854
  Likes Received: 4,528
  Trophy Points: 280
  QUOTE=ejogo;Tanzania ipo huru tangu izaliwe kutoka Tanganyika na Zanji. Hapo tunasheherekea uhuru wa Tanganyika.

  Vyema. Ila mbona uwa haisemwi kama tunasherekea uhuru wa Tanganyika? Na kwanini tusheherekee uhuru wa nchi ya kufikirika?
   
 10. October

  October JF-Expert Member

  #10
  Dec 7, 2010
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 2,147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Tunasherikea Mwisho wa mwaka na Kesho yake tunasherekea Mwaka Mpya.
   
 11. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #11
  Dec 7, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Ni bora tukubali alichozema Waberoya HAKUNA UHURU wowote labda tupate KATIBA mpya itakayotoa majibu ya maswali yetu.
  Kwa kuanzia mimi nina maswali matano.

  1. Tukisema ni uhuru wa Tanganyika kwa nini tunaalika Heads of States kuja kwenye shere Dec 9. Mkuu wa hiyo Tanganyika ni nani???
  2. Tukisema ni uhuru wa Tanzania Bara, historia inaonyesha hakuna nchi inayoitwa jina hilo imewahi kupata uhuru Dec 9.
  3. Tunapokuwa na rais wa muungano kutoka zanzibar, sherehe za Dec 9 nani atakagua gwaride? Akikagua yeye atakagua kama rais wa Tanganyika au mwakilishi wake???
  4. Kwa nini kwenye sherehe za mapinduzi zanzibar Jan 12 viongozi wa mataifa (heads of states) hawahudhurii kama wanavyoalikwa Dec 9. Je ndio kusema Tanganyika inaitawala Zanzibar??
  5. Je JWTZ inahusika kwenye sherehe za Mapinduzi au ni vikosi vya serikali ya mapinduzi tuuu????

  Jibu la mkanganyiko wote huu ni KATIBA mpya na si vinginevyo.
   
Loading...