anonymousafrica
JF-Expert Member
- Aug 24, 2016
- 611
- 639
Siku kama ya leo mwaka 1971, jitu la Miraba minne Idd Amin alijitangaza kuwa Rais wa nchi ya Uganda na hii ni baada ya kugutuka kwamba Milton Obote alikuwa akipanga kumkamata kwa matumizi mabaya ya fedha za jeshi, Awali, Amin alichukua mamlaka kwa kufanya mapinduzi ya kijeshi tarehe 25 Januari 1971, wakati Obote akiwa anahudhuria mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Madola huko Singapore. Wanajeshi watiifu kwa Amin walifunga Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe na kuchukua Kampala.
Kila kitu kina chanzo aisee, hivi ni kwanini walifika hapa? em tuipitie uganda na historia ya wawili hawa kwa ufupi mno (Amini na Obote) Baada ya zaidi ya miaka 70 chini ya utawala wa Uingereza, Uganda ilipata uhuru wake Oktoba 9, 1962
Hapo Milton Obote akawa waziri mkuu wa kwanza wa taifa hilo. Kufikia 1964, Obote alikuwa ameunda muungano na Amin, unaambiwa walikuwa mabest mno na Amini ndiye alisaidia kupanua ukubwa na nguvu ya Jeshi la Uganda.(Mnyonge mnyongeni ukweli wake nausema hapa)
Mnamo Februari 1966, kufuatia shutuma kwamba wawili hao walihusika na kusafirisha dhahabu na pembe za ndovu kutoka nchini Kongo ambazo ziliuzwa kwa silaha,(Congo imepigwa mtungo kwa muda mrefu sana, Marehemu Profesa Baregu aliwahi kutuambia kadhaa (apumzike kwa amani)
Obote alisimamisha katiba na kujitangaza kuwa rais mtendaji na Muda mfupi baadaye, Obote alimtuma Amin kumwondoa mfalme Mutesa wa Pili, anayejulikana pia kama "Mfalme Freddie," ambaye alitawala ufalme wenye nguvu wa Buganda
Kwa uwezo wake na eneo kubwa alilolishikilia huyu tumuite ndiye Rais wa kwanza wa Uganda. Jaribio la kumuua lilifeli hapo awali, ila inahisiwa liliendelea kimya kimya hadi mwaka aliofariki kwa madai ya kunywa sumu (kujiua kupitia kilevi) japo wengine walikana haikuwa kujiua bali ni kuuliwa baada ya kulazimishwa kunywa pombe hiyo yenye sumu na mmoja kati ya wanajeshi watiifu wa Obote. Kuku lazima warudi zizini kulala alisema Malcom X akimaanisha ukifurahia ndugu zako kuua, basi kuna siku mauwaji hayo yatakurudia mwenyewe.
Obote alianza kutilia shaka uaminifu wa Amin na kuamuru akamatwe akiwa njiani kuelekea Singapore kwa Mkutano wa Wakuu wa Serikali wa Jumuiya ya Madola.
Wakati wa kutokuwepo kwake, Amin alichukua hatua hiyo na kufanya mapinduzi Januari 25, 1971, na ndipo tarehe 02 mwezi Februari bwana Idd Amin akajitangaza kama rais wa Uganda.