Tarehe 10 Julai 2011 ni mwisho wa siku 90 za magamba!

Duble Chris

JF-Expert Member
May 28, 2011
3,481
564
Siku 90 zilizo tangazwa CCM chama kinacho tawala nchini TZ kupia kwa katibu wa uenezi wa CCM zitaishia aidha ni;

Siku ambayo mapacha 3 wataachia zote ndani ya CCM.
Siku ambayo CCM itajinasibu kinagaubaga kuwa sasa wamejivua Magamba ya UKWELI.
Siku ambayo CCM itaandika historia mpya ndani na nje ya chama na nchi kuwa sasa ni chama kitakatifu hivyo tukiamini kwa ari zaidi, kasi zaidi,
Siku ya kuanza ukurasa mpya wa uwajibikaji bila UFISADI ktk chama na " nchi " on opposite side !!!!
Ni siku ya kumuumbua Nape kwa kuongea yale asiyoyajua na kufikiri nini anachosema.
Ni siku ambayo mafisadi watashangilia baada kushinda maamuzi ya chama na fikra za Nape.
Ni siku ya Nape kujilaumu kwa kuongea mambo ya wakubwa kabla hajapewa SEMINA ELEKEZI ya namna ya kuchakachua minute za vikao.
Ni siku ambayo NAPE ataambiwa rasmi kuwa CCM ina wenyewe kwake ni CCJ.
Ni siku ya kupeleka mbele siku 90 hadi 120 kwa Mjibu wa MUKAMA HIVYO TUNASUBIRI LIPI LITAFANYIKA KATI YA HAYO
 
Ni siku ambayo tutajua kwamba kauli ya kulivua gamba ni usanii tu haina ukweli wowote na hii inatokana na ukweli kwamba sasa hivi CCM si chama cha Wakulima na Wafanyakazi kama ilivyo miaka ya nyuma bali ni chama cha mafisadi/majambazi.
 
Nyie mnaleta utani . CCM eti wafanye nini ?
Imeshindwa serikali kula na mafisadi sahani eti wana nguvu sana Chama kitaweza kweli ? Haya tuhesabu siku zilizo bakia .
 
Siku 90 zilizo tangazwa CCM chama kinacho tawala nchini TZ kupia kwa katibu wa uenezi wa CCM zitaishia aidha ni;

Siku ambayo mapacha 3 wataachia zote ndani ya CCM.
Siku ambayo CCM itajinasibu kinagaubaga kuwa sasa wamejivua Magamba ya UKWELI.
Siku ambayo CCM itaandika historia mpya ndani na nje ya chama na nchi kuwa sasa ni chama kitakatifu hivyo tukiamini kwa ari zaidi, kasi zaidi,
Siku ya kuanza ukurasa mpya wa uwajibikaji bila UFISADI ktk chama na " nchi " on opposite side !!!!
Ni siku ya kumuumbua Nape kwa kuongea yale asiyoyajua na kufikiri nini anachosema.
Ni siku ambayo mafisadi watashangilia baada kushinda maamuzi ya chama na fikra za Nape.
Ni siku ya Nape kujilaumu kwa kuongea mambo ya wakubwa kabla hajapewa SEMINA ELEKEZI ya namna ya kuchakachua minute za vikao.
Ni siku ambayo NAPE ataambiwa rasmi kuwa CCM ina wenyewe kwake ni CCJ.
Ni siku ya kupeleka mbele siku 90 hadi 120 kwa Mjibu wa MUKAMA HIVYO TUNASUBIRI LIPI LITAFANYIKA KATI YA HAYO

Nashukuru sana mkuu kwa kuleta tarehe maana wengi wetu hatukuwa na exact date. Thanks
 
Jamani hili gamba ni gumu sana maana hata JK alipita jana MZA huku hakuna hata mtu wa kumpungia mkono,,,,,hili gamba linahitaji moto wa jehanamu kuliondoa, ni gumuuuuuuuuuuuu:smow:
 
Vitisho vya Nape ya siku 90 kwa mafisadi vinaanza kukosa nguvu kadri siku zinavyokwenda. Hakuna dalili ya mafisadi kujiondoa ndani ya CCM Dalili ni kuwa Nape na wenzake wamezidiwa na mafisadi kwani vyombe vya habari vya mafisadi havitangazi tena proganda za Nape tena. CCM imebaki na Mzalendo, uhuru magazeti ambayo hayanunuliwi na watu.

Kundi la kina Nape wanazidi kukosa waungaji mkono kwa kuwa ni wanafiki,hawasemi ukweli kuhusu chama chao na wanachama wa CCM.

Katika mitandao ya kijamii Nape anashindwa kujenga hoja.
Nafikiri Nape ana wakati mgumu kuliko kiongozi yeyote ndani ya CCM.

Nape take care!!!!!!!!!
 
Sasa nyoka amejeruhiwa sumu ni kali kuliko aliyevua gamba....mzee Mkama anasema eti UV-CCM kuongelea mafisadi ni kuleta vita kwa maana sahivi mafisadi ndo wanaofariji serikali kwa kulipa mishahara ya watumishi...aaaahaa!CCM wamelewa pombe bila kuinywa,wakiinywa je?
 
Kasema lini haya.
 
Nilishasema hakuna chama chenye wataalam wa mbinu za kisiasa kwa bara la afrika zaidi ya cdm ktk karne hii ya 21,
CCM pumzi ndogo!!!!!!! ruti hii hawaiwezi

Hivi wanajeshi wenye kiwango cha luten wakishindwa vita rikuruti wataiweza?
 
Mukama alitolea ufafanuzi alisema sio siku tisini halisi bali ni za "kiunabii". Kila siku moja inawakilisha mwezi mmoja, na kila mwezi una siku 30. Sasa Zidisha hapo ndiyo utakuwa umepata jibu la NAPE la siku 90. Msiwe na Haraka hivyo.:A S 103:
 
Unafikiri Nape kapata wapi hiyo namba ya siku 90 kama siyo kwenye vikao halali vya chama Maana alitangaza kwa bidii sana tena mno kupitia BBC, TBC, VOA na magazeti labda hofu yao wanogopa kupunguza IDADI ya wafadhiri ndani ya chama:dance:
 
Jamani hili gamba ni gumu sana maana hata JK alipita jana MZA huku hakuna hata mtu wa kumpungia mkono,,,,,hili gamba linahitaji moto wa jehanamu kuliondoa, ni gumuuuuuuuuuuuu:smow:
Si mlisema kapita bila kufungua dirisha sasa imekua stori nyingine, wewe umejuaje kama hapakuwa na watu?
 
Mkuu safi sana, nadhan wataaibika kina nape pale wasipo jivuaa. Ccm sikio la kufa!
 
CCM iliojivua magamba imeshaanza kuonekana jamani?
Ni Dar au Dodoma?
Ni ofisi za juu au kwa wananchi?
magamba yametupwa wapi? humo ndani au nje ya chama?
huyo kiumbe mpya anapendeza?

Au bado tuko kwenye drawing board ya jinsi, bajeti, na mkakakati murua wa kujivua?
 
Wapenzi wa JF, sina uhakika kama Nape Nnauye anatumia kalenda kama tunazotumia watu wengine au la! Nasema hivi kwa sababu kwa kalenda za kawaida naona siku 90 alizoahidi Nape kuwang'oa mafisadi kutoka chama chake cha magamba ndiyo zinaelekea kutimia. Maswali ninayojiuliza na labda Nape anisaidie kuyajibu;
1. Je hadi sasa ni mafisadi wangapi wamempisha kwenye chama chake cha magamba?
2. Je mapacha 3 ni kati ya hao ambao wameshampisha?
3. Je chama chake cha magamba kimeongeza mvuto kiasi gani kwa wa-tz?
4. Kama majibu ya maswali yote hayo ni hapana, kwa nini alikuwa anatupotezea nafasi kwenye vyombo vya habari na longolongo zake ambazo utekelezaji wake ni sifuri?

AKOME KABISA KUWAHADAA WA-TZ!
 
Back
Top Bottom