Tarehe 09/04/2019 vijana wa vyama vya upinzani watafanya maandamano ya kupinga azimio batili la bunge la kutofanya kazi na CAG

ILLICH

JF-Expert Member
Mar 15, 2014
237
180
Tarehe 09/04/2019 vijana wa vyama vya upinzani watafanya maandamano ya kupinga azimio batili la bunge la kutofanya kazi na CAG. Azimio hili ni uvunjaji mkubwa wa katiba. Ukiwa kijana wa nchi hii,tambua ya kwamba,kodi ya kila mtanzania inakaguliwa na CAG na kutolewa report,kupitia CAG ndio kila mtanzania anafahamu namna pesa yetu inavyotumika. CAG ameliambia bunge kuwa limeonesha "udhaifu" katika kuisimamia na kuiwajibisha serikali juu ya matumizi yasiyoidhinishwa na bunge,kuanzia shilingi trilioni 1.5 na nyongeza ya shilingi bilioni 952,zote hizi hazina majibu sahihi zimetumikaje na zimetoka hazina bila idhini ya bunge wala CAG mwenyewe..Mgogoro aliounzisha Speaker wa bunge dhidi ya CAG kisa kuambiwa udhaifu wa bunge,ni njama tu za kujaribu kumdhoofisha CAG asifanye kazi yake au kumfanya ajiuzulu..Vijana wa nchi hii tunapaswa kusimama na kumlinda CAG wetu, Prof. Mussa Assad dhidi ya hizi hujuma na uvunjifu wa katiba..Maandamano yataanzia Nyerere Square mpaka Bungeni..

#ISTANDWITHCAG
 
Back
Top Bottom