Taratibu za kuvunja ndoa ya kanisa kimahakama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taratibu za kuvunja ndoa ya kanisa kimahakama

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Ndjabu Da Dude, Oct 10, 2012.

 1. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #1
  Oct 10, 2012
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,652
  Likes Received: 409
  Trophy Points: 180
  Jee, ni taratibu zipi za kufuata ili mwanandoa aliyefunga ndoa ya Kikristo kanisani aweze kuivunja ndoa hiyo kimahakama au kisheria?

  Wataalamu wa Sheria tafadhali naomba mnifahamishe. Natanguliza shukrani.
   
 2. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #2
  Oct 10, 2012
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Ujue ndoa za kikristo kimsingi hazivunjwi, ni mpaka kifo kiwatenganishe wanandoa. Nadhani inategemea pia umefunga ndoa ya kikristo ktk madhehebu gani. Kuna madhehebu ambayo kukiwa na matatizo fulani mazito ktk ndoa, yanaweza "kuivunja" ndoa hiyo na kukupa nafasi ya kufunga. Lakini kuna madhehebu ambayo nafasi hiyo ni finyu mno-mno.
   
 3. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #3
  Oct 10, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Haivunjwagi hiyo!
   
 4. Baba Collin

  Baba Collin JF-Expert Member

  #4
  Oct 10, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 458
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mkuu kama kwel we ni muumini bora wa ndoa za kikisto kabla cjakushauri hebu jaribu kueleza tatizo la msingi linalokvafanya utake kuvunja ndo.a
   
 5. M

  MKALIKENYA JF-Expert Member

  #5
  Oct 10, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,198
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 133
  Utangulizi.
  Ndoa inaweza kuvunjwa na mahakama iwapo mambo haya yafuatayo yametokea kwenye ndoa husika na mmoja wa wanandoa kuchukua hatua ya kuomba mahakama ivunje ndoa hiyo.
  1.kufumaniwa unazini-(walau iwe mara kwa mara)
  2.ukatiri uliopitiza kwa mwenzi wako.
  3.kumtenga mwenzi wako kwa kipindi kisichopungua miaka 8,aidha kwa kuhama chumba au kuhama nyumba,mji au nchi.

  Sasa iwapo kati ya hayo niliyoyataja hapo juu yametokea mwanandoa anatakiwa kwanza aende kanisani kwa usuluhishi na ikishindika Mchungaji au Padri atatoa cheti cha kushindwa kusuluhisha, kwa faida ya watu wote iki cheti cha kushindwa kusuluhisha ni muhimu sana kwani huwezi kufungua kesi mahakama kuomba mahakama kuvunja ndoa bila kuonesha ulianzia kanisani na wakashindwa kuwasuruhisha.

  Lakini mbali na zile sababu 3 nilizosema zinaweza peleka mahakama kuvunja ndoa, ili ndoa ivunjwe lazima mahakama ijiridhishe bila kutia shaka kuwa ndoa hiyo haiwezi kutengemaa kabisa.
   
 6. m

  mamajack JF-Expert Member

  #6
  Oct 10, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  one must die ndo mwisho wa ndoa,other wise haina mwisho.
   
 7. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #7
  Oct 10, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,828
  Trophy Points: 280
  catholics hawavunji ndoa aslani kwa lolote lile on earth! Hakuna talaka! acha talaka rejea
   
 8. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #8
  Oct 10, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,932
  Likes Received: 2,084
  Trophy Points: 280
  Kwa nini unataka ivunjwe?
   
 9. Mr. Mwalu

  Mr. Mwalu JF-Expert Member

  #9
  Oct 10, 2012
  Joined: Feb 4, 2010
  Messages: 812
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 60
  kuna mwenzio alienda na suala kama lako kwa mchungaji akiomba avunje ndoa! mchungaji hakuwa na tatizo akawakubalia! akawaambia sawa njooni tuombe ili ndoa ivunjike, akaanza kusali kuomba kifo kimchukue mmoja kati ya wanandoa! kumaliza sala akajikuta amebaki mwenyewe jamaa wamesepa!
   
 10. K

  KIBONGOMKUTI JF-Expert Member

  #10
  Oct 10, 2012
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 1,415
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Fanza hivi
  1. Peleka malalamiko yako kwenye Baraza la Usuluishi linalotambulika kisheria (Ofisi ya ustawi wa Jamii, Kiongozi wa Kanisa mwenye mamlaka ya kufungisha ndoa)
  2. Baraza/Kiongozi husika atawasikiliza wanandoa wote na kuona kama anaweza kuwashauri ili msamehane na kuendelea kuishi pamoja. Kutengana kisheria/makubaliano huwa ni mbadala katika hili.
  3. Endapo usuluishi utashindikana Baraza/Kiongozi husika atakupatia Barua/Hati ya kushindwa kusuluishwa. Barua/Hati hiyo itaandikwa ikielekekzwa kupelekwa katika Mahakama husika.
  4. Ukifika Mahakamani unatakiwa kulipia gharama za kufungua Kesi ya Ndoa ili kuomba TALAKA na Kuvunja Ndoa yenu rasmi kisheria ukipenda na mgawanyo wa mali za ndoa plus matunzo ya watoto kama wapo. Kumbuka kuambatanisha Madai yako na Cheti cha ndoa
  5. Mahakama itasajili Kesi yako ya Madai ya Talaka na kukupa Hati ya kumwita Mkeo Mahakamani ili kujibu madai dhidi yake
  Angalizo;
  Sababu kubwa ya kuvunja ndoa na kutoa Talaka huwa ni KUWEZA KUITHIBITISHIA MAHAKAMA KUAMINI KUWA NDOA YAKO IMEVUNJIKA KIASI AMBACHO HAIWEZI KUREKEBISHIKA TENA.
  Aidha Mahakama uangalia mambo muhimu/vigezo vifuatavyo ili kujiridhisha
  (a) Ugoni
  (b)Ukatili
  (c)Kulawiti
  (d)Kichaa
  (e) Kuzembea wajibu kwa makusudi
  (f) Uasi/Utoro
  (g) Kutengana - kusiko pungua miaka 3
  (h) Kifungo
  (i) Dhana ya Kifo
  (j) Tofauti za Dini/Kubadili Dini

  Anyway huo ndo ushauri wangu faster lakini kwanini uvunje ndoa Bana, gangamala maisha sio mchezo etiii.
   
 11. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #11
  Oct 10, 2012
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,652
  Likes Received: 409
  Trophy Points: 180
  Tatizo kubwa ni mke kabadili kabisa muelekeo kiimani kitu ambacho kinakingana na ile imani iliyokuwapo awali wakati wa kutoa kiapo cha ndoa kanisani. Licha ya kuonywa na kukatazwa mume, pia ndugu, jamaa na hata kasisi wamemshauri aondokane na hiyo imani yake mpya, bila mafanikio. Hii inaleta hali ya kutoaminiana na kuvunjika kwa amani nyumbani.
   
 12. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #12
  Oct 10, 2012
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,652
  Likes Received: 409
  Trophy Points: 180
  Hapa naona umezungumza mambo ya maana. Jee, unaweza fafanua zaidi kuhusu kigezo cha "tofauti za dini/kubadili dini"?

  Mfano, inatosheleza kwamba mmoja wa wanandoa amebadili dhehebu ndani ya Ukristo? Asante!
   
 13. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #13
  Oct 10, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Hapa kuna utata.. labda tufafanulie hii imani imekuwake.binafsi naona hauna subira na unachukulia mambo haraka na utakuja juta.kumbuka uliapa kiapo for better for worse. kama unadhani mkeo kapotea wewe ndie mtu wa kwanza kumsaidia kurudi katika msitari. Tafuta hekima na akili ya kuishi na mkeo kwani wanawake ni viumbe dhaifu biblia inasema. Na itakuwaje kama ukioa mwingine nae abadilike utarudi tena mahakamani? Tafakari
   
 14. H

  Haika JF-Expert Member

  #14
  Oct 10, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Du!!
  Si bora kutokuifunga kabisa
  Kuna ndugu yangu mmoja sasa ni mtu mzima kabisa miaka 78
  enzi za ujana wake alikuwa na mke aliemkimbia na kumwachia kichanga, alihangaika kumafuta na kumrudisha nyumbani ikashindikana basi akapata mrembo mwingine, na wakaanza process za kuvunja ndoa ili wafunge ndoa, yani mhhh
  walipata watoto ambao kwa sasa wote wanafamilia zao, ndoa bado haijavunjika, mke mdogo sasa ameshakufa miaka 67 ndoa haijavunjika!!
  Yani hadi yule kichanga laieachwa ana mtoto ila ndoa haikuvunjika,
  Maajabu sasa yule bibi ndio anataka kurudi anadai yeye ni mke halali!!
   
 15. H

  Haika JF-Expert Member

  #15
  Oct 10, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Wengi huwa wanaondoka tu na kuanza maisha mengine bila kuafuta ndoa ingine.
  Hii ni nzuri zaidi kwani kuna uwezekano kuwa baadae akili zikitulia mtarudiana. Shida ni kama mtu bado una hasira na still unataka kufanya maamuzi.
   
 16. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #16
  Oct 10, 2012
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Mkuu, hapa hakuna ground nzito ya kuweza kujinasua kutoka ktk ndoa yako. Kubadili dini/dhehebu siyo sababu ya kuweza wewe kuvunja ndoa hiyo. Mbona zipo ndoa nyingi tu za mchanganyiko wa dini au madhehebu? Huwezi kumuacha mwenzako wa ndoa eti kwa sababu tu kaacha imani yake ya awali ambayo, nadhani, ndiyo hiyo uliyo wewe. Unapaswa kumheshimu, kujifunza kumvumilia na kuongea naye kwa upendo ili ikiwezekana arudi ktk imani yake ya awali; ikishindikana ishi naye hivyohivyo. Ndo ndoa hiyo mkuu: ndoa ndoana.

  Kama suala ni kukosekana kwa amani katika nyumba, kimbilio siyo kuvunja ndoa bali kupatanishwa, kusaidiwa kuvumiliana. Na hiyo kazi wanaweza kuifanya wachungaji wenu au kamati ya usuluhishi ya usharika/parokia, nk. Vinginevyo kama huwezi vumilia basi kimbilia mahakama za serikali upate talaka hata kama kanisani haikusaidii wewe kiroho. Ila ujue hata huko mahakama za uraiani kwa kawaida zitakurudisha kanisani ili lishughulikiwe kikanisa.
   
 17. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #17
  Oct 10, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  KIBONGOMKUTI

  Mbona huo mlolongo mkubwa mno hivyo?!

  Unaweza kukuta watu wanakuwa emotional abused kwenye ndoa wanashindwa kutoka kwa sababu hawawezi kuonyesha wazi mateso, na mmoja kati ya wana ndoa hajakubali kuwa ndoa hiyo haiwezi kuendelea tena.

  Something needs to be done, kulegeza masharti hayo.

  Hii haijakaa sawa
   
 18. Elijah

  Elijah JF-Expert Member

  #18
  Oct 10, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 1,671
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  zini hadi upate ukimwi,halafu ufe ndio utakuwa umeachana naye
   
 19. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #19
  Oct 10, 2012
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,453
  Likes Received: 7,218
  Trophy Points: 280
  kubadili imani sio sababu ya kuwatenga,kifo pekee ndicho kitawatenganisha
   
 20. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #20
  Oct 10, 2012
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,652
  Likes Received: 409
  Trophy Points: 180
  Asante kwa maoni yako. Nachotaka kufahamu ni sheria imekaaje kuhusu tatizo hili. Isitoshe jee kiapo cha ndoa kilichotolewa dhehebu moja bado kitaendelea kuwa halali kama mmoja wa wanandoa baadaye aamue kujitoa kwenye dhehebu lake na kuingia dhehebu lingine?
   
Loading...