Ashura9
JF-Expert Member
- Oct 21, 2012
- 740
- 485
Taratibu za kupata cheti cha kuzaliwa:
RITA Tanzania
Kwa mujibu wa sheria unaweza kupata cheti katika Wilaya uliyozaliwa au katika ofisi za Msajili Mkuu, Makao Makuu ya RITA katika jengo jipya la wakala la Rita Tower lililopo Mtaa wa Makunganya maeneo ya posta mpya mkabala na Club Bilcanas, Dar es Salaam.
Tafadhali fika katika ofisi zetu, utatakiwa
Nenda katika wilaya uliyozaliwa, chukua barua kutoka kwa afisa mtendaji kata wa sehemu uliyozaliwa ambayo ukiiwakilisha kwa msajili wa wilaya hiyo na msajili kujiridhisha utasajiliwa na kupata cheti. Karibu sana
Je, kama cheti cha kuzaliwa kimepotea, kupata cheti kingine natakiwa nifanyeje na ni shiling ngapi natakiwa kuwa nayo?
Tafadhali fika katika ofisi ya RITA ukiwa na taarifa zako sahihi (viambatishi vinavyoonyesha majina yako na tarehe ya kuzaliwa kama inavyosomeka kwenye cheti kilichopotea mfano nakala ya cheti hicho - Toa maelezo sahihi yafuatayo: Jina la mtoto, Jina la baba, Jina la mama, Mahali pa kuzaliwa, Tarehe sahihi ya kuzaliwa na usajili, Tarehe kilipotolewa iwapo kuna uwezekano) kisha tutaangalia kwenye kumbukumbu zetu na rekodi yako ikipatikana utalipa Tshs. 3,500 na kupatiwa cheti kingine.
Ghalama zikoje?
Tafadhali tuambie una umri gani na ulizaliwa wilaya gani, na kama una tangazo la kizazi ili tuweze kukutajia gharama ya cheti.
Ofisi ziko wapi?
Tuna ofisi kila wilaya ila makao makuu ya RITA yapo katika jengo jipya la wakala la Rita Tower lililopo Mtaa wa Makunganya maeneo ya posta mpya mkabala na Club Bilcanas, Dar es Salaam.
Ofisi ya RITA Kinondoni ipo jirani na Magomeni traffic light ukiwa unaenda Morocco. Utaona jengo limeandikwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kinondoni.
Masaa ya kazi:
siku za kazi ni kila siku kuanzia Jumatatu mpaka Ijumaa kuanzia saa 2.30 asubuhi mpaka saa 9.00 jioni.
Kwa maswali zaidi
Contacts ------>>> bonyeza hapa
Chanzo: RITA

- kujaza fomu BD 15
- halafu utaambatisha kiambatishi kimoja kati ya hivi: kadi ya kliniki, cheti cha kupigia kura (2005), pasi ya kusafiria, cheti cha kumaliza elimu ya msingi au secondary (leaving certificate), cheti cha ubatizo. Kimoja wapo kati ya vilivyo tajwa hapo utakiambatanisha kwenye fomu yako utakayoijaza
- halafu msajili atapitia maombi yako
- yakiwa sawa utaandikishwa.