Taratibu za kuomba uhamisho shule uliopangiwa form 5

Jiang Yang

Senior Member
Jul 18, 2012
182
111
Naomba kufahamishwa taratibu za kufuata katika kuomba uhamisho wa shule uliyopangiwa kidato cha 5 kwenda shule nyingine.

Natanguliza shukrani.
 
Wamesema ahamishwi mtu na ukichelewa nafasi inachukuliwa

Wana maanisha mwaka huu watu hawatasikilizwa hata kama wana matatizo na sababu muhimu kama haya?
  • Wanaopangwa mbali sana kutoka sehemu wanazoishi;
  • Walio wagonjwa wanaohitaji kuwa karibu na hospitali;
  • Wanaoomba kuhamia shule za kutwa kwa sababu za kiuchumi;
  • Wanaoomba kubadili ‘combinations’ ambazo hazipo katika shule wanazopangwa.
Ambao miaka ya nyuma wamekua wakisikilizwa.
 
Wana maanisha mwaka huu watu hawatasikilizwa hata kama wana matatizo na sababu muhimu kama haya?
  • Wanaopangwa mbali sana kutoka sehemu wanazoishi;
  • Walio wagonjwa wanaohitaji kuwa karibu na hospitali;
  • Wanaoomba kuhamia shule za kutwa kwa sababu za kiuchumi;
  • Wanaoomba kubadili ‘combinations’ ambazo hazipo katika shule wanazopangwa.
Ambao miaka ya nyuma wamekua wakisikilizwa.
Sio haki mkuu wanachokifanya sasa tamisemi ni ubabe sana mtu umefaulu vizuri masomo ya science unapelekwa arts only kwa hiyo mwaka huu watu wasome vitu wasivyovipenda lengo wafeli tu
 
Watahamisha ila baada ya kusajilwa nakusoma walau muhula.
Uhamisho upo daima, huwezi zuia binadam asihame wakati kiasilia kuhama nikutafuta nafuu ya matatizo n.k.
Wamekataa mwanafunz eti aje na taarif za uhamisho wakat wa kuripot au ktk kipind hicho cha admision mtu anataka kuhama.
Pengine mwez desemba hakutakua na vikwazo kwa anaetaka hama. Nimeexperience hivo vitu.
 
mkuu 2013 nilipangwa advanve kombi moja ya kichokko nkaikataa kwa nguvu zote nkawnda necta mzee akatoa laki tatu nibadilishwe niinde shule niipendayo na lombi niitakayo kweli sikufanikiwa walibadilisha ila walinipekea tena kombi ya kichoko n nayoitaka ilikua imejaa ikabidi niripoti tuu huko nikahama tena mwanzon kule lkabla hata mwezi haujaisha ila nilipitia process ndefu sana kkwa afisa elimu wa wilaya na mkoani pia mwalimu mkuu wa shule unayoenda adhibitishe hio nafasi hapo utahitaji usafiri na mzaz au mleZi maana mdogo unakaziwa kinoma noma. busara inahitajika. picha za passpot size zinahitajika pia afisa elimu wa wilaya unako hamia lazima adhibitishe na mkoani pia. hizi proceaa ni za lazima ukikosea hata moja uhamisho utakwamba na utaweza kosa namba ya mtihani wa taifa wa form six kama vp nipigie nikushauri mapema ndugu yangu.
 
hizi proceaa ni za lazima ukikosea hata moja uhamisho utakwamba na utaweza kosa namba ya mtihani wa taifa wa form six kama vp nipigie nikushauri mapema ndugu yangu.

Nashukuru sana, ngoja nikuchek inbox
 
Back
Top Bottom