Taratibu za kufuata ili kumiliki Silaha ya Moto Tanzania

Je, ukimiliki silaha unaruhusiwa kusafiri nayo nje ya mkoa???

Je, mmiliki akihama atapaswa kuwajulisha kule alikohamia kwamba anamiliki silaha????

Naomba kujua masharti baada ya kupewa kibali cha kumiliki silaha.

Ahsanteni wadau
 
Wangeuza kama simu heshima ingekuwepo.
Nchi zote ambazo wanauza silaha kama simu kuna adabu na watawala pia wana adabu mfano tu zambia kwa afrika. Serikali ikileta timbwili mtaani kila mtu ana mguu wa kuku hadi sub machine gun smg.
 
Sifa ya kwanza upimwe akili,2 una Mali isiyo pungua m50 3:ushapata mashambulio mangapi ya kuvamiwa4: je nimlevi kupita kiasi,5: hauna tamaa ya Mali zingine tofauti na ulizo nazo maana usiitumie kujipatia Mali zingine 6: usiwe na wifu wa kimapenzi,nk
 
Tanganyika Arms kule mjini Dar utapata majibu yote. Mashine nzuri ya "kiume" ipo around TZS. 4.5M. Kawaida ukilipia unaiacha pale na kupewa forms za kupeleka serikali za mitaa na kwingineko. Unaw4za kuimiliki ndani ya miezi mitatu au zaidi ya mwaka
 
Za asubuhi wanaJF. N siku nyingine tena mapambano yanaendelea. Tunapambana.

Nataka kumiliki bastola kisheria kwa ajili ya ulinzi binafsi kutokana na nature ya shughuli yangu.

1. Je, taratibu zake zikoje?

2. Gharama za kununua bastola zikoje?

3. Ipi bastola nzuri?

4. Kuilipia kwa mwaka ni TZS ngapi?

5. Mchakato mpaka unaimiliki unachukua muda gani?

6.Criteria au vigezo vya kuimiliki vikoje?

Naombeni mawazo yenu wakuu.

Asanteni.
Katika mambo ya maana ambayo umejitahidi kuuliza humu jf basi hili linaongoza , kujilinda ni haki ya kikatiba , sijui wabongo ni masikini au hawajui tu , kwa maelezo zaidi nipigie simu .
 
Habarini wana JF,

Nahitaji sana kumiliki silaha kwa ajili ya ulinzi binafsi, iwe Bastola au hata SMG.

Sina ufahamu wa kutosha njia the rahisi au fupi ya kuomba(kihalali) na kumiliki silaha hiyo. Ninachofahamu tu kuna maduka ya silaha hizi na kuna urasimu mwingi hadi kuruhusiwa umiliki wa silaha hizi.

Naomba wenye ufahamu, mnisaidie humu namna nyepesi ili kufanikisha umiliki huo.

Ahsanteni, nawakilisha.
16179ef387ccd927d2a6873f04932990.jpg

0b766ee1f26d750181b6418f0f192fc4.jpg
Andika barua kwa mkuu wa wilaya yako ukimweleza kusudio/ombi la kutaka kumiliki Silaha ya Moto, kwenye barua hiyo umCC Mwenyekiti Seikali ya mtaa wako na afisa mtendaji wa kata yako, Utaratibu Utajadiliwa na kamati ya ulinzi ya mtaa,Kata na ya wilaya, ukikidhi vigezo unapewa kibali cha kwenda kununua silaha *angalizo* Usianze kwenda kununua kabla ya kibali wanaweza kupokea pesa na wakakupa risiti badala ya silaha na maelekezo kashughulikie KIBALI
 
Hamna namna nyepesi! Namna ni kufuata utaratibu unaanza kujadiliwa kwenye vikao vya serikali za mtaa then unaenda kwa OCD, akipitisha inapelekwa kamati ya ulinzi na usalama wilaya na process nyingine then unapewa kama itakuwa umekidhi.
 
unataka ujiyoe muhanga? kama sababu ndio hiyo sema nikuoneshe wapi utaipata chap
 
Back
Top Bottom