Taratibu za kufikisha kesi Mahakamani zikoje? naomba nifafanuliwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taratibu za kufikisha kesi Mahakamani zikoje? naomba nifafanuliwe

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by PascalFlx, Jun 21, 2011.

 1. P

  PascalFlx Member

  #1
  Jun 21, 2011
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 68
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi karibuni nimekuwa nikijiuliza maswali mengi sana na nimeshindwa kabisa kupata jibu kamili kwa matazamo wangu ulikuwa ni tofauti kabisa na ninayoyaona sasa yakitendeka.
  Kwanza kabisa nilidhani Usalama wa Taifa, Polisi na Mahakama ni sekta moja inayofanya kazi kwa ushirikiano na haifungamani na upande wowote.
  na nilijua kuwa uchunguzi ukikamilika Polisi wanapeleka mahakamani kufunguliwa kesi ila kutokana na maneno yanayozungumzwa na wanasiasa sasa nashindwa kabisa kupata picha halisi.
  Maana naona kama kwa Tanzania mara baada ya uchunguzi kufanyika matokea ya uchunguzi yanapelekwa kwanza Serikalini au kwa wafanyabiashara kabla ya Kesi yenyewe kupelekwa mahakamani au kufunguliwa kesi.
  Kwani tumeshawasikia wafanyabiashara mbalimbali wakisema kuwa wanayo majina ya mafisadi, na Viongozi mbalimbali wa Serikali wakisema nao hali kadhalika kuwa wanayomajina ya mafisadi na mengi mengineyo lakini je utaratibu ukoje?
  Je Viongozi wa serikali wanaruhusiwa kuzuia ushahidi uliokamilika kupelekwa mahakani..,

  Hebu jama ni wanasheria naomba mnisaidie katika hili tuwekane wazi ili siku nyingine mtu akisema anamajina ya wahalifu tuweze kumuuliza maswali kutokana na sheria yetu inavyosema
   
Loading...