Taratibu za kufanya kazi bila kibali TANZANIA. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taratibu za kufanya kazi bila kibali TANZANIA.

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Mayolela, Oct 2, 2009.

 1. M

  Mayolela JF-Expert Member

  #1
  Oct 2, 2009
  Joined: Sep 21, 2009
  Messages: 383
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimeleta kama tangazo ,lakini ni kero ambayo,mimi mtanzania mzalendo ninayo-mbona kuna wahamiahaji haramu wengi sana hapa Tanzania,tofauti na majirani zetu k.m Kenya,DRC nk.Wapo tu na wanafanya kazi bila kuwa na vibali,ukitoa taarifa uhamihaji wanakamatwa lakini baada ya siku 2 ,wnanarudi tena ,waliwa wamepewa mbinu na watu wa uhamihaji haohao,baada ya kutoa Rushwa.

  Hivi hili nalo mpaka Rais na Pm wafuatilie,waziri Masha anafanya nini?

  Hii pia ni kero sasa hapa nchini kwani wakenya,wamalawi wapo wengi sana wakifanya kazi hata za ufagizi hata u-house boy.Nenda Kenya au Zambia kama wewe mtanzania utafanya kazi yoyote,zaidi ya kurudishwa kwenu.

  Jamani naomba kuwasilisha.
   
 2. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #2
  Oct 2, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Ila kweli watu wa Malawi wamejaa sana, zaidi wapo sehemu za mikocheni B, Masaki na o'bay wanafanya kazi za house gal na house boy. Tena baadhi wanafanya kazi kwa vigogo wa nchi na hawafanywi chochote, zaidi wanasifiwa kwamba ni waaminifu na wachapa kazi.
   
 3. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #3
  Oct 2, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Masha kafanya kosa gani kwenye hili jambo?. Wahamiaji haramu wamekuwepo Tanzania toka enzi na enzi, huyu Masha kaja jana tu kwanini unataka kuanza kumrushia madongo?. Wasomali wangapi wana passport za ki-tanzania ambazo walizipata miaka mingi iliyopita kabla ya Masha kuwa waziri?.

  Jambo la kupigia kelele ni Rushwa ambayo imezagaa Tanzania nzima, watanzania wote ikiwa ni pamoja na wewe ni wa kubebe lawama hizi kwani watoa na wapokea rushwa ni watanzania.
   
 4. Mama Subi

  Mama Subi Member

  #4
  Oct 2, 2009
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 88
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 15
  Ukweli ni kwamba ma expatriates wengi na wafanyakazi wa mashirika ya kimataifa (including the UN) wana prefer wafanyakazi wanaoweza kuzungumza kiingereza. Sasa hawa kaka na dada zetu hapo ni zero. Halafu pia, sisi watanzania wengu wavivu mno. Mimi nazungumza kama mama ninaeajiri house girl na house boy na pia kama muajiri ofisini.

  Watanzania lazima tubadilike kiutendaji. Tupende kufanya kazi. Tuwe waaminifu na diligent. La sivyo tutamezwa na wahamiaji in all sectors of the econony (especially na hii protocol ya kufungua mipaka ya East Africa).
   
 5. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #5
  Oct 2, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Sasa suluhisho ni nn kifanyike mama? Au ndo twendelee kulala bila majibu.
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  Oct 2, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Tatizo litatatuliwa kwa kufanya yafuatayo kwa sanjari:

  kukomesha rushwa kwa kuwa na law enforcers and well equiped na wanaolipwa vizuri
  kuwa na database itakayoweka record zote za kila mTz.
  kila mTz kupewa kitambulisho cha taifa
  kuwa na sheria zitakazo attrct wageni wote kujiandikisha.

  etc

  Haya ni mawazo yangu tu.
   
 7. Lyceum

  Lyceum JF-Expert Member

  #7
  Oct 2, 2009
  Joined: Oct 1, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 80
  Ni aibu maana these days kuna hadi housegirls hapa dar wanaotoka malawi wasio na vibali. Its a pity
   
 8. Kiroroma

  Kiroroma JF-Expert Member

  #8
  Oct 2, 2009
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Shame on you mama Subi,Again shame on you!!!!Yaani unawatetea wageni haramu kwa kisingizio cha uvivu na umaimuna wa Watanzania????AJABU SANA!!!Shule mmedumaza nyie kwa ubinafsi wenu!!Uvivu mmeusababisha nyie kwa kung'ang'ania ofisi.Sisi tufanye nini ali hali unajua hatuna kisomo kwa sababu mapesa yote ya kuwalipa waalimu mmejengea majumba makubwa ingali kulala kwenyewe chumba kimoja!!!Watoto wenu wanasoma Uingereza na Marekani,I weje sisi walala hoi utuite wavivu na tusiolonga ung'eng'e?
  Haingii akili kwa mama kama wewe kuyasema maneno kama hayo!!Unajua wazi ndugu zako kule Dabaga hawana elimu kwa sababu unazozijua wewe!!U binafsi umetawala roho za watanzania walioko madarakani nawe ukiwa mmojawapo wa kutoa ajira kwa upendeleo na rushwa.Angalia magari ya kifahari,mijumba ya ajabu barabara hakuna huduma za jamii hakuna.Elimu imedumaa,sera za nchi zimeyumba,watoto wanakufa kabla ya kuzaliwa vifo vya kina mama,maradhi ya kuambukiza ,rushwa imetawala,Wewe unakalia kusema watz ni wavivu hawajui kiingereza ndani ya nchi yao hivyo ajira kwa wageni ni halali.Tafadhali sahihisha lugha yako na kuwaomba radhi walalahoi wote wa nchi hii.Acha hizo Masaki mnakaa kuajiri wageni haramu huku ndugu zenu kule Sengerema hawana chakula,maji,mavazi ,elimu nk
   
 9. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #9
  Oct 2, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  aaah kwanza hapa nchini kwetu hilo swala hata sielewi ......maana hata wakati wanaingia sidhani kama serikali huwa inataarifa kama hawa watu wapo mpaka washituliwe

  Hivi TRA ipo au ilishakufa???
   
 10. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #10
  Oct 2, 2009
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Asante Kiroroma, you said it all! Hawa watu wa aina hii wanaotetea ujinga ndo wanasababisha kila siku nchi hii tunaonekana mazezeta. aNASEMA WATANZANIA WAVIVU SI KWELI NI Mismanagement of people na dharau kwa watu wenu ndo inasababisha haya yote. We unaajiri housegal kutoka iringa unataka umlipe elfu ishirini au thelathini kwa mwezi wakati anakutunzia nyumba yako na watoto wako na kufanya kazi zote hata ambazo ulitakiwa ufanye wewe. lakini hao wamalawi mnawalipa elfu sitini hadi themanini, halafu unakuja hapa kusema watanzania wavivu si kweli.

  Na kusema hawajui kiingereza, kama wewe ulibahatika kwa sababu za kifisadi au zingine ukapata elimu bora kwenye st nanihii au ulaya huna sababu ya kuwabeza hawa ambao kwa sababu moja au nyingine hawakubahatika kupata shule nzuri na elimu bora. Btw si wao wa kulaumiwa bali ni mfumo wa elimu mbovu hapa nchini.

  Na mbaya zaidi ni nyiniy mlio na nafasi huko serikalini au mahali pengine kwenye nafasi ya kuleta mabadiliko lakini mmekuwa wabinafsi .

  shame on you mama Subi na uombe radhi kwa maneno kama haya, hayajengi bali ni dharau.
   
 11. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #11
  Oct 2, 2009
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hapo highlighted futa kabisa, waajiri kama nyie hamfai kabisa katika nchi hii na tena ndo mnaoturudisha nyuma, no wonder tunao ma office assistant kutoka kenya kwenye ofisi zetu wakati watu wamejaa nchi hii jobless, una uzalendo gani na nchi hii kama kazi zote unawapa wageni tena ukiwa mstari wa mbele kutoa rushwa uhamiaji ili wapate working permit leave alone those who wortk freely without the permit/

  Hii dhana ya kwamba Tanzania hatuna watu able ni potofu kabisa na kwa taarifa yenu hata maendeleo hayaji kwa sababu hizi maana wengi wakipata mishahara hiyo wanatuma makwao so hakuna tanzania inachonufaika nacho kabisa.
  Tena kinachouma, wao mnawapa mishahara mikubwa maofisini kushinda wazawa kwa sababu tu akili zenu zinaamini kuwa wao ni bora kuliko watanzania. I am so sick of this ah!
   
 12. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #12
  Oct 2, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Sasa naona Tanzanians ndiyo mnaanza kushituka, lakini its too late! suala la uhamiaji haramu si suala la Tanzania peke yake, hata unavyosema Kenya hakuna wahamiaji haramu sijui unatumia data za wapi, Binafsi nimefanya kazi mbalimbali kwa muda wa miaka mitatu, Uganda nimefanya kazi Miaka miwili, Rwanda, Zambia, Botwana, Nigeria, S.A, UAE, bila kutaja bara la ulaya na amerikana, achilia mbali Marekani amabako kulikuwa kimbilio kubwa kwa watanzani awengi hata siku za karibuni. Kinachotuua watanzania ni kuchagua kazi, na kufanya kazi kwa kutesti zali, watanzania wengi tuna tamaa, siyo rilayabo. Opotunities zipo kibao hapa tanzania, na suala la sisi kuzitafuta halipo, tumebaki kusema kila nafasi inayotangazwa itakuwa na mwenyewe! enzi za kuletewa barua ya ajira nyumbani kwenu zilishapitwa. Kuwalaumu Wakenya na wamalawi ni mwanzo wa chuki tu kama za wenzetu wa kule S.A, chuki zilizopelekea waafrika kuuana. Kama wewe bado umelala ujue ndiyo umeliwa, EAC inakuja kasi, kama haujaenda shule na haunakile ambacho soko la ajira linakitaka utabakia kuwa mwanasiasa wa kijiweni. Maisha ya sasa ni kupigana, Wakongo wanaona watanzania wanadharau sekta ya kosmetology kwa nini wasije kuchukua pesa? Sitetei wahamiaji haramu, ila tujue mhamiaji huangalie sehemu yenye fulsa nyingi za wazi. Cha kufanya ni kuhakikisha tu kkuwa Wageni wanaingia na kukaa kihalali bila kuvuruga amani, na hiyo ni kazi ya Uhamiaji.

  Kama bado umelala amka mapema sana, mapema kabla serikali haijagundua kama inaupungufu wa nguvukazi na kuamua kutangazi watu wote wa dunia wenye ujuzi flani WAJE bongo (angalia mwakani UDOM itakuwa na Maprof. wangapi toka India), angali Rwanda ina waalimu wangapi kutoka Tanzania, angalia marekani ina machinga wangapi kutoka India. Tujifunze kusoma ala ma za nyakati na kubadilika kiujuzi na mori ili kukidhi mahitaji ya ajira na fulsa za kujiajiri. Bado mashamba yako mengi Ruvuma, Kigoma, Mara, Mbeya Iringa, na Morogoro, lakin i hatutaki kulima mpaka tupewe matrekta, ninani akupe trekta wakati hata hujakata miti, kama haujaandaa mradi kuwakonvisi wenye pesa kuwa biashara yako italipa!

  Mi nadhani ingekuwa bora kabisa kama mahouse girl na wafagia barabara wote wangetoka malawi na Congo, halafu Malawi kukajaa Madaktari kutoka TANZANIA. Tuachane na chuki zisizomaana, unamchukia mtu kisa anafanya kazi ambayo wewe ullikuwa ukiitaka lakini hukuihangaikia. Sitaki kuamini kama shida na tabu za watanzai zinaletwa na Wamalawi au Wakenya, shida zetu zinaletwa na sisi wenyewe.
   
 13. B

  Bao3 JF-Expert Member

  #13
  Oct 2, 2009
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 318
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hizo ni changamoto za kutufanya tuongeze ujuzi wadau. Soko la pamoja ajira litakapoanza sijui wabongo tutakua wapi. Kama hata kazi zisizo na ujuzi tunazikosa hapa kwetu je zile zingine zinazohitaji ung'eng'e mkali zaidi(sales/marketing,tourism,public relations) watz wataweza kuzipata huko Kenya,Uganda,Zambia,Malawi? Ila hiyo isiwe sababu ya wanaopaswa kukontrol uingiaji wa wahamiaji haram,at least kwa kipindi hiki,kutofanya kazi yao ipasavyo. Waendelee kudhibiti wahamiaji haram mpaka pale soko la africa mashariki litakapoanza(kama kweli kitu hicho kipo).
   
 14. Shishye

  Shishye JF-Expert Member

  #14
  Oct 2, 2009
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umesema vizuri mkuu isipokuwa umechanganya masomo kidooogo. Hatuwazuii wageni (wala hatuwezi kuwazuia) kuja kufanya kazi hapa kwetu kama nafasi zipo, sawa na ambavyo sisi tunafanya kwao. Swala ni kwamba je, wanafuata taratibu zinazotakiwa kuingia nchini?

  Hao mahausi eli na boys wna vibali vinavyowaruhusu kisheria kuwemo nchini na kufanya kazi? Kama hawana, wanaishi kinyume cha sheria na haijalishi ni wachapa kazi kiasi gani au wanajua kimombo kiasi gani; wala haijalishi wanafanya kazi kwa kigogo gani; wanatakiwa warudishwe makwao.

  Ni ukweli usiopingika kwamba kama wapo bila vibali na wanafanya kazi, wizara inayohusika imezembea. Haijalishi tatizo limeanza zamani gani, aliyepo hivi sasa ni mzigo wake. Lazima wizara iweke mkakati wa kuzuia hiyo hali. Hata Marekani na nchi nyingine wana sheria za kuwadhibiti, pindi ukigundulika tu unatimuliwa.

  Kama wizara haijatangaza mikakati ya kuwazuia kufanya kazi, muajiri atakuwa hana kosa kumpa kazi. Mpaka wizara itapokuwa imeweka utaratibu huo wazi kwa umma, then hata hao vigogo wataogopa kuwaajiri maana watajua ni kukiuka sheria na ni tu kama wakipatikana watachukuliwa hatua. Ila kama ni mambo haya haya ya kitu kidogo... haisaidii chochote.
   
 15. m

  manyusi JF-Expert Member

  #15
  Oct 2, 2009
  Joined: Mar 3, 2009
  Messages: 274
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Hao mabwana wa uhamiaji wamegeuza sehemu yao ya kazi kuwa ya kuvuna pesa,wala usishangae mtanzania tatizo sehemu muhimu kama uhamiaji wanaofanya kazi si wazalendo wanachojali ni mslahi yao binafsi kuna watu wa uhamiaji wako kwenye pay roll za baadhi ya makampuni kwa hiyo hilo wala hata lisikupe shaka,hayo mambo yapo na rushwa ndo nyumbani kwake pale uhamiaji,mimi nimefanya kazi na raia wa Sri lanka bila kibali kwa karibia mwaka mzima wakija uhamiaji wanaangalia wanatoka wala hata hawaulizi swali kama unavyojua hawa watu wa sri lanka wanavyojua kuvaa mabomu kuna siku tutalipukiwa ndo serikali itafumbua macho.Hakuna aliye mzalendo kuanzia kiongozi wa juu mpaka wa mwisho mara ngapi tumelalamika kuhusu raia wa china walioko kariakoo wanaouza maua umeona hatua gani imechukuliwa?hakuna cha wziri mdogo wala mkubwa wote sawa tu.
   
 16. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #16
  Oct 2, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Inashangaza sana yani! wamalawi kibao, kiingereza hawajui, kiswahili hawajui!! na bado watu wanawaajiri.

  mke wangu aliwahi kutaka kuajiri mmoja ,ikamwambia huwezi kuajiri mkimbizi asiye-rasmi. kimsingi wamekimbia kwao njaa kali sio kwamba wameona huku ajira nje nje.

  kwani kuna wazungu wangapi wanang'ang'ania kuja bongo kwa kazi za kipuuzi tu bora apate income ya kum-sustain?
   
Loading...