Taratibu za kipagani katika mfumo wetu wa maisha 1 ( majira ya mwaka)

Da Vinci XV

JF-Expert Member
Dec 7, 2019
3,837
6,372
MIEZI YETU NDANI YA MWAKA NA MILA ZA WAPAGANI

Naam
Asilimia kubwa ya wengi wetu tunaamini katika Mungu hilo hata mimi nlifundishwa tangu wakati ule nipo madrasa kule jang'ombe zanzibar.

Na kama tujuavyo Historia tangu kipindi cha Eve na Adam mpaka sasa ni vita kati ya shetani na watoto wa Adamu ili kuhakikisha anawatoa katika mstari ule wa Mungu na kuwavuta kwake.

Kuna mambo mengi sana ikiwemo . Mila, desturi, dini , Ibada, na Life style kwa Ujumla ambayo shetani muasisi wa maovu duniani anajaribu kupenyeza kwenye utaratibu wa maisha kuhakikisha mwanadam anakwenda kinyume na utaratibu wa mungu

Tutaelezea mambo tofauti tofauti katika nyuzi tofauti tofauti,lakini leo tuanze na Wapagan ( haswa warumi na wagiriki) walivyointroduce mila zao na kupachika majina ya miungu yao katika utaratibu wa majira na kalenda ya mwaka)


Maandiko ya kitabu cha Biblia kupitia kinywa cha Nabii Daniel ,kimelielezea jambo hili katika ndoto yake ya mwaka wa 587 B.C

Naye atanena maneno kinyume chake yeye aliye juu naye atawadhohofisha watakatifu wake aliye juu , naye ataazimu kubadili majira na sheria DANIEL 7: 25

Majira ambayo ni hesabu ya mzunguko wa mwaka mzima, katika vipindi vinne tofauti , yaani masika kiangazi , kifukwe na Vuli
Katika kipindi hiki kuna miezi kumi na mbili ambayo Mwanyezimungu aliitaja kwa wana wa Israel

Warumi na Wagiriki walipotawala Yerusalemu waliondoa kabisa mila na desturi za waisraeli,ili kupoteza mafundisho matakatifu na mema ya Mungu

Wana wa Israel walifundishwa majina ya miezi Kumi na mbili kwa Lugha ya Kiebrania

mwanyezimungu aliitaja miezi hiyo kama ifiatavyo

ABIB- Mwezi wa 1
Ziv(iyar) - Mwezi wa 2
SIVAN - Mwezi wa 3
TAMUZ - Mwezi wa 4
ABI - Mwezi wa 5
ELUL - Mwezi wa 6
ETHANIMU - Mwezi wa 7
BULI (heshvan) - mwezi wa 8
KISLEV - Mwezi wa 9
TEBETH - Mwezi wa 10
SHEBETH - mwezi wa 11
ADAR - Mwezi wa 12

Wanahistoria wanatueleza ya kwamba warumi walipoitawala dunia walikuwa na hamu kubwa ya kuingiza utartibu na desturi zao katika mataifa ya duniani kwa ujumla.
Miongoni mwa mila hizo ni kulazimisha miungu yo yote itambulike na iabudiwe na watu wote kwa namna moja au nyingine

Kuna mengi ya kueleze kuhusu mila nyingi zilizoingizwa katika mfumo wetu wa maisha pasi na sisi kujua tutaendelea kujuzana kupitia nyuzi tofauti tofauti leo tuanze na majira ya mwaka ambapo ni miungu ya kipagani ikiingizwa katika mfumo wa maisha ya majira yetu na miezi yetu 12




JANUARI





Jina hili linatokana na jina la mungu wa kipagani (kirumi) aitwaye Janusi, huyu alikuwa ni mungu mwanamume aliyeabudiwa siku 30 za mwezi
Mungu huyu ambaye ndiye wa kwanza kw heshima katika mwaka ana sura mbili zenye kufanana mungu janusi aliabudiwa na kuaminika kama Mungu wa Ulinzi katika milango( Gates) ya nyumba na roho na ndiyo mungu wa mwaka.


FEBRUARY



Huyu alikuwa mungu mwanamke , alikuwa ni mke wa Janusi ,huyu alikuwa akienda hedhi siku 3 na ndiyo sababu hakuabudiwa katma mumewe ,warumi waliamini kuwa mungu huyu ni Utakaso na ustawi kwa wanaadmu jina jingine alijulikana kama februs au Faunus




MARCH


Ni jina la mungu wa kiyunani (kigiriki) aliyeitwa Mars, wagiriki walimwabudu mungu huyu kama mungu wa mabadiliko ya majira ya Mwaka na mungu huyu kwa warumi alikuwa ni mwanamume ila wagiriki alikuwa ni wakike




APRIL

Jina linalotokana na mungu wa kirumie aliyeitwa Aprieel ,huyu walimwabudu kama mungu wa Maradhi na mabadiliko ya hali ya hewa






MAY

Jina hili linatokana na jina la mungu wa kipagani aliyeitwa Maiya huyu alikuwa mungu wa kike wa na mungu wa tano katika mtiririko wa miungu hiyo ya kipagani




JUNE


Huyu alikuwa ndiye mungu wa kike aliyesimamia mambo yote ya kike kama Ndoa, Hedhi, Urembo, Uzazi na mambo mengine
Mungu huyu wagiriki na warumi walimtambua kwa jina la Juno




JULY



Hili ni jina la mfalme wa warumi Kaisari Julius,aliyetawala katika taifa hilo jina ili liliingizwa katika kalenda ya kirumi mnamo mwaka 482(AD)


AUGUST


Hili ni jina la baba yake kaisari julius aliyeitwa Augustos nayeye alipewa heshima ya Uungu katika taifa la Rumi



SEPTEMBER



Neno hili linatokana na jina la mungu septic , au septem mungu wa sabini katika mlolongo wa miungu 300+ ya warumi, naye alipata nafasi ya kuingia katika kalenda




OCTOBER





Huyu alikuwa mungu wa bahari na Mavuno heshima ya jina lake imetokana na neno Octo (Octopus -pweza) huyo alikuwa msimamizi wa maji na viumbe vya huko baharini



NOVEMBER

Huyu alikuwa mungu wa kiume wa kipagani naye aliabudiwa na kuingizwa katika mlolongowa kalenda,alijulikana kama novern




DECEMBER



Huyu alikuwa mungu wa kipagani wa majira na mfungo wa mwaka , alijulikana kama Decern alikuwa ni mungu wa kike aliyewakilisha kufunga mwaka na kuanza mwaka mwingine.




NB: sio kwa ajili ya kule mgongano wowote wa kiimani
Moderator zingatieni hilo


Nyuzi nyingine tutashukana mambo mengine







Da Vinci XV
 
JANUARY- janus

7FA61E64-7FD2-463B-97CB-8852CE300CD3.jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom