Taratibu gani nifuate nipate kibali cha kusafirisha mazao nje ya nchi?

Barikiel

JF-Expert Member
Feb 2, 2014
403
401
Habarini za asubuhi wadau,

Nipende kumshukuru MUNGU kwa kutupatia siku nyingine ya leo. Nilikua naomba msaada wa kujua hili jambo.

Natamani nifanye biashara ya mazao kupeleka nje ya nchi. Tatizo ni vibali au niseme kibali, ni utaratibu upi nitumie ili niweze kupata vibali? Nianzie wapi kupata vibali.

Mazao ninayotaka kuyafanyia biashara ni Mahindi, Maharagwe, na Mchele. Kwa anaefaham taratibu tafadhali.

Asanteni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom