ELNIN0
JF-Expert Member
- Nov 26, 2009
- 4,161
- 1,460
Wana Jamii,
Tarafa ya Kitunda wilaya ya Sikonge ( kabla ya Sikonge kuwa wilaya ilikuwa ipo chini ya wilaya ya Tabora Vijijini) haikawahi tembelewa na Rais yoyote wa nchi hii tangu uhuru.
Si lazima rais atembelee tarafa zote ila mkoa wa tabora wa ujumla umekuwa ukisahaulika sana katika masuala ya ugeni wa kitaifa, mimi binafsi mpaka namaliza darasa la saba sikuwahi kumwona Rais wa nchi wa wakati huo tulikuwa tunamsoma tu kwenye vitabu.
Nimefurahi sana kwamba Rais yupo Tabora katika shughuli maalum ya Siku ya wanawake duniani - baada ya hapo atakwenda moja kwa moja kitunda kuitembelea tarafa hii
Kwa mantihi hii kuna wakazi walio wengi wa tarafa hii hawajawahi kumwona Rais yoyote wa nchi hii tangu uhuru hadi leo- kwa hiyo safari hii itakuwa mara yao ya kwanza kumwona JK live - naona wanyamwezi wataimba Neema imefunuliwa.....
Mtaniuliza hii tarafa ipo wapi hadi kiongozi asiweze kufika kwa miaka takribani 49?
Tarafa hii ipo kusini kabisa - mpakani na mkoa wa Tabora na Mbeya wilaya ya Rugwe. kwa hiyo mtu anayetoka mikoa ya kanda ya ziwa anakwena Mbeya njia rahisi sana ni kupitia Tabora mjini - Sikonge - Ipole - KITUNDA - Rungwe then Mbeya mjini - kama km 500 tu approx.
Tarafa hii ipo nyumba sana kimaendeleo, ni kama vile imesahaulika kabisa - na sina uhakika Rais atatumia usafiri gani kufika kule - may be Helkopita - njia ya barabara na majira haya ya masika ni riski sana - haipitiki kwa urahisi.