Tarafa hii haijawahi tembelewa na Rais tangu Uhuru

ELNIN0

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
4,161
1,460
Wana Jamii,

Tarafa ya Kitunda wilaya ya Sikonge ( kabla ya Sikonge kuwa wilaya ilikuwa ipo chini ya wilaya ya Tabora Vijijini) haikawahi tembelewa na Rais yoyote wa nchi hii tangu uhuru.

Si lazima rais atembelee tarafa zote ila mkoa wa tabora wa ujumla umekuwa ukisahaulika sana katika masuala ya ugeni wa kitaifa, mimi binafsi mpaka namaliza darasa la saba sikuwahi kumwona Rais wa nchi wa wakati huo tulikuwa tunamsoma tu kwenye vitabu.

Nimefurahi sana kwamba Rais yupo Tabora katika shughuli maalum ya Siku ya wanawake duniani - baada ya hapo atakwenda moja kwa moja kitunda kuitembelea tarafa hii

Kwa mantihi hii kuna wakazi walio wengi wa tarafa hii hawajawahi kumwona Rais yoyote wa nchi hii tangu uhuru hadi leo- kwa hiyo safari hii itakuwa mara yao ya kwanza kumwona JK live - naona wanyamwezi wataimba Neema imefunuliwa.....

Mtaniuliza hii tarafa ipo wapi hadi kiongozi asiweze kufika kwa miaka takribani 49?
Tarafa hii ipo kusini kabisa - mpakani na mkoa wa Tabora na Mbeya wilaya ya Rugwe. kwa hiyo mtu anayetoka mikoa ya kanda ya ziwa anakwena Mbeya njia rahisi sana ni kupitia Tabora mjini - Sikonge - Ipole - KITUNDA - Rungwe then Mbeya mjini - kama km 500 tu approx.

Tarafa hii ipo nyumba sana kimaendeleo, ni kama vile imesahaulika kabisa - na sina uhakika Rais atatumia usafiri gani kufika kule - may be Helkopita - njia ya barabara na majira haya ya masika ni riski sana - haipitiki kwa urahisi.
 
Mbona zipo tarafa nyingi tu au maeneo mengi tu amabyo hayajawahi kutembelewa na Rais yeyote?na hata viongozi wengine wakuu labda mbunge tu wa jimbo husika.
 
Mimi nawaomba hao wakazi wahamie sehemu nyingine amabako rais anapitapita kama ni muhimu saana(mfano Chalinze marais wote wamepita pale zaidi ya mara moja)
 
Mimi nawaomba hao wakazi wahamie sehemu nyingine amabako rais anapitapita kama ni muhimu saana(mfano Chalinze marais wote wamepita pale zaidi ya mara moja)

Main point hapa ni kwamba kuna baadhi ya mikoa ina priority kubwa sana kuliko mingine.
Mikoa yenye matatizo na ipo nyumba sana ki maendelea ni hii ifuatayo
1. Kigoma
2. Rukwa
3 Tabora
4 Singida
5 Lindi
6 Mtwara

huwezi kulinganisha na mikoa kama Kilimanjaro, Arusha ambaya ina upendeleo hadi ngazi ya vitongoji..
Mf. Serikali inaamua kupanua barabara Chalinze - Segera wakati mikoa mingine haina hata barabara ya kuunganisha mkoa na mkoa. Mfano hakuna barabara ya kuunganisha Tabora na Kigoma, Rukwa wakati mikoa hii ni jirani.

Kuna watu JF hata hawajui Rukwa kukoje - aisee ni hatari tupu ukiambiwa unahamishiwa huko - kipindi cha mvua hakuna kwenda wilayani kuchukua mshahara hadi masika iishe.
 
Hizi ni dalili za ubunifu hafifu katika kutafuta habari.
Hii ya rais kutembelea kaeneo fulani kwa mara ya kwanza haina hata sifa ya kuwa historia, kama tutaichukulia hii kama historia maana yake hata siku akija mtaani kwetu ambao hapo kabla hakukuwa na sababu ya kutembelewa na kiongozi yeyote wa kitaifa siku akitembelea tutaita tukio la kihistoria.

Hivi tutakuwa na matukio mangapi ya kihistoria. Kwa historia iliyowekwa leo watalii wataweza kuwa wanatembelea hapo kwa kuwa ni sehemu ya kihistoria?

Naamini jibu litakuwa hapana, na hivyo siyo tukio la kihistoria eneo husika kutembelewa na HE JK.
 
Main point hapa ni kwamba kuna baadhi ya mikoa ina priority kubwa sana kuliko mingine.
Mikoa yenye matatizo na ipo nyumba sana ki maendelea ni hii ifuatayo
1. Kigoma
2. Rukwa
3 Tabora
4 Singida
5 Lindi
6 Mtwara
.

Wananchi wa mikoa hii yote (ukitoa labda Kigoma) nadhani are happy with the status-quo. Wanapeleka bungeni 100% wabunge wa CCM tangu uhuru (of course na mwaka huu watafanya hivyo hivyo)
 
Hata akitembelea ndio ni aje? Maji ya kisima yatageuka maziwa? au barabara za vumbi zitageuka fly-overs. Mikokoteni ya kukokota na mbuzi itageuka maglev?
 
Hata akitembelea ndio ni aje? Maji ya kisima yatageuka maziwa? au barabara za vumbi zitageuka fly-overs. Mikokoteni ya kukokota na mbuzi itageuka maglev?

kwa hiyo mkuu hizi ziara za viongozi katika wilaya na tarafa na vijiji ktk nchi yetu huwa na maudhui gani kwa ujumla?
 
Hata akitembelea ndio ni aje? Maji ya kisima yatageuka maziwa? au barabara za vumbi zitageuka fly-overs. Mikokoteni ya kukokota na mbuzi itageuka maglev?

Tena huyu wa sasa hivi wale ambao hawajatembelewa naye they are better than. Hii ni kwa sababu anachosimama kukiongea jukwaani na yale anayoyafanya tofauti yake ni kama kusini ilivyo mbali na magharibi. Sana sana ataenda kama mfalme wa Tanzania ndani ya gari la milioni 300 wakati wao panadol ni muujiza then kama haitoshi atatoa pipi mfukoni na kumpa mmoja wa watoto maskini.Then baada ya hapo atatimua vumbi na kuondoka zake huyoooooo. Infact mimi hata sitaki kuonana naye maana nahisi nitafungwa bure.
 
Ni ajabu kwamba Cpat. Saidi Kitunda aliyekufa siku ile katika maonyesho ya fighter aircraft,alikuwa anatoka huko huko Sikonge
 
Ni ajabu kwamba Cpat. Saidi Kitunda aliyekufa siku ile katika maonyesho ya fighter aircraft,alikuwa anatoka huko huko Sikonge

Kaka hii wilaya ya Sikonge ipo nyumba sana ki maendeleo, hakuna zao kuu lolote la biashara -Zao la Tumbaku ndilo hilo linasuasua, miundo mbinu kama barabara ni matatizo matupu, nikitaka kwenda nyumbani likizo majira ya masika lazima kwanza nipige simu niulize hali ya barabara iko vipi- nikikurupuka nikaenda tarehe 20th Dec basi naweza rudi mwezi April masika ikiisha - ukirudi town na ka-kibarua kashaota majani - hii wilaya ni kama imesahaulika kabisa. ( msiniulize habari za mbunge wangu - kwanza simjui pili sina sababu za kufahamiana naye sababu hasaidii chochote)

Ni habari njema JK ameahidi ujenzi wa barabara toka Nzenga - Tabora utaanza mwaka huu ( Mwananchi page 3 leo) na baadaye Sikonge - Ipole - hadi Chunya Mbeya.

Hapa na sisi wa huko tutapata ahueni sababu nitakuwa nina uhakika kutoka Dar na kufika home the same day - kwa sasa lazima nitumie 2 days na matatizo lukuki.

Bado kuna upendeleo katika ugawaji wa pesa toka serikali kuu kwenda kwenye haya majimbo yetu, kuna majimbo mengine yanasahaulika kabisa. - nafikiri sera ya majimbo ya CHADEMA inaweza kuwa suruhisho ya tatizo hili.

Wana JF mliozaliwa along Northen and Eastern Zone your safe, sisi tuliotoka kanda ya kati yaani tuliokuja town kwa train (Singida, Kigoma na Tabora ) there two things involved:-
Either we move away from those districts or We stay lakini tukubali ku suffer hizi consequences za kukosa umeme, maji na barabara, matibabu nk hadi hapo neema itakapofuniliwa - question is when?
 
Hizi ni dalili za ubunifu hafifu katika kutafuta habari.
Hii ya rais kutembelea kaeneo fulani kwa mara ya kwanza haina hata sifa ya kuwa historia, kama tutaichukulia hii kama historia maana yake hata siku akija mtaani kwetu ambao hapo kabla hakukuwa na sababu ya kutembelewa na kiongozi yeyote wa kitaifa siku akitembelea tutaita tukio la kihistoria.

Hivi tutakuwa na matukio mangapi ya kihistoria. Kwa historia iliyowekwa leo watalii wataweza kuwa wanatembelea hapo kwa kuwa ni sehemu ya kihistoria?

Naamini jibu litakuwa hapana, na hivyo siyo tukio la kihistoria eneo husika kutembelewa na HE JK.
Nahisi hujamuelewa ELNINO au mko opposite directions... point yake ni nzuri sana
 
Maji safi yakiwepo..
Umeme upo..
Hospitali ziko zikiwa na dawa na waganga...
Shule kamili (Walimu,nyumba za walimu na maabara)
Miundominu mingine imekaa vyema..
Hata asipokuja kwa karne 10 I don't care....

Lakini kuja eti kusalimia wananchi afu anasepa kwa mahadi yasiyotekelezwa..
Eti wananchi wanashangilia..
Najiulizaga hivi tumemkosea nini Mungu Kutufanya Majuha na Mazuzu....
 
Back
Top Bottom