TAPSOA yaunga Mkono kauri ya rais Magufuli kuhusu mashine za risti kwwnye vituo vya Mafuta

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Chama Cha Wamiliki Na Waendeshaji wa Vituo Vya Mafuta ya Rejareja Tanzania (TAPSOA), Kinapenda kuunga mkono tamko la Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli la 19 Julai 2017 kuwa ndani ya siku 14 vituo vyote vya kuuza mafuta viwe vimekamilisha zoezi la ufungaji wa mashine maalumu za kutolea risiti yaani-(EFPP).

TAPSOA tunatoa wito kwa Mawakala kupitia TRA kuhakikisha ufungwaji wa EFPPunakamilika kabla ya muda wa ukomo. Wanachama wametekeleza wajibu kwa kulipiagharama zote za ufungwaji wa hizi EFPP, ndani ya muda, ila mpaka tarehe ya hili tangazo,zaidi ya asilimia 95 hawajafungiwa hizi EFPP na mawakala teule wa TRA.

Hapa Kuna sintofahamu inayohitaji mwongozo na msaada kutoka TRA.
Tueleweke kwamba, endapo muda wa ukomo utaisha kabla ya kufungwa hizi EFPP, basi tungeomba Umma, Mheshimiwa Rais na vyombo vyake vya dola kutotuona wamiliki na waendeshaji wa vituo vya mafuta nchini kuwa ni wakaidi wa agizo alilolitoa Mheshimiwa Rais.

Hii itakuwa imetokana na tatizo la wasambazaji na Mamlaka za serikali zinazohusika kuwasimamia wasambazaji hawa, sisi kama wenye vituo hatuna mikataba ya kiutendajikatika kuunganisha Mashine hizi katika pampu zetu za kuuzia mafuta, jukumu la kuwasimamia Mawakala halipo juu yetu bali kwa Mamlaka za Serikali.

Jukumu letu sisi ni kulipia na kusibiri kufungiwa mashine hizi katika vituo vyetu.
Hali kadhalika, tunasisitiza uwepo wa “Serv ice Leve l Agre ements”baina ya Mawakala na Wanachama husika wa TAPSOA kwa kila kituo, ili ifahamike wazi majukumu, gharama na wajibu wa kila mmoja.

TAPSOA tunapenda kumpongeza Rais wetu kwa jinsi anavyopambana na kupigania maende leo ya Taifa letu kwa ujumla kuhakikisha keki ya Taifa inagawanywa sawa kwa kila Mtanzania kupata huduma za muhimu. Tunazidi kumwombea Raisi wetu Mungu ampe Afya njema katika kuwatumikia wananchi wa TANZANIA.

Imetolewa na;
Katibu Mkuu
TAPSOA
 
Back
Top Bottom