Tanzia ya Mzee Jumbe na yaliyomo katika kitabu cha ujasusi wa kidola na kiuchumi

Yericko Nyerere, Mbona hapo kwa Alhaj Aboud Jumbe umeeleza kwa mkato tu kwamba alisema kama ndio hivyo Muungano uvunjike, Je yeye alikosa nini hadhi kuvuliwa Wadhifa wake wa Urais wa SMZ?
 
Sijui nani kaniloga mie kwa uvivu yaani hata sijasoma nikamaliza nimechokea katikati! natamani mtu a summary then mie nimeze tu
 
Mimi napenda kujua zile makala za kiroboto tape/mkanda wa kiroboto zilikuwa zikirushwa na radio sauti ya zanzibar kila siku baada ya taarifa ya habari ya saa 1 usiku zikiikashifu serekali ya jamuhuri.

1. Kwa nini mzee Jumbe alikuwa anaruhusu ziendee kurushwa?
2. Jumbe (R.I.P) nini kilisababisha kuvuliwa nyadhifa zake zote.
 
Hee tunaaminishwa Nyerere alikua kiongozi mbabe sana ,Sasa huyu Karume sijui alikua nini !
 
That's what I believe mkuu...pamoja na mapungufu take.. Uvumilivu wake na busara zake dhidi ya mikingamo ya karume ilisaidia kuendelea kuwepo muungano
Kina yericko wana agenda ya siri na mjomba wao zaidi ni ubinafsi maana mzee nyerere hakuwapa muda ndugu zake wajitajilishe kupitia mgongo wake. Halafu ukichukulia baba yake yericko alalikua mjanja ktk biashara. Jk alitaifisha mpaka shughuli za wadogo zake. Musoma hotels baba ya yericko alikua mwanahisa dabaga farm kaka yake Joseph pia alitendwa hivyo sitashangaa jericko kuponda uongozi wa mwalimu
 
Yericko anadalalia kitabu chake na anataka kutuaminisha alichoandika ktk kitabu chake siyo propaganda ila za wenzake ni propaganda
 
Nadhani mkono wa bara ulikuwepo katika kifo cha Mzee Karume japo kilikaa kwa kisasi zaidi ya yanayoelezewa kuwepo kwa njama za mapinduzi. Uwepo wa Karume Senior kwa miaka zaidi hata ya 5 kuanzia kipindi kile kungevunja muungano kabisaa. Ilikuwa ni rahisi kumbana Abdu Jumbe kuliko mwanzilishi wa Mapinduzi Zanzibar. Ili kuipata Tanzania ya sasa kifo yaliyotokea Zanzibar ilibidi yatokee..ni mtazamo wangu tu. Mzee jumbe na msimamo wa serikali 3 na muungano wa kimkataba ndio ulimfikisha hapo alipofikia..mji Mwema kigamboniii...

Ili kuwa ni rahisi narudia kwa Mwalimu J. Nyerere kumbana Mzee jumbe kuliko kumweka chini Mzee Karume maana alikuwa ni Mzanzibar wa kweli..
 
..................................................................
Mauaji ya Karume:

Misheni ya Tatu:

Baada ya kuona namna mwanamapinduzi halisi alivyoondolewa Zanzibar na kupokwa mamlaka na jinsi Field Marshal John Okello alivyoongoza Mapinduzi ya 1964, na kuundwa kwa Serikali ya Mseto kati ya vyama vya ASP na Umma, kuliibuka lengo la Karume la kuzivunja nguvu za wanaharakati wa Umma Party na za wakomunisti wa ASP walioshabihiana kimawazo na kimtazamo wa kitaifa na wana-Umma Party na kumnyima Karume usingizi katika mda mfupi wa utawala baada ya mapinduzi hayo.Lakini tofauti na matarajio ya Karume, hatua hiyo iliwaleta karibu zaidi wanamapinduzi hao na kumnyima zaidi usingizi kwa hofu ya kupinduliwa, wakimtuhumu kushindwa kuongoza na kusimamia madhumuni ya Mapinduzi Visiwani.

Muungano kati ya Zanzibar na Tanganyika mwaka huo ulikuwa nguzo muhimu kwake kujijenga mamlakani kwakuondoa vikwazo mbele yake, akaona vyema awasambaratishe kwa kuwatafutia nafasi za uongozi Tanzania Bara ambako wasingeweza kufurukuta.Waliokumbwa na kadhia hiyo ni pamoja na Abdulrahman Babu (Umma) na aliyepewa Uwaziri wa Mipango na Uchumi kwenye Serikali ya Muungano; Kassim Hanga (ASP) aliyeteuliwa Waziri katika Ofisi ya Rais wa Jamhuri, Mambo ya Muungano; Salim Ahmed Salim (Umma) aliyeteuliwa Balozi nchini Misri.Wengine ni Othman Sharrif (ASP) aliyeteuliwa Balozi nchini Marekani, lakini Karume akampinga Nyerere akidai hastahili, uteuzi ukafutwa; badala yake akateuliwa kuwa afisa mifugo katika moja ya mikoa ya Kusini Tanzania, Mbeya au Mtwara, na Kanali Ali Mahfoudh (Umma) aliyeteuliwa Mkurugenzi wa Operesheni katika Jeshi la Wananchi (JWT), na wengineo.

Kwa wale wenye maoni tofauti na ya kukosoa Serikali waliobaki Visiwani, hasira ya Karume aliyetawala kwa mkono wa damu iliwashukia, wengi walikamatwa na kutiwa kizuizini na pengine kupoteza au kuuwawa kikatili na katika mazingira ya kutatanisha. Mmoja ya waliouawa kikatili kizuizini ni Mzee (mwanaharakati) Mohamed Hamoud, baba yake Luteni Hamoud Mohamed muuaji wa Karume.Juu ya mapinduzi ya Zanzibar na kuuwa kwaAbeid Karume kumekuwapo na mitazamo mingi kwa watu mbalimbali, lakini nitumie mitazamo ya wanamajumui hawa Prof Harob Othuman ambae yeye alilieleza hili katika mtazamo wake, pia Prof Issa Shivji nae amelisemea katika jicho tofauti, wakaja wazee wangu wa fikra za nera Mohamed Said na Dr Harith Ghassany katika kitabu cha "Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru" hawa wanalandana katika mitazamo yao ambayo kwa undani inabeba dhani ya kidini, lakini mawazo tanzu na fikra tunduizi ya Joseph Mihangwa katika andishi lake kwenye gazeti la Raia Mwema la April11,2012Toleo234 – 237May2,2012 ndio yanabeba dhana yangu juu ya hili tukio.

Tangu Mapinduzi ya Januari 12, 1964, Zanzibar haikuwa na Katiba wala Sheria; iliongozwa kwa Amri za Rais- (Presidential Decrees) kadri alivyoona inafaa.- Na kwa mujibu wa Gazeti la The Tanganyika Standard la March 9, 1968, Karume aliapa kutofanya uchaguzi wala kuwa na Katiba Kisiwani kwa miaka 50 tangu 1964 - 2014 Kwa madai kwambachaguzi zote ni vyombo vya mabeberu kuwakandamiza wananchi.Na kadiri kalamu ya Karume ya wino wa damu ilipozidi kuandika historia ya ukatili, udikteta na umwagaji damu kwenye kurasa ngumu za kukwaruza ndivyo alivyojichongea na kujiongezea upinzani na uadui kwa jamii ya Kizanzibari.
Kulikuwana vuguvugu ama tuseme harakati za hapa na paleza kupinga utawala wa Karume ambazo Utawala wa Karume ulitumia mwanya huo kuziita ni majaribio ya hapa na pale ya kutaka kuiangusha Serikali ya Karume kuanzia mwaka 1964.Thabit Kombo Jecha katika “Simulizi”anayataja baadhi, likiwamo lile la Desemba 1964 lililoongozwa na Amour Zahorwa Unguja, la 1967 likiongozwa na Suleiman Hamad Suleimanwa Pemba, la 1967 tena, likiongozwa na Saleh Ali Nassorwa Unguja, na la 1968 likiongozwa na Salim Mohamed Abdullah wa Pemba. Kufikia mwaka 1967 hofu ya Karume dhidi ya wenzake na kwa nafasi yake ilitia fora kiasi cha kuogopa kivuli chake mwenyewe. Na ili kuendelea kuwamaliza wenzake, mwaka huo zilitungwa tuhuma za uongo dhidi ya watu 14 makada wa ASP katika kumpindua, zikiwalenga hasa wenye fikra za kikomunisti.

Walioingizwa kwenye tuhuma hizo ni pamoja na mawaziri wa Serikali yake mabwana Abdallah Kassim Hanga, Salehe Saadallah Akida, Abdul Aziz Twala na makatibu wakuu wa wizara, Aboud Nadhif na Mdungi Ussi na baadaye Othman Sharrif.Wote waliokuwa Visiwani walikamatwa, kisha wale walokuwa bara, Karume akamuomba Nyerere kuwarejesha Zanzibar kutoka Bara ndugu Othman Sharrif na Kassim Hanga ili "wakahojiwe" lakini wote wakaishia kuuawa kikatili baharini bila kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Mmoja wa mashahidi wa uongo walioandaliwa dhidi ya watuhumiwa kwa vyombo vya Karume, alikuwa Ahmada ambaye kwa uongo wake, watu wanne akiwamo Hanga, Twala, Saadallah na Othman, walinyongwa mwaka 1969.- Kwa uongo huo, Ahmada alizawadiwa cheo cha kapteni jeshini.- Ni Kapteni Ahmada huyu, aliyeshiriki kwenye mauaji ya Karume miaka mitatu baadaye.Kwa hofu ya jamii ya Kizanzibari kufikiwa na fikra na mawazo mapya ya kimaendeleo, Karume alipiga marufuku vijana wa Kizanzibari kwenda nje kwa masomo ya juu ikiwa ni pamoja na Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam; alipiga marufuku pia ujenzi wa Chuo Kikuu Visiwani.
Mbali na kutokuwapo kwa utawala wa sheria enzi za Karume, unyanyasaji wa kijinsia na ubaguzi kwa misingi ya historia na kisiasa ulitia fora. Kwa mfano, mwaka 1966, alitoa amri (decree) kuwanyima wazazi haki ya kuwakataa wanaume walioposa binti zao kama njia ya kuondoa ubaguzi wa rangi.Kwa sababu hii, wasichana, hasa wale wa Kiarabu walilazimishwa kwa nguvu ya Serikali kuolewa kwa nguvu. Karume mwenyewe, wakati huo akiwa na umri wa miaka 65, aliwania kuoa kwa nguvu, wasichana wanne wa Kiajemi, na alipokataliwa, aliamrisha wazazi wao watiwe kizuizini na kuchapwa viboko kwa kosa la kuzuia mpango wa ndoa mchanganyiko, na baadaye kutimuliwa Zanzibar.Chini ya mpango huo, raia wa kigeni waliotaka kuchumbia wasichana wa Kizanzibari walitakiwa kuilipa Serikali Sh. 64,000,000, bila hivyo hawakuruhusiwa kuwaoa.

Karume alikuwa ameanza kuwa mwiba kwa Mwalimu Nyerere pia juu ya Muungano. Kwa mfano, alimkatalia Nyerere kwa lugha ya dharau na kejeli juu ya Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea na Azimio la Arusha kutumika Zanzibar.Na kuhusu akiba ya fedha za kigeni ya Zanzibar iliyofikia dola milioni 80 mwaka 1972, alimuonya asithubutu kuitolea macho, akamwambia:- “Fedha ya kichwa cha Malkia si yako na usiniulize, labda niulize juu ya hii (sh.) yenye picha ya kichwa chako.Na kuhusu Muungano, Karume alikuwa ameanza kuchoka nao. Siku moja alisema, Muungano ni kama koti tu; likikubana unalivua.

Ufa huu kati ya viongozi hao wawili juu ya Muungano, ndio uliosababisha kamati ya kupendekeza Katiba (Constitutional Committee) isiundwe na Bunge la Katiba (Constitutional assembly) lisiteuliwe ndani ya muda wa mwaka mmoja tangu Muungano, kama ilivyotakiwa chini ya Mkataba wa Muungano wa Sheria ya Muungano ya 1964.Wadadisi wa mambo ya siasa wanakubaliana kuwa, kama Karume angeendelea kutawala miaka kadhaa baada ya 1972, Muungano ungefikia kikomo kwa njia ya kutisha na kusikitisha.

Kufikia mwaka 1972, upinzani kwa Serikali ya Karume ulikuwa umechukua harakati za uasi wa umma, chini kwa chini kwa mara ya kwanza tangu Hanga na wenzake wanyongwe mwaka 1969.Kwa vigezo vyovyote vile vya utawala na uongozi, Karume alitawala kwa mkono wa chuma; alitawala kidikteta katika nyanja zote za maisha ya Wazanzibari kisiasa, kiuchumi na kijamii.-- Alikuwa kero pia kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kwa Muungano.
Kwa kusema haya kitabu hiki hakitafsiri kwamba Karume hakutenda mema kwa Zanzibar na kwa Wazanzibari; bali kinajaribu kutafiti tu kuona ni mazingira na sababu zipi zilizochochea na kuharakisha kuuawa kwake; kati ya sababu hizi kuu za kisiasa, kiuchumi, kijamii na kimuungano.- Kwa vyovyote vile, moja au zaidi ya mambo haya manne yalichangia.Tunajua kwa mfano, kwa baadhi ya Wazanzibari, Karume alikuwa mtawala mkatili asiye na huruma wala hakujua kusamehe; lakini pia alikuwa na sifa za pekee nzuri kama kiongozi na binadamu; alikuwa mhimili na mtetezi wa Waafrika wa Kizanzibari na hakuyumbishwa na siasa za migogoro Visiwani.Alikuwa mwenye fikra zenye kujitegemea, alifanya maamuzi yake bila woga wala kuhofia matokeo; alikuwa kiongozi mwenye kuthubutu na mwenye kujituma.

Licha ya Karume kuitawala Zanzibar kwa mkono wa chuma, na namna alivyowaengua wote aliodhani hawakuwa upande wake, ama kwa kuwahamishia kwenye Serikali ya Muungano, ama kwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha, jamii ya Kiarabu wasio Wazanzibari, iliamriwa kuondoka, na wale Waarabu raia waliobaki waliishi chini ya jicho kali la Serikali; waliweza kukamatwa, kama Wazanzibari wengine na kutiwa kizuizini bila kufunguliwa mashitaka.-- Walifanyiwa jinsi serikali ilivyofikiri inafaa; mashamba na mali zao zilitaifishwa bila kufidiwa.Wapo waliohukumiwa na Mahakama ya wananchi, kifungo na kuchapwa viboko, kuonyesha kwamba Serikali ya Karume haikuwa ya mchezo; akaionya jamii ya Ki-Athnasheri wa Kiajemi kwamba kama wangeendelea kuleta mgogoro, wangefukuzwa wote Zanzibar licha ya kuwa raia.Karume alitangaza utawala wa chama kimoja cha ASP na kuamrisha kila Mzanzibari mtu mzima, kuwa mwanachama. Kila familia ilitakiwa kutundika picha ya Karume nyumbani; kutofanya hivyo lilikuwa kosa la jinai lenye adhabu kali.Kikosi cha Usalama wa Taifa chini ya Kanali Seif Bakari, kilichopewa jina la "Viwavi Jeshi", na kufunzwa Ujerumani Mashariki kikaiva kwa mbinu za utesi na mauaji, kilipewa mamlaka ya kukamata, kutesa, kutia kizuizini na hata kuuwa bila mashitaka. Yeyote aliyelalamika, hata juu ya upungufu wa chakula tu, aliitwa adui wa Mapinduzi na hivyo mhaini. Enzi hizo, nduguyo akigongewa mlango usiku na kutakiwa kwa mahojiano na Serikali, usingemwona tena milele.

Wakati wa Karume hapakuwa na utawala wa Sheria wala Katiba;- amri za rais (decrees) ndizo zilizotawala nchi.- Mapema mwaka 1966, mfumo wa mahakama wa kawaida ulipigwa marufuku; na Oktoba 1966, rais alijipa madaraka ya kuteua mahakama maalumu za watu wasiozidi 14 wenye mamlaka ya kusikiliza kesi za makosa ya kisiasa kama vile uhaini, uhujumu uchumi na wizi wa mali ya umma.Mahakama hizi hazikufungwa na kanuni zozote katika kusikiliza kesi; huduma za kisheria kwa watuhumiwa zilifutwa na mawakili kupigwa marufuku Zanzibar.- Upande wa mashitaka ndio uliokuwa pia upande wa utetezi; kwa maana kwamba, mwendesha mashtaka wa serikali alipomaliza kuwasilisha mashtaka dhidi ya mtuhumiwa aligeuka kuwa mtetezi wa mtuhumiwa.Mahakama hizi zilipewa uwezo wa kutoa hukumu za kifo. Mwaka huo huo (1966), Baraza la Mapinduzi lilipiga marufuku pia haki ya kukata rufaa kwenye Mahakama ya Rufaa ya Afrika Mashariki [EACA] na rufaa zote zikawa kwa Rais Karume pekee.Mwaka 1970, Karume alipitisha amri (decree) ya kuanzishwa mahakama (za kienyeji) za watu watatu.Mahakimu wapya wa mahakama hizo waliteuliwa na Karume mwenyewe kutoka miongoni mwa makada wa ASP.Moja ya sifa ya kuteuliwa ni kutokuwa msomi wa sheria, na ikiwezekana uwe hujui kusoma na kuandika.Adhabu ya kifo ilipanuliwa kuingiza makosa kama vile utoroshaji wa karafuu, uhaini na utoaji mimba.Matumizi ya vidonge vya uzazi wa majira lilikuwa kosa kubwa pia.

Karume alichochea hasira na chuki kubwa ya Wafanyabiashara wa Kiasia mwaka 1971, pale alipowapa notisi ya mwaka mmoja kufungasha virago kwa madai ya kuonekana kudhibiti uchumi wa Zanzibar.- Hasira yao iliungana na ile ya Waarabu ugenini waliofukuzwa mwaka 1964 na kupokonywa mali na mashamba yao bila kulipwa fidia; achilia mbali wale ambao mabinti zao waliozwa kwa nguvu kwa Wazanzibari Waafrika.Wakati huo huo, Karume aliendelea kuwaachisha kazi na kuwatimua Visiwani, watumishi wa serikali waliojulikana au ndugu zao kuwa wafuasi wa zamani wa vyama vilivyopigwa marufuku vya ZNP na ZPPP na nafasi zao kujazwa na "watiifu" kwake.Hata hivyo, kwa huruma ya Nyerere, walipewa utumishi serikalini Tanzania Bara.Mapema mwezi Januari 1972, Waziri mdogo, Ahmed Badawi Qualletin, na afisa mwingine wa Serikali, Alli Sultani Issa, walifukuzwa kazi.- Kisha, Februari 1972, ujumbe mzito wa watu sita ulitumwa kwa Nyerere kumwambia awarejeshe Zanzibar, Abdulrahman Babu na wenzake kadhaa wakahojiwe kwa tuhuma za kutaka kuiangusha Serikali.Babu ambaye alikuwa bado mwenye ushawishi mkubwa wa kisiasa Zanzibar, na aliyeamua kutorejea Zanzibar ya Karume kwa kuhofia usalama wake, kivuli chake na mzimu wa wahanga wa ukatili vilimtisha na kumnyima usingizi Karume, mithili ya Macbeth kwa mzimu wa Mfalme Duncan na Banquo, aliowaua kwa upanga ili atawale.

Nyerere, kwa kuhofia yaliyompata Hanga, Twala, Othman Sharrif na wengine kutokea alipowarejesha Zanzibar mwaka 1967, safari hii alikataa kumrejesha Babu Zanzibar, ingawa alikubali shinikizo la Karume la kumwachisha uwaziri katika Serikali ya Muungano.Karume aliwatimua pia wataalamu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) na kufunga Kituo chao cha Utafiti na Udhibiti wa malaria Visiwani kwa madai kwamba, Wazanzibari walikuwa "malaria proof", yaani hawaguswi wala kuugua malaria.Kwa hatua hiyo, ugonjwa wa malaria uliongezeka kwa asilimia 45.- Na ingawa Zanzibar ilikuwa na akiba kubwa ya fedha za kigeni, zaidi ya pauni za Uingereza milioni 14 kwenye Benki ya Urusi mjini London, (taarifa nyingine zinadai dola milioni 80), Karume hakuwa tayari kutumia fedha hizo kudhibiti malaria wala kuagiza chakula; badala yake akaona muhimu zaidi kuanzisha kituo cha televisheni ya rangi na ya pekee barani Afrika wakati huo.Mwaka huo huo (1971), katikati ya mrindimo wa njaa Visiwani, Karume alipiga marufuku uagizaji wa chakula (mchele, sukari, unga wa ngano) kutoka nje, kama hatua ya kujitegemea kwa chakula.

Hatua hii ilizua tafrani na malalamiko na kusababisha biashara ya magendo ya chakula kushamiri; hapo, "Viwavi Jeshi" na mahakama za "kangaroo" zikapata wahanga kukamatwa, kushitakiwa na kunyongwa.- Watu wengi wakaikimbia Zanzibar. Aprili 1972, ukosefu wa chakula ulikithiri. Ni wakati huo Rais Karume alipouawa ghafla.Kwa yote hayo, pamoja na tabia yake ya kutoamini wasomi na kuchukia wataalamu, Karume hatimaye alianza kuchukiwa pia na Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi wenye siasa za mrengo wa ki-Karl Marx.Nyerere alikuwa ameyatosadaka mambo mengi ya Tanganyika kwa Zanzibar, ilimradi tu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ufikiwe. Kwa mfano, wakati Tanganyika ilipoteza hadhi ya kuwa nchi na baadaye jina lake, pale Muungano ulipobadili jina kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, na kuitwa Jamhuri ya Muungano wa Tan-zan-ia, Zanzibar ilibakia kuwa Zanzibar, na Karume akabakia Rais wa Zanzibar na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Tanzania.

Si hivyo tu, Wazanzibari watano walipewa uwaziri kamili katika Baraza la Mawaziri 14 la Muungano.- Na ingawa idadi ya Wazanzibari ilikuwa asilimia tatu tu ya Watanganyika, lakini Zanzibar iliruhusiwa kuwa na Wabunge 52 katika Bunge la Muungano, wakiwamo Wajumbe wote 32 wa Baraza la Mapinduzi.Licha ya upendeleo huu, Nyerere hakufanikiwa kudhibiti mhimili wa kisiasa Zanzibar chini ya Karume.Mfano, Zanzibar chini ya Karume, ilikataa kuhamishia kwenye Muungano mambo mengi yaliyopaswa kuwa chini ya Serikali ya Muungano;- kwa mfano, iliendelea kudhibiti jeshi lake la ulinzi na Idara ya Uhamiaji, Karume akiwa amiri jeshi wake Mkuu. Ndiyo kusema, aliuawa na wanajeshi wa jeshi lake la Zanzibar, si Wanajeshi wa JWTZ.Karume alikataa Serikali ya Muungano kugusa akiba ya fedha za kigeni ya Zanzibar, japokuwa fedha lilikuwa jambo la Muungano.- Aidha, Karume na Baraza lake la Mapinduzi walikiuka mara nyingi mapendekezo ya kisera kutoka Bara kiasi kwamba Nyerere hakuwa na kauli tena juu ya sera za kiserikali.Karume akakataa pia mazungumzo zaidi ya kikatiba kwa hofu ya Zanzibar kupoteza hadhi na mamlaka yake. Karibu kila alichopendekeza Nyerere, alipata jibu la mkato kutoka kwa Karume:"Kama hivyo ndivyo, tuvunje Muungano".

Mitazamo hasi ya viongozi hawa wawili juu ya Muungano, ndiyo iliyosababisha mchakato wa kupata Katiba ya Muungano ndani ya mwaka mmoja kwa mujibu wa Mkataba wa Muungano usifanyike, na Muungano kuongozwa kwa Katiba ya Muda kwa miaka 13 hadi 1977 na baada ya Karume kufariki.Nyerere alipowasilisha na kupitishwa kwenye Bunge la Muungano, Mpango wa kwanza wa Maendeleo wa miaka mitano, na kutangaza nia yake kuona unatumika pia Visiwani, Karume aliupinga; akaja na mpango wake tofauti wa miaka mitatu kwa Zanzibar ulioandaliwa na mchumi kutoka Ujerumani Mashariki.Kwa yote hayo na mengine, Nyerere alianza kuonyesha dhahiri chuki yake kwa utawala wa kimabavu wa Karume.- Naye (Karume) alipotambua hilo, alizuia mwingiliano huru wa watu kati ya Visiwani na Tanzania Bara kwa hofu na kwa sababu zinazofahamika.Si mara moja, hofu na wasiwasi wa kimaasi vilipojionyesha Zanzibar, mamlaka za usalama zilimshauri Mwalimu kufuta ziara zake Visiwani.- Hofu hizi zilijidhihirisha zaidi pale Othman Sharrif, baada ya uteuzi wake wa Ubalozi Marekani kufutwa kwa shinikizo la Karume na kurejea Zanzibar, alipokamatwa na kutiwa kizuizini bila kosa.

Ilibidi Nyerere aingilie kati na kumwita Karume Ikulu, kuonyesha jinsi alivyochukizwa na kitendo hicho; lakini Karume alimkatalia, kuonyesha kwamba Nyerere hakuwa na mamlaka kwake. Sharriff aliachiwa baadaye kwa hiari ya Karume, na Nyerere akamteua kuwa Afisa Mifugo Tanzania Bara.Hata hivyo, Oktoba 1969, wakati Nyerere akiwa ziarani nchi za nje, Sharrif alikamatwa Tanzania Bara na kurejeshwa Zanzibar alikouawa.Mbali ya Karume kuweka wazi kwa kusema kwamba, "Muungano ni kama koti tu; likikubana au kukuzidishia joto unalivua na kuendelea na safari yako", pia alijipa ujasiri usio wa kawaida kwa kumkatalia Nyerere hadharani kila mara juu ya baadhi ya mambo ya Muungano akisema: "..kama ni hivyo, sikubali, bora tuvunje Muungano".Ni ujasiri huu wa Karume usio wa kawaida juu ya jambo nyeti kama hili, uliofanya Nyerere atoe tamko lake maarufu juu ya hatima ya Muungano akisema:"Kama watu wa Zanzibar, bila ya ulaghai kutoka nje, wataona ni bora kuvunja Muungano, mimi siwezi hata kidogo kuwapiga mabomu na kuwaua wananchi wa Zanzibar.- Kama waliingia katika Muungano kwa hiari yao, vivyo hivyo wanaweza pia kujitenga kwa hiari yao.- Hatukuishinda Zanzibar (kuwafanya mateka) vitani" (Soma:- William Edgett Smith, "Mwalimu Julius K. Nyerere", tafsiri ya Kiswahili na Paul Sozigwa, uk. 154).

Wakati Mwalimu alikuwa mstari wa mbele katika kupinga ubeberu wa Marekani wakati wa vita ya Vietnam, na kwa ukombozi wa nchi za dunia ya tatu kwa ujumla, Karume alimbeza na kutangaza adhabu kali Visiwani kwa yeyote aliyelaani na kupinga ubeberu, au kuimba nyimbo za kuikashifu Marekani.Mwalimu alipokosana na Uingereza kwa nchi hiyo kuukingia kifua utawala wa kidhalimu, kibaguzi na wa mabavu (UDI) wa Ian Smith nchini Rhodesia Kusini (sasa Zimbabwe), na kwa sababu hiyo uhusiano wa Mwalimu na Balozi wa Uingereza nchini, Sir Horace Phillip kuingia mkwara, Karume alionyesha hadharani kila mara kusuhubiana na Balozi huyo kwa kicheko cha bashasha na uswahiba kwa chukizo kwa Nyerere.

Tunaweza kutua kidogo hapa kuangalia nyuma mazingira aliyokuwamo Karume, miezi michache kabla ya kifo chake; bila shaka tutabaini kuwa, kiongozi huyo alikuwa katikati ya uhasama na uadui wa kujitakia.Kwanza alikuwa na uhasama mkubwa na jamii pana ya Kizanzibari kwa udikteta wake uliokithiri uliosababisha mauaji, watu kutiwa kizuizini au kuhamishiwa Bara.- Pili, kulikuwa na tatizo la njaa na mlipuko wa malaria; mambo ambayo hakuonekana kujali.Tatu, kulikuwa na uhasama mkubwa wa kisiasa kati yake na makada wenzake wenye siasa za Ki-Karl Marx ndani ya ASP waliomtuhumu kushindwa kuongoza, achilia mbali jamii ya Kiarabu aliyoitimua kikatili Zanzibar na iliyoendelea kutema laana kwake ughaibuni. Nne, -kulikuwa na Nyerere ambaye alianza kumuona kama mzigo na kero kwa Serikali ya Muungano na kwa siasa za kimataifa.- Yote haya yalikuwa baruti tosha kuweza kulipuka na kumdhuru Karume kwa namna yoyote iwayo.

Luteni Hamoud Mohamed Hamoud, alikuwa mtoto wa mzee Mohamed Hamoud ambaye alikamatwa na kutiwa kizuizini na Karume miezi kadhaa baada ya Mapinduzi ya Januari 1964, na hatimaye kufariki dunia akiwa kizuizini.Miaka kadhaa baadaye, wakati Hamoud Hamoud akichukua mafunzo ya kijeshi huko Tashkent nchi iliyokuwa katika -Shirikisho la Urusi ya zamani, alifahamishwa na mmoja wa wanafunzi wenzake juu ya kuuawa kwa baba yake.- Kwa uchungu mkubwa, aliapa sawia na baadaye, kwamba angemuua Karume kulipiza kifo cha baba yake.Mfumo wa Usalama wa Zanzibar ulioenea kila mahali, ulijulishwa haraka na mmoja wa ma-ofisa usalama waliokuwa kwenye mafunzo pamoja na Hamoud, juu ya kusudio hilo la Hamoud.Lakini cha kushangaza ni kwamba, Hamoud aliporejea Zanzibar baada ya mafunzo hakukamatwa wala kuwekwa kwenye uangalizi; badala yake alipandishwa cheo kuwa luteni usu, katika sherehe iliyohudhuriwa na Karume mwenyewe kama Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Zanzibar.

Ikumbukwe kuwa, suala la Usalama wa Taifa halikuwa jambo la Muungano;liliongezwa kwenye orodha mwaka 1984 kufuatia kadhia ya Aboud Jumbe ya kuchafuka kwa hewa ya kisiasa Zanzibar na yey kuwekwa kizuizini Mjimwema Kigamboni jijini Dar es Salaam, likaunganishwa kusomeka kwa pamoja na jambo la Ulinzi kuwa Ulinzi na Usalama. Lakini kila kitu juu ya mipango na njama zote hizoidara ya ujasusi Tanganyika"Tawi Maalumu" ilifahamu.Pale risasi ya Hamoud ilipochukua uhai wa Rais Karume miezi kadhaa baadaye, Serikali ilisisitiza kwamba, mauaji hayo yalikuwa sehemu ya njama kubwa ya kuangamiza Mapinduzi ya 1964, kutokana kwamba, Hamoud na wauaji wenzake walikuwa wanachama wa zamani wa Umma Party, kilichokiunga mkono ASP huko nyuma, na kukipa [ASP] mwelekeo bora wa kiitikadi [Ukomunisti] na kuheshimika kisiasa.
Kufuatia mauaji hayo, watu 1,100 walikamatwa na kuhojiwa.- Babu alikamatwa na kutiwa kizuizini Tanzania Bara kwa tuhuma za kuongoza mpango mzima; nao maofisa wa ngazi za juu wa Kizanzibari Jeshini Bara, kama Ali Mahfoudh na wengine, nao walishukiwa na kuondolewa kwenye utumishi wa Jeshi Tanzania Bara bila kurejeshwa Zanzibar.Kuna dhana mbili zinazogongana, lakini zote zenye nguvu; juu ya sababu za kuuawa kwa Karume.- Dhana ya kwanza ni hii ya Hamoud kulipiza kisasi.Lakini suala la kulipiza kisasi linakoma pale tunapoona watu kama Kapteni Ahmada na raia Ali Chwaya ambao hawakuwa na uhusiano wa kifamilia na marehemu Mohamed Hamoud aliyeuawa, kujiingiza katika kulipiza kisasi.Lakini, kama tutakavyoona baadaye, Kapteni Ahmada alijiingiza kama hatua tu ya kujisafisha kwa kujutia ushahidi wa uongo aliotoa dhidi ya Hanga na wenzake 18 waliouawa mwaka 1969, na yeye kuonekana kama adui na msaliti wa umma wa Kizanzibari.- Inapofikia hapo, inakuwa dhahiri kwamba mpango huo ulibeba hasira za jamii pana ya Kizanzibari.

Dhana ya pili ambayo ndiyo msimamo wa Serikali ni kwamba, mauaji hayo yalikuwa mpango mpana wa kupindua Serikali.- Dhana hii inapata nguvu kutokana na watu wengi kuhusishwa na tuhuma hizi, lakini kama tu tuhuma dhidi yao zilikuwa za kweli; vinginevyo dhana ya kwanza inashinda.Chuki binafsi?- Hapana, Hamoud hakuwa peke yake; ilikuwa ghadhabu ya umma kwenye jamii pana ya Kizanzibari, kila kundi au sehemu ya jamii na malalamiko yake.
Kwa mujibu wa taarifa za Usalama wa Taifa Zanzibar, mipango ya kupindua Serikali ya Karume ilianza kusukwa tangu 1967 -1972 ndani ya Zanzibar na Tanzania Bara, ambako nyumba ya Abdulrahman Babu ilikuwa kituo cha mikutano ya Wazanzibari ya kupanga Mapinduzi hayo.Kama hivi ndivyo, Karume alikuwa na sababu tosha kumtaka Nyerere kumrejesha Babu Zanzibar "kuhojiwa", Februari 1972.Mkutano wa mwisho ulifanyika Aprili 2, 1972, ambapo ilikubaliwa Mapinduzi yatekelezwe Aprili 7, 1972, yakihusisha makundi mawili: kundi la Wazanzibari kutoka Bara, wengi wao wakiwa wanajeshi, na kundi la Wazanzibari ndani ya Zanzibar, likihusisha raia na wanajeshi wachache.

Pamoja na uamuzi huo, kikao kilitoa majukumu mazito kwa baadhi ya washiriki, ikiwa ni pamoja na Hamoud na Ahmada kupewa jukumu la kuiba silaha kutoka kambi ya kijeshi, Bavuai.Ilikubaliwa kuwa, Babu na wafuasi wake kutoka Bara wasafiri kwa mtumbwi kwenda Zanzibar Aprili 6 kuamkia alfajiri ya Aprili 7, na kufikia eneo lililopo kati ya mitambo mikuu ya mawasiliano [Cable and Wireless] na Klabu Starehe.- Baada ya hapo, Babu abakie amejificha kwenye nyumba ya Hamoud Hamoud, iliyotizamana na Klabu Starehe eneo la Shangani, kusubiri saa ya mapambano kuwadia.Kwa mujibu wa taarifa, Babu aliondoka Dar es Salaam kwa mtumbwi uliofungwa redio mbili za mawasiliano, jioni ya Aprili 6, safari iliyoelezwa kuwa ya "kuvua samaki"; wakati madhumuni halisi yalikuwa ni kuwafikisha Babu na wafuasi wake Visiwani usiku wa Aprili 6, kwa maandalizi kamili ya kupindua SerikaliJioni hiyo, Aprili 6, Uongozi wa Jeshi uligundua upotevu wa silaha nyingi Kambini Bavuai.- Na ingawa uongozi ulikuwa bado haujamhusisha mtu yeyote, lakini Hamoud, Hamada na askari wengine walianza kufuatiliwa kwa siri.
Yaelekea kufikia hapo, Babu alijulishwa na kuonywa kwa njia ya redio akiwa baharini, juu ya kugunduliwa kwa mpango mzima wa Mapinduzi; akakatiza safari na kurejea haraka Dar es Salaam hima.- Haijulikani kama wafuasi wake walikuwa wamekwishafika Zanzibar au la; au kama nao walijulishwa na kurejea Dar es Salaam.Lakini kuwapo Visiwani wanajeshi kama Kanali Mahfoudh- (Mkurugenzi wa Operesheni JWTZ, Dar es Salaam) na Luteni Hashil Seif (Kikosi cha Wanamaji, Ukonga, Dar es Salaam) saa ya kuuawa Karume, kunaonyesha baadhi yao tayari walikuwa Zanzibar kusubiri wenzao.Saa 12.00 asubuhi, Aprili 7; Ali Khatibu Chwaya (raia) alikwenda kwa Ali Mshangama Issa (afisa wa tatu, meli M.V. Afrika, mkazi wa Zizi la Ng'ombe, Zanzibar), kumweleza juu ya kutowasili kwa kundi la Dar es Salaam.
Baadaye asubuhi hiyo, Ali Mshangama, Chwaya, Miraji Mpatani -(karani wa shirika moja, Zanzibar), Mohammed Abdullah Baramia (Mtunza Bohari, Idara ya Elimu), Ahmada na Hamoud, walikutana nyumbani kwa Hamoud na kuonyesha kukerwa na kusikitishwa kwa kutowasili kwa wapanga mapinduzi kutoka Dar es Salaam, hasa wakijua pia kwamba, silaha zilizoibwa bado zilikuwa nyumbani kwa Hamoud, na hatari ya kuweza kugunduliwa.Ilipofika saa 6.00 adhuhuri siku hiyo, Mshangama, Hashil Seif, Amar Saad Salim, maarufu kama "Kuku" (afisa usafirishaji, Idara ya Siha, Zanzibar) na Chwaya, walikutana nyumbani kwa Amar Saad ambako Mshangama, Hashil Seif na Baramia walipendekeza mpango wa kupindua Serikali uahirishwe hadi watakapopata taarifa tofauti kutoka Dar es Salaam.
Kwa hiyo, saa 9.00 mchana siku hiyo, saa mbili tu kabla ya kuuawa kwa Karume, Baramia alikwenda nyumbani kwa Hamoud eneo la Shangani kuwasilisha pendekezo hilo.- Alimkuta Miraji Mpatani nje ya nyumba na kumweleza Baramia kwamba, pamoja na kundi la Dar es Salaam kutowasili, Ahmada na Hamoud walishikilia Mapinduzi yafanyike tu siku hiyo, kwa sababu Ahmada alikuwa anatafutwa na maafisa wa Jeshi.Je, ni kwa sababu hii Luteni Hamoud, Kapteni Ahmada na Chwaya waliamua kufanya Mapinduzi, licha ya wenzao kutaka yaahirishwe?.Kwa mujibu wa mkakati wa Mapinduzi uliofikiwa Aprili 2, 1972, Suleiman Mohamed Abdullah Sisi (mwanajeshi wa JWTZ, mkazi wa Ilala Flats, Dar es Salaam) alipangwa kuongoza utekaji wa kambi ya Jeshi, Mtoni, ambapo Kapteni Ahmada, alitakiwa kuteka kambi ya Jeshi, Bavuai, Makao Makuu ya Jeshi na Chuo cha Jeshi cha mafunzo ya Redio, vyote hivi viko eneo la Migombani.

Kituo cha Polisi cha Malindi kingeshambuliwa na kutekwa na kikundi chenye silaha kikiongozwa na Luteni Hamoud ambacho kingeweza kuteka magari yenye Redio za mawasiliano.
Askari Yusufu Ramadhan angeongoza kikundi cha maafisa wa Polisi walioingizwa kwenye mpango huo na kuteka Kituo cha Polisi cha Ziwani.Amour Dughesh (mwanajeshi; Zanzibar), yeye angeteka Ikulu na kumkamata Karume, kisha kumpeleka Kituo cha Redio kumlazimisha atangaze kupinduliwa kwa Serikali yake.- Baada ya hapo, Kituo hicho kingeachwa chini ya udhibiti wa Badawi, Mpatani na Mohamed Said Mtendeni (mwandishi wa habari, gazeti la China, mkazi wa Vuga, Unguja).Uwanja wa Ndege ungetekwa na kikosi cha wanajeshi na baada ya hapo kingeachwa chini ya udhibiti wa Ali Sultan Issa (meneja wa Shirika la Mafuta, Zanzibar).
Mpango huo ulilenga pia kuteka Makao Makuu ya Umoja wa Vijana wa ASP, ambayo yalikuwa pia Makao Makuu ya Idara ya Usalama wa Taifa Zanzibar, ikiongozwa na Kanali Seif Bakari na kuwekwa chini ya udhibiti wa Mohamed Abdullah Baramia, Kapteni Khamis Abdullah Ameir, wa Makao Makuu ya Jeshi, Zanzibar; yeye alipangwa kuzuia mashambulizi kutoka nje kama Mapinduzi yangefanikiwa.Mapinduzi ni kitendo cha kutaka kubadili sawia hali, serikali au mfumo fulani wa kijamii kwa matumizi ya nguvu, ikiwa ni pamoja na kuondoa mhimili wa mfumo huo.Mapinduzi yanaweza kuwa kwa njia ya jeshi kama jeshi limetumika au ya kiraia kama raia walitumika, kama yalivyokuwa Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12, 1964 chini ya John Gidion Okello.

Mauaji ya Karume hayawezi kuitwa mapinduzi ya kijeshi wala ya kiraia kwa sababu kifo chake hakikubadili mfumo wala muundo wa serikali.- Haya yanaweza kuitwa mauaji ya kisiasa yenye lengo la kuondoa chanzo au mhimili wa kero katika jamii bila kubadili serikali.Mwanazuoni mahiri Barani Afrika, Profesa Ali Mazrui, anatafsiri mauaji ya kisiasa (political assassination) kuwa ni kitendo cha siri cha kutoa uhai wa mtu mashuhuri kisiasa, kinachofanywa na wakala asiye wa serikali; kwa sababu za kisiasa au zisizofahamika.Naye Profesa William Gutteridge wa Chuo Kikuu cha Aston, anasema mauaji ya kisiasa kuwa ni kitendo cha kutoa uhai wa mtu mashuhuri katika jamii kwa sababu za kisiasa na kinajumuisha pia jaribio la mapinduzi lililoshindwa na watu wengi kuuawa katika kutekeleza kilichokusudiwa.

Kwa mantiki hii, mauaji ya Karume, kama yalivyokuwa mauaji ya Rais Anwar Sadat wa Misri, kwa kupigwa risasi wakati akiangalia gwaride la jeshi lake, yalikuwa na lengo la kuiondolea jamii kero bila umuhimu wa kubadili serikali.- Katika mauaji kama hayo, mlengwa huwa mmoja tu kama chanzo au mhimili wa kero.Karume aliuawa kwa sababu ya utawala wa kimabavu, ukatili na ukiukaji wa haki za binadamu kama tulivyoona hapo mwanzo, wakati Sadat aliuawa kwa kuisaliti jamii ya Kimisri, kwa kusaini Mkataba wa suluhu kati ya Misri na Israeli uliojulikana kama "Camp David" ili kusitisha harakati za Waarabu dhidi ya Uzayuni wa Kiyahudi.Sababu nyingine ilikuwa ni kukumbatia sera za kiuchumi za Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), hatua iliyoathiri maisha ya Wamisri kiuchumi na matarajio ya kijamii ya Waislamu nchini humo na Jumuiya pana ya Kiarabu kwa ujumla. Baada ya mauaji hayo kamatakata ilikuwa imepamba moto, lakini mtihani mkubwa ilikuwa kumkamata komandoo Ali Mahfoudh, anasimulia Kanali Kashimiri aliyepewa jukumu la kumkamata,
"wakati nikiwa nipo ndani ya ofisi pamoja na askari nikiwapa maelekezo jinsi YA kumkamata kanali Ali Mahfoudh pindi atakapoingia mara kwa ghafla kanali Seif Bakari pamoja na kanali Ali Mahfoudh wakawasili na mara kanali Ali Mahfoudh akafungua mlango akachungulia akanisalimia " kashmiri habari" nikamjibu salama bwana kisha nikamwambia ingieni bwana tulikuwa tunawasubiria nyie tuanze kikao.Ndipo yeye pamoja na kanali Seif Bakari walipoingia ndani . Nakumbuka kabisa kuwa kanali Seif Bakari alikuwa amevaa sare zake za kijeshi bila ya kuwa na silaha lakini kanali Ali Mahfoudh yeye alikuwa amevaa sare za kijeshi na alikuwa amebeba pistol mbili kiunoni na pia alikuwa na visu viwili kiunoni mwake.

Nadhani waliambiwa waje kwenye kikao hivyo walidhania kuwa kikao chenyewe ndio hiki. Nilikuwa tayari nimeshatayarisha viti vyao vya kukaa, kanali Seif Bakari alikaa kilichokuwa upande wa kushoto na kanali Ali Mahfoudh yeye alikaa kiti kilichokuwa upande wa kulia. Wakaanza kunieleza kilichotokea Zanzibar na wakaniambia kuwa wao wenyewe tayari wameshaidhibiti hali ya usalama na hivyo hapana haja ya kupeleka askari wengi Zanzibar na badala yake wapelekwe askari wachache ili kusaidia kutuliza hali ya usalama. Wakati nikiwa naendelea na mazungumzo nao kila baada ya dakika tano mkuu wa majeshi jenerali Sarakikya alikuwa ananipigia simu kuniuliza kama tayari nimeshamkamata nikawa namjibu kimkato kuwa bado huku yeye mwenyewe akiwa mbele yangu na hajui naongea na nani kwenye simu. Wakati huo nilikuwa nawapa ishara kwa siri wale askari kuwa wamkamate kanali Ali Mahfoudh lakini cha ajabu hakuna kumsogelea kumkamata.

Kwa muda wa nusu nzima askari wale walishindwa kumkamata. Tukamaliza mazungumzo yetu nae kanali Seif Bakari akasema "sasa kashmiri sisi tunaondoka zetu"nikawaambia sawa bwana. Wakaondoka wakaelekea kwa kamisaa wa siasa jeshini ili kumueleza tulichoafikiana katika kile kikao. Unajua wao walidhania kuwa kile kilikuwa ni kikao rasmi na hawakujua kuwa ilikuwa ni mbinu yangu ya kujaribu kumkamata kanali Ali Mahfoudh.
Kwa kweli nilichukia sana kuwa askari wale hawakufanya kazi ile niliyowapa. Nikawaambia wale askari " Nyie si nimewapa amri ya kumkamata kanali Ali Mahfoudh kwa nini sasa hamjamkamata muda wote huo haya nendeni sasa mkamlete mje nae hapa "Askari mmoja akaniambia "mkuu una arrest warrant ya kumkamata". Nikamjibu nyie vipi kwani jeshini pana arrest warrant embu nendeni bwana mkamlete hili ni agizo la serikali. Niliona dhahiri kuwa walikuwa wanamuogopa. Unajua Mahfoudh alikuwa ni pande la mtu tena ni komandoo aliyefuzu Cuba na kwa wakati ule alikuwa akisifika sana kwa uhodari wa kivita aliokuwa akiuonesha katika vita vya kupigania uhuru wa nchi ya Msumbiji na pia kumbuka alikuwa na silaha pale. Nikawa mkali nikazidi kuwafokea askari wale huku nikiwaona dhahiri wakionesha wasi wasi wao Ghafla askari mmoja wao akaniambia mkuu mie naenda kumkamata, kwa bahati nzuri walikuwa bado ofisini kwa kamisaa wa siasa jeshini.

Alipofika akamwambia kanali Ali Mahfoudh "kanali jamhuri ya muungano wa Tanzania imeamua ukamatwe tafadhali fuatana nami mpaka kwa kanali kashmiri ukajisalimishe". Katika hali ya kushangaza sana kanali Ali Mahfoudh alikuwa mnyonge na wala hakuleta upinzani au pingamizi. Akaja nae mpaka ofisini kwangu nikamwambia kanali Ali Mahfoudh salimisha silaha zako zote. Ndipo akatoa silaha zake zote akakabidhi.Kisha nikawaambia askari wote waliokuwepo pale watoke nje hivyo nikabaki nae pale ofisini tukiwa wawili peke yetu.

Nikamwambia una maagizo yoyote ambayo ungetaka niyafikishe kwa familia yako, akanijibu ndio akaomba nimpe karatasi aandike barua. Kwa kweli kwa kesi nzito kama ile nilikuwa na matumaini madogo sana kama angetoka salama na sikutaka aende kizuizini bila ya kuacha maagizo yoyote kwa familia yake hivyo akaandika barua ndefu sana na nikamuahidi kuwa itafika kwa familia yake. Muda mchache baadae alikuja kuchukuliwa na maofisa wa upelelezi na makosa ya jinai wakiongozwa na C.I.D Sawaya.Ndivyo ilivyokuwa bwana kumkamata yule jamaa ilikuwa ni shughuli kweli kweli. Anamaliza kusema kanali kashmiri. Nilikuja baadae kugundua kuwa yeye mwenyewe aliona ni salama kwake kukamatiwa Dar es salaam kuliko Zanzibar na ndio maana hakufanya fujo yoyote wakati anakamatwa.

Kanali Ali Mahfoudh pamoja na wenzake walihukumiwa adhabu ya kifo. Lakini baada ya mbinyo mkali kutoka kwa mashirika ya kutetea haki za binadamu washukiwa wote akiwemo kanali Ali Mahfoudh waliachiliwa huru mwaka 1978. Baada ya kuachiliwa huru kanali Ali Mahfoudh alipewa sharti la kutokukaa tena nchini na hivyo alichukuliwa na aliyekuwa rais wa Msumbiji marehemu Samora Machel na huko alifanywa kuwa mshauri mkuu wa maswala ya usalama wa nchi hiyo.Wakati nduli Iddi Amin alipoivamia Tanzania mwaka 1978 kanali Ali Mahfoudh alikuwa yupo nchini Msumbiji alipoona nchi yake imevamiwa alimuomba Samora Machel awasiliane na viongozi wa Tanzania ili nae aweze kwenda kuitetea nchi yake. Lakini taarifa zikaja kuwa hatoruhusiwa kupigana vita hiyo kwani itakuwa hatari kwake maana anaweza kuuawa na wale waliokuwa na machungu na kifo cha Mzee Karume.

Kanali kashmiri na kanali Ali Mahfoudh walikutana tena Mjini Maputo kati kati ya miaka ya 80. Kanali kashmiri anaeleza kuwa nashukuru sana nilipokutana nae alinichangamkia kama kawaida akaniambia kuwa hana kabisa kinyongo na mimi japokuwa kuna watu walimwambia kuwa eti mbaya wake ni mimi. Yeye mwenyewe aliniambia kuwa " kashmiri najua ulikuwa unatimiza amri ya wakuu wako na kwa vyovyote usingeweza kukataa kwani hata ningekuwa mimi pia ningefanya hivyo hivyo na si vinginevyo kwani kanuni ya kwanza kabisa ya uaskari ni kutii amri za wakuu wako ". Baadae alinikaribisha nyumbani kwake na tuliendelea na urafiki mpaka alipokuja kufariki.Kanali Ali Mahfoudh alifariki nchini Msumbiji na alizikwa huko huko katika makaburi ya mashujaa wa nchi hiyo.
Malengo ya mauaji ya Karume yanajidhihirisha kwa vielelezo kwa yale yaliyofuatia chini ya utawala wa mrithi wake, Alhaji Aboud Jumbe Mwinyi, aliyechukua uongozi Aprili 11, 1972.Baraza la Mapinduzi lililoketi Aprili 10 - 11, 1972, pamoja na kumthibitisha Jumbe kuanzia Aprili 7, 1972 kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza hilo, pia lilipitisha azimio la kudumisha, kulinda, kutetea na kuendeleza fikra, malengo ya kimapinduzi na sera alizoacha Karume.Hata hivyo, Wazanzibari wengi walitaka Kanali Seif Bakari amrithi Karume kwa kuwa alikuwa mtu wa karibu zaidi kwa Karume kuliko Jumbe, kwamba ndiye pekee miongoni mwa Wazanzibari ambaye angeweza kuendeleza fikra za kiongo huyo wa Taifa la Zanzibar.Nyerere aliingilia kati akiwa na hoja kwamba, kwa kuwa Rais Karume aliuawa na mwanajeshi, kumteua Bakari ambaye alikuwa mwanajeshi kumrithi kiongozi wa kiraia, kungetafsiriwa kuwa mapinduzi ya kijeshi yaliyoweka mwanajeshi madarakani.- Hoja ya Nyerere ikashinda.Kwa kuanzia, Jumbe alifuta Amri ya Karume ya kutoagiza chakula na bidhaa nyingine kutoka nje; akaruhusu akiba ya fedha za kigeni kutumika kuagiza chakula kumaliza tatizo la njaa na upungufu wa vitu, jambo lililokuwa mwiko wakati wa Karume.Vivyo hivyo, kwa mara ya kwanza, Serikali ya Zanzibar iliruhusu wanafunzi 17 kutoka Zanzibar, kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuahidi kupeleka wengi zaidi.
Desemba 1972, ASP kilifanya Mkutano Mkuu wake wa kwanza tangu 1962 uliohudhuriwa na wajumbe zaidi ya 900 kutoka Visiwani, Mwalimu Nyerere na viongozi wengine wa TANU, pamoja na wageni wengine kutoka nchi 12 za Kiafrika, wakiwamo wawakilishi wa chama cha MPLA cha Angola.Katika hotuba yake ya ufunguzi, Jumbe alilaani tawala za kimabavu na ubabe, ukandamizaji na matumizi mabaya ya vyombo vya dola dhidi ya raia, alisema:- "Viongozi lazima wawatumikie watu, na si watu wawatumikie viongozi"Kwa maneno hayo, alikuwa amefungua milango ya demokrasia Visiwani, utawala bora, uwajibikaji na kuongoza kwa mifano, tofauti na enzi za Karume.

Februari 5, 1977, Nyerere na Jumbe waliunganisha vyama vyao, TANU na ASP, kuunda Chama cha Mapinduzi - CCM, jambo ambalo lisingewezekana wakati wa Karume ambaye hata Muungano wenyewe aliweza kuusigina kwa kisigino cha nguvu.- Vivyo hivyo, mwaka 1979, Zanzibar ilijipatia Katiba yake ya kwanza baada ya Katiba ya Uhuru ya 1963, chini ya Serikali ya Mseto wa Zanzibar Nationalist Party (ZNP) na Zanzibar and Pemba People's Party (ZPPP). Ni wakati wa utawala wa Jumbe, Zanzibar ilipata Bunge (Baraza la Uwakilishi) lake la kwanza kwa njia ya uchaguzi, wakati kabla ya hapo, Karume aliapa pasingekuwa na uchaguzi Zanzibar kwa miaka 50, kuanzia 1964 hadi 2014.Chini ya Jumbe, kwa mara ya kwanza tangu 1964, wanasheria waliruhusiwa kufanya kazi Zanzibar; watu hawakugongewa tena milango usiku na kupotea katika mazingira ya kutatanisha. Na tazama, yote yalifanywa kuwa mapya, ambapo isingewezekana chini ya utawala wa Rais Karume. Mwaka 1984, Jumbe alirejea rasmi kwenye misingi na misimamo ya Karume juu ya Muungano hasa alipokuja na kile kilichoitwa kuvunja katiba ya jamhuri kwa Jumbe kurejea kauli ya "Tuvunje Muungano" hali iliyomuuzi na kumsononesha Mwalimu Nyerere, nakupelekea kuitishwa kikao cha dharula mjini Dodoma nakisha kuvuliwa vyeo vyote vya kichama na kiserikali ikiwemo uanachama na kuwekwa kizuizini Mjimwema Kigambo.

KITABU cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi kinapatikana naeneo yafuatayo kwa Dar.

1. Duka la House of Wisdom lilipo Posta Mtaa wa Samora Jengo la NHC ghorofa ya Kwanza.

2. Dar es Salaam Bookshop lipo Posta mtaa wa Makunganya karibu na Klabu ya starehe Bilz,

3. Imalaseko Supermarket iliyopo Posta mtaa wa Pamba mkabala na ATCL.

Popote ulipo Tanzania na nje ya nchi utapata kitabu. Gharama ni shilingi 30,000 kwa rejareja na shilingi 25,000 kwa jumla

Waweza kulipia kwa M-Pesa +255755865544 utelewe ulipo.

Kwa waliopo nje ya Tanzania pia unaweza kununua nakala laini katika mtandao wa Amazon product ASIN B01GPXFDB6
Mzee wa copy and paste, usisahau kilipia tangazo jf
 
mzee jumbe apate pumziko la millele ametimiza wajibu wake ,kwa jamii ,pia nikupongeze yericko nyerere kwa ukusanyaji huu wa historia ya masuala ya nchi yetu ,tuna wasomi wengi ila wewe umeonyesha mfano wa pekee kwa kuandika si kuhadithia ,
 
Miaka nenda rudi tumekuwa tunasikia nyerere aliua karumue kumbe sio, mleta uzi umetufungua sana, maan huu uzi ni real sio fake, ungekuwa fake ungekuwa unajicontradict sana pia usingekuwa mrefu.
 
Nitakuwa wa mwisho kusoma hiki kitabu sababu kimendikwa na mtu amabaye hana tabiaa ya kusema ukweli mara nyingi. Sasa nitaamini vipi yaliyoandikwa humo kama ni ya kweli?? Je katika kitabu chako ulitoa wapi hizi information? Umehadithiwa au kuna mahali zimeandikwa au umeamua tu kutoa version ya story yako?
 
Shukrani kwa hadith yako nzuri lkn kuna vitu ambavyo cjavielewa unaposema karume alikuwa amsikilkzi nyerere unatumia vigezo gani? Kwani Zanzibar baada ya kupata uhuru iliungana na tanzania kwa malengo yapi? Na kwann Raisvwa Tanganyika wakati huo yeye tu ndo asikilizwe?
Halafu tuambie lini Zanziber ilikuwa koloni la t@nganyika?
Halafu inasemekana uyo kiongozi ambae ulikuwa wewe unayepeda asikilizwe yeye ndo aliongoza kwa kuua watu ikiwamo pamoja na kumuua karume na sokoine? Sasa huo uvumilivu na subira aliokuwa nazo ni zip?
 
Nitakuwa wa mwisho kusoma hiki kitabu sababu kimendikwa na mtu amabaye hana tabiaa ya kusema ukweli mara nyingi. Sasa nitaamini vipi yaliyoandikwa humo kama ni ya kweli?? Je katika kitabu chako ulitoa wapi hizi information? Umehadithiwa au kuna mahali zimeandikwa au umeamua tu kutoa version ya story yako?
Umesema utakuwa wa mwisho kukisoma, amini kuwa binadamu wanaozungumza kiswahili hivi sana wapo milioni 407,sasa mpaka sasa nimeuza nakala miatano tu, hivyo vumilia mpaka wafike milioni 406 ndipo nitajibu maswali yako ili ielewe na kisha kukisom hiki kitabu
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom